Tanzania imeeleza
kwamba juhudi za serikali ya awamuya Tano za kukabiliana na vitendo
vya rushwa hazitawezakufanikiwa kama havita ungwa mkono
na jumuiya ya kimataita.
Ni kwa sababu hiyo, Tanzania, inazitaka nchi zilizoendelea kuwawajibisha
wawekezaji wao na makampuni yao ili yalipe kodi.
Hayo yameelezwa jana jumatatu na Waziri wa Mambo ya Nje
na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Agustine Mahiga (Mb)
wakati alipolihutubia Baraza Kuu la 71la Umoja wa Mataifa na
kutumia fursa hiyo kuelezea vipaumbele vya Serikali ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania.
Waziri Mahinga akafafanua kwamba, lengo nambakumi na sita la maendeleo
endelevu linatambua kuwa, rushwa inakandamiza juhudi za kumbana na
umaskini na usawa wa jinsia, inazuia fursa na inakuwa na
kama kodi kwa familia maskini pale wanapotafuta haki.
Ni katika muktadha huo, akasema, serikali
ya Tanzania imeamua kuanzisha vita dhidi ya rushwa kwa kuhuisha uwazi,
uwajibikani na usahihi katika utoaji wa huduma kwenye taasisi
za umma.
Akasisitiza kwamba serikali imeweka misingi mizuri ya uwajibikaji
inayomtaka mtumishi wa umma kutambua kwamba wajibu wake wa kwanza
ni kutoa huduma bora na kwa wakati kwa umma.
“Juhudi hizi za serikali za kupambana na rushwa hazitaweza kuzaa
matunda bila ya kuungwa mkono wa jumuiya ya kimataifa. Nchi zilizoendelea
zinatakiwa kuwawajibisha wawekezaji wao pamoja na makampuni yao
ili waweze kulipa kodi stahiki.” Akaeleza zaidi Waziri
Mahinga
Na kuongeza.
“Ni lazima wawe tayari kurudisha mali na fedha zilizoibwa kutoka nchi zinazoendelea
na kuzificha katika nchi zao ili mali na fedha hizo ziweze kusaidia maendeleo
yetu”.
Kuhusu fursa za jinsia na uwezeshwaji wa wanawake, Waziri Mahinga
ameelezea juhudi mbalimbali ambazo zimefanywa na serikali katika kuwawezesha
wawanake ikiwamo kushika ngazi za juu za maamuzi kuanzia serikali kuu
hadi bunge na uwezeshwaji wa kiuchumi.
katika kudhibitisha kuwa Tanzania inazingatia usawa wa jinsia katika
uteuzi wa ngazi mbalimbali za maamuzi, Waziri Mahinga ameeleza
kwamba kwa mara ya kwanza wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka
2015, Mhe. Dkt. Rais John Pombe Magufuli alimchangua mwanamke
kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
“Uteuzi huu unathibitisha nia ya nchi yangu ya kuona wanawake
wengi zaidi wanakuwa katika nafasi za ngazi za juu za maamuzi.
Na ajenda hii ya uwezeshwaji wa wanawake wa Tanzania sasa inamilikiwana
wanawake wenyewe” akasisitiza Waziri
Kwa upande wa vijana, Kiongozi huyu wa Ujumbe wa Tanzania ambaye amemwakilisha
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, amesema. Vijana ni nguzo
muhimu kwa maendeleo ya taifa lolote lile, siyo tu kwamba ni viongozi wa kesho
lakini pia ni viongozi wa sasa.
Akatahadharisha kwamba kwa kutowapa kiupaumbele vijana ni
kujitafutia matatizo makubwa kutokana na kile alichosema ni rahisi
kurubuniwa na makundi ambayo ni
hatari kwa ustawi wa jamii na taifa .
“ Kutoka na kwamba idadi ya vijana ni kubwa, Serikali inachukua
hatua mbalimbali za kuliwezesha kundi hili la jamii ambalo ni muhimu katika
utekelezaji wa ajenda 2030. Na ili vijana waweze kutekeleza
jukumu hilo Serikali imeanzisha mfuko wa maendeleo wa
vijana mfuko ambao hadi mwezi March mwaka huu jumla ya shiling 1.6
bilioni
zilipelekwa kwa vikundi 284 ya vijana”.
Kuhusu elimu, eneo ambalo ni kipaumbele kingine cha Tanzania,
Waziri ameeleza kuwa upatikanaji wa elimu jumuishi na ya
viwango ndicho kipaumbele cha serikali
kwa kuwa Serikali inaamini kuwa, elimu ni ni
nyenzo muhimu kwa maendeleo endelevu
Akafafanua kwamba serikali inatekeleza bila kuchoka kuhakikisha
kwamba watoto wote wa kike na wa kiume wanapata elimu bure kuanzia
shule ya msingi hadi sekondari. Pamoja na kutoka Elimu bure, Serikali
imeboresha mitaala yake kwa kuzingatia mahitaji ya karne ya 21.
“Alipoingia madarakani, Mhe. John Pombe Magufuli, Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alitangaza kwamba kuanzia elimu ya msingi
hadi sekondari itakuwa bure. Serikali imetenga zaidi ya
shilingi 263 bilioni ili Kuhakikisha elimu inakuwa bure kwa wote.
Vipaumbele vingine vya Tanzania ambavyo Mhe. Waziri amevianisha
katika hotuba yake ni pamoja na mikakati ambayo
serikali imejiwekea katika utekelezaji wa mkatabawa mabadiliano ya tabia
nchi ( Paris Agreement), utekelezaji wa malengo ya maendeleo
endelevu ( agenda 2030), mapambano dhidi ya dawa haramu za kulevya,
na kukabiliana na ugaidi ambao amesema ni tatizo
ambalo linaendelea kukua na kuwa tishio hata kwa nchi za Afrika Mashariki.
Kwa upande wa utekelezaji wa agenda 2030, Waziriamesema agenda hiyo
imeanishwa katika mipango ya kitaifa ya miaka mitano
ya maendeleo kwa pande zote za muungano. Hata hivyo
amesema kuwa Tanzania imebaini kwamba haitaweza kukamilisha kwa
wakati agenda 2030 pasipo kushirikiana na wadau mbalimbali wa
maendeleo.
Kuhusu migogoro inayoendelea katika nchi za Burundi na Sudani
ya Kusini, Waziri Mahiga amezitaka pande zote zinazopingana nchi Burundi
kutambua kwamba majadiliano ambayo ni jumuishi kwa pande zote ndiyo njia
sahihi ya kutatua matatizo ya nchi yao.
Kwa upande wa Sudani ya Kusini, Waziri amesema Tanzania
inaungana na nchi nyingine kulaani matukio ya hivi karibuni ya
kujirudia kwa machafuko nchini humo.
Na kuongeza, Tanzania ambaye ni Mwenye -Kiti wa sasa
wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, iliitisha Kikao kisicho cha kawaida
ili kuzungumzia hali ya kisiasa ya Burundi na Sudani ya Kusini.
“ Tunatumaini kwamba nchi zote mbili zitaweka maslahi ya
wananchi wao mbele ili kumaliza machafuko”.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki pia aligusia
kuhusu marekebisho ya mfumo wa Baraza Usalama la Umoja wa
Mataifa, ili liwe jumuishi.
Kwa upande wa Uchaguzi wa Katibu
Mkuu, Waziri amesema,Tanzania inaunga mkono hoja ya kuendelea kuheshimu
utaratibu wa kupokezana nafasi ya Katibu Mkuu kwa kuzingatia mzunguko wa
kijiographia.
Balozi wa Tanzania nchi Marekani Wilson Masilingi akimpa mkono wa pongezi Waziri Mahiga baada kumaliza hotuba yake mbele ya wajumbe wa mkutano wa 71 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa. |
Mhe. Anna Lupembe Mbunge wa Viti Maalum (CCM) naye
akimpongeza Mhe, Waziri kwa hotuba yake iliyopokelewa vizuri. |
Dk. Tausi Kida Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF naye
akimpongeza Kiongozi wa Ujumbe wa Tanzania katika Mkutano wa
71 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa. |
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.