Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax amefanya mazungumzo na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Algeria, Mhe. Brahim Boughali alipomtembelea katika Ofisi za Bunge tarehe 2 Agosti 2023 jijini Algiers, Algeria.
Katika mazungumzo yao Waziri Tax alieleza kuwa uhusiano kati ya Tanzania na Algeria ni wa kirafiki na kindugu tangu enzi za kupigania ukombozi wa bara la Afrika.
Pia kupitia ziara yake ya kikazi nchini humo pamoja na kuhuishwa kwa maeneo ya ushirikiano katika Mkutano wa Tano wa Tume ya Pamoja ya Kudumu ya Ushirikiano (JPC) kati ya Tanzania na Algeria ni wazi kwamba nchi zetu zimejidhatiti kupiga hatua za kimaendeleo katika ushirikiano uliopo.
‘’Kuhitimishwa kwa mkutano wa JPC kwa mafanikio ni hatua muhimu katika kuendelea kuimarisha ushirikiano wetu kwenye sekta za kiuchumi kwa maslahi ya pande zote’’ alisema Dkt. Tax.
Naye Spika wa Bunge la Algeria, Mhe. Brahim Boughali ameeleza kuwa Serikali ya Algeria ipo tayari kushirikiana katika masuala mbalimbali ya kibunge ili kwa pamoja tuweza kutatua changamoto mbalimbali zinazoendelea duniani.
‘’ Ni vema Bunge la Tanzania na la Algeria tukajenga mfumo rasmi wa ushirikiano ili kuweka utaratibu rasmi wa kushirikishana katika masuala mbalimbali ya kitaifa, kikanda na dunia kwa ujumla,’’ alisema Mhe. Boughali.
Aidha, Mhe. Spika Boughali amemhakikishia Mhe. Waziri Tax kuwa kwenye Kikao cha Bunge la Algeria la mwezi Septemba, suala la ushirikiano na Tanzania litakuwa ni moja ya eneo la Kipaumbele katika mijadala ya Bunge hilo.
===================================
Mazungumzo yakiendelea. |
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Stergomena Tax akiwasili katika Ofisi za Bunge la Algeria jijini Algiers. |
Picha ya pamoja |
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.