Na Mwandishi Wetu, Dar
Tanzania
na Ufaransa zimekubaliana kuendelea kushirikiana katika maeneo ya kimkakati
ikiwemo Nishati, Elimu, Kilimo na Miundombinu ambapo Ufaransa imekubali
kukarabati Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere ‘Terminal Two’ Jijini
Dar es Salaam
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula
(Mb) ameyasema hayo wakati akizungumza na Waziri wa Biashara za Kimataifa na
Uwekezaji wa Ufaransa, Mhe. Franck Riester leo alipowasili Jijini Dar es Salaam
kwa ziara ya kikazi ya siku moja.
Kumekuwa
na Miradi ambayo Serikali ya Ufaransa kupitia Shirika lao la Maendeleo wamekuwa
wakifadhili Miradi mbalimbali katika Sekta mbalimbali hapa nchini zikiwemo
sekta za Nishati, Elimu, Kilimo na Miundombinu.
Mtakumbuka
kuwa Ufaransa ndiyo waliojenga Uwanja wa Ndege wa “Termirnal Two” wa Julius Kambarage
Nyerere sasa wanakuja na mradi wa kukarabati uwanja huo na kuufanya kuwa wa
kisasa zaidi. Sasa hivi tu terminal three lakini terminal two imekuwa ikitumika
na ndege zinazofanya safari zake za ndani hapa nchini……..mradi huu ni moja kati
ya mradi mkubwa na utakamilika hivi karibuni.
Waziri
wa Biashara za Kimataifa na Uwekezaji wa Ufaransa, Mhe. Franck Riester yupo
nchini Tanzania kuzindua safari za Shirika la ndege la Ufaransa ‘Fance Airline’ kutoka Paris
hadi Zanzibar ambapo mara ya mwisho kwa shirika hilo kufanya safari zake hapa
nchini ilikuwa mwaka 1974.
Septemba
15, 2021 Balozi wa Ufaransa hapa nchini Mhe. Nabil Hajlaouvi alisema Serikali
ya Ufaransa kupitia Shirika lake la ndege ‘Fance Airline’ inategemea kuanzisha
safari mpya ya ndege kutoka Ufaransa moja kwa moja hadi Zanzibar kuanzia 19
Oktoba 2021.
Katika
tukio jingine, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Balozi Liberata Mulamula (Mb) ametoa salamu za rambirambi kufuatia kifo cha aliyewahi
kuwa waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Colin Powell.
“Kwa
kweli Serikali ya Tanzania tumeshtushwa sana na kifo chake………katika kipindi
chake aliendeleza uhusiano wa Marekani na Mataifa mbalimbali, kwa kweli ni
masikitiko makubwa tutamkumbuka daima,” Amesema Balozi Mulamula
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata
Mulamula (Mb) akisalimiana na Waziri wa Biashara za Kimataifa na Uwekezaji wa
Ufaransa, Mhe. Franck Riester leo alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa
Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam kwa ziara ya kikazi ya siku
moja
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata
Mulamula (Mb) (wa saba kutoka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa
Biashara za Kimataifa na Uwekezaji wa Ufaransa, Mhe. Franck Riester (kushoto
kwa Balozi Mulamula) na Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa (wa
tano kutoka kulia) pamoja na viongozi mbalimbali waandamizi wa Serikali katika
Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam kwa ziara
ya kikazi ya siku moja
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata
Mulamula (Mb) akiongea na Waziri wa Biashara za Kimataifa na Uwekezaji wa
Ufaransa, Mhe. Franck Riester katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius
Nyerere Jijini Dar es Salaam
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata
Mulamula (Mb) akiongea na Waziri wa Biashara za Kimataifa na Uwekezaji wa
Ufaransa, Mhe. Franck Riester katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius
Nyerere Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhe.
Prof. Makame Mbarawa (Mb).
Maongeza
baina ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi
Liberata Mulamula (Mb) na Waziri wa Biashara za Kimataifa na Uwekezaji wa
Ufaransa, Mhe. Franck Riester yakiendelea. Maongezi hayo pia yamehudhuriwa na
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano
wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Sokoine, Balozi wa Tanzania Nchini Ufaransa Mhe.
Samwel Shelukindo, Balozi wa Ufaransa Nchini Tanzania Mhe. Nabil Hajlaouvi pamoja
na viongozi mbalimbali.
Katibu
Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph
Sokoine, (kulia) akiwa na Balozi wa Tanzania Nchini Ufaransa Mhe. Samwel Shelukindo,
pamoja na Mkurugezi wa Idara ya Amerika na Ulaya Balozi Swahiba Mndeme wakifuatilia kikao cha Waziri Mulamula na Waziri
wa Biashara za Kimataifa na Uwekezaji wa Ufaransa, Mhe. Franck Riester (hawapo
pichani) leo Jijini Dar es Salaam
Waziri
wa Biashara za Kimataifa na Uwekezaji wa Ufaransa, Mhe. Franck Riester akieleza
jambo kwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi
Liberata Mulamula (Mb) pamoja na Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhe. Prof. Makame
Mbarawa leo Jijini Dar es Salaam
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata
Mulamula (Mb) akimkabidhi zawadi ya picha ya Mlima Kilimanjaro Waziri wa
Biashara za Kimataifa na Uwekezaji wa Ufaransa, Mhe. Franck Riester leo Jijini
Dar es Salaam
Mawaziri
wakiwa katika picha ya pamoja na Mabalozi leo Jijini Dar es Salaam