Na
Mwandishi Wetu, Arusha
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imepongezwa
kwa kufanikisha maonsho ya kwanza ya kitaifa ya kikanda ya Jumuiya ya Afrika
Mashariki yaliyofanyika Jijini Arusha kuanzia tarehe 9 – 11 yaliyolenga
kutangaza vivutio na fursa mbalimbali za utalii ndani ya Jumuiya hiyo.
Pongezi hizo zimetolewa na Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi pamoja na baadhi ya Mawaziri wa Utalii wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wakati wa kufunga maonesho ya kwanza ya utalii kwa nchi
wanachama wa Jumuiya ya Afrika mashariki leo jijini Arusha.
“Nawapongeza kwa kufanikisha maonesho haya ni imani
yangu kuwa kupitia maonesho haya nchi zetu za ukanda wa Jumuiya ya Afrika
Mashariki zimepata fursa ya kutangaza vivutio mbalimbali vya utalii pamoja na
kujadili njia mbalimbali za kukabiliana changamoto zinazoikabili sekta ya
Utalii katika ukanda wa Afrika Mashariki,” Amesema Dkt. Mwinyi
“Natoa wito kupitia maonesho haya ambayo yatakuwa
yanafanyika kila mwaka kwa mzunguko kwa kila nchi mwanachama……..jitihada zaidi
zinahitajika katika kutangaza vivutio vya utalii katika ukanda wetu wa Afrika
Mashariki ikiwa ni pamoja na kuboresha sera zetu za utalii,” ameongeza Dkt.
Mwinyi
Dkt. Mwinyi pia ameitaka Kamati Maalumu ya Kikanda
ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kufanya ziara Zanzibar na kujionea fursa
mbalimbali zinazopatikana katika sekta ya utalii pamoja na zile za biashara na
uwekezaji.
Awali Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dkt. Damas
Ndumbaro amesema kupitia maonesho haya ya kwanza katika ukanda wa Afrika
Mashariki yamekuwa na mafanikio makubwa ambapo zaidi ya waoneshaji 100 kutoka
mataifa mbalimbali duniani wameshiriki, kati yao 41 wakitoka mataifa mbalimbali
na nchi 25 zikishiriki ikiwa ni pamoja na sita za Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Nae Waziri wa Uhifadhi wa Wanyamapori na Utalii
kutoka Sudan ya Kusini Mhe. Luteni Jenerali Rizik Zakaria Hassan ameipongeza
Tanzania kwa kufanikisha maonesho ambayo yemeweza kuvitangaza vivutio
mbalimbali vya utalii ndani ya ukanda wa Afrika Mashariki ambayo pia yametoa
fursa ya kujadili changamoto zinazoikabili sekta ya utalii.
“Maonesho haya yemekuwa na manufaa makubwa sana kwa kutuweka
sekta ya utalii ndani ya jumuiya ya Afrika Mashariki ……….binafsi nawapongeza sana
Tanzania kwa kulifanikisha jambo hili muhimu kwetu, naamini kupitia maonesho
haya tutazidi kuimarika ziadi kama jumuiya kwa maendeleo yetu sote,” Amesema
Luteni Jenerali Hassan.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Forodha na Biashara
Jumuiya ya Afrika Mashariki, Bwn. Keneth Bagamuhunda ambaye alimwakilisha Katibu
Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Mhe. Peter Mathuki, amesema maonesho
yalilenga kutoa fursa kwa kila nchi mwanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki
kutangaza vivutio mbalimbali vya utalii ili kuifahamisha Afrika na Dunia kuwa
ndani ya Afrika Mashariki kuna vivutio vya utalii.
“Tutaendelea na maonesho haya kwa kila mwaka lengo
likiwa ni kutangaza utalii na kuhakikisha soko la utalii ndani ya Jumuiya ya
Afrika Mashariki linakuwa kila mwaka,” Amesema Bwn. Bagamuhanda.
Kwa upande wake, Waziri wa Utalii na Malikale wa
Zanzibar, Mhe. Leila Mohamed Mussa (Mb) amesema Afrika kwa sasa inatakiwa fursa
za utalii na biashara ili kuweza kuziongezea Serikali zetu mapato.
“Afrika Mashariki inayo mambo mengi ya kutoa katika
bara la Afrika na Duniani kwa ujumla hasa katika sekta ya utalii kwa kuwa
tumejaliwa vivutio mbalimbali vya utalii,” amesema Bibi Leila Mohamed Mussa.
Oktoba 09, 2021 maonesho ya kwanza ya utalii kwa
nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika mashariki yalizinduliwa rasmi na Katibu
Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Dkt. Peter Mathuki jijini Arusha.
Kufanyika kwa maonesho hayo kunatokana na
kuzinduliwa hivi karibuni mpango wa pamoja kutangaza utalii katika nchi
wanachama wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki uliozinduliwa rasmi na Mawaziri wa
Maliasili na Utalii wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Maonesho hayo yalihudhuriwa na nchi wanachama wa
Jumuiya ya Afrika Mashariki ambazo ni Tanzania (Mwenyeji), Kenya, Uganda,
Rwanda, Burundi na Sudan Kusini.
|
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi akihutubia washiriki wa maonesho ya
kwanza ya utalii kwa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika mashariki, leo Jijini
Arusha |
|
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi akipata maelezo wakati alipotembelea
banda la Rwanda katika maonesho ya kwanza ya Kikanda ya Utalii kwa nchi
wanachama wa Jumuiya ya Afrika mashariki leo Jijini Arusha |
|
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi akikaribishwa na Balozi wa Kenya nchini
Tanzania katika banda la Kenya wakati alipokuwa akitembelea mabanda mbalimbali katika
maonesho ya kwanza ya utalii kwa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika mashariki,
leo Jijini Arusha |
|
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi akiwa katika picha ya pamoja na Mkewe Mhe.
Mama Mariam Mwinyi na viongozi mbalimbali katika banda la Zanzibar leo Jijini
Arusha |
|
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi pamoja na Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Damas Ndumbaro wakifungua na kuweka jiwe la msingi la kwanza la maonesho
ya kwanza ya utalii kwa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika mashariki, leo
Jijini Arusha |
|
Kikundi cha ngoma kutoka Makumira Arusha kikitumbuiza
wakati wa maonesho ya kwanza ya utalii kwa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika
mashariki leo Jijini Arusha |
|
Kikundi cha ngoma kutoka Sudan Kusini kikitumbuiza
wakati wa maonesho ya kwanza ya utalii kwa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika
mashariki leo Jijini Arusha |
|
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi
mbalimbali mara baada ya kufunga maonesho ya kwanza ya utalii kwa nchi
wanachama wa Jumuiya ya Afrika mashariki leo Jijini Arusha |