Saturday, December 12, 2015

Waziri na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wawasili rasmi Wizarani baada ya kuapishwa


Waziri wa Mambo wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa Balozi Augustine Mahiga akila kiapo mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli
Naibu Waziri wa Mambo wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa Mhe. Suzani Kolimba akila kiapo mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula akimkaribisha  Wizarani kwa mara ya kwanza Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Balozi Augustine Mahiga mara alipowasili Wizarani baada ya kuapishwa Ikulu tarehe 12 Desemba, 2015. Aliyesimama pembeni ni Katibu Mkuu wa iliyokuwa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bibi Joyce Mapunjo.
Mhe. Balozi Mahiga akikaribishwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Simba Yahya.
Mhe. Balozi Mahiga akipokea shada la maua kutoka kwa mmoja wa Watumishi wa Wizara Bi. Nsia Paul wakati wa mapokezi yake Wizarani
Naibu Waziri wa  Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Suzan Kolimba akipokea shada la maua kutoka kwa mmoja wa Watumishi wa Wizara Bi. Tagie Mwakawago mara baada ya kuwasili rasmi Wizarani
Wakurugenzi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa wakimpokea Mhe. Waziri Wizarani. Pichani Mhe. Waziri akisalimiana na Balozi Anisa Mbega, Mkurugenzi wa Idara ya Diaspora.
Sehemu ya Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa wakimkaribisha kwa shangwe na furaha Mhe. Balozi Mahiga Wizarani.
Mhe. Waziri akisalimiana na Watumishi wa Wizara waliojitokeza kumpokea mara baada ya kuwasili Wizarani rasmi baada ya kuapishwa.
Katibu Mkuu wa iliyokuwa Wizara Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bibi Mapunjo akijitambulisha rasmi kwa Waziri, Mhe. Balozi Mahiga na Mhe. Naibu Waziri, Mhe. Kolimba (kushoto).
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Simba Yahya akijitambulisha  rasmi kwa Waziri, Mhe. Balozi Mahiga na Mhe. Naibu Waziri, Mhe. Kolimba (kushoto). Mwingine katika picha ni Katibu Mkuu, Balozi Mulamula
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa akiongea jambo wakati wa mapokezi ya Mhe. Waziri na Naibu Waziri.
Waziri, Mhe. Balozi Mahiga kwa pamoja na Naibu Waziri, Mhe. Kolimba wakiwa katika picha ya pamoja na Makatibu Wakuu, Balozi Mulamula na Bibi Mapunjo na Naibu Makatibu Wakuu, Balozi Yahya na Bw. Amantius Msole (wa kwanza kulia)
Picha ya pamoja

Picha na Reginald Philip

Kenya Embassy Celebrates 52 Independece Anniversary

Permanent Secretary at the Minisry of Foreign Affairs, East Africa, Regional and International Cooperation, Amb. Liberata Mulamula who was the Guest of Honor delivers a speech at the reception hosted by the Kenya Embassy to mark 52 years of Independence.

Kenyan Ambassador to Tanzania, H.E Chirau Ali Mwakwere presents a statement at the 52 Independece anniversary reception held at his residence yesterday.

Invited guests who were Diplomatic Community in the country, government officials and Private Sector follow attentively the statements delivered by the Guest of Honor and Kenyan Ambassador to Tanzania.

Permanent Secretary at the Minisry of Foreign Affairs, East Africa, Regional and International Cooperation, Amb. Liberata Mulamula (L) and Ambassador of Kenya to Tanzania, H.E Chirau Ali Mwakwere raise their glasses in a toast to the health of the Presidents of Tanzania and Kenya and prosperity of these two nations.

Director of Africa Department at the Minisry of Foreign Affairs, East Africa, Regional and International Cooperation, Amb. Samuel Shelukindo (L) exchanges views with Comoros Ambassador to Tanzania, H.E Dr. Ahamada El Badaoui Mohamed during the reception.

Amb. Mulamula (C) chats with the various Diplomats at the Reception.

Invited guests including Medard Ngaiza (R) official from the Ministry of Foreign Affairs enjoy their snacks during the reception.

Executive Director of the Tanzania Investment Centre (TIC), Ms. Juliet R. Kairuki shakes hands with Kenyan Embassy official during her arrival at the reception to mark 52 anniversary of Kenya Independence.

Friday, December 11, 2015

ushiriki wa Tanzania katika Mkutano wa Shirika la Msalaba Mwekundu Duniani jijini Geneva

Pichani ni ushiriki wa Tanzania katika Mkutano wa Shirika la Msalaba Mwekundu Duniani ambao Rais wa Msalaba Mwekundu Tanzania ambapo Dr. Zainab Amir Gama na Mh. Balozi Modest Mero wanashiriki jijini Geneva Uswisi.  Mkutano hio ulioanza tarehe 4 Desemba na utaisha leo tarehe 10 Disemba 2015. Huu ni mkutano mkuu wa Msalaba Mwekundu na Hilari Nyekundu wa dunia ambao maudhui ya mkutano huu ni mjadala na maamuzi ya uongozi, amani, uhamiaji na  unyanyasaji wa wanawake na watoto,  mpango wa kupanua huduma za kibinadamu kufikiakaribu bilioni moja ifikapo mwaka 2030,  umuhimu wa jumuiya za Msalaba Mwekundu na Hilari Nyekundu kuwa mdau mkuu wa serikali bila ya kwenda kinyume na misingi yao saba mwisho,  ushiriki wa vijana na  vile vile kuikaribisha nchi ya Tuvalu kuwa mwanachama wa 190.

Thursday, December 10, 2015

Tawi la TUGHE-Wanawake la Mambo ya Nje wakutana kupanga mikakati ya utendaji kazi

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje n aUshirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula akiwa na Bibi Amisa Mwakawago, Mwenyekiti wa Tawi la TUGHE-Wanawale la Wizara katika Mkutano na wanachama wa Tawi hilo uliofanyika Wizarani hivi karibuni kujadili malengo mbalimbali waliyojiwekea katika utekelezaji wa majukumu ya kazi na yale yanayohusu maendeleo yao. Balozi Mulamula  pia ni Mama Mlezi wa Tawi la TUGHE Wanawake la Wizara.
Sehemu ya Wanawake wakimsikiliza Balozi Mulamula
Mmoja wa Wanachama, Bi. Mindi Kasiga akichangia wakati wa mkutano huo. Kulia ni Mjumbe wa Tawi, Bi. Grace Martin
Balozi Mulamula  kwa pamoja na Bi Mwakawago wakimsikiliza Bi. Kasiga (hayupo pichani) alipochangia mada
Katibu wa Tawi, Bi. Annagrace Rwalanda akitoa ufafanuzi kwa baadhi ya agenda zilizowasilishwa wakati wa mkutano huo.
JUU NA CHINI: Sehemu ya wanachama wakifuatilia mkutano
Wanachama wakisikiliza hoja mbalimbali wakati wa mkutano

Sehemu nyingine ya wanachama

Wanachama wakifuatilia mada na matukio wakati wa mkutano huo






Wednesday, December 9, 2015

Wizara ya Mambo ya Nje na Siku ya Uhuru - 9 Desemba 2015

Tangazo la kurasa za Google Swahili mahsusi kwa siku ya Uhuru wa Tanzania Bara tarehe 9 Disemba 2015. Kufuatia tamko la Mhe. Rais John Pombe Magufuli la kuadhimisha siku hiyo kwa kufanya usafi, Wakuu wa Idara na Vitengo wa Wizara ya Mambo ya nje wameshiriki kwenye zoezi la usafi kwenye maeneo ya makazi yao. Pia mabalozi wanaoziwakilisha nchi zaohapa wameitikia wito huo na kufanya usafi kwenye maeneo mbalimbali jijini Dar es salaam. 

Balozi Liberata Mulamula, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa akiwa katika zoezi la usafi kwenye uzio wa nyumba yake maeneo ya Mbezi jijini Dar es salaam ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Tanzania Bara tarehe 9 Disemba 2015



Nje ya uzio wa nyumba ya Balozi Simba Yahya, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa baada ya kufanyiwa usafi kwenye maeneo ya Mbweni jijini Dar es salaam katika kuadhimisha siku ya Uhuru wa Tanzania Bara tarehe 9 Desemba 2015.

Balozi Mohammed Juma Maharage, Mkuu wa Itifaki na Mkurugenzi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, akiwa kwenye zoezi la usafi kwenye gari maalum la "Rapid Deployment Unit" huko nyumbani kwake maeneo ya Makongo Juu, jijini Dar es salaam.


Mhe. Juma Khalfan Mpango, Balozi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Kiongozi wa Mabalozi wa wanaoziwakilisha nchi zao hapa Tanzania naye akiwa kwenye zoezi la usafi nje ya ofisi za ubalozi maeneo ya Upanga jijini Dar es salaam. Usafi huo ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya uhuru kufuatia maagizo ya Mhe. Rais John Pombe Magufuli ambapo kauli mbiu ya maadhimisho ya mwaka huu ni Uhuru na Kazi. 


Balozi Mbelwa Kairuki, Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa naye akisafisha maeneo ya pembezoni mwa bararabara kuu inayopita nyumbani kwake, Migombani maeneo ya Mikochini jijini Dar es salaam. 
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Wizara ya Mambo ya Nje Bi. Mindi Kasiga akisafisha ngazi za jengo la makazi yake Garden Avenue, jijini Dar es salaam ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya uhuru tarehe 9 Disemba 2015. 

Jumuiya ya Wachina wanaoishi hapa nchini wakifanya usafi kwenye maeneo yao ya kazi huku bendera ya nchi yako ikipepea ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya uhuru wa Tanzania Bara tarehe 9 Disemba 2015.

MHE.BALOZI WILSON M. MASILINGI ATEMBELEA KITENGO CHA VISA KATIKA OFISI ZA UBALOZI WA TANZANIA, WASHINGTON D.C, SIKU YA KUMBUKUMBU YA UHURU, TAREHE 9 DISEMBA, 2015

 Mhe. Balozi Masilingi akisalimiana na Bi. Mariam Mkama, Mtumishi wa Ubalozi, kitengo cha Visa
Mhe. Balozi Wilson M. Masilingi akizungumza na Mkuu wa Kitengo cha Visa na huduma za Uhamiaji na wafanyakazi wa kitengo hicho na watumishi wengine. Kulia ni Bi. Swahiba H. Mndeme, Mkuu wa Utawala na Fedha, Ubalozini.
Mhe. Balozi Wilson M. Masilingi (kulia) akipolewa na Bw. Abass Missana, Mkuu wa Kitengo cha Visa na huduma za Uhamiaji ubalozini hapo.
Mhe. Balozi Masilingi akisalimiana na mmoja wa wateja wa Visa aliyefika Ubalozini kupata huduma hiyo
Mhe. Balozi Masilingi akizungumza na Bw. Arnold NzuaMtemi Nzali wa Las Vegas, Nevada aliyefika Ubalozini kupata huduma ya Pasipoti        
=================================

Katika kutekeleza agizo la Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Ubalozi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Washington D.C umeendelea kufanya kazi na kutoa huduma za Visa na Pasipoti kama sehemu ya maadhimisho ya sikukuu hiyo. 

 Pamoja na kazi zingine za Ubalozi kuendelea kama kawaida, Mhe. Balozi Wilson M.Masilingi alitembelea kitengo cha Visa na huduma za Uhamiaji na kufanya mazungumzo mafupi na Mkuu wa Kitengo hicho Bw. Abbas A. Missana, Afisa Mambo ya Nje Mwandamizi, (Minister Plenipotentiary).  Bw. Missana alimweleza Mhe. Balozi kuwa kumekuwa na ongezeko la wageni wanaokuja Ubalozini kuchukua Visa, mara baada ya Uchaguzi Mkuu uliofanyika tarehe 25 Oktoba, 2015 kumalizika salama. 

Hapo awali, kabla ya uchaguzi idadi ya wageni waliokuwa wanafika Ubalozini kuomba Visa ilipungua kwa kiasi kikubwa.

 Mhe. Balozi aliwapongeza Wafanyakazi wa Ubalozi kwa kuitikia wito wa “Uhuru na Kazi” kwa hamasa kubwa, jambo linalodhihirisha uzalendo na kuheshimu miongozo sahihi toka kwa Mkuu wa Nchi na wasaidizi wake. 

Aidha, aliwataka Watumishi wa Ubalozi kuendelea kuboresha huduma kwa wateja ili kulinda heshima ya nchi yetu.