Picha ya pamoja kutoka kulia Mhe. Balozi Migiro, kijana Samweli ambaye aliambatana na rafiki yake Penina Haika Petitte na Mkuu wa Utawala wa Ubalozi wa Tanzania nchini Uingereza Bi. Rose Kitandula. |
Tuesday, June 20, 2017
Balozi Migiro amtunuku kijana aliyeshinda shindano la kimataifa la kugiga picha.
Monday, June 19, 2017
Balozi wa Tanzania nchini Israel awasilisha Hati za Utambulisho
Balozi wa Tanzania nchini Israel, Mhe. Job Masima (kulia) akiwasilisha Hati za Utambulisho kwa Rais wa Taifa la Israel, Mhe. Reuven Rivlin Ikulu ya nchi hiyo mjini Jerusalem |
Thursday, June 15, 2017
Balozi wa Sweden atembelea Wizara ya Mambo ya Nje
Mheshimiwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Augustine Mahiga (Kulia)akiwa katika mazungumzo na Balozi wa Sweden Nchini Mhe. Katarina Rangnitt katika ukumbi wa mikutano wa Wizara Juni 14,2017. Katika mkutano huo walijadiliana masuala mbalimbali kuhusu ushirikiano wa Tanzania na Sweden pamoja na hali ya usalama nchini Burundi.
Mheshimiwa Waziri Mahiga, Balozi wa Sweden nchini pamoja na Wataalam kutoka Wizarani wakiwa katika mkutano huo,
Mwakilishi Mkaazi wa UNIDO awasilisha Hati za Utambulisho
Mheshimiwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Augustine Mahiga akipokea Hati za Utambulisho kutoka kwa Mwakilishi Mkaazi wa UNIDO nchini, Bw.Stephen Bainous Kargbo, Juni 14,2017, katika ukumbi wa Mikutano Wizarani.
Mhe. Waziri Balozi Augustine Mahiga (Katikati), Mwakilishi Mkaazi wa UNIDO, Bw. Stephen Bainous Kargbo (Kushoto) na kulia ni Balozi Grace Martin, Mkurugenzi Idara ya Itifaki wakiwa katika mazungumzo.
Mhe. Waziri Balozi Mahiga, Mwakilishi Mkaazi wa UNIDO na Wataalam kutoka Wizarani na Ofisi za UNIDO wakiwa katika picha ya pamoja baada ya makabidhiano ya Hati za Utambulisho..
Wizara ya Mambo ya Nje yapokea mashine ya kutengeneza vitambulisho
Balozi Ramadhan Mwinyi (kushoto) akipeana mkono na Bw. Akiromo mara baada ya kupokea mashine ya kutengeneza vitambulisho |
Picha ya pamoja, kutoka kulia ni Bi. Angela Ngaillo, Afisa kutoka Idara ya Itifaki, Bw. Akiromo kutoka MICT Arusha, Bi. Tully Mwaipopo kutoka MICT, Balozi Ramadhan Mwinyi na Balozi Grace Martin. |
TANGAZO KWA UMMA
TAARIFA KUHUSU KUTHIBITISHA VYETI |
Wizara
ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki inapenda kuufahamisha Umma ya
kwamba, wale wote wanaohitaji na watakaohitaji kupata huduma ya kuthibitisha vyeti
na nyaraka mbalimbali kama ifuatavyo:
(1) KuanziaTarehe
01/07/2017 malipo yote ya huduma ya kuthibitisha
vyeti/nyaraka yatafanyika kwa njia ya benki, kupitia akaunti namba 0150275408200, Foreign Collection Account,
CRDB Bank na hati ya malipo ya benki iwasilishwe wizarani kuthibitisha malipo
hayo.
(2) Wizara
haitapokea pesa taslimu kama ilivyokuwa inafanyika hapo awali bali hati ya malipo
kutoka benki.Kila nakala itakayothibitishwa na kugongwa muhuri italipiwa kiasi
cha Shillingi Elfu Kumi na Tano tu (TSHS
15,000/=) benki.
(3) Vyeti
vyote vinavyoletwa Wizarani kwa ajili ya kuthibitishwa, havinabudi kupelekwa
kwanza katika Taasisi zilizotoa vyeti/nyaraka hizo ili vihakikiwe na kuthibitshwa.
(4) Baada
ya kutekeleza maelekezo katikak ifungu cha tatu (3) hapo juu, Mteja anatakiwa kuandika
barua kwa Katibu Mkuu,Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
akiomba nyaraka hizo zithibitishwe na kueleza matumizi tarajiwa ya nyaraka hizo
nje ya nchi. Aidha, barua hiyo iambatishwe na nakala (copies) za nyaraka zilizothibitishwa
na Taasisi husika.
(5) WATEJA WOTE WANAOMBWA KUZINGATIA
RAI KWAMBA HUDUMA HIZI ZITAKUWA ZINATOLEWA SIKU YA JUMANNE NA ALHAMISI TU, KUANZIA
SAA 3.00 - 5.00 ASUBUHI.
Imetolewa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
PUBLIC ANNOUNCEMENT
Subscribe to:
Posts (Atom)