Tuesday, September 27, 2016

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje akutana na Mkurugenzi wa Mambo ya Nje wa Iran

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Ramadhan Muombwa Mwinyi akizungumza na Mkurugenzi anayeshughulikia masuala ya Afrika kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa ya Iran, Balozi Hussein Mollae Abdullahi alipomtembelea katika Ofisi za Wizara Jijini Dar es Salaam tarehe 27 Septemba, 2016. 
Balozi Abdullahi naye akichangia jambo wakati wa mazungumzo yao. Katika mazungumzo yao Mabalozi hao walijadili masuala ya ushirikiano baina ya Tanzania na Iran ikiwemo miradi ya maendeleo inayofadhiliwa na Serikali ya Iran nchini hususan katika sekta ya afya na elimu, sayansi na teknolojia. Vilevile walijadili kuhusu umuhimu wa kufanya Mkutano wa Tume ya Pamoja baina ya nchi zao ili kuweza kuibua maeneo mapya ya ushirikiano ikiwa sambamba na kusaini makubaliano katika sekta ambazo Iran imepiga hatua kubwa za kimaendeleo.
Maafisa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakifuatilia mazungumzo. Kushoto ni Bi. Zainabu Angovi na Bi.Doris Mwaseba
Balozi wa Iran nchini, Mhe. Mehdi Agha Jafari ( wa kwanza kulia ) pamoja na Afisa kutoka Ubalozini wakifuatilia mazungumzo.
Mazungumzo yakiendelea.
Picha ya pamoja

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.