Tanzania
na China zimeahidi kuendeleza ushirikiano wa kidiplomasia ili kuhakikisha kuwa
nchi hizo zinakuwa na maendeleo endelevu.
Makubaliano
hayo yamefanywa na Balozi wa China nchini, Mhe. Wang Ke, wakati alipokutana kwa
mazungumzo na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki, Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge leo jijini Dar es Salaam.
Katibu
Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brigedia
Jenerali Ibuge amesema kuwa wamejadili masuala mbalimbali ikiwemo suala la
namna ya kutekeleza nia ya Viongozi Wakuu wa nchii za China na Tanzania (Rais
wa China, Mhe. Xi Jinping pamoja na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.
John Joseph Pombe Maufuli) ya kupunguza madhara yatokanayo na ugonjwa wa COVID
19 ikiwemo kufutiwa na kusamehewa madeni.
Naishukuru
Serikali ya China kwa uhusiano na ushirikiano ambao imekuwa ikionesha kwa
Tanzania. Uhusiano huo umeendelezwa na viongozi wa pande zote mbili ambao
umekuwa ukiimarika siku hadi siku na kuahidi kuwa serikali ya Tanzania
itaendela kudumisha ushirikiano wake wa kidiplomasia kati yake na China.
Pamoja
na mambo mengine, mazungumzo yalijadili masuala ya biashara na uwekezaji, mradi
wa nyumba 25 za wataalum wa Afya zilizopo Osterbay jijini Dar es Salaam.
Kwa
upande wake Balozi Wang Ke pamoja na mambo mengine, ameipongeza Serikali ya
Tanzania kwa jitihada ilizochukua katika kukukuza uchumi wake hadi kufikia
uchumi wa kati, pamoja na mapambano dhidi ya COVID 19.
"Leo
nimekutana na Katibu Mkuu wa Mambo ya Nje, Balozi Brigedia Jenerali Ibuge na
kuongea mambo mbalimbali ya ushirikiano na tunaipongeza Serikali ya Tanzania
kwa jitihada ilizochukua katika kufanya
kazi kwa bidii na kukuza uchumi wake hadi kufikia uchumi wa kati, pamoja na hatua
ilizochukua katika kupambana na janga la COVID 19 ambapo tumefurahishwa kuona
janga la COVID 19 limeisha," Amesema Balozi Ke.
Balozi
Ke ameongeza kuwa wamekubaliana katika maongezi hayo pia kuendeleza ushirikiano
wa kufanya kazi kwa pamoja kwa manufaa ya mataifa mawili (Tanzania na China)
ili kuhakikisha uhusiano na ushirikiano unazidi kukua na kuimarika.
Tanzania na China zimekuwa zikishirikiana
katika sekta za kilimo, biashara na uwekezaji, miradi ya mikopo nafuu na misaada,
Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA), Uchukuzi, Afya, Utalii na
utamaduni.
China
na Tanzania zilianzisha mahusiano rasmi ya kidiplomasia mwaka 1964.
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo
ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brigedia Jenerali Wilbert
Ibuge akiongea na Balozi wa China nchini, Mhe. Wang Ke, wakati walipokutana kwa
mazungumzo leo jijini Dar es Salaam
|
Balozi wa China nchini,
Mhe. Wang Ke akiongea na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Afrika Mashariki, Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge wakati Walipokutana
kwa mazungumzo leo jijini Dar es Salaam |