Wednesday, May 20, 2015

Rais wa Msumbiji Mhe. Filipe Jacinto Nyusi lihutubia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania



Rais wa Msumbiji, Mhe. Filipe Jacinto Nyusi akilihutubia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mara ya kwanza na pia anakuwa Rais wa kwanza wa Msumbiji kulihutubia Bunge la Tanzania. Katika Hotuba yake nzuri Rais Nyusi iliwasifu Waasisi wa Mataifa ya Msumbiji na Tanzania na kusifia mahusiano mazuri yaliyopo kati ya nchi hizi mbili na kuahidi kuimarisha mahusiano katika Siasa na Uchumi. Rais Nyusi alifanya ziara ya kitaifa ya siku tatu ikiwa ni ziara yake ya  kwanza tangu aingie madarakani. 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) wa kwanza kushoto mstari wa pili, pamoja na Wabunge wengine wakisikiliza Hotuba kutoka kwa Mhe. Rais Nyusi (Hayupo pichani)


Katibu Mkuu Kiongozi Mhe. Balozi Ombeni Sefue (Kushoto) naye akisikiliza Hotuba kutoka kwa Rais Nyusi
Viongozi Mbalimbali wa Serikali wakisikiliza Hotuba ya Mhe. Rais Nyusi Bungeni. 
 Balozi wa Tanzania nchni Msumbiji, Balozi Shamimu Nyanduga (kulia)  naye akiwa bungeni akifuatilia Hotuba ya Mhe. Rais Nyusi.
Mkurugenzi wa Habari, Elimu kwa Umma na Uhusiano wa Kimataifa wa Bunge Bw. Jossey Mwakasyuka (Wa kwanza kulia), na Maafisa Mambo ya Nje (wa pili Kulia) ni Bw. Khatibu Makenga akifuatiwa na Bw. Mudrick Soraga (wa tatu Kushoto)
Spika wa Bunge Mhe. Anna Makinda akizungumza
Rais wa Msumbiji, Mhe. Filipe Jacinto Nyusi akipokelewa na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Anna Makinda alipowasili katika Viwanja vya Bunge mjini Dodoma na kupata fursa ya kulihutubia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (katikati) ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete
Mhe. Rais Filipe Jacinto Nyusi akiwa kwenye Jukwaa Maalum wakati nyimbo za Taifa  zikipigwa.
Kikosi cha Brass Bendi cha Jeshi la Polisi kikipiga Nyimbo za Taifa mara baada ya Rais wa Msumbiji, Mhe. Nyusi kuwasili katika Viwanja vya Bungeni Mjini Dodoma
Makaribisho ya Rais wa Msumbiji, Mhe. Nyusi yakiendelea katika viwanja vya Bungeni.
Rais wa Msumbiji akikagua gwaride la Heshima wakati wa mapokezi yake mjini Dodoma.
Rais wa Msumbiji Mhe. Nyusi pamoja na Mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Jakaya Kikwete wakiongozwa kuingia Bungeni na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Anna Makinda.
Rais wa Msumbiji Mhe. Nyusi na mwenyeji wake Rais Jakaya Mrisho Kikwete wakiongozwa na Spika wa Bunge kutoka Nje ya Bunge mara baada ya Kumaliza kulihutubia Bunge.


Kaimu Mkurugenzi Idara ya Afrika, Bi. Zuhura Bundala (wa kwanza kushoto), Katibu wa Waziri wa Mambo ya Nje Bw. Thobias Makoba (watatu kutoka kushoto), na katikati na Bi Talha Mohamed wakiwa Bungeni. 
Rais wa Msumbiji akipokea Picha yenye mwonekano wa Jengo la Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutoka kwa Spika wa Bunge,  Mhe. Anna Makinda huku ikishuhudiwa na Rais Jakaya Mrisho Kikwete (Wa kwanza Kulia).


Rais wa Msumbiji Mhe. Filipe Jacinto Nyusi na Rais Kikwete wakiwa katika picha ya Pamoja na Viongozi wa Serikali na Wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Picha na Reginald Philip

Monday, May 18, 2015

Rais wa Msumbiji awasili Zanzibar.

Rais wa Msumbiji, Mhe. Filipe Jacinto Nyusi akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Zanzibar akitokea Jijini Dar es Salaam,ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake ya kitaifa ya siku tatu nchini Tanzania.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt.Ali Mohamed Shein akiwa ameongozana na mgeni wake Rais wa Msumbiji, Mhe. Filipe Jacinto Nyusi mara baada ya kuwasili katika  Zanzibar leo tarehe 18 Mei, 2015.
 Rais Shein akiwa na Rais Nyusi kwenye Jukwaa Maalum wakati nyimbo za Taifa  zikipigwa kwa heshima ya Rais Nyusi.
 Rais wa Msumbiji Mhe.Nyusi akikagua Gwaride la Heshima wakati wa mapokezi yake. 
 Rais wa Msumbiji, Mhe.Nyusi pamoja na Rais wa Zanzibar Mhe.Dr.Shein wakifurahia burudani ya kikundi cha ngoma wakati wa mapokezi hayo huku Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mhe.Maalim Seif Sharif Hamad (kulia kwa Rais Shein) na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe.Balozi Seif Ali Iddi (kulia) wakifurahia pia burudani hiyo.
 Rais Nyusi na Rais Shein wakiteta jambo wakati wakiangalia burudani ya ngoma za asili.


Kikundi cha Ngoma kikitumbuiza wakati wa mapokezi hayo

Rais wa Zanzibar Mhe. Dkt.Ali Mohamed Shein akiwa na mgeni wake Rais wa Msumbiji pale alipomkaribisha Ikulu kwa mazungumzo.


.....Kuelekea Hotelini


 Halaiki ya Wanafunzi waliokuwa wamejipanga barabarani kusherehesha mapokezi ya Rais wa Msumbiji Visiwani Zanzibar.
 Rais wa Msumbiji akiangalia  mmoja wa watumbuizaji anavyopuliza kifaa chake  kwa ustadi mkubwa huku akiwa  amejilaza chini wakati Rais huyo akiwasili hotelini kwake 

Picha na Reuben Mchome

Rais wa Msumbiji atembelea Chuo cha Diplomasia, afungua Kongamano la Uwekezaji na kuzungumza na Raia wa Msumbiji waishio hapa nchini



Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Simba Yahya akiwajadiliana jambo na Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Diplomasia (CFR),  Balozi Mwanaidi Maajar  huku Mkuu wa Chuo hicho Balozi Mohammed Maundi akisiskiliza wakati viongozi hao wakisubiri kumpokea Rais wa Jamhuri ya Msumbiji, Mhe. Filipe Jacinto Nyusi alipotembelea Chuoni hapo leo tarehe 18 Mei, 2015 wakati akiendelea na ziara yake ya kitaifa ya siku tatu hapa nchini. Chuo cha Diplomasia kilichopo Kurasini, Dar es Salaam kilianzishwa mwaka 1978 kwa ushirikiano kati ya Tanzania na Msumbiji.
Rais wa Jamhuri ya Msumbiji, Mhe. Filipe Jacinto Nyusi akisalimiana na Mkuu wa Chuo cha Diplomasia, Balozi Maundi alipotembelea Chuoni hapo wakati wa ziara yake hapa nchini
Balozi Maundi akiwatambulisha baadhi ya Wahadhiri wa Chuo hicho kwa Mhe. Rais Nyusi
Juu na Chini:  Mhe. Rais Nyusi akizungumza na Wahadhiri, Wanafunzi na Wageni mbalimbali alipotembelea Chuo cha Diplomasia (CFR)
Wajumbe wakifurahia jambo wakati Rais Nyusi (hayupo pichani) alipozungumza nao 
Mhe. Rais Nyusi akifurahia zawadi ya picha ya kuchora inayowaonesha Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere na Rais wa Kwanza wa Msumbiji, Hayati Samora Machel aliyozawadiwa alipotembelea Chuo cha Diplomasia
Rais Nyusi akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi mbalimbali wa Tanzania na Msumbiji pamoja na  Uongozi wa Chuo cha Diplomasia. Kushoto ni  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI, Mhe. Hawa Ghasia (wa kwanza kushoto) ambaye ni Waziri anayeongozana nae kwenye ziara hii.
Mhe. Rais Nyusi akiwa katika picha ya pamoja na Wanafunzi wa Chuo cha Diplomasia
Rais Nyusi akiangalia bango linalosomeka "CHUO HIKI KILIKUWA CHUO CHA ELIMU YA JUU KWA WAPIGANIA UHURU WA AFRIKA" ikiwa ni jina la awali kabla Chuo cha Diplomasia hakijaanzishwa.
Mhe. Rais Nyusi akiangalia Jiwe la Msingi la kuanzishwa kwa Chuo hicho



......Rais Nyusi alipozugumza na Raia wa Msumbiji waishio hapa nchini


Rais wa Msumbiji, Mhe. Filipe Jacinto Nyusi akifurahia kikundi cha ngoma cha Raia kutoka Msumbiji wanaoishi hapa nchini alipowasili kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC) kwa ajili ya kuzungumza nao.

Sehemu ya umati wa Raia wa Msumbiji wanaoishi hapa nchini wakimpokea kwa shangwe Rais Nyusi alipokutana  na kuzungumza nao wakati wa ziara yake ya kitaifa ya siku tatu hapa nchini


Mhe. Rais Nyusi akizungumza na Raia wa Msumbiji waishio hapa nchini (hawapo pichani)


Mhe. Rais Nyusi akipokea zawadi kutoka kwa mmoja wa Raia wa Msumbiji wanaoishi hapa nchini



......Rais Nyusi aliposhiriki Kongamano la Biashara na Uwekezaji 


Rais wa Msumbiji, Mhe. Filipe Jacinto Nyusi akiwasili kwenye ukumbi wa mikutano kwa ajili ya kushiriki na kufungua rasmi Kongamano la kukuza Biashara na Uwekezaji kati ya Tanzania na Msumbiji. Wakati wa Kongamano hilo mada mbalimbali kuhusu fursa za uwekezaji baina ya nchi hizi mbili zilitolewa.

Mhe. Rais Nyusi kwa pamoja na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwekezaji na Uwezeshaji, Mhe. Christopher Chiza (kushoto) wakifuatilia mada za uwekezaji zilizowasilishwa wakati wa kongamano la kukuza uwekezaji kati ya Tanzania na Msumbiji
Wajumbe waliohudhuria kongamano hilo.







Press Release


H.M King Harald V of  Norway
PRESS RELEASE

H.E President Jakaya Mrisho Kikwete of the United Republic of Tanzania has sent a congratulatory message to H.M. King Harald V of Norway on the occasion to celebrate the Norwegian Constitution Day on 17th May, 2015.

The message reads as follows: -

“Your Majesty King Harald V,
   The King of Norway,
   Oslo,
   NORWAY.

It is my pleasure and privilege to extend to you, my heartfelt congratulations on the occasion of your country’s Constitution Day.

Norway and Tanzania have been enjoying excellent bilateral relations over the years. It is my strong desire that these ties of cooperation are maintained and strengthened for the benefit of our two countries and peoples.

I would like to take this opportunity to reaffirm Tanzania’s commitment to working with Norway on matters of mutual interest.

Please accept, Your Majesty, my personal best wishes for your continued good health and peace and prosperity for the people of Norway”.

Issued by the Ministry of Foreign Affairs and International

Co-operation, Dar es Salaam


18th May, 2015

Sunday, May 17, 2015

Rais wa Msumbiji awasili nchini kwa ziara ya kitaifa ya siku tatu


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa ameongozana na mgeni wake Rais wa Msumbiji, Mhe. FilipeJacinto Nyusi mara baada ya kumpokea katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam. Rais Nyusi ameanza ziara yake ya kitaifa ya siku tatu hapa nchini kuanzia tarehe 17 hadi 19 Mei, 2015.
Rais Kikwete akiwa na Rais Nyusi kwenye Jukwaa Maalum wakati nyimbo za Taifa la Tanzania na Msumbiji zikipigwa kwa heshima ya Rais Nyusi
Mhe. Rais Nyusi akikagua Gwaride la Heshima
Gwaride la Heshima likipita mbele ya Marais
JUU na CHINI: Mhe. Rais Kikwete kwa pamoja na mgeni wake Mhe. Rais Nyusi wakifurahia burudani kutoka kwenye vikundi vya ngoma vilivyokuwepo uwanjani hapo wakati wa mapokezi. Wengine wanaoonekana kwenye picha ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard Membe (mwenye tai nyekundu), Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu-TAMISEMI, Mhe. Hawa Ghasia na Waziri wa Mambo ya Nje wa Msumbiji, Mhe. Oldemiro Baloi (mwenye miwani myeusi)
Shamrashamra za mapokezi kama inavyoonekana.




  




Saturday, May 16, 2015

Rais wa Msumbiji kufanya ziara ya kitaifa nchini


Rais wa Msumbiji, Mhe. Filipe Nyusi 

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Msumbiji, Mhe. Filipe Jacinto Nyusi anatarajiwa kuwasili nchini tarehe 17 Mei, 2015 kwa ziara ya Kitaifa ya siku tatu nchini kwa mwaliko wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete.

Mhe. Rais Nyussi atapokelewa na mwenyeji wake Mhe. Rais Kikwete mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere. Mhe. Rais Nyusi atakagua Gwaride la Heshima na kupigiwa mizinga 21.

Baada ya mapokezi hayo, Mhe. Nyusi atafanya mazungumzo ya faragha na Rais Kikwete yakifuatiwa na mazungumzo ya kuimarisha ushirikiano baina ya Tanzania na Msumbiji.

Baadaye siku hiyo ya Mei 17, Mhe. Rais Nyusi atakutana kwa mazungumzo na Mabalozi kutoka Nchi za Afrika waliopo hapa nchini mkutano utakaofanyika katika Hoteli ya Hyatt Regency, Jijini Dar es Salaam na kushiriki Dhifa ya Kitaifa itakayoandaliwa na mwenyeji wake Mhe. Rais Kikwete, Ikulu.

Mhe. Rais Nyusi ambaye ataongozana na Viongozi Waandamizi kutoka Serikali ya Msumbiji atahutubia Kongamano la Biashara litakalowakutanisha Wafanyabiashara wa nchi hizi mbili ambalo litafanyika tarehe 18 Mei, 2015 kwenye Hoteli ya Hyatt Regency Jijini Dar es Salaam.

Aidha, siku hiyo ya tarehe 18 Mei, Mhe. Nyusi atapata fursa ya kukitembelea Chuo cha Diplomasia kinachotambulika kama “Tanzania-Mozambique Centre for Foreign Relations” kilichopo Kurasini ambacho kilianzishwa mwaka 1978 kama mradi wa ubia ili kuendeleza mahusiano ya kindugu ya muda mrefu kwa lengo la kutoa mafunzo ya diplomasia na masuala ya kimataifa kwa manufaa ya wananchi wa nchi hizi mbili.

Mhe. Nyusi atakutana na Raia wa Msumbiji waishio hapa nchini kabla ya kuelekea Zanzibar ambako atafanya mazungumzo rasmi na Mhe. Dkt. Ali Mohammed Shein, Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na pia kuzungumza na raia wa Msumbiji waliopo Zanzibar.

Akiendelea na ziara yake hapa nchini, Mhe. Rais Nyusi ataondoka Zanzibar tarehe 19 Mei, 2015 kuelekea Dodoma. Akiwa Mkoani humo atatembelea Makao Makuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) na kuzungumza na Mwenyekiti wa CCM, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Aidha, Mhe. Rais Nyusi atalihutubia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na baadaye kutembelea Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM).

Mhe. Rais Nyusi anatarajiwa kumaliza ziara yake hapa nchini tarehe 19 Mei, 2015 na kuondokea Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) kurejea Msumbiji.


Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali kwa Umma,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,
Dar es Salaam.
16 Mei, 2015