Thursday, March 26, 2015

Rais Kagame awasili Dar es Salaam kushiriki Mkutano wa Uwekezaaji wa Ukanda wa Kati

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe.Bernard K. Membe (Mb) akisalimiana na Rais wa Rwanda Mhe. Paul Kagame  alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Jijini Dar es Salaam. Mhe. Rais Kagame yupo nchini kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi wa Ukanda wa Kati kuhusu Uwekezaji na Viwanda unaofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere.
Rais Kagame akipokea shada la maua kutoka kwa mtoto Elizabeth Jackson kama ishara ya kumkaribisha nchini Tanzania.
Rais Kagame akikagua gwaride la heshima 
Rais Kagame na Waziri Membe wakiangalia burudani ya ngoma za asili uwanjani hapo.
Waziri Membe akiwa ameongozana na Rais Kagame mara baada ya kukagua gwaride na kushuhudia ngoma za asili.



Picha na Reginald Philip.

Wednesday, March 25, 2015

Rais Kikwete afungua Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Ukanda wa Kati


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akifungua Mkutano wa Wakuu wa Nchi zinazounda Ukanda wa Kati yaani Tanzania, Uganda, Burundi, Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC). Ufunguzi huo ulifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam ulihudhuriwa na Rais wa Uganda, Mhe. Yoweri Kaguta Museveni, Rais wa Burundi, Mhe. Pierre Nkurunziza na Mawaziri waliowawakilisha Marais wa DRC na Rwanda. Pamoja na mambo mengine mkutano huo ulijadili umuhimu wakuendelea kuimarisha miundombinu ya nchi za Kanda ya Kati hususan barabara, reli na bandari ili kukuza uwekezaji na maendeleo kwa ujumla.
Rais wa Uganda, Mhe. Yoweri Museveni nae akizungumza wakati wa mkutano huo.
Rais wa Burundi, Mhe. Pierre Nkurunziza nae akizungumza.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (kushoto) akiwa na Waziri wa Uchukuzi, Mhe. Samwel Sitta na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe wakifuatiliaufunguzi wa Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Ukanda wa Kati.
Sehemu ya wageni waalikwa wakati wa ufunguzi wa mkutano huo
Marais na Mawaziri waliowawakilisha viongozi wao wakiwa katika picha ya pamoja.


Waziri Membe awapokea Rais Museveni na Rais Nkurunziza kwa ajili ya Mkutano wa Ukanda wa Kati kuhusu Uwekezaji

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe.Bernard K. Membe (Mb) akimpokea Rais wa Uganda Mhe.Yoweri Kaguta Museveni  alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Jijini Dar es Salaam. Mhe. Rais Museveni yupo nchini kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi wa Ukanda wa Kati kuhusu Uwekezaji na Viwanda unaofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere kuanzia tarehe 25 hadi 26 Machi, 2015.
Rais Museveni akipokea shada la maua kutoka kwa mtoto Balkis Mvungi kama ishara ya kumkaribisha nchini Tanzania.
 Rais Museveni akikagua gwaride la heshima 
Rais Museveni na Waziri Membe wakiangalia burudani ya ngoma za asili uwanjani hapo.
Waziri Membe akiwa ameongozana na Rais Museveni mara baada ya kukagua gwaride na kushuhudia ngoma za asili.

.....Waziri Membe akimpokea Rais wa Burundi Mhe.Piere Nkurunziza.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe.Bernard Membe akimpokea Rais wa Burundi Mhe.Pierre Nkurunziza mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimatafa wa Mwalimu Julius Njerere.
Rais Nkurunziza akipokea shada la maua kutoka kwa mtoto Balkis Mvungi kama ishara ya kumkaribisha nchini Tanzania.
Mheshimiwa Nkurunziza akifurahia ngoma za asili muda mfupi mara baada ya kuwasili.
Waziri Membe akimtambulisha Waziri wa Fedha Mhe. Saada Mkuya kwa Rais Nkurunziza mara baada ya kuwasili nchini.

Picha na Reginald Philip. 

Tuesday, March 24, 2015

Waziri Membe mgeni rasmi Maadhimisho ya miaka 25 ya Uhuru wa Namibia

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akitoa hotuba wakati wa maadhimisho ya miaka 25 ya Uhuru wa Jamhuri ya Namibia. Maadhimisho hayo ambayo yaliandaliwa na Ubalozi wa Namibia hapa nchini yalifanyika katika Hoteli ya Hyatt Regency Jijini Dar es Salaam tarehe 23 Machi, 2015. Namibia ilipata uhuru wake mwaka 1990.
Sehemu ya Mabalozi na Wakuu wa Mashirika ya Kimataifa waliopo hapa nchini wakifuatilia hotuba ya Mhe. Waziri Membe (hayupo pichani) wakati wa maadhimisho ya miaka 25 ya uhuru wa Namibia. Kulia ni Mkuu wa Mabalozi na Balozi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Balozi Juma Alfani Mpango.
Sehemu nyingine ya Mabalozi na Wageni waalikwa wakati wa maadhimisho hayo
Waziri Membe akiwa na Balozi wa Namibia hapa nchini, Mhe. Japhet Isaack wakisikiliza wimbo wa Taifa la Namibia kusherehekea miaka 25 ya uhuru
Balozi Isaack akitoa hotuba wakati wa maadhimisho hayo
Waziri Membe na Balozi Isaack wakikata keki kuadhimisha miaka 25 ya Uhuru wa Namibia
Mabalozi na Wageni waalikwa wakifuatilia matukio wakati wa maadhimisho ya miaka 25 ya uhuru wa Namibia
Wageni waalikwa 
Kikundi cha burudani kikitumbuiza kuadhimisha miaka 25 ya uhuru wa Namibia
===========================================


STATEMENT FOR HON. BERNARD K. MEMBE (MP), MINISTER FOR FOREIGN AFFAIRS AND INTERNATIONAL COOPERATION OF THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA ON THE OCCASION OF COMMEMORATING 25TH INDEPENDENCE ANNIVERSARY OF THE REPUBLIC OF NAMIBIA, 23RD MARCH 2015

Your Excellency,. Japhet Isaack, High Commissioner of the Republic of Namibia,

Your Excellency, Juma Alfani Mpango, Ambassador of the Democratic Republic of Congo and Dean of the Diplomatic Corps,

Your Excellency, Prof. Ambrósio Lukoki, Ambassador of the Republic of Angola and Dean of the African Diplomatic Group,

Your Excellencies Ambassadors and High Commissioners,

Heads of International Organizations,

Distinguished Guests,

Ladies and Gentlemen,

It gives me a great pleasure to grace this historic event of commemorating 25 years of the Independence Anniversary of the Republic of Namibia. On behalf of the Government and people of the United Republic of Tanzania, and indeed on my own behalf, I would like to take this opportunity to extend to Your Excellency, and through you to the Government and the People of the Republic of Namibia, our profound and heartfelt congratulations on the occasion of celebrating this Silver Jubilee.

Your Excellency,
Since independence Namibia has experienced smooth transfer of power. It would be recalled that Namibia held its general elections on 28th November, 2014. The elections were declared peaceful, transparent, free and fair by the Election
observers; I therefore take this opportunity to congratulate Namibia for its maturity in democracy. I would also like to congratulate the ruling party; South West African People’s Organization (SWAPO) for the landslide victory as well as congratulating H.E. Dr. Hage Gottfried Geingob, President of the Republic of Namibia for assuming such high office, his victory is a clear reflection of the confidence reposed in him by the Namibian people.  Moreover on behalf of my government I would like to assure the new Government of the Republic of Namibia the commitment of the Government of the United Republic of Tanzania to work with it closely, for the mutual benefit of our two countries and their peoples.
Excellencies
To many in Africa and the world at large, Namibia was considered as a young country. But to the surprise of many and to our jubilation, the country has grown into an advanced economy unmatched by other African countries. To date, Namibia stands as one of the fastest growing economies in the Southern African region. Its impeccable record in poverty alleviation and improving the living standards of many Namibians has won it many accolades in the world. All these achievements were realized under the excellent leadership of the Namibian leaders, from H.E Sam Nujoma to H.E Hifikepunye Pohamba. With the new leadership in place, we in Tanzania are convinced that H.E Geinghob will uphold the excellent principles set by his predecessors.
Your Excellency,
Two days ago, I attended the 25th Independence Anniversary of the Republic of Namibia in Windhoek. The celebration was one of its kind as it was attended by many dignitaries from across Africa and and beyond. One thing that striked me the most was the high level of patriotism demonstrated by the Namibian people towards their Country and leaders. The peaceful hand over of power from H.E Hifikepunye Pohamba to H.E Dr. Hage Geinghob was done amidst chants and cheers from the thousands of Namibians who attended the celebrations. This is a true testament to the level of democratic maturity that has been achieved by Namibia. What was clear to many is that Namibians have chosen their destiny well. They choose peace, over chaos, political stability over dissent and harmony over instability. In line with its motto, it is clear that unity, liberty and justice prevails in Namibia and it is indeed the land of the brave.
Today’s Celebrations gives us a rare glimpse into the historic events that led to the independence of our long time friend, Namibia. Although, 25 years have passed since Namibia was relieved from colonialism, we cannot help but reminisce how Namibians were strongly united during the liberation struggle to ensure they put an end to colonial domination in their country. That unity went further till postcolonial era, Namibians have worked together to combat poverty and improve the living conditions of the people, thus moving Namibia closer to the realization of their medium- and long-term development objectives. The 2014 Mo Ibrahim Prize for African Leadership awarded to H.E. Hifikipunye Pohamba, Former President of the Republic of Namibia in recognition of the strides that the country has made over the years.
Excellencies,
Tanzania and Namibia enjoy excellent bilateral relations that have existed for time immemorial. These relations go back prior to independence of our sisterly country Namibia. As you may all recall, Tanzania supported Namibia’s liberation struggle. During that time the SWAPO office was here in Dar es salaam. Since that time our relations have remained excellent. It is our sincere hope that the new Government will leverage and translate the relations into more meaningful and beneficial economic relations to reflect the current Economic Foreign Policies of our two countries focusing on Economic Diplomacy as the second phase of Economic Liberalization. 
Your Excellencies,
Relations between Tanzania and Namibia are even stronger on sub-regional, regional and global spheres, our countries have been cooperating well in all matters of common concerns. We have been cooperating very well in  SADC, AU and UN.
­­­­­­
Your Excellencies,
Ladies and Gentlemen,
There is a lot to say about Namibia but today is not a day for making long speeches; it is a day for us to rejoice, a day to look back with satisfaction and to look forward with hope for we need to achieve more.  I therefore would like to conclude by reiterating our sincere congratulations to Your Excellency and, through you, to the Government and the People of the Republic of Namibia on celebrating 25th anniversary of independence. We wish Namibia Government and all Namibians happiness and more expedited progress.
Your Excellency,
Distinguished Guests,
Ladies and Gentlemen,
May I now ask all of you present here to rise and join me in a toast:
·       To the continued good health of H.E. Dr. Hage Gottfried Geingob, President of the Republic of Namibia;

·       To the excellent relations existing between our two sisterly countries;

·       To the continued good health of all of us present here tonight.

 Ahsante Sana

Monday, March 23, 2015

PRESS RELEASE

Prime Minister of Singapore, H.E. Lee Hsien Loong

 PRESS RELEASE

H.E. Dr. Jakaya Mrisho Kikwete, President of the United Republic of Tanzania has sent a condolence message to H.E. Lee Hsien Loong, Prime Minister of Singapore following the death of his father and founding Prime Minister of Singapore, the late Mr. Lee Kuan Yew.

The message reads as follows:

“H.E. Lee Hsien Loong,
Prime Minister of Singapore,
SINGAPORE.


Your Excellency and dear brother,

I am writing to extend my deep condolences and that of the government and the people of the United Republic of Tanzania following the death of your father and founding Prime Minister of your nation Mr. Lee Kuan Yew.

The demise of Prime Minister Yew is a great loss not only to Singapore but also to all who saw in him an example of a nation builder. The late Yew was admired by the people of Tanzania as a leader whose input in building Singapore is immeasurable, a selfless leader and a friend of all.

May sincere wish in remembering the late Yew is to emulate him in practice and always embracing his contribution as a leader and role model.

The People and the Government of the United Republic of Tanzania                        will continue to pray for peace, compassion and strength for the family and the People of Singapore in the time of sorrow and also for the nation as ending’s demise is an immense loss to all Singaporeans.

Your Excellency,

Please accept my condolences and may the Almighty God rest his soul in eternal peace.


Please accept, Your Excellency the assurances of my highest consideration”.

Issued by: The Ministry of Foreign Affairs and International Cooperation, Dar es Salaam

23rd March 2015

Waziri Membe awaasa waimbaji wa nyimbo za injili nchini kuwa chachu ya amani na uadilifu nchini

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard K. Membe (Mb.) amezindua albamu mbili za nyimbo za injili zinazokwenda kwa majina ya "Pisha Mbele" na "Ni Ujumbe wa Bwana" za mwimbaji Mercy Nyagwaswa katika hafla fupi ya uzinduzi iliyofanyika katika Ukumbi wa Ubungo Plaza uliopo Jijini Dar es Salaam tarehe 22 Machi, 2015. 
Askofu Mstaafu na Baba mzazi wa Mercy Askofu Nyagwaswa (wa kwanza kulia) akiwa pamoja na Mchungaji David Mangoti (wa pili kulia) na  Balozi Mstaafu Costa Mahalu wakimsikiliza Mhe. Membe (hayupo pichani) alipokuwa akihutubia wakati wa uzinduzi huo.  
Sehemu ya Wachungaji walioudhuria  uzinduzi wa albamu hiyo.
Mwimbaji wa Nyimbo za Injili, Bi. Mercy Nyagwaswa kulia akiwa na Mwimbaji mwenzake Bi. Upendo Nkone kwa pamoja wakimsikiliza Mhe. Membe ambaye  hayupo pichani alipozindua albamu zake za "Pisha Mbele" na Ni "Ujumbe wa Bwana". Wakati wa uzinduzi huo Waziri Membe alitoa rai kwa waimbaji wa nyimbo za injili nchini kuwa chachu ya amani na uadilifu ili nchi iendelee kuwa na utulivu na upendo. 
Mhe. Membe akiendelea kuzungumza
Bi. Mercy Nyagwaswa na kikundi chake akitoa burudani kwa mgeni rasmi pamoja na wageni waalikwa katika uzinduzi wa Albamu zake
Mhe. Membe na Askofu Mtaafu Nyagwaswa pamoja na wageni waalikwa wengine wakifurahia nyimbo zilizoimbwa na Bi. Mercy wakati wa uzinduzi wa album zake. 
Waziri Membe akikata utepe kuzindua  Albamu mbili za Bi Mercy Nyagwaswa.
Waziri Membe akimpongeza Bi. Mercy kwa kuandaag Albamu mbili kwa mara moja. 
Waziri Membe akiwa katika picha ya pamoja.

Picha na Reginald Philip

Sunday, March 22, 2015

Magari ya Kitalii ya Tanzania ruksa kuingia Uwanja wa Jomo Kenyatta: Waziri Membe



 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akizungumza na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) kuhusu makubaliano ya pamoja yaliyofikiwa kati ya  Serikali za Tanzania na Kenya juu ya kuruhusu tena magari ya kitalii ya Tanzania kuingia Uwanja wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta na kurudisha idadi ya awali ya safari za ndege za Kenya ambazo ni 42. Wengine katika picha ni Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Balozi Rajabu Gamaha (kushoto) na Mkurugenzi wa Kitengo cha Sheria, Balozi Irene Kasyanju.
Sehemu ya Waandishi wa Habari wakimsikiliza Waziri Membe
Sehemu ya Wakuu wa Idara na Vitengo wa Wizara  ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wakifuatlia mazungumzo kati ya Waziri Membe na Waandhishi wa Habari. Kutoka kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Diaspora, Bibi Rosemary Jairo, Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika, Balozi Joseph Sokoine,  Bw. Innocent Shiyo, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kikanda, Balozi Mbelwa Kairuki, Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia na Bi. Mindi Kasiga, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali.


Wakuu wa Idara na Vitengo wakifuatilia mazungumzo ya Waziri Membe na Waandishi wa Habari ambao hawapo pichani. (Picha na Reginald Philip)
================================



JOINT STATEMENT BY FOREIGN MINISTERS OF TANZANIA AND KENYA FOLLOWING THE MEETING BETWEEN HIS EXCELLENCY JAKAYA KIKWETE, PRESIDENT OF TANZANIA AND HIS EXCELLENCY UHURU KENYATTA, PRESIDENT OF KENYA HELD IN WINDHOEK, NAMIBIA ON 21ST MARCH, 2015

His Excellency Jakaya Mrisho Kikwete, President of the United Republic of Tanzania and His Excellency Uhuru Kenyatta, President of the Republic of Kenya met in Windhoek, Namibia on 21st March, 2015 to discuss bilateral issues.

Both Presidents were in Windhoek to attend the 25th Independence Anniversary and Inauguration of the 3rd President of the Republic of Namibia, His Excellency Dr. Hage G. Geingob. Also in attendance were the Foreign Ministers Bernard K. Membe of Tanzania and Ambassador Amina Mohamed of Kenya as well as Engineer Michael Kamau, Kenya’s Transport and Infrastructure Minister. 

The main issues of the meeting revolved around transport and tourism sectors. In particular, the two Heads of State discussed the decision by the Ministry of Tourism of Kenya to bar Tanzania registered vehicles from accessing the Jomo Kenyatta International Airport. They also discussed the decision by Tanzania Civil Aviation Authority to reduce the frequency of Kenya Airways flights operating between Kenya and Tanzanian Airports.

On the two issues under deliberation, the two leaders agreed on the following actions:

1.  To reinstate the status quo. This means, with immediate effect, Tanzania registered vehicles will access the Jomo Kenyatta International Airport as before, while Kenya Airways will continue with its normal operations.

2.  Within four weeks, Ministers of Foreign Affairs will convene and chair a meeting of the parties including Ministers of Transport, Ministers of Tourism and Chiefs of Staffs in the two Presidencies to discuss and reach a mutual beneficial agreement. The first meeting will be held in Dar es Salaam on a date to be agreed by the conveners.

The meeting was held under a very cordial atmosphere with two Heads of State emphasizing the need to continue discuss openly issues affecting the brotherly and a long-standing bilateral relationship that exists between Tanzania and Kenya.

Done in Windhoek, Namibia on 21st March, 2015.




TANZANIA CHILDREN'S PROJECT YAFANYA HARAMBEE KUSAIDIA WATOTO TANZANIA COLUMBIA, MARYLAN

Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Liberata Mulamula akihudhuria harambee ya Tanzania Children's Project inayoshughulisha na miradi ya afya na elimu Tanzania iliyofanyika siku ya Jumamosi March 21, 2015 Columbia, Maryland. Kulia ni Timothy Lynch ambaye ni Rais wa NGO hiyo, Mhe. Balozi Liberata Mulamula aliongozana na Afisa wa Ubalozi Bw. Switebert Mkama(pichani kushoto)
Wadau mbalimbali waliohudhuria harambee ya Tanzania Children's Project iliyofanyika siku ya Jumamosi March 21, 2015 Columbia, Maryland nchini Marekani. 
picha ya pamoja
Picha ya pamoja
Kikundi cha muziki kikitoa burudani.