Tuesday, July 16, 2019

Prof. Kabudi akutana na Mabalozi wa Nchi za SADC



Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb.) amekutana na kufanya mazungumzo na Mabalozi wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) waliopo hapa nchini.


Katika mazungumzo hayo Prof. Palamagaba John Kabudi amewafahamisha hatua iliyofikiwa katika maandalizi ya Mkutanao ya wakuu wa nchi na Serikali wa nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) uliyopangwa kufanyika nchini mwezi Agosti 2019 



Kwa upande wa waheshimiwa Mabalozi hao walifurahishwa kwa hatua ya maandalizi iliyofikiwa, na kuelezea furaha yao kuhusu uwamuzi wa Serikali kuwashirikisha mapema katika maandalizi hayo.


Sehemu ya Mabalozi wa Nchi za Afrika na wanachama wa Jumuiya ya SADC wakimsikiliza Prof. Palamagamba John Kabudi (hayupo pichani)

Sehemu nyingine ya watumishi kutoka Balozi za Afrika zilizopo nchini
Prof. Palamagamba John Kabudi akifafanua jambo kwa Waheshimiwa Mabalozi alipokutana nao
Balozi wa Afrika Kusini Mhe. Thamsanga Mseleku akielezea jambo katika mkutano na Waziri Prof. Palamagamba John Kabudi 



Mkutano ukiendelea.




Wawekezaji kutoka Jamhuri ya Czech watua nchini kutafuta fursa za biashara na uwekezaji



TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Wafanyabiashara na wawekezaji kutoka Jamhuri ya Czech watafuta fursa za biashara na uwekezaji nchini Tanzania

Ujumbe wa wafanyabiashara na wawekezaji kutoka Jamhuri ya Czech wamewasili nchini tarehe 13 Julai, 2019 kwa lengo la kukutana na kufanya mazungumzo na wadau mbalimbali nchini ili kujadili fursa za biashara na uwekezaji nchini katika sekta mbalimbali hususan afya, kilimo, miundombinu ya barabara na reli,nishati, madini,utalii na wa ujenzi wa viwanda vya madawa na vifaa tiba.

Ziara hiyo inatokana na juhudi za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kupitia Ubalozi wa Tanzania uliopo nchini Ujerumani ambao pia unawakilisha Tanzania katika Jamhuri ya Czech na wadau wengine muhimu katika kushawishi wafanyabiashara wakubwa kuja kuwekeza nchini katika sekta mbalimbali.

Ujumbe huo wa watu kumi na mbili (12) ukiwa nchini, pamoja na masuala mengine, unategemea kukutana na uongozi wa Wizara naTaasisi mbalimbali zikiwemo, Wizara ya Viwanda na Biashara, Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Wizara ya Nishati, Wizara ya Madini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Bohari Kuu ya Dawa na Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. 

Vilevile, ujumbe huo unategemea kushiriki katika Kongamano la Uwekezaji wa Viwanda vya Kutengeneza Madawa na Vifaa Tiba kwa ubia kati ya Serikali na Sekta Binafsi, lililoandaliwa na Bohari Kuu ya Dawa. Kongamano hilo limepangwa kufanyika tarehe 17 Julai, 2019 katika Ukumbi wa Mkutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

Ziara ya ujumbe huo nchini ni chachu ya kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi kati ya Tanzania na Czech. Kadhalika, ziara ya ujumbe huo ni moja ya mikakati ya utekelezaji wa Sera ya Mambo ya Nje inayojikita katika diplomasia ya uchumi na kuhamasisha uwekezaji katika sekta ya viwanda ili kutimiza azma ya Serikali ya Awamu ya Tano chini ya uongozi wa Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda na uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.

Mhe. Dkt. Abdallah Saleh Possi, Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani ambaye pia ni Balozi wa Tanzania asiye na makazi nchini Czech ameambatana na ujumbe huo wa wafanyabiashara na wawekezaji.

Ujumbe huo kutoka Jamhuri ya Czech unategemea kukamilisha ziara yao nchini tarehe 17 Julai, 2019.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Dodoma.

16 Julai 2019


Mhe. Dkt. Abdallah Saleh Possi, Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani ambaye pia ni Balozi wa Tanzania asiye na makazi nchini Czech akiwa kwenye mkutano kati ya ujumbe wa wafanyabiashara na wawekezaji kutoka Jamhuri ya Czech na Kituo cha UwekezajiTanzania (TIC) uliofanyika jijini Dar es Salaam tarehe 15 Julai 2019. Mhe. Balozi Possi ameambatana na ujumbe huo hapa nchini ambao una lengo la kutafuta fursa za biashara na uwekezaji kwenye sekta za afya, kilimo, nishati na madini na ujenzi wa viwanda vya madawa na vifaa tiba.
Sehemu ya Wafanyabiashara na Wawekezaji kutoka Jamhuri ya Czech ukufuatilia mada mbalimbali zilizowasilishwa kwao na Wataalam kutoka Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC)
Sehemu nyingine ya Wafanyabiashara na wawekezaji kutoka Jamhuri ya Czech 
Mkutano ukiendelea
Mhe. Balozi Possi (wa tatu kulia) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Viongozi wa TIC na wafanyabiashara na wawekezaji kutoka Jamhuri ya Czech.

Friday, July 12, 2019

MASHINE YA KWANZA INAYOPIMA UDONGO NA KUKUAMBIA KIASI CHA MAZAO UTAKACHOPATA


Maabara ya kisasa ya kupima afya ya udongo kwa kutumia gari maalum yazinduliwa

Makamu Waziri wa Uholanzi Bi. Marjolijn Sonnema (watatu kushoto) na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi wa Tanzania Bw.Abdallah Ulega(watatu kulia) akikata utepe kuashilia uzinduzi wa Teknolojia ya Maaabara ya kupima afya udongo kwa kutumia gari maalum uliofanyika Jijini Arusha hivi karibuni. kushoo ni Balozi wa Uholanzi nchini Tanzania Joroen Verheul, wapili kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa SAGCOT centre ltd Bw.Geoffrey Kirenga, wa pili kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Mhandisi Methew Mtigumwe na kulia ni Mkurugeni Mkuu wa Kampuni ya Life Support System Tanzania (LSSL) Dkt.Edmond Matafu ambaye ndie mwekezaji wa teknolojia hiyo nchini.
Mkurugeni Mkuu wa Kampuni ya Life Support System Tanzania (LSSL) Dk. Edmond Matafu (kulia) akitoa maelekezo ya namna Maabara ya kupima afya ya udongo inavyofanya kazi kwa Makamu Waziri wa Uholanzi Bi.Marjolijn Sonnema(wapili kulia) mara baada ya kuzindua maabara hiyo inayotumia gari maalum hivi
karibuni jiijini Arusha. Wapili kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa SAGCOT Centre Ltd, Geoffrey Kirenga.
Gari Maalum yenye maabara ya kupima afya ya udongo limezinduliwa hvi karibuni jijini Arusha. Kampuni ya Life Support System Tanzania (LSSL) ndiyo itakayoendesha zoezi la kupima afya ya udongo katika mashamba ya wakulima kote nchini kwa gharama ya shilingi 25,000 mpaka 30,000.
Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega akipeana mkono na Dk. Edmond Matafu, ambaye ni moja wa wawekezaji walioleta maabara hiyo ambayo itaidia sana wakulima kwani watakuwa wanapima udongo huo kabla ya kulima. 
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega, akizungumza jambo mara baada ya kuzindua maabara hiyo ya upimaji wa udongo. 
Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega, Naibu Waziri wa Kilimo Maliasili na Usalama wa Chakula Bi. Marjolyn kutoka nchini Uholanzi, pamoja na Dk. Edmond Matafu, wakikata utepe ikiwa ni ishara ya maabara hiyo ya kutembea imezinduliwa rasmi. 
Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega akizungumza jambo mara baada ya kuzindua maabara hiyo ya upimaji wa udongo.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega pamoja na Naibu Waziri wa Kilimo maliasili na Usalama wa Chakula Bi Marjolyn kutoka nchini Uholanzi wakikata utepe ishara ya kufungua rasmi maabara za utupimaji wa udongo. (Picha zote na Ahmed Mahmoud, Arusha).


Na Mwandsihi Wetu, Arusha

TEKNOLOJIA ya maabara ya kupima afya ya udongo kwa kutumia gari maalumu lenye uwezo kupima zaidi ya sampuli 100 za udongo kwa siku moja limezinduliwa hapa nchini ili kupima udongo na kumhakikishia mkulima uzalishaji wa mazao kwa wingi na yenye tija sokoni.



Uzinduzi wa Teknolojia hiyo kutoka nchini Uholanzi ulifanyika jijini Arusha kati ya Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi wa Tanzania Bw.Abdallah Ulega kwa niaba ya Tanzania na Makamu Waziri wa Kilimo na Ubora wa Chakula wa Uholanzi, Bi.Marjolijn Sonnema kwa niaba ya nchi yake ili kufanikisha mageuzi katika sekta ya kilimo.

Akizungumza mara baada ya kufanya uzinduzi wa teknolojia hiyo, Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Bw Ulega aliishukuru Serikali ya Uholanzi kwa kutoa teknolojia yake kwa Tanzania na kusema kuwa itasaidia kuleta mapinduzi katika uzalishaji mazao.

“Kupima afya ya udongo inatoa majibu juu ya ubora wa ardhi husika, mazao yanayofaa kulimwa katika eneo hilo, kiwango cha mbolea kinachotakiwa na kutoa makadirio ya kiwango cha mavuno katika eneo husika,” alisema Naibu Waziri Ulega.

Aliongezea kuwa gharama ya kupima shamba iliyowekwa ya shilingi 25,000 mpaka 30,000 wakulima wanaweza kumudu na kuwataka wapema mashamba yao kabla ya kufanya kilimo ili kujua matatizo yaliyopo kwenye ardhi yake na nini afanye ili tija ya uzalishaji iongezeke.

“Teknolojia hii imeletwa kwetu hivyo tunakila sababu ya kuhamasisha wakulima nchini kupima mashamba yao ili wajipatie uhakika wa zao lilalofaa katika ardhi yake na nini afanye katika kuboresha ili aweze kuongeza tija ya uzalishaji,” alisema.

Naibu Waziri Ulega aliesema kuwa mageuzi katika sekta ya kilimo yatapatikana kupitia teknolojia hii ya kupima afya ya udongo na kupelekea kuongezeka kwa uzalishaji wa mazao ya kilimo hali itakayochochea ujenzi wa viwanda vya kuchakata na kuongezea thamani ya mazao.

“Ushirikiano kati ya Serikali na sekta binafsi kunachochea kasi ya maendeleo kwa kuibua teknolojia na ujuzi mbalimbali katika kuiletea nchi maendeleo, naipongeza kampuni ya Life Support System Tanzania (LSSL) kwa kuwekeza kwenye ketnolojia hii,” alisema Ulega Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa LSSL, Dkt.Edmond Matafu alisema magari manne yapo tayari pamoja na handheld soil scanner 100 ambazo zitatumiwa na maafisa ugani kwa ajili ya kuchukua sampuli za udongo katika maeneo ya vijiji kote nchini.

“Hii itasaidia kufanya zoezi la kupima afya ya udongo kwa wakati pasipo kuchelewa kipindi cha kulima ambapo itampa unafuu mkulima kujua mahitaji katika shamba lake ili aweze kupata tija katika uzalishaji mazao,” alisema Dkt. Matafu.

Aliongezea kuwa juhudi za Serikali za kujenga uchumi wa kati na viwanda zitatekelezeka kwa ushirikiano kati ya sekta binafsi na Serikali kufanya kazi kwa pamoja kuhakikisha vikwazo vyote vinavyokwamisha maendeleo vinatatuliwa ili maendeleo tunayoyatarajia yaweze kufikiwa kwa vitendo.

“Zoezi la kupima afya ya udongo litafanyika kote nchini kwani tumejipanga vizuri katika kutoa huduma hii kwa wakulima hivyo ushirikiano ndio kitu muhimu katika kufanikisha zoezi hili ambalo litakwenda kuinua hali ya uzalishaji zao nchini,” alisema Dkt. Matafu.

Uzinduzi wa Maabara ya kupima udongo kwa kutumia gari maalum ulishuhudiwa na Makamu Waziri wa Kilimo na Ubora wa Chakula kutoka Uholanzi, Bi. Marjolijn Sonnema, Balozi wa Uholanzi nchini Tanzania

Joroen Verheul, Katibu Mkuu Wizara ya Mifungo na Uvuvi Profesa Elisante Ole Gabriel na Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Mhandisi Methew Mtigumwe na Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Kuendeleza Kilimo Nyanda za Juu Kusini, Bw. Geoffrey Kirenga.






Watanzania wachangamkia soko la biashara Komoro


Balozi wa Tanzania nchini Komoro, Mhe. Balozi Sylvester Mabumba akitoa hotuba yake kwenye ufunguzi wa  mkutano wa wafanyabiashara (hawapo pichani) wa Tanzania na Komoro, katika hotuba yake aliwahakikishia wafanyabiashara kutoka Tanzania kuwa Ubalozi unaendelea kufanya kazi kwa bidii katika kuratibu shughuli za biashara baina ya Tanzania na Komoro, pamoja na kuwashauri wafanyabiashara hao kufika Ubalozini pindi watakapo kabiliwa na changamoto za aina yoyote ile.

Katika Mkutano huo Mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Biashara wa Komoro Mhe. Mohamed M'saidie, ambapo aliambata na 
Rais wa Chamber of Commerce ya Comoro, Ndg. Ahmed Bazi, Rais wa Chamber of Commerce wa Anjouan, Ndg. Soyad Mohamed, Rais wa Chamber of Commerce ya Ngazidja, Ndg. Soibroi Eddine Mohamed Balozi wa Sudan, Mhe. Issam Muhi El Dine Khalili na Kaimu Balozi kutoka Ubalozi wa Afrika Kusini Bi. Chwane Nomcebo Valentia Mthethwa.

Aidha, 
washiriki kutoka Tanzania walipata fursa ya kuonesha, kuuza na kutangaza bidhaa zao. Sambamba na hilo washiriki waliweza pia kufanya majadiliano ya kibishara (B2B) na kuweza kuingia makubaliano ya kufanya biashara na Wakomoro.

 Sekta ambazo zimeonekana kuchangamkiwa zaidi ni sekta ya ufugaji wa kuku, mayai, bidhaa za mboga mboga na biashara ya nyama ya Ng’ombe.


Mkutano huo umefanyika katika Hoteli ya Retaj nje kigodo ya mji wa Moroni. 
Mhe Ahmed Bazi Rais wa Chamber of Commerce ya Komoro naye akitoa hotuba yake kwenye ufunguzi wa Mkutano uliowakutanisha wafanyabiashara kutoka Tanzania na Komoro
Mwakilishi wa Waziri wa Uchumi na Uwekezaji wa Komoro naye akitoa hotuba yake kwenye ufunguzi wa mkutano wa wafanyabiashara.
Add caption
Wadau wa Biashara kutoka Tanzania na Komoro wakisikiliza Hotuba zilizokuwa zikiendelea 
Maonyesho ya Bidhaa za Tanzania yakiendelea nje ya Hotel Retaj Moroni
Wajumbe wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumaliza ufunguiz wa Mkutano ulio wakutanisha wafanyabiashara kutoka Tanzania na Komoro.