Thursday, September 15, 2016

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje afungua Kongamano la Kimataifa la Chama cha Kiswahili Afrika Mashariki

Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Susan A. Kolimba (katikati) pamoja na meza kuu wakitoa heshima wakati Wimbo wa Taifa ukiimbwa kwenye ufunguzi wa kongamano la Kimataifa la Chama cha Kiswahili Afrika Mashariki (CHAKAMA) uliofanyika katika Ukumbi wa Nkurumah, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Naibu Waziri, Mhe. Dkt. Susan A. Kolimba (kushoto) akifurahia jambo wakati wa ufunguzi wa kongamano la Kimataifa la CHAMAKA, kulia ni Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Profesa Florens D. A. M Luoga.
Mheshimiwa Dkt. Susan A. Kolimba akimpongeza mtunzi na mwimbaji wa mashairi Bw. Issa Ally.
 Mhe. Dkt. Susan A. Kolimba akitoa hotuba ya ufunguzi wa kongamano la CHAKAMA.
 Mhe. Dkt. Susan A. Kolimba akiwa akionesha kitabu kilichozinduliwa kwenye kongamano la Kiswahili la CHAKAMA kulia ni Kaimu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Profesa Florens D. A. M Luoga.
Sehemu ya wadau wa lugha ya kiswahili waliohudhuria kongamano la Kimataifa la CHAKAMA wakifuatilia jambo.
Meza kuu (walioketi) wakiwa katika picha ya pamoja na Wahadhiri wa chuo Kikuu cha Dar es Salaam.


No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.