Katibu Mkuu wa Umoja wa Posta Afrika (Pan African Postal Union - PAPU) Mhe. Younouss Djibrine akisaini kitabu cha wageni alipowasili alipowasili katika ofisi za Wizara jijini Dodoma. |
Wednesday, February 17, 2021
WIZARA YA MAMBO YA NJE YAIAHIDI USHIRIKIANO PAPU
Tuesday, February 16, 2021
BALOZI BRIGEDIA JENERALI IBUGE; USHAWISHI WA TANZANIA BADO NI IMARA KIKANDA NA KIMATAIFA
Sehemu ya Wadau kutoka NDC wakifuatilia mhadhara uliokuwa ukitolewa na viongozi wa Wizara |
Mkurugenzi wa Siasa,Ulinzi na Usalama Balozi Stephen P. Mbundi akifafanua jambo kwa wadau kutoka NDC wakati walipofanya ziara ya mafunzo Wizarani |
TANZANIA MBIONI KUSAINI MKATABA WA ENEO HURU LA BIASHARA YA UTATU COMESA-EAC-SADC
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhe. Dkt. Leonard Chamuriho akichangia jambo katika Mkutano wa Pili wa Dharura wa Baraza la Mawaziri la Utatu uliofanyika kwa njia ya video |
Badhi ya Watumishi wa Serikali waliohudhuria Mkutano wa Pili wa Dharura wa Baraza la Mawaziri la Utatu uliokuwa ukiendelea kwa njia ya video wakifualia mjadala uliokuwa ukiendelea |
Mkutano ukiendelea |
Saturday, February 13, 2021
BALOZI IBUGE: SIJARIDHISHWA NA MAENDELEO YA UJENZI WA MAJENGO CHUO CHA DIPLOMASI
Na Mwandishi wetu,
Katibu
Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Brigedia
Jenerali Wilbert Ibuge ameonesha kutoridhishwa na maendeleo ya ujenzi wa
majengo ya mihadhara katika chuo cha Diplomasia na kumuagiza Mkandarasi anayetekeleza
mradi huo kuzingatia thamani ya fedha, muda wa mkataba na ubora.
Balozi
Ibuge ametoa maagizo kwa Mkandarasi huyo ambaye ni Kampuni ya Casco
Construction pamoja na mshauri muelekezi Ask architects wakati alipotembelea
mradi huo katika chuo cha Diplomasia leo jijini Dar es Salaam kusema kuwa endapo
Mkandarasi hata fanya hivyo atakuwa amekiuka masharti ya mkataba na mkataba
wake utasitishwa mara moja.
“Huu
mradi ni mradi wenye maslahi ya Taifa majadiliano yaishe leo mkataba ulishaisha
tangu mwezi Disemba 2020, hizi ni hela za walipa kodi…..nataka nione thamani
halisi ya fedha [Value for Money] ya walipa kodi katika mradi huu, siatakubali
kupoteza fedha za walipa kodi,” Amesema Balozi Ibuge
Katibu
Mkuu ameuagizo pia uongozi wa chuo hicho kuhakikisha kuwa unasimamia ujenzi wa
majengo hayo kwa karibu zaidi na umakini ili kuiwezesha serikali kupata thamani
halisi ya fedha katika mradi huo wenye maslahi mapana ya Taifa.
Awalia
akiongea na wahadhiri pamoja na wafanyakazi katika chuo hicho Balozi Ibuge
amewataka wote kwa pamoja kuhakikisha kuwa wanatekeleza diplomasia ya uchumi
kutokana na mabadiliko ya dunia.
“Najua
mmeanzisha mitaala inayogusia masuala ya diplomasia ya uchumi hadi mmeanza kuanzia
baadhi ya matawi katika baadhi ya mikoa hili ni jambo jema, lakini uwezo wa
nyinyi kuleta [link] ya utekelezaji wa diplomasia ya uchumi ambao ndiyo Wizara
yetu inasimamia…unapohusisha na nchi nyingine ni lazima utafiti wenu pamoja na
kuboresha wigo wa utekelezaji wa diplomasia ya uchumi,”
Balozi
Ibuge ameongeza kuwa diplomasia ya uchumia inaambatana na siasa pamoja na
diplomasia ya utamaduni wetu hasa kwenye lugha ya kiswahili hiyo ndiyo sehemu
ya mahusiano yetu na wengine.
“Urathi
wa ukombozi kusini mwa Afrika anayehusika ni Tanzania sasa Chuo cha Diplomasia
ambapo ndipo mawazo mazuri ya namna bora ya sisi kuhakikisha tunaiendeleza na
kuishindania na kuhakikisha hakuna mwingine wa kushindana na sisi, njia pekee
ni kupitia kwenu nyinyi na tafiti zenu,” Amesema Balozi Ibuge
Kwa
upande wake Mkandarasi anayetekeleza mradi huo Mhandisi Cosmas Salufu kutoka
kamupuni ya ujenzi ya Casco, pamoja na mshauri elekezi mhandisi Ally Simbano
kutoka kampuni Ask Architects kwa pamoja wameahidi kutekeleza maagizo ya Katibu
Mkuu na kuhakikisha kuwa thanami halisi ya fedha inapatikana katika mradi huo.
Katibu
Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Brigedia
Jenerali Wilbert Ibuge (aliyesimama) akiongea na wahadhiri pamoja na
wafanyakazi wa chuo cha Diplomasia leo Jijini Dar es Salaam wakati alipofanya
ziara chuoni hapo
Katibu
Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Brigedia
Jenerali Wilbert Ibuge akiongea na uongozi wa chuo cha Diplomasia leo Jijini
Dar es Salaam
Afisa
Miliki wa Chuo cha Diplomasia, Mhandisi Athumani Mashaka akimueleza jambo Katibu
Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Brigedia
Jenerali Wilbert Ibuge wakati akitembelea mradi wa ujenzi wa majengo chuoni
hapo
Mhandisi
Cosmas Salufu pamoja na Mshauri Elekezi Mhandisi Ally wakimsikiliza Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya
Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge
wakati wa ziara ya ukaguzi wa majengo
Friday, February 12, 2021
MKUTANO WA SADC TROIKA WASOGEZA MBELE MKUTANO WA WAKUU WA NCHI
Na Mwandishi wetu,
Mkutano
wa Wakuu wa nchi na Serikali za Utatu wa Jumuiya ya Maendeleo ya nchi za Kusini
mwa Afrika (SADC- TROIKA) uliopangwa kufanyika
mwezi Machi 2021 umesogezwa mbele hadi mwezi Mei au Juni 2021 kutokana na
changamoto za (Covid 19).
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. William Ole Nasha (Mb) amesema kuwa
mkutano huo umekutana kwa lengo la kupitia na kuridhia mapendekezo ya Mawaziri
wa afya wa SADC uliofanyika mwishoni wa mwezi Februari 2021.
“Awali mawaziri wa Afya wa SADC walipendekeza
kuwa mkutano wa Baraza la Mawaziri ufanyike kwa njia ya mtandao pamoja na ule
wa Wakuu wa Nchi uliokuwa umepangwa pia kufanyika mwezi Machi usogezwe mbele hadi
mwezi Mei au Juni 2021 kutegemeana na hali ya maambukizi ya ugonjwa wa COVID 19
itakavyokuwa na kuongeza kuwa mikutano mingine yote itafanyika kwa njia ya mtandao
(Video Conference) hadi hapo hali ya maambukizi itakapokuwa imetengemaa,”
Amesema Mhe. Ole Nasha
Mkutano
wa (SADC TROIKA) umetanguliwa na Mkutano wa Makatibu Wakuu ambapo, Katibu Mkuu
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brigedia
Jenerali Wilbert Ibuge ameeleza kutokana na hali halisi ya kujitokeza kwa
kirusi cha Covid 19 kilichojitokeza kusini mwa Jangwa la Afrika imekuwa vigumu
kufanyika kwa mkutano huo wa ana kwa ana na badala yake imeamuliwa mkutano huo
usogezwe mbele hadi mwezi Mei au Juni 2021.
“Mwezi
Januari 2021 Mawaziri wa Afya wa SADC walikutana na kufanya mkutano kwa njia ya
mtandao na kufikia maazimio kuwa mkutano wa Wakuu wa nchi na Serikali
uhairishwe hadi mwezi Mei au Juni kutegemeana na hali ya COVID 19 itakapokuwa
imetengemaa……. ambapo pamoja na mambo mengine, mkutano wa Baraza la Mawaziri
umeridhia kusogezwa mbele kwa mkutano huo,” Amesema Balozi Ibuge
Utatu wa SADC TROIKA kwa sasa
unaundwa na nchi za Msumbiji, Tanzania na Malawi.
Naibu Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. William Ole Nasha (Mb)
akiwa amesimama wakati wimbo wa Taifa wa Msumbiji ulipokuwa ukipigwa wakati wa
ufunguzi wa Mkutano wa Utatu wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC
TROIKA) uliofanyika kwa njia ya mtandao
Naibu
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. William Ole
Nasha (Mb) akiandika jambo wakati wa mkutano cha SADC TROIKA) uliofanyika kwa
njia ya mtandao
Katibu
Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Brigedia
Jenerali Wilbert Ibuge akichangia mada katika mkutano wa Makatibu Wakuu wa SADC
TROIKA
Katibu
Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Brigedia
Jenerali Wilbert Ibuge akifuatilia mkutano wa Makatibu Wakuu wa SADC TROIKA