Sehemu ya Meza Kuu wakifuatilia Mkutano uliokuwa ukiendelea |
Wednesday, June 8, 2022
WAZIRI MULAMULA ATOA WITO KWA JUMUIYA ZA KIKANDA KUSHIRIKIANA KATIKA KUTEKELEZA MAKUBALIANO YA AfCFTA
Saturday, June 4, 2022
WIZARA YA MAMBO YA NJE YAWAPIGA MSASA WABUNGE KUHUSU UMUHIMU WA KUDHIBITI MIGOGORO
Serikali ya Tanzania
imechangia kwa kiasi kikubwa jitihada za kuleta amani barani Afrika hususan
eneo la ukanda wa maziwa makuu, kupitia ushiriki wake katika kutatua migogoro
na kuchangia vikosi vya kulinda amani.
Kauli hiyo imetolewa na Kaimu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Balozi Fatma Mohammed Rajab alipozungumza leo jijini Dodoma wakati wa ufunguzi
wa warsha kuhusu Utatuzi wa Migogoro iliyotolewa na Wizara kwa Wajumbe wa
Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama kwa lengo la kuwajengea
uwezo.
Amesema kuwa, kwa miaka mingi
Tanzania imeendeelea kushirikishwa kwenye utatuzi wa migogoro na kuchangia vikosi
vya kulinda amani kutokana na kuaminika kwake kikanda na kimataifa kwenye eneo
hilo na hii inatokana na hali ya amani
na utulivu wa kisiasa, kiuchumi na kijamii iliyopo nchini.
“Jukumu la Wizara ni kusimamia
uhusiano baina ya Tanzania na nchi mbalimbali na mashirika ya kikanda na
kimataifa kwa lengo la kulinda maslahi ya nchi. Ni kutokana na kutekeleza jukumu
hilo, Tanzania imeendelea kuaminika na kushirikishwa katika utatuzi wa migogoro
mbalimbali Afrika. Hiki ni kielelezo cha kuaminika”, amesema Balozi Rajab.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa
Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, Mhe. Vita Kawawa amesema
kuwa viongozi wakiwemo Wabunge wanayo nafasi kubwa katika kuchangia amani
kupitia nafasi zao kwa kutoa elimu ya uzalendo kwa wananchi kwa kuwaelimisha
kutojiingiza kwenye masuala yanaweza kusababisha migogoro na uvunjifu wa amani
ndani ya jamii.
“Kila mmoja wetu atumie nafasi
yake kuzuia migogoro katika jamii ikiwemo ile inayosababishwa na siasa. Wizara
iendelee kutoa semina hizi na Kamati itaendelea kutoa ushirikiano na ushauri
unaohitajika kwa Wizara”, alisisitiza Mhe. Kawawa.
Akiwasilisha mada kuhusu “Utatuzi,
Udhibiti na Usuluhishi wa Migogoro” Mkufunzi kutoka Chuo cha Diplomasia
cha jijini Dar es Salaam, Dkt. Ally Masabo amesema ujenzi wa imani na kujiamini
kwa wananchi na siasa safi ni njia mojawapo ya kudhibiti migogoro ndani ya
jamii. Pia ameongeza kuwa, Tanzania ipo mstari wa mbele katika utatuzi wa
migogoro na uchangiaji wa vikosi vya ulinzi wa amani kutokana na ukweli kwamba
eneo lote linaloizunguka Tanzania likiwa salama nchi inanufaika zaidi.
“Tanzania ni nchi ya 13
ulimwenguni katika kuchangia walinzi wa amani na ya sita Afrika. Hii inatokana
na imani ya Tanzania kwamba amani ni chanzo cha maendeleo. Tanzania inaamini
kwamba nchi zinazotuzunguka zikiwa salama nchi inanufaika kuliko zikiwa katika
migogoro” amesema Dkt. Masabo.
Wakichangia mada hiyo, Wajumbe
hao wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama wamepongeza utaratibu
wa Wizara wa kutoa semina za aina hiyo kwao na kuongeza kuwa, ipo haja kwa
Serikali kuwa na Program za uelimishaji umma kuanzia ngazi za chini kuhusu
umuhimu wa amani na madhara yanayotokana na migogoro katika jamii.
Pia wamesisitiza elimu ya
kuwawezesha wananchi kujikwamua kiuchumi kwa kufanya kazi na kujishughulisha
itolewe kwa wingi ili kuepuka migogoro inayosababishwa na wananchi kutojishughulisha
na kusubiri Serikali iwanyie kila kitu.
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, Mhe. Vita Kawawa akifafanua jambo wakati wa majadiliano kwenye mafunzo hayo. |
Mkurugenzi wa Idara wa Siasa, Ulinzi na Usalama katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Stephen Mbundi akitoa neno la shukurani kwa jumbe wa kamati hiyo. |
Mhe. Cosato Chumi akichangia hoja wakati wa majadiliano, kulia ni Mhe. Janeth Masaburi akifatilia mafunzo. |
Sehemu ya Wajumbe wa kati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, kutoka kushoto ni Mhe. Bonnah Kamol na Mhe. Fakharia Shomar Khamis wakifuatilia uwasilishaji wa mada ya migogoro. |
Mhe. Abeid Ramadhani akichangia hoja wakati wa majadiliano kwenye mafunzo hayo. |
Mkufunzi kutoka Chuo cha Diplomasia, Dkt. Ally Masabo akiwasilisha mada ua udhibiti wa migogoro kwa kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama. |
Mafunzo yakiendelea, wa kwanza kulia ni Mhe. Stella Ikupa akifuatilia majadiliano. |
Mhe. Zahor Mohamed Haji akifafanua juu ya umuhimu wa mafunzo hayo kwa Waheshimiwa Wabunge na umuhimu wa kulinda kauli zao ili kuepuka kuwa vyanzo vya migogoro katika jamii na Taifa kwa ujumla. |
TZ, ITALIA KUONGEZA NGUVU SEKTA YA BIASHARA NA UWEKEZAJI
Na Mwandishi wetu, Dar
Tanzania na Italia zimeahidi kushirikiana kukuza na kuendeleza sekta ya biashara ya uwekezaji kwa maslahi mapana ya pande zote mbili.
Akihutubia sherehe za maadhimisho ya 76 ya siku ya Kitaifa ya Jamhuri ya Italia, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula (Mb) alisema Tanzania imeboresha mazingira ya biashara na uwekezaji na kuwasihi wafanyabiashara wa Italia kuja kuwekeza nchini kwa kuwa ni salama zaidi.
“Natumia fursa hii kuwahakikishia ushirikiano wetu wa kukuza na kuendeleza biashara na uwekezaji nchini, Serikali imechukua jitihada mbalimbali za kuwavutia wawekezaji kuwekeza hapa nchini ikiwemo kuondoa vikwazo vya biashara,” alisema Balozi Mulamula
Balozi Mulamula aliongeza kuwa, Tanzania na Italia zimekuwa na utamaduni wa kuwakutanisha wafanyabiashara na wawekezaji kupitia majukwaa mbalimbali ya biashara na matokeo chanya ya majukwaa hayo yameanza kuonekana ambapo Disemba, 2021 kupitia kongamano la biashara na uwekezaji lililofanyika Italia, kampuni ya Kiitaliano ‘Suness Limited’ inayojishughulisha na uchimbaji wa madini ilisaini makubaliano na Shirika la Taifa la madini (Stamico) kwa ajili ya kuendeleza mradi wa shaba inayopatikana Kilimanjaro.
“Ni Imani yangu kuwa kupitia kongamano la biashara na uwekezaji litakalofanyika mwezi Septemba 2022 Jijini Dar es Salaam na Zanzibar litatoa fursa nyingi zaidi kwa pande zote mbili kuchangamkia fursa zinazopatikana kwenye sekta za kilimo, viwanda, miundombinu, elimu, utalii na uchumi wa buluu,” alisema Balozi Mulamula
Pamoja na mambo mengine, Balozi Mulamula aliishukuru Serikali ya Italia kwa ushirikiano imara wa kuchangia maendeleo ya Tanzania ambapo wiki ijayo Tanzania na Italia zitasaini makubaliano ya mkopo wa masharti nafuu wa Euro milioni 20 kwa ajili ya kuboresha elimu ya ufundi katika mikoa ya Mbeya, Arusha, mwanza, Songwe, Zanzibar na Dar es Salaam.
Kwa upande wake, Balozi wa Italia nchini, Mhe. Marco Lombardi ameipongeza Tanzania kwa jitihada kubwa za kuboresha na kuimarisha mazingira ya biashara nchini.
“Kwa kweli tunafurahishwa sana na namna mazingira ya biashara yanavyoboreshwa hapa Tanzania, kwa kweli tutaendelea kuwashawishi wafanyabiashara wetu waje kuwekeza hapa kwani ni sehemu salama uya kuwekeza,” alisema Balozi Lombardi
Aliongeza kuwa kitendo cha Tanzania kuviondoa vikwazo vya biashara kimeongeza imani kubwa kwa wafanyabiashara na wawekezaji wengi duniani kuiona Tanzania ni salama. Aidha, Balozi Lombard alimpongeza Rais wa Jamahuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa ya kuimarisha Diplomasia ya Uchumi na mataifa mengine duniani.
“Napenda kuwahakikishia kuwa Italia itaendelea kushirikiana na Tanzania katika kukuza na kuimarisha uhusiano uliopo baina yetu kwa maslahi mapana ya pande zote mbili,” aliongeza Balozi Lombardi.
Tanzania na Italia zimekuwa zikishirikiana katika Nyanja za kilimo, afya, elimu, maji, nishati, utalii na maendeleo ya sekta binafsi.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akisalimiana na Kiongozi wa Mabalozi nchini ambaye pia ni Balozi wa Visiwa vya Comoro nchini Mhe. Dkt. Ahmada El Badaoui Mohamed katika sherehe za maadhimisho ya 76 ya siku ya Kitaifa ya Jamhuri ya Italia, jana jioni Jijini Dar es Salaam |
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akiwasilisha hotuba yake katika sherehe za maadhimisho ya 76 ya siku ya Kitaifa ya Jamhuri ya Italia, jana jioni Jijini Dar es Salaam |
Balozi wa Italia nchini, Mhe. Marco Lombardi akiwasilisha hotuba yake katika sherehe za maadhimisho ya 76 ya siku ya Kitaifa ya Jamhuri ya Italia, jana jioni Jijini Dar es Salaam |
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akikata keki katika sherehe za maadhimisho ya 76 ya siku ya Kitaifa ya Jamhuri ya Italia, jana jioni Jijini Dar es Salaam |
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula na Balozi wa Italia nchini, Mhe. Marco Lombardi wakishangilia baada ya kukata keki katika sherehe za maadhimisho ya 76 ya siku ya Kitaifa ya Jamhuri ya Italia, jana jioni Jijini Dar es Salaam |
Friday, June 3, 2022
TANZANIA, IRELAND KUONGEZA MAENEO YA USHIRIKIANO
Na Mwandishi wetu, Dar
Tanzania na Ireland zimeahidi kuongeza maeneo mapya ya ushirikiano ambayo ni biashara na uwekezaji, kilimo, viwanda vya nguo pamoja na ujenzi.
Ahadi hiyo imetolewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula (Mb) alipokutana kwa mazungumzo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Ireland, Bw. Joe Hackett katika Ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam
“Ireland imekuwa mdau mkubwa wa maendeleo kwa Tanzania katika masuala ya kijamii ikiwemo elimu, kusaidia kaya masikini na kuwajengea uwezo wanawake, kupitia kikao chetu cha leo tumekubaliana kuangalia namna ya kuongeza wigo wa ushirikiano katika sekta ya biashara na uwekezaji, kilimo hasa parachichi, viwanda vya nguo pamoja na ujenzi ili kuweza kuinua zaidi uchumi wetu kwa maslahi ya pande zote mbili,” amesema Balozi Mulamula
Balozi Mulamula ameongeza kuwa kupitia biashara na uwekezaji wafanyabiashara wa Kitanzania watapata fursa ya kuchangamkia biashara zinazopatikana nchini Ireland lakini pia wafanyabiashara wa Ireland watapata fursa ya kuwekeza nchini Tanzania.
Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje wa Ireland, Bw. Joe Hackett amesema Ireland wamefurahishwa na hatua ambazo Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan imekuwa ikizichukua katika kuimarisha na kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji pamoja na kuinganisha Tanzania na mataifa mengine ulimwenguni.
“Ireland tunaiona Tanzania ikiwa tulivu na mazingira mazuri ya kuwavutia wafanyabiashara, tutaongea na wafanyabiashara na kuwaeleza kuwa Tanzania ni sehemu salama kuwekeza,” amesema Bw. Hackett
Pamoja na mambo mengine, viongozi hao walijadili masuala mbalimbali ya uhusiano baina ya Tanzania na Ireland katika maeneo yenye maslahi kwa pande zote mbili.
Katika tukio jingine, Balozi Mulamula ameongoza majadiliano ya mpango wa kuimarisha diplomasia ya uchumi ya Tanzania. Wengine walioshiriki katik majadiliano hayo ni Balozi wa Uswisi nchini mhe. Didier Chassot, Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa (UN), Bw. Zlatan Milišić na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) Christine Musisi, Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Swahiba Mndeme pamoja na wadau wengine wa maendeleo.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akizungumza na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Ireland, Bw. Joe Hackett katika Ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam |
Maongezi ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Ireland, Bw. Joe Hackett yakiendelea katika Ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam |
Mkurugenzi wa Idara ya Amerika na Ulaya kutoka Wizara ya mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Swahiba Mndeme (Mwenye Koti Jekundu) akifuatiwa na Afisa Dawati Bw. Laurian Ntwale, Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mindi Kasiga pamoja na Katibu wa Mhe. Waziri, Bw. Seif Kamtunda wakifuatilia kikao cha Balozi Liberata Mulamula na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Ireland, Bw. Joe Hackett katika Ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam |
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Ireland, Bw. Joe Hackett katika picha ya pamoja na Balozi Mindim Kasiga, Balozi Swahiba Mndeme na Bw. Laurian Ntwale kutoka wizarani pamoja na Balozi wa Ireland nchini, Mhe. Mary O’Neil na maafisa waandamizi kutoka ubalozi wa Ireland nchini. |
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akiongoza kikao cha majadiliano ya Mpango wa kuimarisha diplomasia ya uchumi ya Tanzania katika kikao cha majadiliano ya Mpango wa kuimarisha diplomasia ya uchumi ya Tanzania katika Ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam |
Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) Christine Musisi akieleza jambo katika kikao cha majadiliano ya Mpango wa kuimarisha diplomasia ya uchumi ya Tanzania katika Ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam |
Mtaalam akiwasilisha mada katika kikao cha majadiliano ya Mpango wa kuimarisha diplomasia ya uchumi ya Tanzania katika Ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam |
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula katika picha ya pamoja na washiriki wa majadiliano ya Mpango wa kuimarisha diplomasia ya uchumi ya Tanzania katika Ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam |
Thursday, June 2, 2022
SERIKALI NA KAMPUNI YA LONGPIN WAKUBALIANA KUHARAKISHA UWEKEZAJI KATIKA KILIMO CHA SOYA
Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. Antony Mavunde akizungumza wakati wa kikao baina ya Viongozi,Watendaji na Maafisa Waandamizi wa Serikali na Watendaji wa Kampuni ya Longping High Tech ya China kilichofanyika katika ofisi ya Wizara hiyo jijini Dodoma. |
Balozi wa Tanzania nchini Brazil Mhe. Balozi Prof. Adelardus Kirangi akizungumza wakati wa kikao baina ya Viongozi, Watendaji na Maafisa Waandamizi wa Serikali na Watendaji wa Kampuni ya Longping High Tech ya China kilichofanyika katika ofisi ya Wizara hiyo jijini Dodoma. |
Balozi wa Tanzania nchini China Mhe. Mbelwa Kairuki akizungumza wakati wa kikao baina ya Viongozi, Watendaji na Maafisa Waandamizi wa Serikali na Watendaji wa Kampuni ya Longping High Tech ya China kilichofanyika katika ofisi ya Wizara hiyo jijini Dodoma. |
Mkurugenzi wa Biashara za Nje na Fedha wa Kampuni hiyo Bw. Shangyang Wu akizungumza kwenye kikao baina ya Viongozi, Watendaji na Maafisa Waandamizi wa Serikali na Watendaji wa Kampuni ya Longping High Tech ya China kilichofanyika katika ofisi ya hiyo jijini Dodoma. |
Mkutano ukiendelea |
Mkutano ukiendelea |
Viongozi,Watendaji, Maafisa Waandamizi wa Serikali, wadau kutoka sekta binafsi na Watendaji wa Kampuni ya Longping High Tech ya nchina China wakiwa katika picha ya pamoja baada ya mkutano uliofanyika katika ofisi ya Wizara ya Kilimo jijini Dodoma |
TANZANIA KUENDELEA KUCHANGIA OPERESHENI ZA ULINZI WA AMANI
Na Mwandishi wetu, Dar
Katika jitihada za kuwaunga mkono walinda amani, Tanzania imeahidi kuendelea kuchangia zaidi katika operesheni za ulinzi wa amani duniani ili kuendelea kunufaika na matunda ya amani.
Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula (Mb) alipohutubia maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Walinzi wa Amani katika viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam.
“Walinda amani wa Umoja wa Mataifa ni kiungo muhimu katika mfumo wa amani na usalama wa dunia kwani wamejitolea maisha yao kutumikia katika hali ngumu ili mamilioni ya watu ulimwenguni waishi kwa amani,” amesema Balozi Mulamula.
Balozi Mulamula ameongeza kuwa nchi nyingi duniani zimekuwa zikifanya kazi kwa bidii ili kutekeleza na kufikia Malengo ya Maendeleo Endelevu ifikapo 2030, amani ni sehemu muhimu katika azma hiyo.
Jumuiya ya Kimataifa inapaswa kuendelea kupaza sauti katika kuhakikisha amani inapatikana duniani kama kaulimbiu ya mwaka huu inavyosisitiza, ni juu yetu kuchukua jukumu hili kwa pamoja, kutafuta misingi ya pamoja, kuzingatia umuhimu wa mazungumzo na upatanishi kama njia ya kutatua migogoro kwa njia za amani.
“Tanzania inajivunia kushika nafasi ya 13 kwa mchango mkubwa katika operesheni za ulinzi wa amani za Umoja wa Mataifa duniani. Hadi Machi mwaka huu, Tanzania imechangia walinda amani 1,485 katika nchi za Lebanon, Afrika ya Kati, Sudan Kusini na DRC ambapo matokeo chanya ya uwepo wao katika nchi hizi yameonekana,” ameongeza Balozi Mulamula.
Awali akihutubia maadhimisho hayo kwa Niaba ya Katibu Mkuu Umoja wa Mataifa, Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa (UN), Bw. Zlatan Milišić ameipongeza Tanzania kwa kuungana na Umoja wa Mataifa kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Walinzi wa Amani.
“Tanzania imekuwa na mchango mkubwa katika jitihada za kuendelea kuchangia walinda amani katika mataifa mbalimbali ikiwemo DRC, Lebanon na Sudani Kusini, Amesema Bw. Milišić na kuongeza kuwa amani ni ustawi wa maendeleo kwa taifa lolote lile duniani.
Pamoja na mambo mengine, Bw. Milišić amesema Umoja wa Mataifa unatambua mchango wa Tanzania katika kulinda amani ndani ya nchi na amani katika mataifa mengine.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akiongoza viongozi wa vyombo vya ulinzi na usalama pamoja na mabalozi katika maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Walinzi wa Amani wa Umoja wa Mataifa katika viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam |
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula na Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa (UN), Bw. Zlatan Milišić pamoja na baadhi wa viongozi wa vyombo vya ulinzi na usalama wakiimba nyimbo ya taifa wakati wa maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Walinzi wa Amani wa Umoja wa Mataifa |
Meza kuu wakifuatilia maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Walinzi wa Amani wa Umoja wa Mataifa |
Sehemu ya Mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini wakifuatilia maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Walinzi wa Amani wa Umoja wa Mataifa |
Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa (UN), Bw. Zlatan Milišić akiwasilisha hotuba yake katika maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Walinzi wa Amani wa Umoja wa Mataifa |
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akiwasilisha hotuba yake katika maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Walinzi wa Amani wa Umoja wa Mataifa |
Mabalozi pamoja na maafisa waandamizi wa vyombo vya ulinzi na usalama katika picha ya pamoja |