Tuesday, October 22, 2024

MHE. PINDA AZINDUA MISHENI YA UANGALIZI WA UCHAGUZI YA JUMUIYA YA MAENDELEO YA KUSINI MWA AFRIKA (SEOM) JIJINI GABORONE

 







 

 

 

Mkuu wa Misheni ya Uangalizi wa Uchaguzi ya SADC (SEOM) katika Uchaguzi Mkuu wa Botswana, Mhe. Mizengo Pinda, amezindua misheni hiyo kwa niaba ya Mwenyekiti wa Baraza la SADC la Siasa, Ulinzi na Usalama na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, jijini Gaborone, Botswana.

 

Akizungumza katika uzinduzi huo Mhe. Pinda aliwasihi wapiga kura wa Botswana kujitokeza kwa kwa wingi kupiga kura tarehe 30 Oktoba 2024, kufanya mamuzi sahihi, kuheshimu mitazamo tofauti ya kisiasa na kuwajibikaji katika kipindi cha baada ya uchaguzi, bila kujali chama au mgombea anayependwa na atakayechaguliwa na wananchi wengi.

 

“Katika siku zilizobaki kuelekea siku hii muhimu kwenu, SADC inawasihi wote kujitokeza kwa wingi, kufanya maamuzi sahihi, kuheshimu mitazamo tofauti ya kisiasa, na kuwajibika katika kipindi cha baada ya uchaguzi, bila kujali chama au mgombea anayependwa atakayechaguliwa na wananchi,” alisema Mhe. Pinda.

 

Alisema SEOM inatekeleza jukumu la uangalizi wa uchaguzi katika nchi wanachama, kwa kuzingatia misingi na miongozo ya SADC ya uchaguzi wa Kidemokrasia, ambayo Nchi Wanachama wa SADC waliridhia kutekeleza.

 

Mhe. Pinda alisema misingi na miongozo hiyo inatoa mbinu za kisayansi na za kimantiki za kuangalia uchaguzi ili kuchangia katika kuimarisha demokrasia katika ukanda huo kwa kuboresha mbinu bora za uchaguzi na kushughulikia kasoro zozote za uchaguzi na kuongeza kuwa misingi na miongozo hiyo pia inategemea nyaraka muhimu za Umoja wa Afrika (AU), kama vile Mkataba wa Afrika wa Demokrasia, Uchaguzi, na Utawala wa mwaka 2007, pamoja na Mikataba husika ya Umoja wa Mataifa (UN).

 

Alifafanua kuwa kwa kufuata masharti ya misingi na miongozo ya SADC inayohusiana na uchaguzi wa kidemokrasia ya mwaka 2021 na mifumo, kanuni, na taratibu za SEAC, Baraza la Ushauri wa Uchaguzi la SADC (SEAC) lilifanya tathmini ya awali ya uwezo wa uchaguzi nchini Botswana tarehe 22 hadi 29 Aprili 2024.

 

Alisema lengo la misheni hiyo lilikuwa kutathmini kama mazingira ya kisiasa na usalama nchini Botswana yanaruhusu kufanyika kwa uchaguzi kwa kufuata kanuni na miongozo, mfumo wa kisheria unaoshughulikia uchaguzi uko katika nafasi, mipaka ya majimbo ilitekelezwa kwa mujibu wa sheria ya nchi, na kama Tume Huru ya Uchaguzi (IEC) ya Botswana iko tayari kufanya uchaguzi wa kidemokrasia.

 

Aliongeza kuwa wakati huo, misheni hiyo ilifanya mazungumzo na wadau kutoka katika sehemu mbalimbali nchini Botswana, ikiwemo vyama vya siasa, mashirika ya kiraia, wataalamu wa uchaguzi, mashirika ya dini, na jumuiya ya kidiplomasia.

 

Alisema jukumu la SEOM ni kuangalia kama Nchi Wanachama wanafanya uchaguzi kwa kuzingatia Misingi na Miongozo ya SADC iliyorekebishwa mwaka 2021.

“Tupo hapa kusaidiana kuboresha ubora wa chaguzi zetu na ubora wa harakati zetu za muda mrefu kwa ajili ya uhuru na demokrasia.”

 

Mhe. Pinda alisema SEOM itatoa taarifa yake ya awali kuhusu uchaguzi wa Botswana tarehe Mosi Novemba 2024, na ripoti ya mwisho itawasilishwa kwa Serikali ya Jamhuri ya Botswana siku 30 baada ya uchaguzi.

 

Naye Katibu Mtendaji wa SADC, Mhe. Elias Magosi, alisema ndoto ya kubadilisha kanda ya SADC kuwa kanda iliyoungana kikamilifu yenye kuhifadhi ustawi kwa wote inategemea uwezo wake wa kudumisha demokrasia, utawala bora, amani na utulivu na ndoto hiyo itakamilika pale Nchi Wanachama zitakapozingatia na kutekeleza mapendekezo ya SEOM kikamilifu.

 

“Uzingatiaji wa Misingi na Miongozo ya SADC unatarajiwa kuziinua Nchi Mwanachama wa SADC na utafanya kanda hii kufikia Mpango wa Maendeleo wa Kistratejia wa Kanda (RISDP), Dira ya SADC 2050 na Ajenda pana ya Umoja wa Afrika ya 2063 kuhusu Afrika tunayotaka, bila kuacha Nchi Mwanachama au mtu yeyote nyuma,” alisisitiza.

 

Alisema SADC inaendelea kuzihimiza Nchi Wanachama kufikiria utekelezaji wa mapendekezo yanayotolewa na misheni mbalimbali za uchaguzi (SEOMs) na kuongeza kuwa SEOM hutoa mapendekezo yake baada ya kuzingatia ripoti za waangalizi wake na mitazamo ya wadau mbalimbali wanaoshirikiana nao katika nchi zinazofanya chaguzi.

 

Aliongeza kuwa utekelezaji wa mapendekezo ya SEOM utachangia na kukuza demokrasia kwa Nchi Wanachama, kuhakikisha utawala bora na kuimarisha imani ya wananchi na wadau wa nje na kusisitiza kuwa uangalizi wa uchaguzi, ambao una gharama kubwa, unafaida na ni kitu cha thamani, na si kitu tu cha kutimiza wajibu na safari rahisi kwa waangalizi.

 

Hafla hiyo ya uzinduzi ilihudhuriwa na Baraza la Ushauri wa Uchaguzi la SADC, Wawakilishi wa Serikali ya Botswana, Jumuiya ya wanadiplomasia waliyopo Botswana, Tume Huru ya Uchaguzi ya Botswana (IEC), vyama vya kisiasa, viongozi wa dini, mashirika yasiyo ya kiserikali, vyombo vya Habari na wanahabari, waangalizi wa uchaguzi wa ndani, waangalizi wa kimataifa, vyama vya kiraia na waangalizi wa SADC.

 

SEOM inajumuisha wajumbe 72, kutoka nchi wanachama wa Troika na SEAC, Wajumbe wa Sekretarieti ya SADC, waangalizi wa SEOM ambao wametoka katika Nchi 10 Wanachama wa SADC za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Falme ya Eswatini, Falme ya Lesotho, Jamhuri ya Malawi, Jamhuri ya Msumbiji, Jamhuri  ya Namibia, Jamhuri ya Afrika Kusini, Jamhuri ya Zambia na Jamhuri ya Zimbabwe ambao watakwenda katika wilaya zote, miji, na majiji makubwa ya Jamhuri ya Botswana.

 

 

 

 


MHESHIMIWA PINDA AKUTANA NA KATIBU MTENDAJI WA SADC JIJINI GABORONE

 

 

Mkuu wa Missoni ya Uangalizi wa Uchaguzi ya Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Africa (SADC-SEOM) Mhe. Mizengo Pinda (kulia)  akisalimiana na Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) Mhe. Elias Magosi walipokutana jijini Gaborone, Botswana, kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Said Shaib Mussa.

Mkuu wa Missoni ya Uangalizi wa Uchaguzi ya Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Africa (SADC-SEOM) Mhe. Mizengo Pinda na Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) Mhe. Elias Magosi katika mazungumzo walipokutana jijini Gaborone, Botswana

Mkuu wa Missoni ya Uangalizi wa Uchaguzi ya Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Africa (SADC-SEOM) Mhe. Mizengo Pinda na Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) Mhe. Elias Magosi katika picha walipokutana jijini Gaborone, Botswana

Mkuu wa Missoni ya Uangalizi wa Uchaguzi ya Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Africa (SADC-SEOM) Mheshimiwa Mizengo Pinda, amekutana na kuzungumza na Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) Mhe. Elias Magosi jijini Gaborone , Botswana








MHE. PINDA AKUTANA NA VIONGOZI WA SERIKALI YA BOTSWANA JIJINI GABORONE

Mkuu wa Misheni ya Uangalizi wa Uchaguzi ya Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC-SEOM) Mhe. Mizengo Pinda, akisalimiana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mhe. Kabo Morwaeng  alipotembelea Ofisi ya Rais wa Botswana jijini Gaborone.
Mkuu wa Misheni ya Uangalizi wa Uchaguzi ya Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC-SEOM) Mhe. Mizengo Pinda, (kulia) akizungumza na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mhe. Kabo Morwaeng na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Botswana Mhe. Dkt. Lemongang Kwape hawapo pichani alipotembelea Ofisi ya Rais wa Botswana jijini Gaborone.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mhe. Kabo Morwaeng na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Botswana Mhe. Dkt. Lemongang Kwape (kulia) akizungumza na Mkuu wa Misheni ya Uangalizi wa Uchaguzi ya Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC-SEOM) Mhe. Mizengo Pinda, (wa pili kulia)  alipoembelea Ofisi ya Rais wa Botswana jijini Gaborone.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mhe. Kabo Morwaeng (kushoto) na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Botswana Mhe. Dkt. Lemongang Kwape (wa pili kushoto) na ujumbe wao wakizungumza na Mkuu wa Misheni ya Uangalizi wa Uchaguzi ya Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC-SEOM) Mhe. Mizengo Pinda, (kulia) na ujumbe wake hawapo pichani alipotembelea Ofisi ya Rais wa Botswana jijini Gaborone


ujumbe wa SEOM ukifuatilia mazungumzo

Mazungumzo yakiendelea
 



Mkuu wa Misheni ya Uangalizi wa Uchaguzi ya Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC-SEOM) Mhe. Mizengo Pinda, amekutana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mhe. Kabo Morwaeng na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Botswana Mhe. Dkt. Lemongang Kwape alipotembelea Ofisi ya Rais wa Botswana jijini Gaborone.

Mhe. Pinda amekutana na viongozi hao kwa lengo la kujitambulisha kama Mkuu wa Misheni ya SADC na kuwatambulisha wajumbe wa misheni hiyo ambao wako nchini Botswana kwa ajili ya Uangalizi wa Uchaguzi Mkuu wa nchi hiyo uliopangwa kufanyika tarehe 30 Oktoba, 2024.

Mhe.Pinda aliambatana na  Sekretarieti ya SADC, wajumbe wa SADC Organ TROIKA, Baraza la Ushauri wa Uchaguzi la SADC, na Waangalizi wa SADC.

Mhe. Pinda aliwaambia wenyeji wake kwamba SEOM ipo Botswana tayari kwa kutekeleza wajibu wao kwa ufanisi.

Mhe. Pinda aliisifu Botswana kwa maendeleo makubwa ya kiuchumi pamoja na amani na usalama vilivyopo nchini humo, ambavyo vinaifanya Botswana kuwa bora zaidi.

Pia aliwapongeza kwa kuwa wazalishaji wakubwa wa  madini ya almasi na kusaidia watu kutumia madini hayo halisi badala ya almasi bandia.

Kadhalika, aliwaambia wafikirie kuanzisha uzalishaji wa asali na bidhaa zake, kwani wana misitu katika nchi yao ambayo wanaweza kuitumia kama biashara kwa wakulima wao ili wapate kipato.

Akizungumza kwenye kikao hicho, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Mhe. Kabo Morwaeng, aliikaribisha SEOM nchini Botswana na kumhakikishia kwamba Serikali ya Botswana iko tayari kufanya kazi nao na imejipanga vizuri  kuhakikisha uchaguzi mkuu unafanyika kwa amani na utulivu

“Karibuni Botswana, hii ni nchi ya amani, na tumejipanga kuhakikisha uchaguzi mkuu unakuwa huru na wa haki kwa kila anayeshiriki,” alisisitiza.

Alisema Serikali ya Botswana imejiandaa kwa uchaguzi mkuu na kwamba wako tayari kwa uchaguzi na kuihakikishia SEOM kwamba uchaguzi utakuwa huru na wa haki na kuendelea kudumisha amani na usalama katika nchi yao.

Akizungumza kwenye mkutano, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Botswana, Dkt. Lemongang Kwape, aliahidi kwamba Botswana itafanya Uchaguzi wake kwa amani na itaendelea kushirikiana na wanachama wengine wa SADC kwa manufaa ya wote.

MKUU WA MISHENI YA UANGALIZI UCHAGUZI YA SADC AKUTANA NA UONGOZI WA JESHI LA POLISI BOTSWANA


Mkuu wa Misheni ya Uangalizi wa Uchaguzi ya Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC-SEOM) Mhe. Mizengo Pinda na ujumbe wake wakizungumza na Uongozi wa Jeshi la Polisi  nchini Botswana walipotembelea Makao Makuu ya Jeshi hilo jijini Gaborone kwa ajili ya kujitambulisha .

 

Mkuu wa Misheni ya Uangalizi wa Uchaguzi ya Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC-SEOM) Mhe. Mizengo Pinda (katikati) akimsikiliza Kiongozi wa Jeshi la Polisi nchini Botswana alipotembelea Makao Makuu ya Jeshi hilo jijini Gaborone kwa ajili ya kujitambulisha .

 

Kamishna wa Polisi nchini Botswana bi. Dinah Marathe (kushoto) akizungumza na Mkuu wa Misheni ya Uangalizi wa Uchaguzi ya Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC-SEOM) Mhe. Mizengo Pinda na ujumbe wake walipotembelea Makao Makuu ya Polisi  jijini Gaborone kwa ajili ya kujitambulisha .


Maafisa wa Polisi wa Botswana wakimsikiliza Mkuu wa Misheni ya Uangalizi wa Uchaguzi ya Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC-SEOM) Mhe. Mizengo Pinda na ujumbe (hawako katika picha)

 

 

Mkuu wa Misheni ya Uangalizi wa Uchaguzi ya Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC-SEOM) Mhe. Mizengo Pinda, amekutana na kuzungumza na uongozi wa Jeshi la Polisi nchini Botswana alipotembelea Makao Makuu ya Jeshi hilo jijini Gaborone.


Mhe. Pinda a
likwenda katika ofisi hizo kwa ajili ya kujitambulisha pamoja na ujumbe wake ambako alikutana na kuzungumza na Kamishna wa Polisi wa Botswana Bi. Dinah Marathe.

 

Mhe. Pinda na ujumbe wake walitembelea Ofisi za Jeshi la Polisi kwa lengo la kujitambulisha kama Mkuu wa Misheni ya uangalizi ya SADC na ujumbe wa misheni hiyo ambao wako nchini Botswana kwa ajili ya kazi ya Uangalizi wa Uchaguzi Mkuu  uliopangwa kufanyika tarehe 30 Oktoba, 2024.

Mhe.Pinda aliambatana na Sekretarieti ya SADC, wajumbe wa SADC Organ TROIKA, Baraza la Ushauri wa Uchaguzi la SADC, na Waangalizi wa SADC.

Mhe. Pinda aliwaambia
maafisa hao wa Polisi kuwa SEOM ipo nchini Botswana kwa ajili ya kutekeleza jukumu la uangalizi katika uchaguzi huo ambalo wamekabidhiwa na SADC ikiwa ni sehemu ya kukuza na kuimarisha demokrasia katika nchi za ukanda huo.


Mhe. Pinda ali
elezea jinsi  SEOM ilivyojipanga kutekeleza jukumu hilo ambapo wametoa mafunzo kwa waangalizi wao ili wajue taratibu na miongozo ya kufuata wakati wa kutekeleza jukumu hilo.

 

ziara hiyo ya Mhe. Pinda pia ililenga kufahamu jinsi Jeshi la Polisi nchini humo lilivyojipanga kuelekea kwenye uchaguzi, wakati wa uchaguzi na baada ya uchaguzi.

 

Akizungumza katika kikao hicho Kamishna wa Polisi wa Botswana Bi. Marathe alimkaribisha Mkuu wa Misheni ya SEOM na ujumbe wake nchini Botswana na kumshukuru kwa kwenda kuwatembelea na kuahidi kushirikiana nao katika kutekeleza jukumu hilo muhimu kwa Jumuiya na nchi yao kwa ujumla.

 

Amesema Jeshi la Polisi la Botswana limejipanga kikamilifu kuhakikisha Uchaguzi Mkuu wa nchi hiyo unafanyika kwa amani na utulivu na nchi kuendelea kuwa na usalama. 

 

Alisema Botswana ni nchi ya amani na kwamba askari wa nchi hiyo hutembea bila silaha na kuongeza kuwa maafisa wa polisi nchini humo wako tayari kutekeleza kikamilifu majukumu yao katika kipindi chote cha uchaguzi kwa kuendelea kulinda amani,  raia na mali zao.

 

MHE. PINDA AKUTANA NA MABALOZI WA SADC WANAOWAKILISHA NCHI ZAO BOTSWANA

 

Mkuu wa Misheni ya Uangalizi wa Uchaguzi ya Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC-SEOM) Mhe. Mizengo Pinda, (katikati amekaa) akizungumza katika kikao na  Mabalozi wa SADC wanaoziwakilisha nchi zao nchini Botswana walipokutana jijini Gaborone tarehe 21 Oktoba 2024.

 

  Mabalozi wa SADC wanaoziwakilisha nci zao nchini Botswana wakimsikiliza Mkuu wa Misheni ya Uangalizi wa Uchaguzi ya Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC-SEOM) Mhe. Mizengo Pinda, (katikati amekaa) walipokutana jijini Gaborone tarehe 21 Oktoba 2024.

Mkuu wa Misheni ya Uangalizi wa Uchaguzi ya Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC-SEOM) Mhe. Mizengo Pinda, (katikati amekaa) akiwa na  Mabalozi wa SADC wanaoziwakilisha nci zao nchini Botswana walipokutana jijini Gaborone tarehe 21 Oktoba 2024.




Mkuu wa Misheni ya Uangalizi wa Uchaguzi ya Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC-SEOM) Mhe. Mizengo Pinda, (katikati) akiwa na Balozi wa Angola na Kiongozi wa mabalozi wa SADC nchini Botswana Mhe. Beatriz Morais (kulia) na Balozi wa Tanzania nchini Botswana Mhe. James Bwana (kushoto) alipokutana kuwaarifu juu ya uwepo wa misheni ya uangalizi wa SADC katika uchaguzi Mkuu wa Botswana ,  jijini Gaborone tarehe 21 Oktoba 2024.

 

 

Mkuu wa Misheni ya Uangalizi wa Uchaguzi ya Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC-SEOM) Mhe. Mizengo Pinda, (katikati amekaa) akiwa na  Mabalozi wa SADC wanaoziwakilisha nci zao nchini Botswana walipokutana jijini Gaborone tarehe 21 Oktoba 2024.

 

 

 
 

 

Mkuu wa Misheni ya Uangalizi wa Uchaguzi ya Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC-SEOM) Mhe. Mizengo Pinda, amekutana na Mabalozi kutoka nchi za SADC wanaoziwakilisha nchi zao nchini Botswana katika kikao kilichofanyika jijini Gaborone tarehe 21 Oktoba 2024.

Akizungumza katika kikao hicho Mhe. Pinda amesema amewaarifu Mabalozi hao juu ya uwepo wake kama Mkuu wa misheni ya Uangalizi ya Uchaguzi ya SADC Pamoja na waangalizi wengine kutoka nchi wanachama wa SADC.

Ameeleza kuwa amekutana nao ikiwa ni sehemu ya ratiba zake mbalimbali ili kuwasiliana nao moja kwa moja  na hivyo kusaidia waangalizi kupata picha halisi ya jinsi maandalizi ya uchaguzi huo kwa ujumla yanavyokwenda.

Amesema SEOM imejipanga na iko tayari kutekeleza jukumu lake la Uangalizi kwa ukamilifu kama walivyoaminiwa na Jumuiya na kuwatuma kuifanya kwa niaba yao.

Amesema wao kama viongozi wa SEOM watakuwa na mikutano na watu mbalimbali ikiwa ni sehemu ya kusikiliza na kupata maoni ili kuhakikisha kazi yao ya uangalizi inakwenda vizuri

Akizungumza kwa niaba ya Mabalozi hao Mkuu wa Mabalozi wa SADC nchini Botswana Mheshimiwa Beatriz Morais ameshukuru kukutana na uongozi wa SEOM na kuahidi kushirikiana nao ili  kuhakikisha kazi yao ya uangalizi inafanyika kwa mafanikio na hivyo kuleta tija na ufanisi kwa Jumuiya na nchi inayohusika.

Sunday, October 20, 2024

MHE. PINDA APOKEA TAARIFA YA MAANDALIZI YA UANGALIZI WA UCHAGUZI NCHINI BOTSWANA

 

Mkuu wa Misheni ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) ya Uangalizi wa Uchaguzi Mkuu nchini Botswana (SEOM) Mhe. Mizengo Pinda akisikiliza taarifa ya maandalizi ya uangalizi wa uchaguzi mkuu wa Botswana kutoka kwa Sekretarieti ya SADC jijini Gaborone Botswana

 

Mkuu wa Misheni ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) ya Uangalizi wa Uchaguzi Mkuu nchini Botswana (SEOM) Mhe. Mizengo Pinda akiwa na baadhi. ya wajumbe wa misheni ya SEOM wakisikiliza taarifa ya maandalizi ya uangalizi wa uchaguzi mkuu wa Botswana kutoka kwa Sekretarieti ya SADC jijini Gaborone Botswana

Mkuu wa Misheni ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) ya Uangalizi wa Uchaguzi Mkuu nchini Botswana (SEOM) Mhe. Mizengo Pinda akichangia alipopokea taarifa ya maandalizi ya uangalizi wa uchaguzi mkuu wa Botswana kutoka kwa Sekretarieti ya SADC jijini Gaborone Botswana
Mkuu wa Misheni ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) ya Uangalizi wa Uchaguzi Mkuu nchini Botswana (SEOM) Mhe. Mizengo Pinda akizungumza wakati alipopokea taarifa ya maandalizi ya uangalizi wa uchaguzi mkuu wa Botswana kutoka kwa Sekretarieti ya SADC jijini Gaborone Botswana


Wajumbe wa Misheni ya SEOM ukiongozwa na Mkuu wa Misheni hiyo wakisikiliza taarifa ya maandalizi ya Uangalizi wa Uchaguzi Mkuu wa Botswana kutoka kwa Sekretarieti ya SADC jijini Gaborone, Botswana
wajumbe wa Sekretarieti ya SADC waliposhiriki kikao cha kuwasilisha taarifa ya maandalizi ya uangalizi wa uchaguzi mkuu wa Botswana jijini Gaborone, Botswanakwa Mkuu wa Misheni ya SADC Mhe. Mizengo Pinda


 

Mkuu wa Misheni ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) ya Uangalizi wa Uchaguzi Mkuu nchini Botswana (SEOM) Mhe. Mizengo Pinda ameongoza kikao cha Asasi ya Siasa Ulinzi na Usalama ya SADC TROIKA kupitia taarifa ya maandalizi ya Misheni hiyo nchini Botswana.

Kikao hicho kilichofanyika jijini Gaborone tarehe 20 Oktoba 2024 na kilihudhuriwa na wajumbe kutoka Tanzania ambayo ni Mwenyekiti wa Organ; Malawi  Mwenyekiti ajaye na Zambia ambayo ni Mwenyekiti aliyemaliza muda wake na Sekretarieti ya SADC.

Kikao kimepokea na kujadili taarifa iliyowasilishwa na Sekretarieti ya SADC kuhusu maandalizi ya Uangalizi wa Uchaguzi Mkuu wa Botswana utakaofanyika tarehe 30 Oktoba,2024.

Sekretarieti pia iliwasilisha mgawanyo wa majukumu kwa timu mbalimbali za misheni hiyo katika uchaguzi huo.

Katika kikao hicho Mhe. Pinda amesema ni matumaini yake kuwa maandalizi na Mipango ya Uangalizi itaenda sawa na hivyo kuifanya SEOM kutekeleza jukumu lake kwa tija na ufanisi.

Amesema pia SEOM ıkifanya kazi yake ya uangalizi na kuandaa taarifa za Uangalizi wa uchaguzi huo itasaidia nchi husika kufanya maboresho katika mifumo yake ya demokrasia na hivyo kuwa sehemu ya kukuza demokrasia katika nchi wanachama.


MHESHIMIWA PINDA AWASILI GABORONE KUONGOZA MISHENI YA SADC YA UANGALIZI UCHAGUZI NCHINI BOTSWANA

 

Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mizengo Kayanza Peter Pinda akiwa na Balozi wa Tanzania nchini Botswana mwenye makazi yake Afrika Kusini Mhe. James Bwana alipompokea katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Sir Seretse Khama wa Gaborone, alipowasili kuongoza Misheni ya SADC ya uangalizi wa Uchaguzi Mkuu wa Botswana uliopangwa kufanyika tarehe 30 Oktoba 2024

Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mizengo Kayanza Peter Pinda akiwa na Balozi wa Tanzania nchini Botswana mwenye makazi yake Afrika Kusini Mhe. James Bwana alipompokea katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Sir Seretse Khama wa Gaborone, alipowasili kuongoza Misheni ya SADC ya Uangalizi wa Uchaguzi Mkuu wa Botswana uliopangwa kufanyika tarehe 30 Oktoba 2024
 
Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mizengo Kayanza Peter Pinda akiwa katika chumba cha mapumziko alipowasili Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Sir Seretse Khama wa Gaborone,  kuongoza Misheni ya SADC ya uangalizi wa Uchaguzi Mkuu wa Botswana uliopangwa kufanyika tarehe 30 Oktoba 2024


Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Said Shaib Mussa akizungumza na Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Mizengo Pinda alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Sir Seretse Khama wa Gaborone kuongoza Misheni ya Uangalizi Uchaguzi ya SADC nchini Botswana

Mwakilishi wa Mratbu wa Masuala ya SADC Tanzania bi. Lilian Mukasa (aliyesimama) akitoa taarifa kwa Waziri Mkuu Mstaafu na Mkuu wa Misheni ya SADC Uangalizi Uchaguzi Mkuu wa Botswana Mhe. Mizengo Pinda alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Sir Seretse Khama, Gaborone kuongoza Misheni ya Uangalizi Uchaguzi ya SADC nchini Botswana

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Said Shaib Mussa akimkabidhi  nyaraka mbalimbali Waziri Mkuu Mstaafu na Mkuu wa Misheni ya SADC Uangalizi Uchaguzi Mkuu wa Botswana Mhe. Mizengo Pinda  alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Sir Seretse Khama wa Gaborone kuongoza Misheni ya Uangalizi Uchaguzi ya SADC nchini Botswana

Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mizengo Kayanza Peter Pinda  katika picha ya pamoja na viongozi waliofika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Sir Seretse Khama jijini Gaborone , Botswana kwa ajili ya kuongoza Misheni ya SADC ya Uangalizi Uchaguzi Mkuu wa Botswana utakaofanyika tarehe 30 Oktoba, 2024





Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mizengo Kayanza Peter Pinda amewasili jijini Gaborone, Botswana tarehe 19 Oktoba, 2024.
 

Mhe. Mizengo Pinda ataongoza Misheni ya Uangalizi ya Uchaguzi ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC- SEOM) katika Uchaguzi Mkuu wa Jamhuri ya Botswana uliopangwa kufanyika tarehe 30 Oktoba, 2024.

Katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Sir Seretse Khama jijini Gaborone Mhe. Pinda amelakiwa na Balozi wa Tanzania nchini Botswana mwenye makazi yake Afrika Kusini Mhe. James Bwana.

Mhe. Pinda ataongoza SEOM kufuatia kuteuliwa kuongoza Misheni hiyo na Mwenyekiti wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya SADC (Troika) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Mhe. Pinda atazindua rasmi Misheni ya SEOM inayoundwa na wajumbe kutoka Nchi Wanachama wa SADC tarehe 22 Oktoba, 2024.

Mhe. Pinda kwa kushirikiana na Wajumbe wengine wa Troika (Zambia na Malawi) atakutana na wadau mbalimbali wa uchaguzi ikiwemo Tume ya Uchaguzi ya Botswana (IEC), Mabalozi wa Nchi za SADC waliopo Botswana, Vyama vya siasa, Asasi za Kiraia, Taasisi za dini na Vyombo vya Habari kwa ajili ya kuelezea kazi ambayo SEOM itafanya katika kipindi hiki kuelekea uchaguzi mkuu  hadi kukamilika kwake.

Friday, October 18, 2024

WAZIRI KOMBO AFANYA MAZUNGUMZO NA KATIBU MTENDAJI WA ALMA


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo tarehe 17 Oktoba, 2024 amefanya mazungumzo na Katibu Mtendaji wa Muungano wa Viongozi wa Nchi za Afrika katika kupambana na Malaria (ALMA), Dkt. Joy Phumaphi katika Ofisi za Wizara jijini Dodoma.

Mazungumzo ya viongozi hao yalijikita katika kuimarisha ushirikiano katika sekta ya afya hususan suala la kutokomeza malaria kwa kuboresha maabara na viwanda vya bidhaa za afya ikiwemo za kupambana na ugonjwa wa Malaria.

Kwa upande wa Waziri Kombo ameipongeza taasisi ya ALMA kwa kuendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika mapambano ya kutokomeza ugonjwa wa Malaria pamoja na maradhi yasiyoambukiza kama vile shinikizo la damu, kisukari, saratani na kichocho.

Pia, Waziri Kombo ameeleza kuwa Serikali ya Tanzania itaendelea kufanya kazi na ALMA kupitia Balozi zake za New York, Addis Ababa na Geneva ili kusaidia kusukuma agenda za afya zinazopendekezwa na kufanyiwa maamuzi katika maeneo hayo ya uwakilishi wa kikanda na kimataifa.

“Balozi zetu za Addis Ababa, New York na Geneva zitaendelea kufanya kazi nanyi kwa karibu kwakuwa Serikali inathamini mchango wenu katika kuimarisha sekta ya afya, hivyo msisite kuwasiliana nasi pale tunapohitajika kusaidia kufanya maamuzi kwa maslahi ya uum” Balozi Kombo.

Vilevile, amesisitiza kuwa Tanzania itaendelea kutoa kipaumbele katika suala la kutokomeza malaria kwakuwa tangu ALMA iwekeze jitihada zake nchini, Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Kikwete amekuwa kinara katika kutokomeza Malaria kupitia taasisi ya ALMA, hivyo jitihada alizozifanya pamoja na viongozi wengine wa Afrika zitaendelezwa ili kuhakikisha malaria inatokomezwa.

Naye Dkt. Phumaphi ameishukuru Serikali kwa ushirikiano wake katika kuimarisha sekta ya afya nchini pamoja na namna ambavyo inafanya vizuri katika matumizi ya kadi ya ALMA inayotumika katika kujipima utendaji na uwajibikaji kwenye mapambano dhidi ya malaria nchini. 

Kadhalika, amemshukuru Waziri Kombo kwa  kuihakikishia ALMA kuendelea kupata ushirikiano kupitia Balozi za Tanzania jijini Addis Ababa, Newyok na Geneva na kueleza kuwa hii ni hatua kubwa kwa ALMA katika kuziwezesha agenda za mapana ya Afrika na kuwezesha kupafa fedha za miradi.

“Tumeomba usaidizi wa Tanzania kwakuwa tuna imani na nafasi yake ya ushawishi katika majukwaa ya kikanda na kimataifa kwakuwa siku zote imekuwa ikiheshimika na kuungwa mkono katika agenda mbalimbali zenye tija kwa watanzania na Afrika kwa ujumla,” alisema Dkt. Phumaphi.

Hata hivyo, jitihada zilizofanyika zimewezesha kutokomeza malaria kwa asilimia kubwa hususan Zanzibar katika awamu tatu inasomeka katika taarifa za kiafya kuwa ni eneo huru kwa malaria.

Jitihada nyingine ni pamoja na kuziwezesha taasisi za Tanzania ikiwemoTaasisi ya Afya ya Ifakara kufanya kazi na Kituo cha kudhibiti magonjwa barani Afrika “Africa CDC’’ na kuwezesha miradi ya sekta kama za mazingira na kilimo kuzinufaisha jamii katika masuala ya afya mfano, miradi ya kilimo kugawa vyandarua kwa wakulima na miradi ya umwagiliaji kwa wakulima kusaidia jitihada nyingine.

Jitihada hizo zinaendelea pia kwa nchi nyingine za Afrika kwa kufanya tafiti ili kuona maeneo mengine yatakayosaidia jitihada hizo badala ya kutegemea sekta ya afya pekee kusimamia afya ya wananchi ambapo wakati mwingine imekuwa ikielemewa katika bajeti zake kukamilisha malengo ya kutokomeza maradhi.


MAREKANI YARIDHISHWA NA MAGEUZI YA KIUTENDAJI YA SERIKALI YA RAIS SAMIA

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo akifafanua jambo wakati wa mazungumzo na ujumbe wa Shirika la Changamoto za Milenia (Millennium Challenge Corporation-MCC) la Serikali ya Marekani yaliyofanyika jijini Dodoma, Oktoba 17, 2024. 

Yaahidi kuendelea kutoa fedha kuisaidia Tanzania kutatua vikwazo vya ukuaji uchumi
Shirika la Changamoto za Milenia (Millennium Challenge Corporation-MCC) la Serikali ya Marekani limeeleza kuridhishwa kwake na mageuzi ya mifumo ya kiutendaji, yaliyofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita katika maeneo mbalimbali ikiwemo uimarishwaji wa demokrasia, utawala bora na haki za binadamu. 

Hayo yamebainishwa wakati wa mkutano uliofanyika kati ya ujumbe wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ujumbe wa Shirika la Changamoto za Milenia uliofanyika terehe 17 Oktoba 2024 jijini Dodoma. 

Akizungumza kwenye mkutano huo Bw. Dan Barnes, Mkurugenzi wa Sera na Tathmini wa shirika hilo ambaye pia ameongoza ujumbe wa Marekani kwenye mkutano huo, ameeleza kuwa katika kipindi cha miaka mitatu ya Serikali hii, wameridhishwa na hatua mbalimbali zilizochukuliwa na Tanzania ambazo zimechangia kuongeza kasi ya maendeleo ya kiuchumi nchini. 

Kadhalika, katika mkutano huo, Bw. Barnes alieleza kuwa Bunge la Marekani nalo limeridhia Tanzania kuendelea kunufaika na ufadhili wa Shirika hilo la MCC, baada ya kuridhishwa na utendaji wa Serikali ya Tanzania. Maamuzi hayo yataifaya Tanzania kuendelea kupewa misaada katika shughuli za maendeleo ambazo zitasaidia kuinua uchumi wa mwananchi mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla.

Hatua hii iliyofikiwa na MCC inatokana na dhamira ya dhati ya Serikali ya Awamu ya Sita ya kufanya mageuzi na maboresho katika utendaji wake. Pamoja na sera madhubuti na uongozi thabit wa Serikali, mageuzi hayo yamefikiwa kupitia falsafa ya _4Rs_ ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya maridhiano, ustahimilivu, mageuzi na ujenzi mpya iliyoleta mshikamano wa kisiasa, kijamii na kiuchumi nchini Tanzania. Falsafa hii imesaidia kuwavutia washirika mbalimbali wa maendeleo kote duniani wakiwemo MCC kwa manufaa ya pande zote.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Mahamoud Thabit Kombo ameshiriki mkutano huo ambao ulijumuisha Mawaziri wanaosimamia sekta mbalimbali kutoka Tanzania Bara na Zanzibar zinazohusika moja kwa moja katika usimamizi na utekelezaji wa miradi mbalimbali inayofadhiliwa na MCC.

Akichangia katika mkutano huo Waziri Kombo ameeleza kuwa, Tanzania itaendelea kuheshimu na kuenzi uhusiano mzuri uliopo kati yake na Marekani uliodumu kwa zaidi ya miongo sita, huku zikishirikiana katika sekta mbalimbali ikiwemo elimu, afya, biashara na uwekezaji, kilimo, nishati, utalii, Teknolojia, ulinzi na madini. Sekta hizo zinafadhiliwa kupitia programu mbalimbali ikiwemo USAID, PEPFAR na Peace Corps. 

Aidha, Waziri Kombo alisisitiza kuwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itaendelea kuheshimu na kutekeleza misingi ya demokrasia na utawala bora na haki za binadamu ambazo ni tunu za Tanzania na Marekani.

Uhusiano huo mzuri wa kidiplomasia kati ya Tanzania na Marekani umeendelea kujidhihirisha kupitia ziara za viongozi Wakuu wa nchi ambapo mwaka 2023 Makamu wa Rais wa Marekani na Mgombea wa Urais wa Nchi hiyo kupitia chama cha Democrat Mhe. Kamala Harris alizuru nchini Tanzania. 

Tanzania imekuwa ikinufaika na ufadhili wa miradi ya maendeleo kutoka MCC tangu mwaka 2005. Miradi hiyo ni pamoja na: ujenzi wa barabara ya Tunduma hadi Sumbawanga, Barabara za vijijini Pemba, barabara ya Tanga had Horohoro na barabara za ushoroba wa Mtwara.

Miradi mingine ni pamoja na; uwanja wa ndege wa Mafia, kuongezea uwezo mtambo wa kusukuma maji wa Ruvu chini na mradi wa kusambaza maji mjini Morogoro, maboresho na upanuzi wa njia za usambazaji wa nishati, mradi wa nishati ya jua mkoani Kigoma na miradi ya kujenga uwezo wa Shirika la Umeme la Tanzania (TANESCO) na Shirika la Umeme la Zanzibar (ZECO).

Shirika la Changamoto za Milenia ni taasisi ya Serikali ya Marekani iliyojikita katika kupunguza umasikini duniani kupitia programu mbalimbali zinazolenga kusaidia ukuaji wa uchumi, kwa kutoa ruzuku na misaada kwa nchi zinazokidhi viwango na vigezo thabiti vya utawala bora, mapambano dhidi ya rushwa, kuheshimu haki za binadamu na misingi ya kidemokrasia.


Mkurugenzi wa Sera na Tathmini wa Shirika la Changamoto za Milenia Bw. Dan Barnes akielezea jambo kwenye mkutano na ujumbe wa Serikali ya Tanzania uliofanyika jijini Dodoma, Oktoba 17, 2024.

Ujumbe wa Shirika la Changamoto za Milenia la Marekani ukiwa kwenye mazungumzo na ujumbe wa Serikali ya Tanzania yaliyofanyika jijini Dodoma, Oktoba 17, 2024.
Sehemu ya Ujumbe wa Serikali ya Tanzania kwenye mkutano na Ujumbe wa Shirika la Changamoto za Milenia la Marekani uliofanyika jijini Dodoma, Oktoba 17, 2024.
Sehemu ya Ujumbe wa Serikali ya Tanzania kwenye mkutano na Ujumbe wa Shirika la Changamoto za Milenia la Marekani uliofanyika jijini Dodoma, Oktoba 17, 2024.

Ujumbe wa Serikali ya Tanzania na Shirika la Changamoto za Milenia la Marekani katika picha ya pamoja.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji Mhe. Prof. Kitila Alexander Mkumbo akifafanua jambo wakati wa mazungumzo na ujumbe wa Shirika la Changamoto za Milenia (Millennium Challenge Corporation-MCC) la Serikali ya Marekani yaliyofanyika jijini Dodoma, Oktoba 17, 2024.

WABUNGE WA EALA WATAKIWA KUWEKA MASLAHI YA UMMA MBELE, BALOZI KOMBO

 

Wabunge wa Tanzania kwenye Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki wamesisitizwa kuyabeba majukumu waliyopewa kwa uzito unaostahili, huku wakiweka mbele maslahi ya umma wakati wanatekeleza majukumu yao.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo (Mb.), alipokutana na Wabunge hao jijini Dodoma Oktoba 17, 2024.

Waziri Kombo amewasisitiza wabunge hao kutumia nafasi walizopewa katika Bunge hilo kuhimiza umoja, mshikamano na ushirikiano baina ya nchi wanachama wa umoja huo. “Nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) tokea enzi zimekuwa na umoja wa kindugu, hivyo ni jukumu lenu kuhakikisha kuwa umoja huo unaendelezwa, unaimarishwa na kuenziwa ili kutimiza lengo la Wakuu wa Nchi la kuwa na mtangamano imara katika Jumuiya ya Afrika Mashariki”, Waziri Kombo alisema.

Mhe. Waziri amewaambia wabunge hao kuwa ili kutimiza majukumu yao ipasavyo katika chombo hicho muhimu katika jumuiya, wanatakiwa kujua mipango mbalimbali ya Serikali ili waweze kuisemea na kuitetea vyema. Hivyo, aliwahimiza kuirejea mara kwa mara Ilani ya Chama cha Mapinduzi ili kuelewa malengo yanayotakiwa kufikiwa katika mtangamanao wa Afrika Mashariki na mipango mingine ya maendeleo ya Serikali kama vile, Mpango wa Mwaka wa Bajeti ya Serikali.

Ameedelea kueleza kuwa, Wizara yake ipo tayari kupokea ushauri wakati wowote kutoka kwa wabunge hao unaolenga kuboresha utekelezaji mzuri wa programu za Jumuiya ya Afrika Mashariki. ”Wizara ina Naibu Waziri anayesimamia masuala ya Afrika Mashariki, Mhe. Denis Londo; Katibu Mkuu anayesimamia masuala ya Afrika Mashariki, Balozi Stephen Mbundi; Wakurugenzi wa Idara zinazotekeleza masuala ya Afrika Mashariki na nipo mimi mwenyewe, Waziri, njooni tushauriane wakati wowote yanapoibuka masuala yanayohitaji ushauri au mwongozo wetu”, Balozi Kombo alisisitiza.

Amehitimisha maelezo yake kwa Waheshimiwa Wabunge kwa kuwakumbusha kuwa Wizara yake ina dhamana kubwa ya utekelezaji wa Sera ya Mambo ya Nje inayohimiza diplomasia ya uchumi, hivyo aliwataka kutumia nafasi walizonazo kutangaza fursa za Tanzania ikiwa ni pamoja na fursa ya Tanzania kupakana na nchi nyingi ambazo hazina bandari.

Kwa upande wa Wabunge, wakiwakilishwa na Katibu wao, Mhe. Ngwaru Maghembe wamemshukuru Mhe. Waziri kwa kutenga muda wa kukutana nao. Wameahidi kuwa wataendelea kushirikiana na Wizara katika kufanikisha majukumu ya bunge kwa kuzingatia maslahi ya nchi na Jumuiya kwa ujumla.  

Katika kikao hicho ambacho kilikuwa cha kujitambulisha, Waziri Kombo aliambatana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki anayesimamia masuala ya Afrika Mashariki, Balozi Stephen Mbundi, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Samwel Shelukindo na Wakuu wa Idara na Vitengo wa Wizara hiyo. 

Kwa upande wa Wabunge walioshiriki kikao hicho ni Mhe. Dkt. Ngwaru Maghembe (CCM), Mhe. Mashaka Ngole (CUF), Mhe. Kachwamba Ansar (CCM), Mhe. Nadra Juma Mohamed (CCM) na Mbunge Mteule, Mhe. Gladness Salema (CCM).

Tanzania na Iran kuimarisha ushirikiano wa kidiplomasia katika biashara na uwekezaji


Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Jamhuri ya Kiislam ya Irani zimekusudia kusaini hati mbalimbali za makubaliano ili kuimarisha ushirikiano wa kidiplomasia katika biashara na uwekezaji kwa manufaa ya pande zote mbili.

Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Abdalah Kilima amesema hayo leo 17 Oktoba, 2024, katika kikao cha ngazi ya Wataalamu na Maafisa Waandamizi kutoka Tanzania na Iran, kilichofanyika katika Kituo cha Mikutano  cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC), kilichojikita katika kuandaa ajenda za kuimarisha ushirikiano wa kidiplomasia kwa manufaa ya nchi hizo.

Balozi Kilima ambaye pia alikuwa mwenyekiti mwenza katika kikao hicho, amesema hatua ya ukuzaji Biashara na Uwekezaji baina ya Tanzania na Iran, itahusisha maeneo ya kipaumbele katika sekta ya Kilimo, Mifugo, Uvuvi, Nishati, Teknolojia ya Habari na Utunzaji wa Maji Kale.

Maeneo mengine ni mafuta na gesi, ulinzi na usalama, maeneo ya kupambana na majanga na sheria; hatua ambayo itaziwezesha nchi hizi kutia saini hati za makubaliano ya ushirikiano kwa utekelezaji. 

Hati hizo za makubaliano zitatiwa saini na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Tanzania Mhe. Balozi Thabit Kombo (Mb) na Naibu Waziri wa Kilimo wa Iran Mhe. Dkt. Gholamreza Nouri katika kikao cha kilele cha Mawaziri wa nchi hizo kitakachofanyika tarehe 19 Octoba 2024, JNICC, jijini Dar es Salaam.

Balozi Kilima amesema hati zitakazosainiwa ni pamoja na hati ya kutotoza kodi mara mbili, ushirikiano katika sekta ya ulinzi, kupambana na majanga, Sanaa na Michezo na ushirikino katika sekta ya kumbukumbu na nyaraka.

Naye Mwenyekiti mwenza wa Kikao hicho cha Wataalam na Maafisa Wandamizi kwa upande wa Iran, ambaye pia ni Naibu Waziri wa Kilimo wa nchi hiyo Mhe. Dkt. Gholamreza Nouri ameishukuru Tanzania kwa kuimarisha ushirikiano wa kimataifa na Iran kwani utawezesha mataifa hayo kukuza na kuendeleza mahusiano mema yaliyopo ya kidiplomasia.