Saturday, September 7, 2013

Brasilia hosts a Seminar of International Best Practices between Africa and Colombia


Mr. David Mwakanjuki (2nd right), Minister Plenipotentiary of the Embassy of the United Republic of Tanzania in Brasilia recently attended a Seminar of the International Best Practices between Africa and Colombia.  The Seminar was held on 2nd of September through 5th of September, 2013 and was also attended by Columbian ACP Vice Foreign Minister (3rd right) and participants from Kenya. 

Mr. David Mwakanjuki (center) in a photo with  Vice Minister of Foreign Affairs of Colombia (left) and Egyptian Ambassador to Colombia (right).

Vice Minister of Foreign Affairs of Colombia in a photo with David Mwakanjuki, Minister Plenipotentiary of the United Republic of Tanzania in Brasilia.



All photos and details courtesy of Mr. Mwakanjuki in Brasilia


Membe: Tanzania haijamfukuza mtu yoyote nchini


Mhe. Waziri Bernard K. Membe (MP), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, akiongea na waandishi wa habari jana mchana katika Ofisi za Wizara ya Mambo ya Nje.  Kulia ni Balozi Vincent Kibwana, Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.  

Baadhi ya waandishi wa habari waliokusanyika kumsikiliza Mhe. Waziri Membe. 

Balozi Celestine Mushy (kushoto), Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Bw. Elibariki Maleko (kulia), Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati katika Wizara ya Mambo ya Nje wakimsikiliza Mhe. Waziri Membe.  

Balozi Dora Msechu (kulia), Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Bw. Omari Mjenga, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia katika Wizara ya Mambo ya Nje nao wakimsikiliza Mhe. Waziri Membe.  

Mhe. Waziri Membe akifafanua jambo wakati wa mazungumzo yake na waandishi wa habari alipokutana nao jana Wizarani. 

 
Waandishi wa habari waliokusanyika kumsikiliza Mhe. Waziri Membe.  (picha hii na Reginald Philip)


Picha nyingine zote na Tagie Daisy Mwakawago 





Membe: Tanzania haijamfukuza mtu yoyote nchini
Na Ally Kondo
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard K. Membe (Mb) ameuambia Umma wa Tanzania na dunia kwa ujumla kuwa Serikali ya Tanzania haijamfukuza mtu yeyote nchini mwenye sifa za ukiimbizi kama inavyodaiwa na baadhi ya watu.
Mhe. Waziri aliyasema hayo alipokutana na waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dar es Salaam siku ya Ijumaa tarehe 06 Septemba, 2013.
“Serikai haikumfukuza mkimbizi yeyote isipokuwa iliwafukuza wahamiaji haramu, Aidha, wahamiaji haramu hao walipewa onyo la kuondoka nchini na wengi wao wametii kabla ya operesheni maalum ya kuwatia mbaroni haijaanza” Waziri Membe alisikika akisema.
Kuhusu hoja kuwa operesheni ya kuwafukuza wahamiaji haramu inawalenga Wanyarwanda, Waziri Membe alisema kuwa hoja hiyo sio ya kweli. Alisema kuwa hadi kufikia wakati huu zaidi ya wahamiaji haramu 31,000 wameondoka nchini. Kati ya hao Warundi ni 21,000, Wanyarwanda ni 6,000 tu na waliobaki ni kutoka nchi nyingine..
Mhe. Membe aliwaambia waandishi wa habari kuwa Tanzania imekuwa kimbilio la wakimbizi kwa muda mrefu na hadi sasa inahifadhi wakimbizi zaidi ya laki 4. Wakati wote wakimbizi wamekuwa wakipewa huduma nzuri na haijawahi kusikika kuwa Tanzania inalaaniwa na Shirika la Wakimbizi la Umoja wa Mataifa au Jumuiya ya Kimataifa kwamba Serikali inawanyanyasa wakimbizi.
Sambamba na taarifa hiyo, Mhe. Waziri aliwaambia waandishi wa habari kuhusu mikutano inayofanywa na baadhi ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (Kenya, Uganda na Rwanda) bila kuhusisha nchi nyingine wanachama wa jumuiya hiyo.
Mhe. Membe alisema kuwa yeye binafsi hana tatizo na mikutano hiyo endapo tu, imepata kibali cha Wakuu wa Nchi wa EAC pamoja na kutoa ripoti ya masuala yanayozungumzwa katika vikao vya jumuiya. “Mimi binafsi sioni tatizo kwa nchi hizo kukutana endapo zimepewa Baraka na Wakuu wote wa Nchi wa EAC na ripoti za mikutano yao kuwasilishwa katika vikao rasmi vya jumuiya” alisema Mhe. Membe.
Aliwatoa shaka Watanzania kutokuwa na hofu na mikutano hiyo kwa kuwa Tanzania ni nchi muhimu katika Jumuiya ya Afrika Mashariki, hivyo hainabudi nchi nyingine kuitegemea kutokana na rasilimali zilizopo  na jiografia yake.
Alihitimisha mazungumzo yake kwa kusema kuwa anaamini vikao vinavyofanywa, vinafanywa kwa nia njema pasipo kuwa na dhamira ya kuleta mgawanyiko ndani ya jumuiya. Na endapo vinafanywa kwa dhamira ya kuleta mgawanyiko basi muda wa kurekebisha hali hiyo upo. 


Waziri Membe aelezea kuhusu Mkutano wa ICGLR


Mhe. Bernard K. Membe (Mb), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa jana alikutana na waandishi wa habari katika ofisi za Wizara ya Mambo ya Nje mjini Dar es Salaam.  Katika mazungumzo yake, Mhe. Waziri Membe alielezea yaliyojiri katika Mkutano wa Wakuu wa Nchi wa Sekretarieti ya Maziwa Makuu (ICGLR) uliofanyika mjini Kampala, Uganda hivi karibuni.  

Waandishi wa habari wakimsikiliza Mhe. Waziri Membe wakati wa mazungumzo nao jana.

Mhe. Waziri Membe akiendelea kuongea na waandishi, wakati Balozi Vincent Kibwana, Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa akisikiliza kwa makini.  

Mhe. Waziri Membe akiongea na waandishi wa habari.


Picha zote na Tagie Daisy Mwakawago 



Waziri Membe aelezea kuhusu Mkutano wa ICGLR
Na Zainabu Abdallah
Wakuu wa Nchi wa Sekretarieti ya Maziwa Makuu (ICGLR) wamemaliza kikao chao kilichofanyika Jijini Kampala, Uganda 05/9/2013. Kikao hicho  kilijadili hali ya kuzorota kwa amani Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) kutokana na mashambulizi yanayoendelea kufanywa na M23 katika mji wa Goma.
Akioengea na Waandishi wa Habari ofisini kwake jijini Dar es Salaam 06 Septemba, 2013, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mheshimiwa  Bernard Membe (Mb) alisema kuwa Wakuu wa Nchi walifikia maamuzi mbalimbali ikiwa ni pamoja na kulaani vikali mashambulizi  ya M23 katika mji wa Goma yaliyosababibisha vifo na majeruhi kwa raia na askari wa kulinda amani.
 Aidha, Wakuu wa Nchi na Serikali walitoa pole kwa Umoja wa Mataifa na Tanzania kutokana na kifo cha Meja  Khatibu Mshindo, mwanajeshi wa Tanzania aliyeuwawa katika shambulio lililofanywa na Kikundi cha Waasi cha M23. Katika shambulio hilo pia wanajeshi watano walijeruhiwa na hali zao zinaendelea vizuri.
Vile vile, Mhe. Membe alisema kuwa ujumbe wa Umoja wa Mataifa ukiongozwa na Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa Nchi za Maziwa Makuu, Mhe. Marry Robinson upo Goma kuangalia hali ya usalama
Katika hatua nyingine, Wakuu wa Nchi waliagiza Serikali ya DRC na M23 kufanya mazungumzo ili kumaliza mgogoro huo kwa amani na kutoa siku 17 kukamilisha zoezi hilo.   Siku tatu kati ya hizo ni kwa ajili ya maandalizi na siku kumi na nne ni kwa ajili ya majadiliano na makubaliano ya kufikia muafaka wa kumaliza mgogoro huo.
Kando ya mkutano huo, Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete alipata fursa ya kuongea na  Rais Paul Kagame wa Rwanda. Katika mazungumzo hayo, Viongozi hao waliazimia kudumisha na kukuza uhusiano wa kihistoria kati ya Tanzania na Rwanda.




Thursday, September 5, 2013

Kaimu Mkurugenzi wa Mashariki ya Kati akutana na Naibu Balozi wa Urusi kwa mazungumzo


Naibu Balozi wa Urusi hapa nchini, Bw. Vincent Kalchenko (kushoto) akimweleza jambo Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Elibariki Maleko wakati wa mazungumzo yao kuhusu mgogoro wa Syria. Mazungumzo hayo yalifanyika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa tarehe 5 Septemba, 2013.

Bw. Maleko akisisitiza jambo wakati wa mazungumzo yao.

Mazungumzo yakiendelea kati ya Bw. Maleko na Bw. Kalchenko huku Bw. Emmanuel Luangisa (kulia), Afisa Mambo ya Nje akinukuu mazungumzo hayo.

Bw. Maleko akiagana na  Bw. Kalchenko mara baada ya mazungumzo yao.