Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Samwel Shelukindo amewataka watumishi wa Wizara hiyo kufanya kazi kwa maarifa, ubunifu na kitimu ili kutimiza azma ya Serikali ya awamu ya sita ya kuimarisha diplomasia ya uchumi.
Balozi Dkt. Shelukindo ametoa rai hiyo Agosti, 30, 2023 jijini Dodoma w
Balozi Shelukindo alisisitiza umuhimu wa watumishi kuboresha maarifa yao kila mara kwa kusoma vitabu ili wawe na ujuzi na mbinu za kutosha za kutekeleza majukumu yanayowakabili ambayo yanabadilika kulingana na wakati na teknolojia.
Dkt. Shelukindo aliwahimiza watumishi hao ambayo Wizara wanayoitumikia ni mtambuka kuhakikisha wanafuatilia utekelezaji wa makubaliano ambayo nchi imesaini na nchi nyingine kutoka kwa wadau wote ili iweze kufaidika na makubaliano hayo.
“Tuwe wepesi kujibu wadau wetu tanaofanya nao kazi na kuhakikisha tunatoa huduma bora kwa wateja wa Wizara, huku tukizingatia ufanisi na hatimaye kuleta tija kwa nchi”, Balozi Shelukindo alisisitiza.
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Samwel Shelukindo akifuatilia kikao cha watumishi wa Wizara kilichokuwa kikiendelea |
Mkurugenzi wa Idara ya Siasa, Ulinzi na Usalama na Kaimu Naibu Katibu Mkuu Balozi Stephen P. Mbundi akifuatilia kikao cha watumishi wa Wizara kilichokuwa kikiendelea |
Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi Rasilimali Watu Bi. Chiku Kiguhe akifafanua jambo kwenye kikao cha watumishi wa Wizara kilichofanyika kwenye jijini Dodoma. |
Sehemu ya Menejimenti ya Wizara wakifuatilia kikao kilichokuwa kikiendelea
Watumishi wa Wizara wakifuatilia kikao
Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi Rasilimali Watu Bi. Chiku Kiguhe akifuatilia kikoa cha Watumishi kilichokuwa kikiendelea |
Picha ya pamoja Meza Kuu na Menejimenti ya Wizara
Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika Balozi Swahiba Mndeme akizungumza kwenye kikao cha Watumishi wa Wizara kilichofanyika jijini Dodoma |
Sehemu ya Watumishi wakifuatilia kikao |
Kikao kikiendelea |
Sehemu ya Menejimenti ya Wizara wakifuatilia kikao kilichokuwa kikiendelea |
Sehemu ya Menejimenti ya Wizara wakifuatilia kikao cha watumishi wa Wizara kilichokuwa kikiendelea |
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.