Tuesday, September 27, 2016

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje apokea msaada kutoka Burundi kusaidia waathirika wa tetemeko Kagera

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Susan Kolimba akipokea msaada wa chakula kutoka kwa Mhe. Leontine Nzeyimana, Waziri wa Afrika Mashariki wa Burundi ikiwa ni msaada kutoka Serikali ya Burundi kwa ajili ya Waathirika wa tetemeko la ardhi huko Mkoani Kagera.  Msaada huo ni pamoja na mchele tani 100, sukari tani 30, mahindi tani 50 na majani ya chai tani 3.
Mhe. Dkt. Kolimba akitoa shukrani za dhati kwa niaba ya Serikali kwenda Serikali ya Burundi baada ya kupokea msaada huo wa chakula.
Mhe. Nzeyimana naye akitoa salamu za pole za Rais wa Burundi, Mhe. Pierre Nkurunziza kwa Serikali ya Tanzania kufuatia tetemeko hilo.
Mhe. Dkt. Kolimba akiwa katika picha ya pamoja Mhe. Nzeyimana na wadau wengine. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Meja Jenerali Mstaafu Salim Mustafa Kijuu akifuatiwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani wa Burundi.





Monday, September 26, 2016

TANZANIA YATAKA USHIRIKIANO KATIKA VITA DHIDI YA RUSHWA NA UKWEPAJI KODI


Tanzania imeeleza kwamba juhudi za serikali ya awamuya Tano za kukabiliana na  vitendo vya rushwa  hazitawezakufanikiwa kama havita ungwa mkono na  jumuiya ya kimataita.

Ni kwa sababu hiyo, Tanzania, inazitaka nchi zilizoendelea kuwawajibisha wawekezaji wao na makampuni yao ili  yalipe kodi.

Hayo yameelezwa jana  jumatatu na  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa  Afrika Mashariki, Dkt. Agustine Mahiga (Mb)  wakati alipolihutubia  Baraza Kuu la 71la Umoja wa Mataifa na kutumia  fursa hiyo kuelezea vipaumbele vya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Waziri Mahinga akafafanua kwamba, lengo nambakumi na sita la  maendeleo endelevu linatambua kuwa,  rushwa inakandamiza juhudi za kumbana na  umaskini na   usawa wa jinsia,  inazuia fursa na inakuwa na kama kodi kwa familia maskini pale wanapotafuta  haki.

Ni katika muktadha  huo,   akasema, serikali  ya Tanzania imeamua kuanzisha vita dhidi ya rushwa  kwa kuhuisha uwazi, uwajibikani  na usahihi katika utoaji wa huduma  kwenye taasisi za  umma.

Akasisitiza kwamba serikali  imeweka misingi mizuri ya uwajibikaji inayomtaka mtumishi wa umma kutambua kwamba  wajibu wake wa kwanza ni  kutoa huduma bora na kwa wakati kwa umma.

“Juhudi hizi za serikali za kupambana na rushwa hazitaweza kuzaa matunda bila ya kuungwa mkono wa jumuiya ya kimataifa. Nchi zilizoendelea zinatakiwa  kuwawajibisha wawekezaji wao  pamoja na makampuni yao ili  waweze kulipa kodi stahiki.” Akaeleza zaidi  Waziri  Mahinga

Na  kuongeza. “Ni lazima wawe tayari kurudisha mali na fedha  zilizoibwa kutoka nchi zinazoendelea na kuzificha katika nchi zao ili mali  na fedha hizo ziweze kusaidia maendeleo  yetu”.

Kuhusu fursa za jinsia na uwezeshwaji wa wanawake, Waziri Mahinga ameelezea juhudi mbalimbali ambazo zimefanywa na serikali katika kuwawezesha  wawanake ikiwamo kushika ngazi za juu za maamuzi kuanzia serikali kuu  hadi bunge na uwezeshwaji wa kiuchumi.

katika kudhibitisha kuwa Tanzania  inazingatia usawa wa jinsia katika uteuzi wa ngazi  mbalimbali za maamuzi, Waziri Mahinga  ameeleza kwamba kwa mara ya kwanza  wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, Mhe. Dkt. Rais John Pombe Magufuli  alimchangua mwanamke  kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

“Uteuzi  huu unathibitisha nia ya nchi yangu ya kuona wanawake  wengi zaidi wanakuwa katika   nafasi za ngazi za  juu  za maamuzi. Na ajenda hii ya uwezeshwaji wa wanawake wa Tanzania sasa inamilikiwana wanawake wenyewe” akasisitiza  Waziri

 Kwa upande wa vijana, Kiongozi huyu wa Ujumbe wa Tanzania ambaye amemwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  amesema. Vijana ni nguzo muhimu kwa maendeleo ya taifa lolote lile, siyo tu kwamba ni viongozi wa kesho lakini pia ni viongozi wa sasa.

Akatahadharisha kwamba kwa  kutowapa kiupaumbele vijana  ni kujitafutia  matatizo makubwa kutokana na kile alichosema ni rahisi  kurubuniwa na makundi ambayo ni
hatari kwa ustawi wa jamii na taifa .

“ Kutoka na  kwamba idadi ya vijana ni kubwa,  Serikali inachukua hatua mbalimbali za  kuliwezesha kundi hili la jamii ambalo ni muhimu katika utekelezaji wa ajenda 2030. Na ili vijana   waweze kutekeleza  jukumu hilo  Serikali imeanzisha  mfuko wa maendeleo wa  vijana mfuko ambao hadi mwezi March mwaka huu jumla ya  shiling 1.6 bilioni
zilipelekwa  kwa vikundi 284 ya  vijana”.

 Kuhusu elimu, eneo ambalo ni kipaumbele kingine cha Tanzania,   Waziri ameeleza kuwa   upatikanaji wa elimu jumuishi  na ya viwango ndicho kipaumbele cha serikali
kwa  kuwa    Serikali inaamini kuwa, elimu ni  ni nyenzo muhimu   kwa maendeleo endelevu

Akafafanua  kwamba serikali  inatekeleza bila kuchoka kuhakikisha kwamba  watoto wote wa kike na wa kiume wanapata  elimu bure kuanzia shule ya msingi hadi sekondari. Pamoja na kutoka   Elimu bure, Serikali imeboresha mitaala yake kwa kuzingatia mahitaji ya karne ya 21.

“Alipoingia madarakani,  Mhe.  John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alitangaza kwamba kuanzia elimu ya msingi  hadi sekondari itakuwa bure. Serikali  imetenga zaidi ya  shilingi 263 bilioni ili Kuhakikisha elimu  inakuwa bure kwa wote.

Vipaumbele vingine vya  Tanzania ambavyo Mhe. Waziri amevianisha katika  hotuba  yake ni pamoja na  mikakati ambayo  serikali imejiwekea  katika utekelezaji wa mkatabawa mabadiliano ya tabia nchi ( Paris Agreement),  utekelezaji wa   malengo ya maendeleo endelevu ( agenda 2030), mapambano dhidi ya  dawa haramu za kulevya,  na kukabiliana na  ugaidi ambao  amesema  ni tatizo ambalo linaendelea kukua na kuwa tishio  hata kwa  nchi za Afrika Mashariki.




Kwa upande wa utekelezaji wa  agenda 2030, Waziriamesema agenda hiyo imeanishwa  katika mipango ya kitaifa ya  miaka  mitano ya maendeleo  kwa pande zote za muungano.  Hata hivyo  amesema kuwa Tanzania  imebaini kwamba haitaweza kukamilisha kwa  wakati agenda 2030 pasipo kushirikiana na wadau  mbalimbali  wa maendeleo. 

Kuhusu  migogoro inayoendelea katika nchi za Burundi na Sudani ya Kusini, Waziri Mahiga amezitaka pande zote zinazopingana  nchi Burundi kutambua kwamba majadiliano ambayo ni jumuishi kwa pande zote ndiyo  njia sahihi ya kutatua matatizo ya nchi yao.

Kwa upande wa Sudani ya Kusini,  Waziri  amesema Tanzania inaungana na   nchi nyingine kulaani matukio ya hivi karibuni ya kujirudia kwa machafuko nchini humo.

Na kuongeza,  Tanzania ambaye ni  Mwenye -Kiti wa sasa wa Jumuiya ya Afrika Mashariki,  iliitisha Kikao kisicho cha kawaida ili  kuzungumzia hali ya kisiasa ya Burundi na Sudani ya Kusini. “ Tunatumaini kwamba nchi  zote mbili  zitaweka maslahi  ya wananchi wao mbele ili kumaliza machafuko”.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa  Afrika Mashariki pia aligusia kuhusu marekebisho ya mfumo wa   Baraza  Usalama la Umoja wa Mataifa,  ili liwe jumuishi. 


Kwa upande wa   Uchaguzi wa Katibu Mkuu, Waziri amesema,Tanzania  inaunga mkono  hoja ya kuendelea  kuheshimu utaratibu wa kupokezana nafasi ya  Katibu Mkuu kwa kuzingatia mzunguko wa   kijiographia. 


Waziri wa Mambo ya Nje  na  Ushirikiano wa  Afrika Mashariki, Dkt. Augustine Mahiga  anayemwakilisha  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mhe. John Pombe Magufuli katika  Mkutano wa 71 wa Baraza Kuu  la Umoja wa Mataifa akiwasilisha mbele  ya wajumbe waliohudhuria mkutano huo  ( hawapo pichani) vipaumbele vya Tanzania.
 Balozi wa Tanzania nchi Marekani  Wilson  Masilingi akimpa  mkono wa pongezi Waziri  Mahiga  baada kumaliza hotuba yake mbele ya   wajumbe wa  mkutano wa  71 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.
Mhe.  Anna Lupembe   Mbunge wa Viti Maalum (CCM) naye akimpongeza Mhe, Waziri kwa hotuba yake iliyopokelewa vizuri.


Dk. Tausi Kida Mkurugenzi  Mtendaji wa  ESRF naye  akimpongeza  Kiongozi wa Ujumbe wa Tanzania  katika Mkutano wa  71 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.
Baadhi ya Wajumbe wa  Mkutano wa 71 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa wakiwa  katika mstari tayari kumpa mkono  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Augustine Mahiga  mara baada ya kumaliza hotuba yake
 

Saturday, September 24, 2016

Wizara yashiriki maadhimisho ya 86 ya Ufalme wa Saudii Arabia

Rais Mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Pili ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Ali Hassan Mwinyi akisalimiana na Maafisa wa Ubalozi wa Saudi Arabia nchini waliojitokeza kumpokea wakati wa hafla ya kuadhimisha  miaka 86 ya Ufalme wa Saudi Arabia iliyofanyika katika Hoteli ya Hyatt Jijini Dar es Salaam
Kaimu Balozi wa Saud Arabia nchini, Bw. Bandar Abdullah Alhazani akizungumza wakati wa hafla ya maadhimisho ya Siku ya Ufalme wa Saudi Arabia.
Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Kamishna Ngosha Magonya akizungumza wakati wa hafla ya maadhimisho ya Siku ya Ufalme wa Saudi Arabia.
Rais Mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Pili ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Ali Hassan Mwinyi  akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi na watendaji wa Serikali na Waheshimiwa Mabalozi walioshiriki maadhimisho hayo

Thursday, September 22, 2016

BAN KI MOON AISIHI TANZANIA ISICHOKE KUZISAIDIA NCHI ZENYE MIGOGORO

Katibu Mkuu Ban Ki Moon alipomkaribisha Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dk. Augutine Mahiga ambaye anamwakilisha Rais John Pombe Magufuli katika Mkutano wa 71 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa 
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon na ujumbe wake akiwa katika Mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki anayeongoza Ujumbe wa Tanzania katika Mkutano wa 71 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.    
Ban Ki Moon akimkabidhi kitabu Waziri Mahiga, kitabu ambacho Mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa anasema kimeandika na kuelezea utekelezaji wa majukumu yake na kwamba ni kitabu kizuri kutumika kama hadidu ya rejea.

********************************************
Na Mwandishi Maalum, New York 

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon, ameitaka Tanzania kuendelea na kazi nzuri ya usuluhishi wa migogoro katika baadhi ya nchi za Maziwa Makuu.Ban Ki Moon ametoa wito huo jana ( jumatano) wakati alipokutana Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dk. Augustine Mahiga, ambaye anamwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika mkutano wa 71 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa unaoendelea hapa Jijini New York, Marekani.Katika mazungumzo hayo Mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa amesema, Tanzania ni kutovu cha Amani, usalama na demokrasia, na kutokana na sifa hizo Tanzania, inapashwa kuendelea na juhudi zake za kuzisaidia nchi zenye migogoro.

Akazitaja nchi hizo kuwa ni Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, Burundi na Sudani ya Kusini ambayo ameitaja kuwa ipo katika kipindi kigumu sana. “ Ninawashukuru sana viongozi wa Serikali ya Tanzania kwa kazi nzuri ya utafutaji wa Amani katika nchi zenye matatizo, Sudani ya Kusini ni nchi ambayo inatupa mashaka makubwa. Rais asaidie katika kurejesha hali ya utulivu.Tanzania ni nchi kubwa kwa hiyo bado ninaendelea kuitumainia.” akasisitiza Ban Ki Moon.Vile vile Katibu Mkuu Ban Ki Moon ametoa pia shukrani wa ushiriki wa Tanzania katika operesheni za ulinzi wa Amani na kazi na weledi mkubwa unaoonyeshwa na wanajeshi wa Tanzania.

Akatumia fursa hii kuishukuru Tanzania na viongozi wake kwa mchango wao mkubwa uliofanikisha yeye kuchaguliwa kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa. Na akatoa pole zake kwa serikali na kwa watanzania baada ya kupata taarifa kuhusu tetemeko la ardhi lililosababisha vifo na uharibifu wa mali.

“Naishukuru sana Tanzania, namshukuru Rais Mstaafu Jakaya Kiwete na wewe ( Waziri) na viongozi wengine, mlichangia sana kwangu mimi kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa. Ninawashukuru sana sana. ” .Katibu Mkuu Ban Ki Moon anamaliza kipindi chake cha uongozi cha miaka kumi mwishoni wa Mwaka huu.Na tayari mchakato wa upigaji kura wakumtafuta mrithi wake unaendelea katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.Kwa upande wake, akiwasilisha salamau za Rais John Pombe Magufuli, Waziri Mahiga amesema. “ Ninawasilisha salamu za Mhe. Rais, alipenda sana kuhudhuria mkutano huu wa 71 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, kwa bahati mbaya ilimbidi kuahirisha safari yake kutokana na tetemeko la ardhi lililotokea hivi karibu nchini kwetu ”.
Aidha Waziri Mahinga ametumia pia fursa hiyo kumshukuru na kumpongeza Katibu Mkuu kwa utekelezaji wa kutukuka wa majukumu yake katika kipindi cha miaka kumi ya uongozi wake. 

“Kwa niaba ya serikali ya Tanzania nikupongeza kwa utekeleaji wa majukumu yake. Ulionyesha ushirikiano wa karibu na Tanzania, ushirikiano uliokuwezesha kumteua Dkt. Asha-Rose Migiro kuwa Naibu Katibu Mkuu na msaidizi wako wa karibu. Lakini pia uliniteua mimi kuwa Mjumbe wako Maalum huko Somalia . Tanzania inashukuru kwa haya na mengine” akasema Mahiga. 


Aidha amemwelezea Katibu Mkuu kama kiongozi ambaye aliifanya Afrika kuwa kipaumbele chake, lakini pia aliibeba sana ajenda ya wanawake jambo ambalo amesema limemjenga sifa kubwa.Akizungumzia kuhusu Tanzania kuendelea na juhudi za usuluhishi wa migogoro. Waziri amemhakikisha Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwamba, Tanzania na viongozi wake wataendelea na kujukumu hilo.

“Ni kuhakikishie kwamba Serikali yangu itendelea na jukumu hili la usuluhisi. Na kwa upande wa Burundi Tanzania, inaushukuru Umoja wa Mataifa, kwa kutambua na kuamini kwamba Jumuiya ya Afrika Mashariki inaweza kuushughulikia mgogoro huu. Tanzania ambayo imekabidhiwa jukumu la uwezeshaji wa mazungumzo ya Amani inataka kufanya kazi kwa karibu na Umoja wa Mataifa hivyo misaada ya hali na mali kutoka Idara za Umoja wa Matifa ni jambo muhimu”.Amesisitiza Waziri Mahiga.