Wednesday, August 30, 2023

DKT. SHELUKINDO AHIMIZA WELEDI KATIKA KUIMARISHA DIPLOMASIA YA UCHUMI


Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Samwel Shelukindo akizungumza na Watumishi wa Wizara (hawapo pichani) kwenye kikoa kilichofanyika Ukumbi wa Mtakatifu Gasper jijini Dodoma

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Samwel Shelukindo amewataka watumishi wa Wizara hiyo kufanya kazi kwa maarifa, ubunifu na kitimu ili kutimiza azma ya Serikali ya awamu ya sita ya kuimarisha diplomasia ya uchumi.

Balozi Dkt. Shelukindo ametoa rai hiyo Agosti, 30, 2023 jijini Dodoma w 

Balozi Shelukindo alisisitiza umuhimu wa watumishi kuboresha maarifa yao kila mara kwa kusoma vitabu ili wawe na ujuzi na mbinu za kutosha za kutekeleza majukumu yanayowakabili ambayo yanabadilika kulingana na wakati na teknolojia.

Dkt. Shelukindo aliwahimiza watumishi hao ambayo Wizara wanayoitumikia ni mtambuka kuhakikisha wanafuatilia utekelezaji wa makubaliano ambayo nchi imesaini na nchi nyingine kutoka kwa wadau wote ili iweze kufaidika na makubaliano hayo.

Tuwe wepesi kujibu wadau wetu tanaofanya nao kazi na kuhakikisha tunatoa huduma bora kwa wateja wa Wizara, huku tukizingatia ufanisi na hatimaye kuleta tija kwa nchi”, Balozi Shelukindo alisisitiza.
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Samwel Shelukindo akifuatilia kikao cha watumishi wa Wizara kilichokuwa kikiendelea

Walioketi; Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Samwel Shelukindo (katika), Mkurugenzi wa Idara ya Siasa, Ulinzi na Usalama na Kaimu Naibu Katibu Mkuu Balozi Stephen P. Mbundi (kushoto) na Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi Rasilimali Watu Bi. Chiku Kiguhe (kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watumishi kwenye kikao cha watumishi wa Wizara kilichokuwa kikiendelea
Mkurugenzi wa Idara ya Siasa, Ulinzi na Usalama na Kaimu Naibu Katibu Mkuu Balozi Stephen P. Mbundi akifuatilia kikao cha watumishi wa Wizara kilichokuwa kikiendelea
Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi Rasilimali Watu Bi. Chiku Kiguhe akifafanua jambo kwenye kikao cha watumishi wa Wizara kilichofanyika kwenye jijini Dodoma. 

Sehemu ya Menejimenti ya Wizara wakifuatilia kikao kilichokuwa kikiendelea
Watumishi wa Wizara wakifuatilia kikao
Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi Rasilimali Watu Bi. Chiku Kiguhe akifuatilia kikoa cha Watumishi kilichokuwa kikiendelea
Picha ya pamoja Meza Kuu na Menejimenti ya Wizara
Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika Balozi Swahiba Mndeme akizungumza kwenye kikao cha Watumishi wa Wizara kilichofanyika jijini Dodoma
Sehemu ya Watumishi wakifuatilia kikao

Kikao kikiendelea

Sehemu ya Menejimenti ya Wizara wakifuatilia kikao kilichokuwa kikiendelea

Sehemu ya Menejimenti ya Wizara wakifuatilia kikao cha watumishi wa Wizara kilichokuwa kikiendelea

BALOZI SHELUKINDO AIHAKIKISHIA USHIRIKIANO WFP


Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Samwel Shelukindo akisalimiana na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Mpango wa Chakula la Umoja wa Mataifa (WFP), Bi. Sarah Gordon-Gibson walipokutana kwa mazungumzo jijini Dodoma


Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Samwel Shelukindo amemhakikishia ushirikiano Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Mpango wa Chakula la Umoja wa Mataifa (WFP), Bi. Sarah Gordon-Gibson.

Balozi Dkt. Shelukindo ametoa ahadi hiyo alipokutana na Bi Gibson aliyemtembelea Ofisini kwake jijini Dodoma.

Katika mazungumzo yao viongozi hao wamejikita katika kuimarisha ushirikiano na kuongeza maeneo mapya ya ushirikiano.

Balozi Shelukindo ameeleza kuwa Tanzania inatambua mchango mkubwa unaotolewa na WFP katika ukanda wa Afrika na Tanzania katika utekelezaji wa vipaumbele vyake.

“Tanzania chini ya uongozi wa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan inatambua mchango wa WFP hivyo, itaendelea kutoa ushirikiano katika utekelezaji wa majukumu ya kitaifa na kikanda.” Alisema Dkt. Shelukindo.

Naye Bi. Sarah ameeleza kuwa katika mpango mkakati wa miaka mitano (5) (2022-2027) Shirika hilo limejielekeza katika usaidizi wa masuala ya kibinadamu kwa wakimbizi waliopo Kigoma, shughuli za maendeleo kwa nchi ya Tanzania na Watanzania kwakuwa ongezeko la idadai ya watu kupitia uwepo wa wakimbizis linaathiri mfumo wa nchi katika namna mbalimbali.

Maeneo mengine ni pamoja na kujenga uwezo katika mpango wa tahadhari za kukabiliana na majanga, vifaa vya TEHAMA, lishe kwa jamii hususan katika uzalishaji wa vyakula na uelewa juu ya lishe bora ili kuondoa utapiamlo na usaidizi wa wanawake na watoto.

Kadhalika, WFP imeweka mkazo katika kilimo cha mahindi, maharage na mtama, kuongeza maeneo mapya ya usaidizi katika uzalishaji wa maua, matunda na mbogamboga na kujenga uwezo katika kukuza mnyororo wa thamani wa mazao ya chakula na biashara kuanzia kwenye uzalishaji hadi usambazaji kupitia bandari za Dar es Salaam, Kigoma na Mwanza. 

WFP imeweka mpango wa kushirikiana na Shirika la Reli (TRC) nchini ili kuwezesha kuwa na vituo vya ukusanyaji wa vyakula na kuwezesha usafirishaji wa vakula hivyo kwa walengwa. 

WFP kwasasa ina ofisi katika mikoa ya Dar es Salaam, Dodoma na inatarajiwa kufungua ofisi mpya mkoani Arusha.
Mazungumzo yakiendelea 

 Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Mpango wa Chakula la Umoja wa Mataifa (WFP) Bi. Sarah Gordon-Gibson akifafanua jambo wakati wa mazungumzo na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Samwel Shelukindo yaliyofanyika jijini Dodoma

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Samwel Shelukindo na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Mpango wa Chakula la Umoja wa Mataifa (WFP) Bi. Sarah Gordon-Gibson katika picha ya pamoja

Picha ya pamoja











Tuesday, August 29, 2023

TANZANIA INATHAMINI MCHANGO WA ASASI ZA KIRAIA

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imesema inathamini mchango wa Asasi za Kiraia katika kutekeleza mipango na sera mbalimbali za maendeleo.

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Samwel Shelukindo amebainisha hayo wakati wa uzinduzi wa Warsha ya Baraza la Umoja wa Afrika la Uchumi, Kijamii, na Utamaduni la Umoja wa Afrika (ECOSSOC) Jijini Dar es Salaam

Dkt. Shelukindo amesema kuwa Serikali ya Tanzania chini ya Uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan inathamini mchango wa Asasi za Kiraia ambazo hushiriki kwa kiasi kikubwa katika kutekeleza  shughuli mbalimbali zinazofanywa na Serikali. Hivyo, ni vyema kuwa na asasi za kiraia zenye ubora ambazo zitaleta mchango chanya katika maendeleo.

“Serikali imekuwa ikipanga Mipango na Sera za maendeleo ambayo utekelezaji wake hufanywa na wadau mbalimbali ikiwemo Asasi za Kiraia. 

Hivyo, utekelezaji wa sera na mipango hiyo inahitaji asasi za kiraia zenye ubora,” alisema Balozi Shelukindo

“Nimeona mada mbalimbali katika Warsha ya leo ambazo zinazungumzia masuala mengi, ikiwemo misingi ya kidemokrasia, haki za binadamu, utawala bora na vitu vya msingi katika kukuza uchumi wa nchi yetu ambapo vitu vyote vinakwenda sambamba,” aliongeza Dkt. Shelukindo.

Kwa upande wake, Balozi wa Tanzania Nchini Ethiopia na Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Afrika (AU), Balozi Innocent Shiyo amesema Warsha hiyo ni muhimu ambapo mwaka 2002, uliokuwa Umoja wa Nchi Huru za Afrika (OAU) uliibadilishwa na kugeuzwa kuwa Umoja wa Afrika. Lengo la hayo ilikuwa ni kuongeza ushiriki wa wananchi kwenye shughuli za Umoja wa Afrika. Ili kufikia azma hiyo, mwaka 2004, Umoja wa Afrika ulipitisha Mkataba wa kuanzisha Baraza la Uchumi, Kijamii na Kitamaduni (ECOSOCC).

“Baraza la Uchumi, Kijamii na Kitamaduni linatoa fursa kwa asasi za kiraia zilizopo Barani Afrika kushiriki kwenye shughuli za Umoja wa Afrika kwa kutoa ushauri kwenye Vyombo vya Kisera vya Umoja wa Afrika na kuwaelimisha pia wananchi kuhusu mipango na mikakati mbalimbali ya Umoja wa Afrika ili kurahisha utekelezaji wake,” alisema Balozi Shiyo.

Balozi Shiyo aliongeza kuwa utendaji kazi wa Baraza la Uchumi, Kijamii na Kitamaduni la Umoja wa Afrika hufanyika katika ngazi ya Kanda, ambapo kila nchi inawakilishwa kwenye Kamati Tendaji (Permanent General Assembly). Sambamba na hilo, kila nchi ina jukumu la kuanzisha Jukwaa la Kitaifa (ECOSOCC National Chapters) ili kuhamasisha asasi nyingi zaidi za kiraia kushiriki kwenye masuala ya Umoja wa Afrika.

“Lengo la warsha ni kuhamasisha na kuongeza uelewa na kuzijengea uwezo wa Asasi za Kiraia za Tanzania kushiriki kwenye shughuli za Umoja wa Afrika. Pamoja na Mambo mengine, Warsha hii itasaidia kuongeza ushiriki na uelewa wa Asasi za Kiraia na Watanzania kwa ujumla kuhusu shughuli mbalimbali zinazofanywa na Umoja wa Afrika,” aliongeza Balozi Shiyo. 

Naye Mkuu wa Mkuu wa Sekretarieti ya ECOSOCC, Bw. William Carew amesema kuwa ECOSOCC itasaidia kuimarisha zaidi ushirikiano kati ya Umoja wa Afrika (AU) na Asasi za Kiraia nchini Tanzania. Hivyo kutoa fursa ya jukwaa la ushirikishwaji katika kutafuta Afrika bora.

“lengo letu kama ECOSOCC ni kusaidia kuimarisha ushirikiano kati ya Umoja wa Afrika (AU) na Asasi za Kiraia Tanzania na bara la Afrika kwa ujumla,” alisema Br. Carew.  

Tanzania ni miongoni mwa nchi ya tano za awali kuanzisha majukwaa ya kitaifa ya Ecosocc ili kuwa karibu na asasi za kiraia kwa lengo la kuhamasisha maendeleo nchini pamoja na kufikia malengo ya Ajenda ya 2063 inayohusu masuala mbalimbali ikiwemo elimu, afya na demokrasia. Mbali na Tanzania, nchi nyingine ni Mauritius, Sierra Leone, Zambia na Misri.

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Samwel Shelukindo akizungumza wakati wa uzinduzi wa Warsha ya Baraza la Umoja wa Afrika la Uchumi, Kijamii, na Utamaduni la Umoja wa Afrika (ECOSSOC) Jijini Dar es Salaam

Balozi wa Tanzania Nchini Ethiopia na Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Afrika (AU), Balozi Innocent Shiyo akizungumza wakati wa uzinduzi wa Warsha ya Baraza la Umoja wa Afrika la Uchumi, Kijamii, na Utamaduni la Umoja wa Afrika (ECOSSOC) Jijini Dar es Salaam

Mkuu wa Mkuu wa Sekretarieti ya ECOSOCC, Bw. William Carew akieleza jambo wakati wa uzinduzi wa Warsha ya Baraza la Umoja wa Afrika la Uchumi, Kijamii, na Utamaduni la Umoja wa Afrika (ECOSSOC) Jijini Dar es Salaam

Sehemu ya Washiriki wakifuatilia Warsha ya Baraza la Umoja wa Afrika la Uchumi, Kijamii, na Utamaduni la Umoja wa Afrika (ECOSSOC) Jijini Dar es Salaam

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Samwel Shelukindo na Balozi wa Tanzania Nchini Ethiopia na Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Afrika (AU), Balozi Innocent Shiyo katika picha ya pamoja Washiriki wa Warsha ya Baraza la Umoja wa Afrika la Uchumi, Kijamii, na Utamaduni la Umoja wa Afrika (ECOSSOC) Jijini Dar es Salaam


Monday, August 28, 2023

UBALOZI WA TANZANIA NCHINI NAMIBIA WASHIRIKI MAONESHO YA MWAKA YA KIBIASHARA YA ONGWEDIVA

Mkuu wa Utawala katika Ubalozi wa Tanzania nchini Namibia, Bi. Upendo Mwasha (kushoto) akimwonesha mteja vazi aina ya batiki kutoka Tanzania wakati wa Maonesho ya Mwaka ya Kibiashara ya Ongwediva ambayo yanafanyika nchini humo kuanzia tarehe 27 Agosti, 2023. Maonesho hayo ambayo yalifunguliwa rasmi na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara wa Namibia, Mhe. Verna Sinimbo yamewashirikisha Wajasiriamali kutoka Tanzania na Diaspora wanaoishi nchini Namibia. Mbali na kuonesha bidhaa mbalimbali za Tanzania, Ubalozi  umetumia maonesho hayo kutangaza Lugha ya Kiswahili kwa kuweka vitabu vya kiswahili katika Banda la Ubalozi na kuhamasisha wateja kusoma na kujifunza Lugha hiyo kupitia Ubalozi ambao umeanzisha Maktaba ya Kiswahili.  
Wadau mbalimbali wakitembelea Banda la Tanzania kwenye maonesho hayo

Baadhi ya Wajasiriamali wa Tanzania wakishiriki maonesho ya Mwaka ya Kibiashara ya Ongwediva yanayofayika nchini Namibia

Banda la Tanzania kama linavyoonekana pichani. Bidhaa mbalimbali kutoka Tanzania zinazooneshwa kwenye maonesho hayo ikiwa ni pamoja na nguo za batiki, vikapu, viatu vya asili, shanga, kahawa na majani ya chai.



Sunday, August 27, 2023

DKT. TAX AWAPA WAKUU WA MIKOA MBINU ZA KUTEKELEZA DIPLOMASIA YA UCHUMI

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb.) amewapa Wakuu wa Mikoa mbinu mbalimbali za kutekeleza Diplomasia ya Uchumi katika Mikoa yao.

Dkt. Tax ametoa mbinu hizo tarehe 26 Agosti, 2023 wakati wa Mafunzo ya Uongozi kwa Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa yanayofanyika katika Shule ya Uongozi ya Mwalimu Nyerere iliyopo Kibaha mkoani Pwani.

“Mbinu za kuibua na kutekeleza diplomasia ya uchumi ni nyingi kama vile kufungua balozi, kukusanya taarifa na uchambuzi, majadiliano,……………….lakini kwenu nyie Wakuu wa Mikoa mnaweza kufanya makongamano ya biashara na uwekezaji na kuzitangaza fursa mbailmbali za biashara katika mikoa yenu pamoja na elimu kwa Umma,” alisema Dkt. Tax.

“Kupitia mikoa yenu mnaweza mkafanya makongamano ya biashara na uwekezaji na kuzitangaza fursa za biashara katika mikoa yenu, ninyi ni wadau wakubwa wa kutekeleza diplomasia ya uchumi kwa vitendo na kuchangia maendeleo,” alisema Dkt. Tax

Alisema kuwa Serikali itaendelea kuboresha  mifumo ya sheiria, kiutendaji na kukuza mazingira ya kushindana Kimataifa na Ofisi za Wakuu wa Mikoa zina mchango mkubwa kufanikisha utekelezaji wa Diplomasia ya Uchumi na hivyo kuchangia maendeleo ya kiuchumi nchini.

“Serikali itaendelea kuboresha mifumo ya kisheria, kiutendaji na kukuza mazingira wezeshi kushindana kimataifa ambapo ofisi za wakuu wa Mikoa zina nafasi na mchango mkubwa wa kufanikisha utekelezaji wa Diplomasia ya uchumi, na kuchangia kasi ya maendeleo nchini,” alisema Dkt. Tax. 

Waziri Tax aliongeza kuwa Wakuu wa Mikoa ni wadau wakubwa katika kutekeleza diplomasia ya uchumi kwenye mikoa yao kwani huibua fursa mbalimbali za biashara na uwekezaji zinazopatikana katika mikoa yao.

Pamoja na mambo mengine Waziri Tax aliongeza kuwa ofisi za Wakuu wa Mikoa ni wadau muhimu na wanalo jukumu la kibua fursa katika maeneo yao kama Mamlaka za msingi zinazobuni mipango ya biashara, miradi ya uwekezaji, uzalishaji, na utumiaji wa rasilimali katika ngazi ya mikoa.

Mafunzo ya Uongozi kwa Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa katika Shule ya Uongozi ya Mwalimu Nyerere, Kibaha mkoani Pwani yalianza tarehe 21 – 28 Agosti, 2023.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax akiwaeleza Wakuu wa Mikoa (hawapo pichani) mbinu za kutekeleza Diplomasia ya Uchumi katika mikoa yao.  Dkt. Tax ametoa mbinu hizo tarehe 26 Agosti, 2023 wakati wa Mafunzo ya Uongozi kwa Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa yanayofanyika katika Shule ya Uongozi ya Mwalimu Nyerere iliyopo Kibaha mkoani Pwani.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax akiwaeleza Wakuu wa Mikoa (hawapo pichani) mbinu za kutekeleza Diplomasia ya Uchumi katika mikoa yao.  Dkt. Tax ametoa mbinu hizo tarehe 26 Agosti, 2023 wakati wa Mafunzo ya Uongozi kwa Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa yanayofanyika katika Shule ya Uongozi ya Mwalimu Nyerere iliyopo Kibaha mkoani Pwani.



Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax akiwaeleza Wakuu wa Mikoa mbinu za kutekeleza Diplomasia ya Uchumi katika mikoa yao.  Dkt. Tax ametoa mbinu hizo tarehe 26 Agosti, 2023 wakati wa Mafunzo ya Uongozi kwa Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa yanayofanyika katika Shule ya Uongozi ya Mwalimu Nyerere iliyopo Kibaha mkoani Pwani.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax akiwaeleza Wakuu wa Mikoa mbinu za kutekeleza Diplomasia ya Uchumi katika mikoa yao.  Dkt. Tax ametoa mbinu hizo tarehe 26 Agosti, 2023 wakati wa Mafunzo ya Uongozi kwa Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa yanayofanyika katika Shule ya Uongozi ya Mwalimu Nyerere iliyopo Kibaha mkoani Pwani.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax akiwaeleza Wakuu wa Mikoa mbinu za kutekeleza Diplomasia ya Uchumi katika mikoa yao.  Dkt. Tax ametoa mbinu hizo tarehe 26 Agosti, 2023 wakati wa Mafunzo ya Uongozi kwa Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa yanayofanyika katika Shule ya Uongozi ya Mwalimu Nyerere iliyopo Kibaha mkoani Pwani.

Sehemu ya Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa wakifuatilia mafunzo katika Shule ya Uongozi ya Mwalimu Nyerere iliyopo Kibaha mkoani Pwani



Wednesday, August 23, 2023

TANZANIA NA CUBA KUIMARISHA MISINGI YA KISIASA

Tanzania na Cuba zimekubaliana kushirikiana na kuimarisha misingi ya kisiasa, ujengaji wa uwezo kwa wanasiasa vijana, sekta za elimu, afya, utalii, biashara na uwekezaji 

Hayo yamebainishwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk (Mb.) alipokutana na kuzungumza na Balozi wa Cuba nchini, Mhe. Yordenis Despaigne Vera katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.

“Tanzania imekuwa ikishirikiana na Cuba kwa muda mrefu na ushirikiano baina ya mataifa haya umekuwa imara tangu ulipooasisiwa na viongozi wakuu wa Mataifa hayo Hayati Fidel Castro na Hayati Baba wa Taifa  Mwalimu Julius Kambarage Nyerere,” alisema Balozi Mbarouk.

Balozi Mbarouk ameongeza kuwa kwa sasa Cuba imeonesha dhamira ya kushirikiana Tanzania katika kuimarisha misingi ya siasa, kuwajengea uwezo wanasiasa vijana pamoja na sekta nyingine kama vile elimu, afya, na utalii pamoja na kuimarisha ushirikiano kwenye sekta ya biashara na uwekezaji 

Kwa upande wake Balozi wa Cuba nchini, Mhe. Yordenis Despaigne Vera amesema kwamba Cuba inajivunia kuwa na uhusiano imara na Tanzania kwa takribani miaka 60. 

Cuba itaendelea kushirikiana na Tanzania kuimarisha misingi ya kisiasa kwa manufaa ya wananchi wa pande zote mbili. “Wakati umefika sasa kwa serikali zetu mbili (Cuba na Tanzania) kuimarisha ushirikiano wake kisiasa na kuhakikisha kuwa mataifa yetu yanakuwa na misingi imara ya kisiasa, kijamii, na kiuchumi pia kwa manufaa ya pande zote mbili,” alisema Balozi Vera.

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk akizungumza na Balozi wa Cuba nchini, Mhe. Yordenis Despaigne Vera walipokutana kwa mazungumzo katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk akizungumza na Balozi wa Cuba nchini, Mhe. Yordenis Despaigne Vera walipokutana kwa mazungumzo katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk katika picha ya pamoja na Balozi wa Cuba nchini, Mhe. Yordenis Despaigne Vera baada ya kumaliza mazungumzo yao  katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk katika picha ya pamoja na Balozi wa Cuba nchini, Mhe. Yordenis Despaigne Vera pamoja na maafisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Ubalozi wa Cuba



Tuesday, August 22, 2023

TANZANIA, INDONESIA KUIMARISHA USHIRIKIANO

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Jamhuri ya Indonesia zimekubaliana kuimarisha ushirikiano katika sekta za biashara na uwekezaji, viwanda, kilimo, nishati, madini, mafuta na gesi pamoja na uchumi wa buluu. 

Makubaliano hayo yamefikiwa wakati wa hafla ya utiaji Saini wa Hati mbalimbali za makubaliano ya ushirikiano baina ya Serikali ya Tanzania na Serikali ya Indonesia iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam na kushuhudiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan pamoja na Rais wa Jamhuri ya Indonesia Mheshimiwa Joko Widodo.

Hati za makubaliano (MoUs) zilizosainiwa ni saba ambazo ni uanzishwaji wa Tume ya Pamoja ya Kudumu (JPC), msamaha wa visa kwa wamiliki wa hati za kusafiria za Kidiplomasia, Huduma za Afya, nishati, mafuta na gesi mapoja na madini. 

Mara baada ya kusainiwa kwa Hati hizo za makubaliano, Marais wote wawili waliongea na vyombo vya Habari ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia alisema kuwa chimbuko la uhusiano kati ya Tanzania na Indonesia ni Mkutano wa Bandung uliofanyika mwaka 1955 ambapo nchi nyingi za Afrika na Asia zilikuwa katika utawala wa kikoloni kwa kipindi hicho. 

“Tanzania na Indonesia zina uhusiano wa muda mrefu na wa kihistoria. Uhusiano huo uliasisiwa na Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Rais wa Kwanza wa Indonesia Mheshimiwa Soekarno. Uhusiano wa kidiplomasia ulianza mwaka 1964, ambapo Indonesia ilifungua Ubalozi wake nchini mwaka 1964 na kuwa miongoni mwa nchi za mwanzo kabisa kufungua Ubalozi wake nchini miaka michache baada ya uhuru,” alisema Rais Samia.

Rais Dkt. Samia ameongeza kuwa Tanzania na Indonesia zimekubaliana kukuza biashara na uwekezaji kwa kuzileta pamoja sekta za umma na binafsi ili kuimarisha ushirikiano katika sekta za biashara na uwekezaji, viwanda, kilimo, nishati, madini, mafuta na gesi, uvuvi na utalii pamoja na uchumi wa buluu.

Kadhalika, Mhe. Rais Samia amesema majadiliano baina yake na mgeni wake pamoja na mambo mengine, wamebainisha nia ya Tanzania kupata uzoefu wa uzalishaji mafuta ya mawese kutoka kwa Indonesia ambapo imekuwa mzalishaji mkubwa zaidi wa mafuta ya mawese duniani.

Kwa upande wake Rais wa Jamhuri ya Indonesia, Mheshimiwa Joko Widodo amesema kuwa Indonesia itaendelea kushirikiana na Tanzania na kuhakikisha uhusiano wa kidiplomasia uliopo baina ya mataifa hayo unazidi kuimarika zaidi.

“Indonesia itaendelea kushirikiana na Tanzania katika sekta mbalimbali hususan sekta ya afya ambapo tumekusudia kuanzisha kiwanda cha dawa na vifaa tiba nchini Tanzania kwa maslahi ya pande zote,” alisema Mhe. Widodo

Rais Widodo ameongeza kuwa Indonesia imekubaliana na Tanzania katika kuboresha kilimo na kukifanya kuwa cha kisasa na chenye tija. “Indonesia itaendelea kuboresha Kituo cha Mafunzo ya Kilimo kwa Wakulima Vijijini (FARTC) kilichopo Mkindo – Morogoro na kuwawezesha wakulima wengi nchini Tanzania kulima kisasa zaidi,” aliongeza Rais Widodo.

Rais Widodo aliwasili nchini tarehe 21 Agosti 2023 kwa ziara ya Kitaifa ya siku mbili na amehitimisha ziara yake leo tarehe 22 Agosti 2023 na kureje Indonesia.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) Ikulu Jijini Dar es Salaam

Rais wa Jamhuri ya Indonesia, Mhe. Joko Widodo akizungumza na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) Ikulu Jijini Dar es Salaam

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan (kulia) pamoja na Mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Indonesia, Mhe. Joko Widodo (kushoto) wakizungumza na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) Ikulu Jijini Dar es Salaam

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje wa Indonesia, Mhe. Retno Marsudi wakisaini Hati za Makubaliano (MoUs) kati ya Tanzania na Indonesia. Kati ya MoUs saba zilizosainiwa viongozi hao wawili wamesaini Hati za uanzishwaji wa Tume ya Pamoja ya Kudumu (JPC), msamaha wa visa kwa wamiliki wa hati za kusafiria za Kidiplomasia pamoja Huduma za Afya.