Balozi wa kenya nchini Tanzania akichangia mada kuhusu kaulimbiu ya Siku ya Afrika. |
Waheshimiwa Mabalozi wa Nchi za Afrika nchini Tanzania na wana habari wakiendelea na mkutano. |
Balozi wa kenya nchini Tanzania akichangia mada kuhusu kaulimbiu ya Siku ya Afrika. |
Waheshimiwa Mabalozi wa Nchi za Afrika nchini Tanzania na wana habari wakiendelea na mkutano. |
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akipokea Hati za Utambulisho za Balozi mpya wa Marekani nchini, Mhe. Mark Childress IKULU, Dar es Salaam tarehe 22 Mei, 2014. |
Mhe. Childress akisaini Kitabu cha Wageni mara baada ya kuwasili IKULU. |
Mhe. Rais Kikwete akimtambulisha kwa Balozi Childress Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. John Haule |
Mhe. Rais Kikwete akimtambulisha kwa Balozi Childress Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bibi Victoria Mwakasege |
Balozi Childress akisalimiana na Afisa Dawati la Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bi. Redemptor Tibaigana. |
Mhe. Rais Kikwete katika mazungumzo na Balozi Childress |
Mhe. Rais Kikwete katika picha ya pamoja na Balozi Childress |
Picha ya Pamoja |
Brass Band ikipiga wimbo wa Taifa la Marekani mara baada ya Balozi wa Marekani kuwasili IKULU kwa ajili ya kuwasilisha Hati zake za utambulisho kwa Rais.
Picha na Reginald Philip
|
Baadhi ya Wafanyakazi Bora wakiwa na nyuso za furaha. |
Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. |
Katibu Mkuu na Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi, Bw. Haule akimkabidhi Cheti Mfanyakazi Hodari wa Wizara Bw. Bujiku Sakila kutoka Idara ya Afrika. |
Katibu Mkuu akimkabidhi Cheti Mfanyakazi Bora wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali, Bw. Ally Kondo. |
Katibu Mkuu akimkabidhi Cheti Mfanyakazi Bora wa Idara ya Mambo ya Nje Zanzibar, Bi. Asya Hamdani. |
Katibu Mkuu akimkabidhi Cheti Mfanyakazi Bora wa Idara ya Sera na Mipango, Bw. Elly Chuma. |
Katibu Mkuu akimkabidhi Cheti Mfanyakazi Bora wa Idara ya DIASPORA, Bw. Seif Kamtunda. |
Katibu Mkuu akimkabidhi Cheti Mfanyakazi Bora wa Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani, Bw. Ibrahim Mamboya. |
Katibu Mkuu akimkabidhi Cheti Mfanyakazi Bora wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa, Bi. Rose Kitandula. |
Katibu Mkuu akimkabidhi Cheti Mfanyakazi wa Kada ya Makatibu Muhtasi , Bi. Faith Masaka. |
Katibu Mkuu akimkabidhi Cheti Mfanyakazi Bora wa Kada ya Wahudumu, Bi. Hadija Mwichande. |
Baadhi ya Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wakifuatilia tukio la utoaji vyeti kwa Wafanayakazi Bora wa Wizara |
Bw. Iman Njalikai, Mwenyekiti wa TUGHE wa Wizara akizungumza mara baada ya utoaji vyeti kwa Wafanyakazi Bora wa Wizara. |
Katibu Mkuu akibadilishana neno na baadhi ya Wajumbe mara baada ya kikao. |
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Dkt. Mahadhi Juma Maalim (Mb.) akizungumza na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Vietnam, Mhe. Nguyen Phuong Nga mara baada ya kumpokea katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere. Mhe. Nguyen yupo nchini kwa ziara ya kikazi ya siku tano.
|
Mhe. Nguyen akimkabidhi zawadi Dkt. Maalim mara baada ya mazungumzo yao. |
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimwapisha Lt. Gen. Wynjones Mattew Kisamba kuwa Balozi wa Tanzania nchini Urusi. Hafla hiyo fupi ilifanyika Ikulu, Dar es Salaam tarehe 15 Mei 2014. |
Picha ya Pamoja |
Mhe. Rais Kikwete akiwa kwenye picha ya pamoja na Familia ya Balozi Kisamba |
Balozi Kisamba akisalimiana na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika Bibi Victoria Mwakasege mara baada ya kuapishwa.
Picha na Reginald Philip
|
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.)-katikati) kwa pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. John Haule (wa tatu kutoka kushoto) na viongozi wengine wakiimba wimbo wa "Solidarity" wakati wa ufunguzi wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa uliofanyika kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam tarehe 15 Mei, 2014. |
Mhe. Membe akitoa hotuba ya ufunguzi wa Baraza la Wafanayakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa ambapo alitoa rai kwa Wafanyakazi hao kujituma na kuongeza bidii katika utendaji kazi wao wa kila siku. |
Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wakimsikiliza Waziri Membe alipofungua kikao cha Baraza hilo. |
Katibu Mkuu, Bw. Haule nae akizungumza wakati wa ufunguzi wa Baraza hilo. |
Baadhi ya Wajumbe wakimsikiliza Katibu Mkuu (hayupo pichani) wakati akizungumza. Kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Dushhood Mndeme. |
Katibu wa Baraza la Wafanyakazi, Bibi Naomi Zegezege nae akizungumza wakati wa ufunguzi wa Baraza hilo huku Mhe. Membe na Viongozi wengine wakimsikiliza. |
Kikao kikiendelea. |
Mkurugenzi wa Idara ya Afrika na Mjumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Baloiz Vincent Kibwana akitoa neno la shukrani kwa niaba ya Wajumbe wa Baraza hilo. |
Katibu Mkuu, Bw. Haule, Naibu Katibu Mkuu, Balozi Rajabu Gamaha na Viongozi wengine wakifurahia jambo wakati wa kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa Mambo ya Nje. |
Waandishi wa Habari nao pia walikuwepo.
|
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushiriano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akisoma kwa majonzi Salamu za Pole za Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa Rais wa Malawi, Mhe. Joyce Banda kufuatia kifo cha ghafla cha aliyekuwa Balozi wa Malawi nchini Tanzania, Marehemu Flossie Gomile-Chidyaonga. Mhe. Waziri Membe alisoma salamu hizo wakati wa kumuaga Marehemu Balozi Flossie tukio hilo lilifanyika nyumbani kwa marehemu Kitongoji cha Limbe katika mji wa Blantyre nchini Malawi. Mhe. Membe alimwakilisha Rais Kikwete kwenye mazishi ya Balozi Flossie yaliyofanyika tarehe 14 Mei, 2014. |
Mhe. Membe akiendelea kusoma salamu hizo huku Waziri wa Mambo ya Nje wa Malawi, Mhe. Ephraim Chiume (mwanye tai nyeusi) na Mume wa Rais wa Malawi, Jaji Mkuu Mstaafu, Banda (wa kwanza kulia mstari wa kwanza) wakimsikiliza. |
Baadhi ya wananchi wakimsikiliza Mhe. Membe (hayupo pichani) |
Mhe. Membe akimkabidhi Mhe. Chiume Salamu hizo mara baada ya kuzisoma. |
Mhe. Chiume nae akisema machache wakati wa shughuli za kumuaga Balozi Flossie. Katika maelezo yake Mhe. Chiume kwa niaba ya Serikali ya Malawi alitoa shukrani za dhati kwa Serikali ya Tanzania kwa ushirikiano mkubwa wakati wote wa msiba wa Marehemu Balozi Flossie. |
Mhe. Chiume akimtambulisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. John Haule ambaye alikuwa miongoni mwa wajumbe waliofuatana na Mhe. Membe nchini Malawi. |
Baba Mdogo wa Marehemu Balozi Flossie, Dkt. Joseph Gomile nae akitoa neno wakati wa shughuli hizo za kumuaga Marehemu Balozi Flossie. Dkt. Gomile ambaye anaishi nchini Tanzania kwa kipindi kirefu sasa nae aliishukuru Serikali ya Tanzania kwa mchango mkubwa katika msiba huo mzito wa mtoto wake. |
Mhe. Membe. Mhe. Chiume na Mhe. Jaji Mstaafu Banda wakimsikiliza Dkt. Gomile (hayupo pichani)
|
Jeneza lililobeba mwili wa Marehemu Baloz Flossie kama linavyoonekana katika eneo la nyumbani kwake likiwa limezungukwa na waombolezaji. |
Balozi wa Tanzania nchini Malawi, Mhe. PatrickTsere (kushoto) akiwa na Balozi Vincent Kibwana, Mkurugenzi wa Idara ya Afrika na Mwakilishi kutoka Ubalozi wa Malawi hapa nchini mara baada ya shughuli za kuaga mwili wa Marehemu Balozi Flossie kumalizika. |
Baadhi ya viongozi wa dini waliokuwepo. |
Viongozi mbalimbali walioshiriki kumuaga Balozi Flossie katika eneo la nyumbani kwake kabla ya mazishi. |
Marafiki wa Marehemu Balozi Flossie wakiwa katika simanzi kufuatia kifo cha mpendwa wao. |
Mhe. Membe akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Mabalozi aliofuatana nao nchini Malawi mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere. |