TAARIFA KUHUSU KUTHIBITISHA VYETI |
Wizara
ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki inapenda kuufahamisha Umma ya
kwamba, wale wote wanaohitaji na watakaohitaji kupata huduma ya kuthibitisha vyeti
na nyaraka mbalimbali kama ifuatavyo:
(1) KuanziaTarehe
01/07/2017 malipo yote ya huduma ya kuthibitisha
vyeti/nyaraka yatafanyika kwa njia ya benki, kupitia akaunti namba 0150275408200, Foreign Collection Account,
CRDB Bank na hati ya malipo ya benki iwasilishwe wizarani kuthibitisha malipo
hayo.
(2) Wizara
haitapokea pesa taslimu kama ilivyokuwa inafanyika hapo awali bali hati ya malipo
kutoka benki.Kila nakala itakayothibitishwa na kugongwa muhuri italipiwa kiasi
cha Shillingi Elfu Kumi na Tano tu (TSHS
15,000/=) benki.
(3) Vyeti
vyote vinavyoletwa Wizarani kwa ajili ya kuthibitishwa, havinabudi kupelekwa
kwanza katika Taasisi zilizotoa vyeti/nyaraka hizo ili vihakikiwe na kuthibitshwa.
(4) Baada
ya kutekeleza maelekezo katikak ifungu cha tatu (3) hapo juu, Mteja anatakiwa kuandika
barua kwa Katibu Mkuu,Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
akiomba nyaraka hizo zithibitishwe na kueleza matumizi tarajiwa ya nyaraka hizo
nje ya nchi. Aidha, barua hiyo iambatishwe na nakala (copies) za nyaraka zilizothibitishwa
na Taasisi husika.
(5) WATEJA WOTE WANAOMBWA KUZINGATIA
RAI KWAMBA HUDUMA HIZI ZITAKUWA ZINATOLEWA SIKU YA JUMANNE NA ALHAMISI TU, KUANZIA
SAA 3.00 - 5.00 ASUBUHI.
Imetolewa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.