Friday, August 14, 2020
Thursday, August 13, 2020
TANZANIA YAJIVUNIA MAFANIKIO WAKATI WA UENYEKITI WA SADC
Tanzania imejivunia mafanikio yaliyopatikana wakati ikiwa mwenyekiti wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli.
Mafanikio
hayo yameelezewa katika Mkutano wa 40 wa Baraza la Mawaziri na Waziri wa Mambo
ya Nje na Ushirikano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi ulifanyika
kwa njia ya mtandao jijini Dar es Salaam.
Kupitia
mkutano huo, Prof. Kabudi amekabidhi
uenyekiti wa Baraza la Mawaziri kwa Balozi wa Msumbiji nchini, Mhe. Monica P.
Clemente kwa niaba ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Msumbiji Mhe. Verónica Nataniel
Macamo Dlhovo
Prof.
Kabudi amesema pamoja na janga la ugonjwa wa homa kali ya mapafu (COVID 19)
jumuiya ya SADC imeendelea kufanya kazi zake, mikutano yake chini ya uongozi wa
Tanzania kwa ufanisi wa hali ya juu kwa kupitia njia ya mtandao (video
conference)
"Nasema
ni mafanikio makubwa kwa sababu Jumuiya nyingine za kikanda zimeshindwa kufanya
hivyo, sisi ndiyo jumuiya pekee iliyoanza utaratibu huu wa aina hii ya mikutano
kwa sababu kwetu tuliona COVID 19 ni changamoto ambayo haiwezi kutuzuia kufanya
shughuli zetu,". Amesema Prof. Kabudi
Prof.
Kabudi ameongeza kuwa mbali na kupambana a janga la COVID 19, mafanikio mengine
ni kuifanya lugha ya Kiswahili kuwa lugha rasmi ya nne katika jumuiya ya SADC,
lugha nyingine ni Kiingereza, Kireno na Kifaransa.
"Lugha
ya Kiswahili kwa Tanzania ni lugha ya ukombozi wa Afrika, ndiyo lugha
iliyotumika wakati wa kuwafundisha wapigania uhuru mbinu za kuwasiliana wakati
wa ukombozi kwa mataifa ya Afrika," Amesema Prof. Kabudi.
Prof.
Kabudi ameyataja mafanikio mengine yaliyopatikana wakati Tanzania ikiwa
mwenyekiti wa SADC ni kusimamia na kukamilika kwa Mwongozo wa kusafirisha
bidhaa na huduma kwa nchi wanachama katika kipindi cha (COVID-19). Mwongozo huo
umelenga kudhibiti kuenea kwa maambukizi ya virusi vya Corona na kurahisisha
usafirishaji wa bidhaa na huduma mbambali baina ya nchi wanachama.
Tanzania
imewezesha agenda ya viwanda kutekelezwa ambapo wakati wa COVID 19 tumeweza
kuongeza uwezo wetu wa kutengeneza dawa kwa kuwa mataifa makubwa duniani mara
baada ya kuibuka kwa covid 19 walisitisha kuuza dawa katika nchi nyingine ili
wazitumie dawa hizo ndani ya nchi zao.
"Tunaimani
kuwa msingi uliowekwa wakati wa COVID 19 utaimarisha jitiada zetu za kuwa na uchumi
wa viwanda, uchumi wa kati na uchumi wa juu. Na sisi imekuwa jambo la faraja
kubwa kuingia katika uchumi wa kati kabla ya miaka mitano iliyokuwa imepangwa
hapo awali," Amesema Prof. Kabudi.
"Chaguzi
katika nchi za Malawi, Mauritius, Namibia zimefanyika kwa amani na utulivu. Ii
imedhihirisha wazi kuwa demokrasia katika ukanda wetu inazidi kukua………haya yote
ni mafanikio makubwa kwetu tukiwa mwenyekiti wa SADC," ameongeza Prof.
Kabudi.
Nae
Balozi wa Msumbiji nchini, Mhe. Monica Clemente aliyemuwakilisha Waziri wa
Mambo ya Nje Msumbiji, amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kwa kazi kubwa aliyofanya wakati wa
Uenyekiti wake wa SADC.
Amefanya
mambo makubwa kabisa kwa nchi wanachama wa SADC na amekuwa kama Mwalimu kwa
nchi nyingine kutokana na maendeleo yaliyopatikana wakati wa uongozi wake akiwa
mwenyekiti wa SADC.
"Sisi
Msumbiji tunashukuru kwa kupokea Uenyekiti wa SADC na tunaahidi kujitahidi
kadri ya uwezo wetu kuendeleza yale yote yaliyofanywa na Tanzania wakati akiwa
Mwenyekiti, kwani Tanzania amekuwa mwalimu kwetu na nchi nyingine za SADC,"
amesema Balozi Monica.
Mkutano wa 40 wa baraza la mawaziri umehudhuriwa na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango, Waziri wa Afya , Maendeleoya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu, Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba, Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Innocent Bashungwa wakifuatilia mkutano kwa njia ya Mtandao (Video Comnference)
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John
Kabudi akifungua mkutano wa 40 wa Baraza la Mawaziri uliofanyika jijini Dar
es Salaam kwa njia Mtandao (Video Comnference)
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi akikabidhi uenyekiti wa SADC ngazi ya mawaziri kwa Balozi wa Msumbiji nchini, Mhe. Monica P. Clemente ambaye amemwakilisha Waziri wa Mambo ya Nje Msumbiji Mhe.Verónica Nataniel Macamo Dlhovo
Baadhi ya viongozi waandamizi wa Serikali wakifuatilia Mkutano wa 40 wa Baraza la Mawaziri wa SADC uliofanyika kwa njia ya mtandao jijini Dar es Salaam
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikano wa Afrika Mashariki, Prof. Kabudi pamoja na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu, Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba, Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Innocent Bashungwa wakifuatilia mkutano kwa njia ya Mtandao (Video Conference)
Baadhi ya maafisa waandamizi/Makatibu Wakuu wakifuatilia mkutano wa 40 wa Baraza la Mawaziri uliofanyika leo kwa nnjia mtandao jijini Dar es Salaam
Sunday, August 9, 2020
MKUTANO WA 40 WA SADC KUFANYIKA JIJINI DODOMA
Mkutano wa 40 wa Wakuu wa Nchi na
Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), unaotarajiwa
kufanyika tarehe 17 Agosti, 2020 kwa njia ya mtandao (video conference) Ikulu Chamwino
Jijini Dodoma.
Akiongea na waandishi wa habari jijini
Dar es Salaam, Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Balozi, Brigedia Jenerali, Wilbert Ibuge amesema mkutano wa Wakuu wa Nchi na
Serikali utatanguliwa na vikao vya Kamati ya kudumu ya Maafisa Waandamizi/Makatibu
Wakuu na Mkutano wa Baraza la Mawaziri itakayoanza kufanyika tarehe 10 -13
Agosti, 2020 jijini Dar es Salaam kwa njia ya mtandao (video conference).
"Kulingana na taratibu na miongozo ya uendeshaji wa SADC, nafasi ya uenyekiti hushikiliwa na nchi wanachama kwa kupokezana kwa kipindi cha mwaka mmoja mmoja. Tanzania imekuwa Mwenyekiti tangu Mwezi Agosti, 2019 na inatarajwa kukabidhi Uenyekiti kwa Jamhuri ya Msumbiji katika Mkutano huo. Aidha, itakumbukwa kuwa mara ya mwisho Tanzania ilishika nafasi hii mwaka 2003," Amesema Balozi Ibuge.
Ameongeza kuwa, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa sasa wa SADC, atakabidhi Uenyekiti kwa Mheshimiwa Philipe Jacinto Nyusi, Rais wa Jamhuri ya Msumbiji tarehe 17 Agosti 2020 jijini Dodoma kwa njia ya Video Conference.
Balozi
Ibuge ameongeza kuwa, kwa kuwa kwa sasa Kiswahili ni moja kati ya lugha rasmi
za mikutano ya SADC, lugha hiyo itatumika katika ngazi ya Mkutano wa Baraza la
Mawaziri na ngazi ya Wakuu wa Nchi na Serikali.
Aidha, Katibu Mkuu, Balozi Ibuge amesema
kuwa, kutokana na janga la COVID-19 na
mwongozo uliotolewa na Shirika la Afya Duniani (WHO) juu ya kufanya
mikutano ya ana kwa ana, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania italazimika kukabidhi
uenyekiti kwa njia ya mtandao ambapo Balozi wa Msumbiji hapa nchini
atakabidhiwa uenyekiti kwa niaba ya nchi yake. Hali kadhalika, Balozi wa
Tanzania nchini Msumbiji atakabidhi Uenyekiti kwa Serikali ya Jamhuri ya
Msumbiji kwa niaba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Katika hatua nyingine, Balozi Ibuge amesema kuwa mkutano huo utaongozwa na kauli mbiu ambayo ni “Miaka 40 ya Kuimarisha Amani na Usalama, Kukuza Maendeleo na kuhimili Changamoto zinazoikabili Dunia” ambapo kauli mbiu hiyo inatakiwa kutekelezwa na nchi zote Wanachama.
Mkutano huo unatarajiwa kushirikisha Wakuu wa Nchi na Serikali kutoka nchi 16 wanachama wa SADC wakiwa katika nchi zao. Nchi hizo ni Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jamhuri ya Angola, Jamhuri ya Botswana, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Muungano wa Visiwa vya Comoro, Ufalme wa Eswatini, Ufalme wa Lesotho, Jamhuri ya Namibia, Jamhuri ya Visiwa vya Shelisheli, Jamhuri ya Afrika Kusini, Jamhuri ya Malawi, Jamhuri ya Msumbiji, Jamhuri ya Mauritius, Jamhuri ya Madagascar na Jamhuri ya Zambia, Jamhuri ya Zimbabwe.
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi, Briedia Jenerali, Wilbert Ibuge akiongea
na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi, Briedia Jenerali, Wilbert Ibuge akiongea
na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam
Mkutano ukiendelea jijini Dar es Salaam
Friday, August 7, 2020
SADC NGAZI YA MAKATIBU WAKUU WAJADILI, KUBORESHA RASIMU ZA NYARAKA ZA KISERA NA KIMKAKATI
TANZANIA YASAINI MKATABA WA MAPITIO WA GEORGETOWN WA JUMUIYA YA NCHI ZA AFRIKA, CARIBBEAN NA PACIFIC
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
TANZANIA YASAINI MKATABA WA MAPITIO WA GEORGETOWN WA
JUMUIYA YA NCHI ZA AFRIKA, CARIBBEAN NA PACIFIC
Dodoma, 06 Agosti 2020
Tanzania imesaini Mkataba wa mapitio wa Georgetown unaosimamia mahusiano na uendeshaji wa Jumuiya ya Nchi za Afrika, Caribbean na Pacific ambayo zamani ilikuwa ikiitwa ACP na sasa Organisation of African, Carribean and Pacific States (OACPS) iliyo na nchi wanachama 79.
Mkataba huo ulisainiwa na balozi wa Tanzania nchini Ubelgiji, Mhe. Jestas Abuok Nyamanga kwa niaba ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jijini Brussels, Ubelgiji tarehe 31 Julai 2020. Hivyo Tanzania inakuwa nchi ya 42 kati ya nchi 79 kusaini Mkataba wa mapitio wa Georgetown.
Mkataba wa Georgetown umefanyiwa mapitio ili uweze kuendana na wakati kwa kuzingatia mabadiliko makubwa yanayoendelea kutokea duniani katika nyanja za kisiasa, kiuchumi, kijamii na kimazingira tangu kuanzishwa kwa ACP mwaka 1975. Mchakato wa kufanya mapitio ya mkataba huu ulianza mwezi Machi 2013 kupitia timu maalum iliyoanzishwa kukusanya maoni na kuleta mapendekezo chini ya Uenyekiti wa Rais Mstaafu wa Nigeria, Mhe. Olusegun Obasanjo.
Aidha, Mwaka 2019 mchakato wa mapitio hayo ulihitimishwa kwa kuridhiwa na Wakuu wa Nchi na Serikali wa nchi za OACPS katika mkutano wao uliofanyika mwezi Desemba 2019 jijini Nairobi, Kenya.
Mkataba wa Georgetown ndiyo ulianzisha ACP mwaka 1975 katika mji wa Georgetown nchini Guyana. Tanzania ilisaini Mkataba huo wa awali tarehe 11 Desemba 1975 na imedumu ikiwa mwanachama wa ACP tangu wakati huo.
Pamoja na kuwa mwanachama Tanzania imekuwa ikinufaika katika masuala ya kiuchumi, kijamii, biashara, na uwekezaji kupitia ushirikiano maalum baina ya nchi za ACP na Umoja wa Ulaya unaosimamiwa na mikataba ya Lome na Cotonou. Vilevile miradi ya ubia wa maendeleo na ile ya mtangamano wa nchi za ACP chini ya ufadhili wa Mfuko wa Maendeleo wa Ulaya. Pia ushirikiano katika masuala ya kubadilishana ujuzi na uzoefu na nchi za ACP, mshikamano wa kisiasa na kidiplomasia katika kutetea maslahi ya Tanzania kimataifa kupitia jukwaa la ACP.
Imetolewa
na;
Kitengo
cha Mawasiliano ya Serikali
==============================================
Balozi wa Tanzania nchini Ubelgiji, Mhe. Jestas Abuok Nyamanga
akisaini Mkataba wa Mapitio wa Georgetown mjini Brussels, Ubelgiji
Mhe. Nyamanga, Maafisa wa Ubalozi na Mwanasheria wa Jumuiya ya OACPS, Dkt. Emmanuel Opoku wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kukamilisha zoezi la kusaini Mkataba.
Thursday, August 6, 2020
TANZANIA YACHAGULIWA KUWA RAIS WA BARAZA LA MAWAZIRI WA JUMUIYA YA NCHI ZA AFRIKA, CARRIBEAN NA PACIFIC
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
TANZANIA YACHAGULIWA KUWA RAIS WA BARAZA LA MAWAZIRI WA JUMUIYA YA NCHI ZA AFRIKA, CARRIBEAN NA PACIFIC
Dodoma, 6 Agosti 2020
Serikali ya Tanzania imechaguliwa kuwa Rais wa Baraza la Mawaziri wa
Jumuiya ya Nchi za Afrika, Carribean na Pacific (Organisation of African,
Carribean and Pacific States-OACPS) kwa
kipindi cha miezi sita kuanzia tarehe 1 Agosti 2020 hadi tarehe 31 Januari
2021.
Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi, Waziri wa Mambo ya
Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki alikabidhiwa rasmi nafasi hiyo
iliyopokelewa kwa niaba yake na Mhe. Dkt. Damas Daniel Ndumbaro, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano
wa Afrika Mashariki wakati wa Mkutano wa Dharura wa Baraza la Mawaziri wa
Jumuiya hiyo uliofanyika kwa njia ya mtandao tarehe 28 Julai 2020.
Tanzania inakuwa Rais wa Baraza hilo kutokana na Balozi wa Tanzania nchini Ubelgiji, Mhe. Jestas
Abuok Nyamanga kuchaguliwa kwa kauli moja kuwa Mwenyekiti wa Mabalozi wa Nchi
za OACPS waliopo Brussels. Kwa mujibu wa Jumuiya ya OACPS, nchi inayotoa Mwenyekiti wa Mabalozi wa
Jumuiya hiyo, Waziri wake anayesimamia masuala ya OACPS ambaye ni Waziri wa
Mambo ya Nje moja kwa moja anakuwa Rais wa Baraza la Mawaziri. Uamuzi wa
kuichagua Tanzania ulifanywa na Mabalozi kutoka nchi 15 za Ukanda wa Mashariki
mwa Afrika kwenye kikao kilichofanyika tarehe 2 Julai 2020 na kuthibitishwa kwa
kauli moja na mabalozi wote wa nchi 79 wa OACPS kupitia kikao chao kilichofanyika
Brussels tarehe 14 Julai 2020.
Tanzania ambayo inachukua nafasi hiyo kutoka kwa Gambia, imejipanga
kutekeleza masuala mbalimbali yenye maslahi kwa Nchi za OACPS ikiwa ni pamoja
na kusimamia ukamilishwaji wa majadiliano kuhusu Mkataba mpya wa ushirikiano wa
Nchi za OACPS na Umoja wa Ulaya (EU) unaotarajiwa kuanza kutumika mwezi Januari
2021 baada ya mkataba wa sasa wa Cotonou (Cotonou Partnership Agreement)
kufikia ukomo mwezi Desemba 2020, pamoja na kuhakikisha maslahi ya nchi za OACPS yanaingizwa kwenye
mkataba huo mpya. Aidha, Tanzania imejipanga kusimamia utekelezaji wa mikakati
mbalimbali ya Jumuiya ya OACPS katika kukabiliana na janga la ugonjwa wa COVID-19
na madhara yake kiuchumi kwa nchi wanachama.
Kadhalika, maeneo mengine ya kipaumbele yatakayosimamiwa na Tanzania
katika kipindi cha Urais wa Baraza hilo ni kusimamia mikakati ya kuongeza mtangamano na ushirikiano
miongoni mwa nchi wanachama wa jumuiya; kusimamia mabadiliko ya kiutendaji na
mifumo ili kuendana na wakati pamoja na kudumisha mshikamano na umoja miongoni
mwa nchi wanachama wa Jumuiya.
Vilevile miongoni mwa manufaa ya Tanzania kuwa Rais wa Baraza hilo ni pamoja na kuongeza ushawishi wa nchi yetu
katika kupanga na kutekeleza mikakati, miradi na programu mbalimbali za Jumuiya
ya OACPS ambazo ni pamoja na zile zinazotekelezwa kwa kushirikiana na Umoja wa
Ulaya na wabia wengine wa maendeleo kama vile kilimo, uwekezaji, biashara na
ujasiriamali, mazingira, miundombinu, vijana na utamaduni.
Hii ni mara ya tatu kwa Tanzania kuwa Rais wa
Baraza la Mawaziri na Mwenyekiti wa Mabalozi wa nchi za OACPS tangu ilipojiunga mwaka 1975. Miongoni mwa sababu zilizopelekea Tanzania kuchaguliwa
kwenye nafasi hiyo ni kutokana na kuongozeka kwa ushawishi wake kwenye Jumuiya
ya OACPS, Sera na hatua thabiti zinazochukuliwa na Mhe. Dkt. John Pombe Joseph
Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kusimamia masuala
mbalimbali ya kitaifa na kimataifa pamoja na utendaji madhubuti wa Wizara ya
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki katika kusimamia Sera ya Mambo
ya Nje ikiwemo ushiriki mahiri wa
Tanzania katika masuala yanayogusa maslahi ya nchi wanachama wa Jumuiya ya
OACPS.
Imetolewa
na;
Kitengo
cha Mawasiliano ya Serikali.
Wednesday, August 5, 2020
TROIKA YAJADILI NAMNA YA KUIMARISHA HALI YA USALAMA NCHINI DRC
Mkutano ukiendelea
BALOZI WA TANZANIA NCHINI UBELGIJI NA MWAKILISHI KATIKA UMOJA WA ULAYA AWASILISHA HATI ZA UTAMBULISHO
Balozi Nyamanga akitoa maelezo
mafupi kwa Mhe. Ursula von der Leyen kabla ya kuwasilisha rasmi Hati za
Utambulisho. |
Picha ya pamoja baada ya
kukamilika kwa zoezi la kuwasilisha Hati za Utambulisho. |
MKUTANO MAALUM WA 41 WA BARAZA LA MAWAZIRI LA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI
Kutoka Kushoto; Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki (Mb) Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro, Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba (Mb) na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary M. Mwanjelwa (Mb) wakiwa katika Mkutano Maalum wa 41 uliokuwa ukiendelea kwa njia ya Mtandao (Video Conferencing).
Wajumbe wa Mkutano wakifuatilia wa Mkutano Maalum wa 41 wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Afrika Mashariki uliokuwa ukiendelea kwa njia ya Mtandao (Video Conferencing).
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki (Mb) Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro akifuatilia Mkutano wa Maalum wa 41 wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Afrika Masahariki uliokuwa ukiendelea
Kutoka Kushoto; Mkurugenzi wa Siasa, Ulinzi na Usalama Mhe. Balozi Stephen Mbundi, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki (Mb) Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro, Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba (Mb) na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary M. Mwanjelwa (Mb) wakiwa katika Mkutano Maalum wa 41 uliokuwa ukiendelea kwa njia ya Mtandao (Video Conferencing).
Sunday, August 2, 2020
BALOZI MTEULE WA MAREKANI NA BALOZI MTEULE WA VIET NAM WAKABADHI NAKALA ZA HATI ZA UTAMBULISHO
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi akipokea nakala ya hati ya utambulisho kutoka kwa Balozi Mteule wa Viet Nam Nchini Tanzania Mhe.Nguyen Nam Tien,na baadae kuwasilisha hati za utambulisho kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi akiwa katika mazungumzo na Balozi Mteule wa Viet Nam Nchini Tanzania Mhe.Nguyen Nam Tien,muda mfupi kabla ya kuwasilisha hati za utambulisho kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli.
Balozi Mteule wa Viet Nam Nchini Tanzania Mhe.Nguyen Nam Tien akimsikiliza Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi mara baada ya kumkabidhi nakala ya hati za utambulisho
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi na Balozi Mteule wa Viet Nam Nchini Tanzania Mhe.Nguyen Nam Tien wakiwa katika mazungumzo pamoja na baadhi ya maafisa na Wakurugenzi kutoka pande zote mbili |
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi akipokea nakala ya hati ya utambulisho kutoka kwa Balozi Mteule wa Marekani Dkt. Donald John Wright na baadae kuwasilisha hati za utambulisho kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli. |
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi akiwa katika mazungumzo na Balozi Mteule wa Viet Nam Nchini Tanzania Mhe.Nguyen Nam Tien,muda mfupi kabla ya kuwasilisha hati za utambulisho kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge akisalimiana na Balozi Mteule wa Viet Nam hapa Nchini Mhe. Nguyen Nam Tien muda mfupi kabla ya kukabidhi nakala ya hati za utambulisho kwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (hayupo pichani) |
Saturday, August 1, 2020
PROF. KABUDI AZINDUA MAONESHO YA NANE NANE MKOANI MOROGORO
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi akisaini kitabu cha wageni alipowasili katika viwanja vya Mwalimu Nyerere kunakofanyika maonesho ya siku ya wakulima nane nane Mkoani Morogoro.Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo na kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Abubakar Kunenge
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi akimsikiliza mmoja wa wafanyakazi wa bodi ya Sukari katika viwanja vya Mwalimu Nyerere kunakofanyika maonesho ya siku ya wakulima nane nane Mkoani Morogoro
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi akiangalia moja ya mashine ya mano ya uzalishaji wa sukari katika viwanja vya Mwalimu Nyerere kunakofanyika maonesho ya siku ya wakulima nane nane Mkoani Morogoro
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi akiangalia moja ya teknolojia ya kisasa ya umwagiliaji wa mboga mboga katika viwanja vya Mwalimu Nyerere kunakofanyika maonesho ya siku ya wakulima nane nane Mkoani Morogoro
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki akizungumza na kaumu ya wananchi (hawapo pichani) waliohudhuria sherehe za ufunguzi wa maonesho ya wakulima nane nane yaliyofanyika katika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere Mkoani Morogoro.