Wednesday, October 13, 2021
Balozi Bana awapokea Wanajeshi watakao shiriki Michezo ya Amani na Mshikamano ya Kijeshi, nchini Nigeria.
Tuesday, October 12, 2021
EALA WAKUTANA MKUTANO WA KWANZA JIJINI ARUSHA
Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki (Eala) limeanza leo mkutano wake wa kwanza, kikao cha tano, bunge la nne ambapo pamoja na mambo mengine, Bunge hilo limejadili masuala mbalimbali ya kamati ya sheria na maendeleo yake ndani ya Jumuiya hiyo.
Spika wa Bunge la Afrika Mashariki (Eala) Mhe. Martin
Ngoga akifungua Mkutano wa Kwanza, Kikao cha tano, Bunge la nne ulioanza leo Jijini
Arusha
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Afrika Mashariki kutoka Tanzania, Mhe. Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk (Mb) pamoja
na wabunge wengine wa Bunge hilo wakifuatilia Mkutano kwanza wa (Eala), leo
Jijini Arusha
Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki (Eala), Mhe.
Wanjiku Muhya kutoka Kenya akichangia hoja kuhusu Kamati ya Sheria katika Mkutano
Kwanza leo Jijini Arusha
Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki (Eala), Mhe. Gasinzigwa
Oda kutoka Rwanda akichangia hoja kuhusu Kamati ya Sheria katika Mkutano Kwanza
leo Jijini Arusha
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Afrika Mashariki kutoka Tanzania, Mhe. Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk (Mb) akinukuu
jambo wakati wa Mkutano Kwanza wa (Eala), ukiendelea leo Jijini Arusha
Mbunge wa Eala kutoka Sudan Kusini Mhe. Mukulia
Kennedy Ayason akichangia hoja kuhusu
Kamati ya Sheria katika Mkutano Kwanza leo Jijini Arusha
Waziri wa Afrika Mashariki na Maendeleo ya Kanda wa
Kenya, Adan Mohamed (kulia) akijadili jambo na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki kutoka Tanzania, Mhe. Balozi Mbarouk Nassor
Mbarouk (Mb) nje ya Ukumbi wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki (Eala), mara
baada ya kuahirishwa kwa Mkutano wa Kwanza, Kikao cha tano, Bunge la nne, ulioanza
leo Jijini Arusha
Monday, October 11, 2021
TANZANIA YAPONGEZWA KUFANIKISHA MAONESHO YA UTALII UKANDA WA AFRIKA MASHARIKI
Na Mwandishi Wetu, Arusha
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imepongezwa kwa kufanikisha maonsho ya kwanza ya kitaifa ya kikanda ya Jumuiya ya Afrika Mashariki yaliyofanyika Jijini Arusha kuanzia tarehe 9 – 11 yaliyolenga kutangaza vivutio na fursa mbalimbali za utalii ndani ya Jumuiya hiyo.
Pongezi hizo zimetolewa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi pamoja na baadhi ya Mawaziri wa Utalii wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wakati wa kufunga maonesho ya kwanza ya utalii kwa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika mashariki leo jijini Arusha.
“Nawapongeza kwa kufanikisha maonesho haya ni imani yangu kuwa kupitia maonesho haya nchi zetu za ukanda wa Jumuiya ya Afrika Mashariki zimepata fursa ya kutangaza vivutio mbalimbali vya utalii pamoja na kujadili njia mbalimbali za kukabiliana changamoto zinazoikabili sekta ya Utalii katika ukanda wa Afrika Mashariki,” Amesema Dkt. Mwinyi
“Natoa wito kupitia maonesho haya ambayo yatakuwa yanafanyika kila mwaka kwa mzunguko kwa kila nchi mwanachama……..jitihada zaidi zinahitajika katika kutangaza vivutio vya utalii katika ukanda wetu wa Afrika Mashariki ikiwa ni pamoja na kuboresha sera zetu za utalii,” ameongeza Dkt. Mwinyi
Dkt. Mwinyi pia ameitaka Kamati Maalumu ya Kikanda ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kufanya ziara Zanzibar na kujionea fursa mbalimbali zinazopatikana katika sekta ya utalii pamoja na zile za biashara na uwekezaji.
Awali Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amesema kupitia maonesho haya ya kwanza katika ukanda wa Afrika Mashariki yamekuwa na mafanikio makubwa ambapo zaidi ya waoneshaji 100 kutoka mataifa mbalimbali duniani wameshiriki, kati yao 41 wakitoka mataifa mbalimbali na nchi 25 zikishiriki ikiwa ni pamoja na sita za Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Nae Waziri wa Uhifadhi wa Wanyamapori na Utalii kutoka Sudan ya Kusini Mhe. Luteni Jenerali Rizik Zakaria Hassan ameipongeza Tanzania kwa kufanikisha maonesho ambayo yemeweza kuvitangaza vivutio mbalimbali vya utalii ndani ya ukanda wa Afrika Mashariki ambayo pia yametoa fursa ya kujadili changamoto zinazoikabili sekta ya utalii.
“Maonesho haya yemekuwa na manufaa makubwa sana kwa kutuweka sekta ya utalii ndani ya jumuiya ya Afrika Mashariki ……….binafsi nawapongeza sana Tanzania kwa kulifanikisha jambo hili muhimu kwetu, naamini kupitia maonesho haya tutazidi kuimarika ziadi kama jumuiya kwa maendeleo yetu sote,” Amesema Luteni Jenerali Hassan.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Forodha na Biashara Jumuiya ya Afrika Mashariki, Bwn. Keneth Bagamuhunda ambaye alimwakilisha Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Mhe. Peter Mathuki, amesema maonesho yalilenga kutoa fursa kwa kila nchi mwanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kutangaza vivutio mbalimbali vya utalii ili kuifahamisha Afrika na Dunia kuwa ndani ya Afrika Mashariki kuna vivutio vya utalii.
“Tutaendelea na maonesho haya kwa kila mwaka lengo likiwa ni kutangaza utalii na kuhakikisha soko la utalii ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki linakuwa kila mwaka,” Amesema Bwn. Bagamuhanda.
Kwa upande wake, Waziri wa Utalii na Malikale wa Zanzibar, Mhe. Leila Mohamed Mussa (Mb) amesema Afrika kwa sasa inatakiwa fursa za utalii na biashara ili kuweza kuziongezea Serikali zetu mapato.
“Afrika Mashariki inayo mambo mengi ya kutoa katika bara la Afrika na Duniani kwa ujumla hasa katika sekta ya utalii kwa kuwa tumejaliwa vivutio mbalimbali vya utalii,” amesema Bibi Leila Mohamed Mussa.
Oktoba 09, 2021 maonesho ya kwanza ya utalii kwa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika mashariki yalizinduliwa rasmi na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Dkt. Peter Mathuki jijini Arusha.
Kufanyika kwa maonesho hayo kunatokana na kuzinduliwa hivi karibuni mpango wa pamoja kutangaza utalii katika nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki uliozinduliwa rasmi na Mawaziri wa Maliasili na Utalii wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Maonesho hayo yalihudhuriwa na nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ambazo ni Tanzania (Mwenyeji), Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi na Sudan Kusini.
Kikundi cha ngoma kutoka Makumira Arusha kikitumbuiza
wakati wa maonesho ya kwanza ya utalii kwa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika
mashariki leo Jijini Arusha |
Kikundi cha ngoma kutoka Sudan Kusini kikitumbuiza
wakati wa maonesho ya kwanza ya utalii kwa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika
mashariki leo Jijini Arusha |
Sekta zaidi nchini kunufaika na mikopo nafuu ya Benki ya Uwekezaji ya Umoja wa Ulaya
Friday, October 8, 2021
WAZIRI WA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI BALOZI LIBERATA MULAMULA KATIKA MKUTANO WA KIMATAIFA WA AMANI - ROMA,ITALIA
Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis (aliyevaa kanzu nyeupe) akiwa pamoja na viongozi wa dini na madhehebu mbalimbali duniani wakati wa kufunga Mkutano wa Kimataifa kuhusu Amani. Mkutano huo umefanyika Roma,Italia. |
Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb) akiwa ameshika ujumbe wa Amani aliokabidhiwa katika hafla ya kufunga Mkutano wa Kimataifa wa Amani ambar umehudhuriwa na Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis. Mkutano huo umefanyika Roma,Italia |
TANZANIA, CZECH ZAAHIDI KUIMARISHA BIASHARA NA UWEKEZAJI
Na Mwandishi wetu, Dar
Katika jitihada za kukuza na kuendeleza diplomasia
ya uchumi, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Jamhuri ya Czech zimeahidi
kukuza na kuimarisha sekta ya biashara na uwekezaji.
Ahadi hiyo imetolewa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Czech Mhe. Miloslav Staŝek wakati alipokutana kwa mazungumzo na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk leo katika Ofisi Ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam.
Mhe. Staŝek amesema kuwa wamejadili masuala mbalimbali ya kukuza na kuimarisha ushirikiano baina ya Tanzania na Czech hasa katika sekta ya biashara na uwekezaji wa viwanda hapa nchini………..”na leo nimeambatana na wafanyabiashara mbalimbali kutoka Czech ambao wamekuja kuangalia fursa za biashara zinazopatikana hapa Tanzania” amesema Mhe. Staŝek.
“Pia tunajitahidi kuleta teknolojia mpya hapa Tanzania kuinua uchumi, ambapo tunaamini itasaidia kutangaza fursa mbalimbali katika sekta ya biashara na uwekezaji,” Ameongeza Mhe. Staŝek
Kwa Upande wake, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk amesema katika mazungumzo yake na Waziri wa Jamhuri wa Czech Mhe. Staŝek yamejikita zaidi katika kukuza uhusiano wa uchumi hasa masuala ya biashara na uwekezaji.
Leo Mhe. Waziri ameambata na ujumbe wa wafanyabiashara waliokuja kujione fursa mbalimbali hapa nchini ili kuinua sekta ya biashara na uwekezaji…………..”leo pia watakuwa na mkutano ambao utawakutanisha na wafanyabiashara wa Tanzania ili kuona fursa za ushirikiano baina ya Tanzania na Czech,” Amesema Balozi Mbarouk.
“Tumeongelea suala la kuongeza uhusiano katika sekta ya elimu kwa kutoa fursa za masomo kwa wanafunzi wa Tanzania kwenda kusoma Czech ambapo wamekubali na kuahidi kuongeza nafasi za masomo kwa wanafunzi wa Tanzania ili kutoa fursa ya watanzania wengi kunufaika na elimu,” Ameongeza Balozi Mbarouk.
Pia viongozi hao wamejadili suala la kukuza sekta ya utalii hapa nchini ambapo Czech ipo katika mchakato wa kuanzisha safari ya ndege ya kuja Tanzania moja kwa moja ili kukuza na kutangaza Utalii lakini pia kukuza biashara kwa maslahi mapana ya pande zote mbili.
Kadhalika, Balozi Mbarouk amemuahidi Mhe. Staŝek
kuwa Serikali ya Tanzania itaendelea kuhakikisha inalinda na kuimarisha
uhusiano wa kidiplomasia uliopo baina yake na Jamhuri ya Czech kwa kuwa
uhusiano wa mataifa hayo mawili ni wa muda mrefu na wenye maslahi ya mataifa
yote mawili.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Czech Mhe.
Miloslav Staŝek akiongea na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk (Mb) wakati walipokutana leo
kwa mazungumzo katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk (Mb) akimueleza jambo Waziri wa
Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Czech Mhe. Miloslav Staŝek wakati walipokutana leo
kwa mazungumzo katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam
Majadiliano baina ya Waziri wa Mambo ya Nje wa
Jamhuri ya Czech Mhe. Miloslav Staŝek akiongea na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje
na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk (Mb) yakiendelea
wakati wa mazungumzo leo katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam Majadiliano baina ya Waziri wa Mambo ya Nje wa
Jamhuri ya Czech Mhe. Miloslav Staŝek akiongea na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje
na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk (Mb) yakiendelea
wakati wa mazungumzo leo katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam
Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Czech Mhe.
Miloslav Staŝek akiongea akipokea zawadi ya picha ya Mlima Kilimanjaro kutoka
kwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi
Mbarouk Nassor Mbarouk (Mb) leo Jijini Dar es Salaam
Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Czech Mhe.
Miloslav Staŝek katika picha ya pamoja na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk (Mb) leo Jijini
Dar es Salaam
Thursday, October 7, 2021
JAMHURI YA CZECH YAKABIDHI VITANDA VIWILI VYA KISASA VYA WAGONJWA OCEAN ROAD
Na Mwandishi wetu, Dar
Jamhuri ya Czech kwa kushirikiana na kampuni ya Linet Group pamoja na Gama Pharmaceuticals (T) Limited imefanikiwa kuchangia vitanda viwili vya kisasa katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Road vyenye thamani ya shilingi milioni 16 za kitanzania.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Czech Mhe. Miloslav Staŝek amekabidhi vitanda hivyo kwa taasisi hiyo na kupokelewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Saratani Ocean Road Dr. Julius Mwaiselage pamoja na viongozi wengine wa taasisi mbalimbali za Serikali.
Mhe. Staŝek amesema Serikali ya Czech itaendelea kushirikiana na Tanzania kwa karibu katika kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia uliopo baina ya mataifa hayo mawili.
Kwa upande wake Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani, Mhe. Dkt. Abdallah Possi ameishukuru Czech kwa ushirikiano ambao imekuwa ikiutoa kwa Tanzania na kuahidi kuwa Serikali ya Tanzania itaendelea kudumisha ushirikiano wake na Czech kwa maslahi ya pande zote mbili.
Awali akitoa salamu za shukrani, Mkurugenzi Mtendaji
wa Taasisi ya Saratani Ocean Road Dr. Julius Mwaiselage ameishukuru Jamhuri ya
Czech kwa msaada huo na kuongeza kuwa pamoja na msaada huo, bado taasisi hiyo
ina kabiliwa na changamoto ya uhitaji wa vitanda vya kisasa 25 ambapo hadi sasa
wanavyo vitanda nane (8) tu hivyo kuwa na uhitaji wa vitanda vingine 17.
Meza kuu wakifuatilia hafla fupi ya makabidhiano ya
vitanda viwili vya kisasa vilivyotolewa na Jamhuri ya Czech kwa kushirikiana na
kampuni ya Linet Group pamoja na Gama Pharmaceuticals (T) Limited
Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani, Mhe. Dkt.
Abdallah Possi akitoa shukrani kwa Jamhuri ya Czech kwa kushirikiana na kampuni
ya Linet Group pamoja na Gama Pharmaceuticals (T) Limited kwa msaada wa vitanda
vya kisasa katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Road
Balozi wa Jamhuri ya Czech Mhe. Martin Klepetko, mwenye
makazi nchini Kenya akiongea na watumishi pamoja na waandishi wa habari waliohudhuria
hafla fupi ya makabidhiano ya vitanda viwili vya kisasa vya Ocean Road Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Czech Mhe.
Miloslav Staŝek akitoa salamu za Serikali yake wakati wa hafla fupi ya
makabidhiano ya vitanda viwili vya kisasa vya Ocean Road Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Czech Mhe.
Miloslav Staŝek pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Saratani Ocean Road
Dr. Julius Mwaiselage wakikata utepe wakati wa makabidhiano ya vitanda viwili
vya kisasa vitakavyotumika kuhudumia wagonjwa Ocean Road
Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Czech Mhe.
Miloslav Staŝek pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Saratani Ocean Road
Dr. Julius Mwaiselage wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watumishi na
wawakilishi wa Taasisi mbalimbali mara baada ya kukabidhi vitanda viwili vya
kisasa Ocean Road
WAFANYABIASHARA, WAWEKEZAJI KUTOKA CZECH WAONYESHA UTAYARI KUWEKEZA TANZANIA
Na Mwandishi wetu, Dar
Wafanyabiashara
na Wawekezaji kutoka Jamhuri ya Czech wameonesha nia ya kuwekeza katika sekta
ya kilimo hasa Pamba pamoja na viwanda vya nguo hapa nchini.
Akibainisha
kuhusu utayari wa Wafanyabiashara na Wawekezaji wa Czech, kuwekeza hapa nchini,
Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Czech Mhe. Miloslav Staŝek amesema
wamefurahishwa sana na mazingira ya biashara hapa Tanzania na wapo tayari
kuwekeza katika sekta kilimo na viwanda.
Mhe.
Staŝek ameyasema hayo wakati alipokutana kwa mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji
wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Dkt. Maduhu Kazi leo jijini Dar es
Salaam.
Katika
ziara yake ya kikazi hapa nchini, Mhe. Staŝek ameambatana na viongozi
mbalimbali wa Jamhuri ya Czech akiwemo Naibu Waziri wa Fedha wa Jamhuri ya
Czech, mhe. Karel Tyll pamoja na Wafanyabiashara na Wawekezaji kutoka nchini
humo.
Waziri
wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Czech Meh. Miloslav Staŝek amesema yeye pamoja na
wajumbe alioongozana nao wamejadiliana na uongozi wa TIC na kupata fursa ya
kutambua masuala mbalimbali ya kuongeza ushirikiano ili kuimarisha sekta ya
uwekezaji kati ya Czech na Tanzania kwa maslahi ya pande zote mbili.
“Mimi
na Timu yangu tumejadili mambo mbalimbali ya kuwekeza hapa Tanzania ikiwa ni
pamoja na utengezaji wa ndege, kilimo, teknolojia pamoja na viwanda.
“Moja
ya kampuni niliyoambatana nayo inauzoefu mkubwa katika uzalisha dawa na vifaa
tiba, hivyo kampuni hii itakapo pata fursa ya kuwekeza hapa Tanzania itasaidia
kuimarisha mahusiano yetu pamoja na kuboresha sekta ya afya,” Amesema mhe. Staŝek.
Mhe.
Staŝek ameongeza kuwa wamekubaliana na uongozi wa TIC pamoja na Waziri wa
Viwanda na Biashara kutafuta namna bora ya kuwaunganisha wafanyabiashara wa
Tanzania na wale wa Czech ili kutoa fursa kwa kampuni mbalimbali za Czech kuja
kuwekeza kwa wingi hapa Tanzania na wafanyabiashara wa Tanzania kuwekeza nchini
Czech kwa maslahi ya pande zote mbili.
Kwa
upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Dkt.
Maduhu Kazi amesema kuwa mara baada ya mazungumzo ya awali, wawekezaji hao
wameonsha nia kubwa sana ya kuwekeza katika Pamba na viwanda vya nguo hapa
nchini.
“Wameonesha
uwezo mkubwa katika biashara na uwekezaji kwenye maeneo ya ufundi wa ndege ambapo
baadae kutakuwa na mafunzo mbalimbali ya kubadilishana ujuzi na fursa za uwekezaji……...lakini
pia wamevutiwa na sekta ya kilimo hasa katika viwanda vya kutengeneza mafuta ya
kula,” Amesema Dkt. Kazi
Nae
Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani, Mhe. Dkt. Abdallah Possi amesema kuwa
lengo la Serikali ni kuhakikisha kuwa tunatangaza fursa za biashara na
uwekezaji.
“Fursa
za kupata wafanyabiashara kutoka Zchec zinazidi kuongezeka hapa nchini, hivyo
nitoe rai kwa sekta binafsi kuchangamkia fursa za biashara na uwekezaji,”
Amesema Dkt. Posi
Pamoja
na mambo mengine, viongozi hao wamejadili masuala mbalimbali yaliyolenga kukuza
na kuimarisha sekta ya uwekezaji baina ya Tanzania na Czech hapa nchini.
Waziri
wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Czech Mhe. Miloslav Staŝek akiongea na uongozi wa
Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), ulioongozwa na Mkurugenzi Mtendaji Dkt.
Maduhu Kazi leo jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi
Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Dkt. Maduhu Kazi akimueleza
jambo Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Czech Mhe. Miloslav Staŝek wakati
Waziri Staŝek alipotembelea taasisi hiyo leo jijini Dar es Salaam
Balozi
wa Tanzania nchini Ujerumani, Mhe. Dkt. Abdallah Possi (wa kwanza kulia) akieleza jambo wakati wa
mkutano baina ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Czech Mhe. Miloslav
Staŝek na uongozi wa TIC
Waziri
wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Czech Mhe. Miloslav Staŝek akimueleza jambo
Waziri wa Viwanda na Biashara, Prof. Kitila Mkumbo walipokutana kwa mazungumzo leo
jijini Dar es Salaam
Mkutano
ukiendelea