Thursday, November 24, 2022

DKT. TAX AFANYA MAZUNGUMZO NA MENEJIMENTI YA UDOM

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb.) ambaye pia ni Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) leo tarehe 24 Novemba 2022 amefika chuoni hapo na kufanya mazungumzo na Menejimenti.

Akiwa chuoni hapo pamoja na masuala mengine Dkt. Tax amepokea taarifa kuhusu maendeleo ya maandalizi ya shughuli mbalimbali zinazotarajiwa kufanyika chuoni hapo katika kipindi cha mwisho wa mwaka huu 2022. Taarifa hiyo ilihusisha maendeleo ya maandalizi ya Sherehe ya Mahafali ya 13 ya Chuo hicho yanayotarajiwa kufanyika tarehe 1 na 2 Disemba 2022, na kufanyika kwa Mkutano wa Wanazuoni wa Chuo hicho. 

Akizungumza muda mfupi baada ya Dkt. Tax kuwasili chuoni hapo, Makamu Mkuu wa Chuo hicho Prof. Lughano Jeremy Kusiluka ameeleza kuwa ni utaratibu wa kawaida wa utendaji wa Menejimenti kutoa taarifa kwa Mkuu wa Chuo kila mara kuhusu maendeleo ya shughuli mbalimbali zinazoendelea Chuoni hapo. 

Mhe. Waziri Dkt. Tax aliteuliwa kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan tarehe 16 Juni 2021.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb.) na Mkuu wa Chuo cha Dodoma akisaini kitabu cha wageni alipowasili katika Chuo Kikuu cha Dodoma.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax na Mkuu wa Chuo cha Dodoma akiwa na Manejimenti ya UDOM muda mfupi baada ya kuwasili chuoni hapo kwa mazungumzo na Menejimenti ya Chuo.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb.) na Mkuu wa Chuo cha Dodoma akiagana na Makamu Mkuu wa Chuo hicho Prof. Lughano Jeremy Kusiluka (kushoto), Naibu Makamu wa Chuo Taaluma, Utafiti na Huduma kwa Jamii Prof. Razack Bakari Lokina (katikati) na Naibu Makamu wa Chuo Mipango, Fedha na Utawala Prof.Wineaster Anderson Saria (haonekani pichani) 

MABALOZI WARIDHISHWA NA MIPANGO YA HOSPITALI YA BENJAMIN MKAPA

Mabalozi wa Tanzania wameahidi kufanya kazi kwa karibu na Hospitali ya Benjamin Mkapa ya jijini Dodoma ili iweze kutekeleza mpango mkakati iliyojipangia wa kutoa huduma bora za afya nchini
.
Mabalozi walitoa kauli hiyo wakati wa kikao cha pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa hospitali hiyo, Dkt. Alphonce Chandika kilichofanyika leo jijini Dar Es Salaam kujadili namna Mabalozi watakavyoweza kuvutia wadau watakaoshirikiana na hospitali hiyo kutekeleza mpango mkakati huo.

"Umeongea mengi na yote uliyoyaongea unaonekana unayaishi na umedhamiria yatokee, ni jambo jema kuwa na dira inayoonesha hospitali inapoelekea katika kuimarisha huduma za afya nchini", Mwakilishi wa Kudumu kwenye Ofisi za Umoja wa Mataifa, Geneva, Balozi Maimuna Tarishi alisema.  

Dkt. Chitanda aliwaeleza Mabalozi hao mipango ya hospitali hiyo ya kuanzisha huduma mbalimbali za kibingwa na kuimarisha zilizopo, hivyo aliwomba mabalozi kutafuta wadau kwenye maeneo yao ya uwakilishi ili washirikiane na hospitali hiyo kuimarisha huduma za afya nchini.

Baadhi ya maeneo ambayo Mkurugenzi aliomba Mabalozi washirikiane ni pamoja na huduma za matibabu ya magonjwa ya mfumo wa mkojo, saratani, moyo, upandikizaji wa figo na uboho na upasuaji wa nyonga na mishipa ya fahamu. Misaada inayohitajika ni pamoja na mafunzo ya kibingwa, ujenzi wa majengo na ununuzi wa vifaa tiba. 

Mabalozi wa Tanzania wapo nchini wakiendelea na ratiba mbalimbali baada ya kushiriki Mkutano na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan uliofanyika Zanzibar kuanzia tarehe 14 hadi 21 Novemba 2022.
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Benjamin Mkapa, Dkt. Alphonce Chandika akiongea na Mabalozi wa Tanzania kuhusu mipango ya hospitali hiyo yenye lengo la kutoa huduma bora kwa jamii. Mwingine katika picha ni Mkurugenzi wa Mafunzo na Utafiti, Dkt. Monica Kessy.


Balozi wa Tanzania nchini Uingereza na Amidi wa Mabalozi, Mhe. Dkt. Asha-Rose Migiro (katikati), Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania kwenye Ofisi za Umoja wa Mataifa, Genrva, Balozi Maimuna Tarishi (kushoto) na Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afruka Mashariki, Bslozi Swahiba Mndeme wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Benjamin Mkapa, Dkt. Alphonce Chandika

Waheshimiwa Mabalozi wa Tanzania katika nchi za Ufaransa, Japan na Brazil wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Benjamin Mkapa, Dkt. Alphonce Chandika

Waheshimiwa Mabalozi wa Tanzania katika nchi za Urusi na Austria wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Benjamin Mkapa, Dkt. Alphonce Chandika

Waheshimiwa Mabalozi wa Tanzania wakiwa katika mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Benjamin Mkapa, Dkt. Alphonce Chandika

Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Benjamin Mkapa, Dkt. Alphonce Chandika akiwa katika picha ya pamoja na Waheshimiwa Mabalozi wa Tanzania





Wednesday, November 23, 2022

DKT.TAX AFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA URUSI NA IRAN


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax leo tarehe 23 Novemba 2022 kwa nyakati tofauti amekutana kwa mazungumzo na Balozi wa Shirikisho la Urusi nchini Mhe. Andrey Levonovich Avetisyan na Balozi wa Iran nchini Mhe. Hossein Alvandi Bahineh yaliyofanyika jijini Dodoma. 

Katika mazungumzo hayo mbali na kudumisha na kuendeleza uhusiano wa kidiplomasia, vilevile yalijikita katika kujadili masuala mbalimbali yenye maslahi mapana kwa pande zote mbili na kimataifa ikiwemo biashara na uwekezaji, utalii, amani na usalama na kuendeleza sekta ya uvuvi na kilimo nchini. 

Dkt. Tax akizungumza na Balozi wa Shirikisho la Urusi nchini Mhe. Andrey Levonovich Avetisyan ameeleza kuwa licha uhusiano wa muda mrefu wa kidiplomasia uliopo kati ya mataifa haya mawili, Urusi imeendelea kuwa mshirika muhimu wa maendeleo ya sekta mbalimbali nchini. Hivyo serikali itaendelea kudumisha na kuendeleza uhusiano mzuri uliopo na kuangalia maeno mapya ya ushirikiano kwa manufaa ya pande zote mbili.

Kwa upande wake Balozi Avetisyan ameeleza kuwa Urusi itaendelea kushirikiana na Tanzania ikiwemo kuongeza msukumo katika masuala ya uwekezaji, biashara, na utalii. Vilevile aliongeza kusema kuwa katika siku za usoni Urusi inatarajia kuongeza kiwango cha ufadhili wa masomo kwa vijana wa Tanzania kwenda kusoma nchini humo. 

Sambamba na hayo, Balozi Avetisyan alisisitiza utayari wa Urusi kushirikiana na Tanzania katika masuala ya utamadumi ikiwemo kuendeleza lugha ya Kiswahili nchini humo. Amebanisha juhudi mbalimbali zinazofanywa na Urusi katika kuendeleza lugha hiyo nchini humo, ambapo ameeleza kuwa hadi sasa kuna takriban Vyuo Vikuu vitano vinavyofundisha Kishwahili nchini humo. 

Kwa upande wake Balozi wa Irani nchini Mhe. Hossein Alvandi Bahineh akizungumza na Waziri Dkt. Tax ameeleza kuwa Iran inaingalia Tanzania kama mbia muhimu wa uwekezaji katika ukanda wa Afrika Mashariki, huku akielezea nia ya Iran ya kuwekeza nchini katika sekta ya kilimo, uvuvi na uendelezaji wa makazi.

Aidha Waziri Dkt. Tax ameeleza utayari wa Serikali ya Tanzania katika kuendelea kuboresha mazingira ya uwekezaji na biashara nchini. Alieleza kuwa juhudi hizo zinahusisha hatua mbalimbali zinazoendelea kuchukuliwa na Serikali katika kufanya maboresho ya kanuni, sera na sheria mbalimbali kwa lengo la kuboresha mazingira ya bishara na uwekezaji nchini. 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax na Balozi wa Shirikisho la Urusi nchini Mhe. Andrey Levonovich Avetisyan wakiwa katika mazungumzo yaliyofanyika jijini Dodoma.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax akielezea jambo wakati wa mazungumzo na Balozi wa Iran nchini Mhe. Hossein Alvandi Bahineh yaliyofanyika jijini Dodoma. 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax akimkaribisha Balozi wa Iran nchini Mhe. Hossein Alvandi Bahineh wakati wa mazungumzo yaliyofanyika jijini Dodoma.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax na Balozi wa Iran nchini Mhe. Hossein Alvandi Bahineh wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika jijini Dodoma.

Sunday, November 20, 2022

MABALOZI WAHIMIZWA KUBIDHAISHA KISWAHILI

 


Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Saidi Yakubu akizungumzia umuhimu wa wadau wa lugha ya Kiswahili kushirikian katika kutekeleza Mkakati wa kubidhaisha lugha ya Kiswahili wakati wa mkutano wa Mabalozi wa Tanzania uliomalizika Zanzibar tarehe 20 Novemba 2022

Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili Tanzania (BAKITA), Bi. Consolata Mushi akiwasilisha mada ya mkakati wa kubidhaisha lugha ya Kiswahili katika mkutano wa Mabalozi wa Tanzania uliomalizika Zanzibar tarehe 20 Novemba 2022

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Saidi Yakubu akimkabidhi tuzo maalum Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa, Mhe. Samwel Shelukindo kwa kutambua mchango wake wa kuipigania lugha ya Kiswahili kwenye medani za kimataifa na kupelekea Unesco kutangaza Julai 7 ya kila mwaka kuwa siku ya Kiswahili 

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Sokoine akipokea vitabu vya lugha ya Kiswahili kutoka kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Saidi Yakubu kwa ajili ya kutumiwa na Balozi za Tanzania Nje kufundishia lugha ya Kiswahili katika maeneo yao ya uwakilishi 





Saturday, November 19, 2022

RAIS SAMIA AWATAKA MABALOZI KUENDANA NA MABADILIKO YA DUNIA

 



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwahutubia Mabalozi wa Tanzania Nje ya Nchi wakati wa mkutano uliofanyika Zanzibar tarehe 19 Novemba, 2022 


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax akiwatambulisha Mabalozi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan wakati wa Mkutano wa mabalozi wa Tanzania Nje ya Nchi

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk akitoa neno la shukrani kwa niaba ya wizara wakati wa mkutano kati ya Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan na Mabalozi wa Tanzania

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Sokoine akitoa neno la utangulizi  wakati wa mkutano kati ya Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan na Mabalozi 

Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mindi Kasiga  ambaye pia alikuwa mshereheshaji akizungumza wakati wa mkutano wa Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan na Mabalozi 

Sehemu ya Mabalozi wakifuatilia mkutano kati yao na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan uliofanyika Zanzibar 19 Novemba 2022

Meza kuu ikiongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan katika picha ya pamoja

Meza kuu ikiongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan katika picha ya pamoja na uongozi wa Wizara ya mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki 

Friday, November 18, 2022

DKT. MWINYI: MABALOZI JENGENI UHUSIANO MZURI NA SEKTA ZA UMMA, BINAFSI

 



Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi akiwahutubia Mabalozi wa Tanzania Nje ya Nchi wakati wa mkutano uliofanyika Zanzibar 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax akiwasilisha salamu za Wizara kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi wakati wa Mkutano wa mabalozi wa Tanzania Nje ya Nchi

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk akitoa neno la shukrani kwa niaba ya wizara wakati wa mkutano kati ya Mhe. Rais Hussein Ali Mwinyi na Mabalozi 

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Fatma Rajab akitoa neno la utangulizi  wakati wa mkutano kati ya Mhe. Rais Hussein Ali Mwinyi na Mabalozi 

Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mindi Kasiga  akizungumza kama mshereheshaji wakati wa mkutano kati ya Mhe. Rais Hussein Ali Mwinyi na Mabalozi 

Sehemu ya Mabalozi wakifuatilia mkutano kati yao na Mhe. Rais Hussein Ali Mwinyi

Sehemu ya Mabalozi wakifuatilia mkutano kati yao na Mhe. Rais Hussein Ali Mwinyi

Meza Kuu ikiongozwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi katika picha ya pamoja Uongozi na Menejimenti ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi katika picha ya pamoja na kamati ya maandalizi ya mkutano




MABALOZI WATEMBELEA BANDARI YA MALINDI


Amidi wa Mabalozi Tanzania Mhe.Dkt. Asha-Rose Migiro (aliyeshika Mic) akiwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Fatma Rajab (kushoto) akizungumza katika ziara ya kutembelea eneo la ujenzi wa bandari ya Mangapwani Mkoa wa Kaskazini wakati Mabalozi wa Tanzania walioko mkutanoni Zanzibar walipotembelea Shirika la Bandari Zanzibar ili kujionea shirika hilo linavyofanya kazi

Amidi wa Mabalozi Tanzania Mhe.Dkt. Asha-Rose Migiro (katikati) akisikiliza maelezo kutoka kwa Mtumishi wa Shirika la Bandari Zanzibar (hayuko pichani)  kwa Mabalozi wa Tanzania waliotembelea eneo la ujenzi wa bandari ya Mangapwani Mkoa wa Kaskazini Unguja  Zanzibar


Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Bandari Zanzibar Bw. Nahmat Mahfoudh akizungumza na Mabalozi Tanzania waliotembelea eneo la ujenzi wa bandari ya Mangapwani Mkoa wa Kaskazini Unguja 


Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Mhe. Ayoub Mohamed Mahmoud akizungumza na Mabalozi Tanzania waliotembelea eneo la ujenzi wa bandari ya Mangapwani Mkoa wa Kaskazini Unguja

 Mabalozi Tanzania wakiongozwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Fatma Rajab akiwa na mabalozi wa Tanzania wakisikiliza maelezo kutoka kwa Viongozi wa Shirika la Bandari Zanzibar walipotembelea eneo la ujenzi wa bandari ya Mangapwani Mkoa wa Kaskazini Unguja

 

Balozi wa Tanzania nchini Uhlonzi Mhe. Caroline Chipeta (katikati) akiwa na baadhi ya wajumbe wa Menejiment ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakati Mabalozi wa Tanzania  walipotembelea eneo la Mangapwani Mkoa wa Kaskazini Unguja ambako Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imepanga kujenga Bandari mpya  na ya kisasa
 


Mabalozi wa Tanzania wanaoshiriki Mkutano wa Mabalozi unaofanyika mjini Zanzibar wametembelea bandari ya Malindi leo tarehe 17 Novemba 2022 na kujionea jinsi bandari hiyo inavyofanya kazi.


Mabalozi hao pia wametembelea eneo la Mangapwani ambako Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imepanga kujenga bandari kubwa mpya na ya kisasa ambayo itaipunguzia mzigo bandari ya Malindi.
Katika ziara hiyo iliyoongozwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Fatma Rajab imewawezesha Mabalozi hao kujionea jinsi bandari ya Malindi inavyofanya kazi na hivyo kusaidia juhudi za kukuza uchumi wa Zanzibar

Akizungumza na mabalozi hao katika bandari ya Malindi na eneo la Mangapwani, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Bandari Zanzibar Bw. Nahmat Mahfoudh amesema bandari ya Malindi kwa sasa imekuwa ikikabiliwa na changamoto ya kupokea makontena mengi na makubwa na meli za kisasa kuliko uwezo wa bandari hiyo ambao ujenzi wake hauruhusu kupokea meli na contena hizo.

 ‘‘Bandari hii inakabiliwa na changamoto ya ufinyu wa nafasi na uwezo wa kuhudumia meli na makontena makubwa, kwa hiyo bandari hii itabakia kuwa bandari ya meli za abiria kati ya Zanzibar na Dar es Salaam, kiufupi hii itakuwa bandari ya kitalii’’, alisema Bw. Mahfoudh.

Amesema wameamua kujenga bandari ya mangapwani ili iweze kwenda na mahitaji ya nyakati hizi kwa kuwa uwezo wake ni kupokea Tus 80,000 lakini bandari mpya itakayojengwa Mangapwani itakuwa na uwezo wa kupokea Tus 800,000 hadi 1,800,000. 

Akiongelea changamoto zinazolikabili Shirika la Bandari Zanzibar Bw. Mahfoudh amesema bado wanapambana kuondokana na madhara yaliyotokana na janga la Covid 19 ambalo limelilitea shirika madhara makubwa.

Akizingumza katika ziara hiyo, Amidi wa Mabalozi nchini, Mhe.Dkt. Asha-Rose Migiro amelishukuru Shirika la Bandari kwa kuwapokea na kuzungumza nao na kuwapongeza kwa kazi nzuri wanayoifanya. 

Amempongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt. Hussein Ali Mwinyi kwa utayari wake wa kuwa na Miradi ya kimkakati kama huo wa bandari ya Mangapwani uliopangwa kufanyika katika mkoa wa Kaskazini 

Amesema kwa niaba ya mabalozi wenzake wanaahidi kuwa Mabalozi wazuri ambao wataendelea na kazi ya kuwavutia na kuwashawishi wawekezaji wenye mitaji mikubwa ili kuweza kutimiza nia na dhamira ya kuiendeleza Zanzibar.