Thursday, July 16, 2020

DKT. NDUMBARO AFANYA MAZUNGUMZO NA KAMATI YA ULINZI NA USALAMA YA MKOA WA RUVUMA

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amekutana na kufanya mazungumzo na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Ruvuma ikiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Wilaya hiyo Mhe. Christina Mndeme ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo.

Mazungumzo hayo yamefanyika baada kuhitimisha ziara iliyofanywa na Dkt. Ndumbaro ya kutembelea mipaka inayoinganisha Tanzania na nchi jirani ya Msumbiji iliyopo katika Mkoa wa Ruvuma. 

Dkt. Ndumbaro kwa nyakati tofauti katika mwaka huu amefanya ziara maalumu katika mpaka wa Magazini uliopo Wilayani Namtumbo-Ruvuma, Wenje uliopo Wilayani Tunduru-Ruvuma, Chiwindi uliopo Wilayani Nyasa-Ruvuma  na baadaye mpaka wa Mkenda uliopo Wilaya ya Songea Vijijini. Mipaka yote inaiunganisha Tanzania na Nchi jirani ya Msumbiji. 

Lengo la kufanya ziara ilikuwa ni kubaini na kutatua changamoto zinazokabili maeneo ya mipakani sambamba na kufanya ufuatiliaji wa utekelezaji wa Diplomasia ya Uchumi. Katika ziara hizo Dkt. Ndumbaro alikutana na kuafanya mazungumzo na baadhi ya wananchi na watumishi katika mipaka husika. Sambamba na changamoto kadhaa alizozibaini aliridhishwa na utendaji wa Watumishi waliopo mpakani na kuwahimiza kundelea kufanyakazi kwa bidii,ubunifu na kwa kuzingatia maadali.

Aidha, Dkt. Ndumbaro katika kikao chake na Kamati ya Ulinzi ya Mkoa wa Ruma amebainisha kuwa changamoto nyingi zilizoelezwa mipakani zikiwemo ukosefu wa umeme, barabara za kiwango cha lami, mawasiliano na Vituo vya kutoa huduma Pamoja Mpakani (OSBP), Serikali chini ya usimamizi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli tayari zimeanza kufanyiwa kazi.

Dkt. Ndumbaro kwa upande wake amehimiza umuhimu wa Mamlaka za Mkoa hasa zilizopo maeneo ya Mipakani kuendelea kushirikiana na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki katika kutekeleza Diplomasia ya Uchumi, kudumisha na kulinda uhusiano wa kidiplomasia na nchi jirani.

Wakati huo huo Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma na Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Mhe. Christina Mndeme kwa niaba ya Kamati ya Ulinzi ya Mkoa, amempongeza Naibu Waziri Mhe. Dkt. Ndumbaro kwa ziara hiyo na jitihada anazifanya katika kuhakikisha Diplomasia ya Uchumi inaendelea kutekelezwa kwa mafanikio makubwa. 

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma  Mhe. Christina Mndeme wakisalimia walipokutana kwa mazungumzo katika Ofisi za Makao Makuu ya Mkoa huo.
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro akisaini kitabu cha Wageni alipo wasili katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mhe. Christina Mideme
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro akifafanua jambo alipokutana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Ruvuma.

Kikao kikiendelea

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.