Tuesday, June 20, 2017

Balozi Migiro amtunuku kijana aliyeshinda shindano la kimataifa la kugiga picha.


Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Mhe. Asha-Rose Migiro (kulia) akimvisha begi ya bendera ya Taifa kijana wa miaka 18 Samwel Mwanyika, aliyeshinda shindano la kimataifa la kupiga picha kwa vijana wenye utindio wa Ubongo maarufu kama "The Stephen Thomas Awards" lililofanyika mapema wiki hii Jijini London, Uingereza.

Kijana Samwel Mwanyika akiwa ameshika picha iliyompa ushindi katika shindano la Tuzo za Stephen Thomas, mara baada ya kuwasili katika ofisi za Ubalozi wa Tanzania nchini Uingereza, kwaajili ya hafla iliyoandaliwa na Mhe. Balozi Migiro kwa lengo la kumpongeza kijana huyo ambaye aliweza kuibuka mshindi miongoni mwa vijana wengi walioshindanishwa.
Mhe. Migiro akizungumza na Mony Teri Petitte mwasisi wa Taasisi inayohudumia watu wenye mtindio wa Ubongo “Pearl of People with Down Syndrome” anayejitolea kuendesha Jumuiya ya Watanzania wenye matatizo ya ubongo sambamba na kuratibu tuzo ya Stephen Thomas.

Picha ya pamoja kutoka kulia Mhe. Balozi Migiro, kijana Samweli ambaye aliambatana na rafiki yake Penina Haika Petitte na  Mkuu wa  Utawala wa Ubalozi wa Tanzania nchini Uingereza Bi.  Rose Kitandula.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.