Naibu Waziri, Wizara ya Mambo ya Nje
na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro (Mb) amekutana na
kufanya mazungumzo na Balozi wa Palestina nchini Mhe. Balozi Hamdi Mansour AbuAli
Pamoja na Kaimu Balozi wa Uswisi nchini Bw. Leo Nascher, katika Ofisi ndogo za
Wizara Jijini Dar es Salaam.
Mazungumzo ya Mhe. Dkt. Ndumbaro
pamoja na Balozi wa Palestina, Mhe. Balozi Abuali walikubaliana kuendelea kuimarisha
diplomasia ya uchumi hasa katika sekta ya uwekezaji wa kiwanda cha dawa na
vifaa tiba pamoja na kilimo.
Katika hatua nyingine, Naibu Waziri Dkt.
Ndumbaro na Kaimu Balozi wa Uswisi nchini Bw. Leo Nascher mazungumzo yao yalihusu
maandalizi ya mpango mpya wa maendeleo wa mwaka 2021-2024 baina ya Tanzania na
Uswisi yanayoendelea.
Mpango wa maendeleo uliopo unatarajiwa
kufikia ukomo mwaka huu 2020. Ambapo mpango mpya utajikita zaidi katika
kuimarisha sekta ya afya, mazingira, utawala bora na kukuza ajira kwa vijana na
wanawake nchini.
Masuala mengine yaliyojadiliwa
yalihusu programu ya Ukuzaji Ujuzi wa Ajira nchini (Skills for Employment
Tanzania) na shuguli zinazofanywa na NGOs za Uswisi zilizopo nchini.
Pia Kaimu Balozi huyo alieleza kuwa
Uswisi itaendelea kusaidia mradi wa malaria na kuchangia fedha katika Mfuko wa
Afya ya Jamii (CHF).
Kwa upande wake Mhe. Dkt. Ndumbaro alisifu
uhusiano baina ya nchi hizi mbili kwa kueleza kuwa Tanzania itaendelea
kushirikiana na Uswisi katika kukuza zaidi mahusiano hayo.
Balozi wa Palestina Nchini Mhe. Balozi
Hamdi Mansour AbuAli akimuelezea jambo Naibu Waziri, Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro (Mb) walipokutana kwa
mazungumzo leo katika Ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam
Naibu Waziri, Wizara ya Mambo ya Nje
na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro (Mb) akiongea na Balozi
wa Palestina Nchini Mhe. Balozi Hamdi Mansour AbuAli walipokutana kwa
mazungumzo leo katika Ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam
Kaimu Balozi wa Uswisi nchini Bw. Leo
Nascher akiongea na Naibu Waziri, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro (Mb) walipokutana kwa mazungumzo leo
katika Ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam
Naibu Waziri, Wizara ya Mambo ya Nje
na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro (Mb) akimfafanulia
jambo Kaimu Balozi wa Uswisi nchini Bw. Leo Nascher wakati wa mazungumzo leo katika
Ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.