Friday, August 30, 2019
WAZIRI MKUU MHE MAJALIWA AKUTANA NA KAMISHNA MKUU WA UNHCR
Thursday, August 29, 2019
WAZIRI WA MAMBO YA NJE, MHE. PROF. PALAMAGAMBA JOHN KABUDI AFANYA MAZUNGUMZO NA MEYA WA JIJI LA NAGAI NCHINI JAPAN
Meya wa Jiji la Nagai, Bw. Shigeharu Uchiya akimweleza jambo Mhe. Prof. Kabudi wakati wa mazungumzo kati yao |
Ujumbe uliongozana na Meya wa jiji la Nagai, Mhe. Shigeharu Uchiya ukifuatilia mazungumzo. |
Sehemu nyingine ya ujumbe wa Tanzania ukifuatilia mazungumzo |
Mhe. Prof. Kabudi akimwonesha Mhe. Uchiya jarida linaloonesha vivutio mbalimbali vya utalii vilivyopo nchini |
Mhe. Prof. Kabudi akiagana na Mhe. Shigeharu Uchiya mara baada ya kumaliza mazungumzo kati yao |
TAARIFA KWA VYOMBO VYA
HABARI
Prof. Kabudi afanya
mazungumzo na Meya wa Jiji la Nagai nchini Japan
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi ameishukuru Serikali ya Japan kwa
kuishirikisha Tanzania kikamilifu kwenye maandalizi ya Michezo ya Olympic
inayotarajiwa kufanyika jijini Tokyo mwaka 2020 ikiwa ni pamoja na kutoa
mafunzo kwa wanamichezo wanawake kutoka Tanzania.
Mhe.Prof. Kabudi ametoa shukrani hizo wakati wa
mkutano wake na Meya wa Jiji la Nagai, Mhe. Shigeharu Uchiya uliofanyika leo
tarehe 29 Agosti 2019 jijini Yokohama pembezoni mwa Mkutano wa Saba wa
Kimataifa wa Tokyo kuhusu Ushirikiano na Afrika (TICAD 7).
Mhe. Prof. Kabudi alisema kuwa, anaishukuru Japan kwa
kuwa imeonesha nia ya dhati ya kuifanya Tanzania ishiriki kwenye Michezo hiyo
muhimu ya Olympic ambayo itafanyika nchini humo mwaka 2020 na kuzishirikisha nchi zote duniani. Mhe. Waziri alifafanua kuwa tayari Serikali hiyo imesaini Hati
ya Makubaliano na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo mwezi Julai 2019
kuhusu ushiriki wa Tanzania kwenye michezo hiyo pamoja na kufanikisha ziara ya Timu
ya wanariadha kutoka nchini wakiongozwa na mkimbiaji wa mbio za marathon
mstaafu, Bw. Juma Ikangaa iliyofanyika mwezi Oktoba 2018. Pia Japan imeahidi
kutoa mafunzo kwa wanamichezo wanawake yatakayotolewa jijini Nagai.
“Ushikiano wa
kirafiki kati ya Japan na Tanzania ni wa miaka mingi hususan kwenye medani za siasa, uchumi na diplomasia.
Umefika wakati sasa nchi hizi mbili zishirikiane katika masuala ya kijamii na utamaduni
ili kuwaunganisha mtu mmoja mmoja na kwamba ushirikiano huo ndio muhimu kwa
ukuaji wa Taifa lolote” alisema Prof. Kabudi.
Aidha, alieleza
kufurahishwa na ahadi kuwa Japan itatoa mafunzo kwa wanamichezo wanawake ili
kuwajengea uwezo kwenye michezo mbalimbali ikiwemo ile ya Olympic
itakayofanyika Tokyo mwaka 2020. “Tumepokea kwa furaha taarifa kwamba Nagai
itatoa mafunzo kwa wanamichezo wetu wanawake. Hii itawajengea uwezo mkubwa
wanamichezo hao wakati wakijiandaa na mashindano ya Olympic” alisisitiza Prof.
Kabudi.
Kadhalika, Mhe. Prof. Kabudi alitumia fursa hiyo kumweleza
Mhe. Uchiya kuwa Serikali ya Tanzania imehamishia shughuli zake jijini Dodoma
ambako ni Makao Makuu ya nchi na kwamba ipo tayari kuanzisha ushirikiano wa
kidada kati ya Jiji la Dodoma na Jiji la Nagai.
Kwa upande wake, Meya wa Jiji la Nagai, Mhe. Shigeharu
Uchiya alisema kwamba jiji hilo litaendelea kushirikiana kwa karibu na Tanzania
na tayari limeanzisha program ya kubadilishana uzoefu kwenye masuala ya michezo
ambapo Mtanzania, Bw. Bahati Rogers ni miongoni mwa vijana wanaoshiriki program
hiyo jijini humo. Pia alisema kuwa aliongoza ujumbe wa watu ishirini kutembelea
Tanzania mwaka 2017 kwa ajili ya kubadilisha uzoefu kuhusu michezo.
Serikali ya Japan ambayo imeanza maandalizi ya Michezo
ya Kimataifa ya Olympic itakayofanyika jijini Tokyo mwaka 2020, imetenga Jiji
la Nagai kuwa kituo cha Wanamichezo wote wa Tanzania kitakachotumika kuwaadaa
kabla ya kuanza kushiriki michezo hiyo rasmi. Maandalizi hayo ni pamoja na
kuwawezesha wanamichezo kuzoea hali ya hewa, tamaduni, chakula na masuala
mengine muhimu kuhusu Japan kabla ya ushiriki wao rasmi wa michezo hiyo.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasil
iano ya Serikali,
Wizara
ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Yokohama,
Japan
29 Agosti 2019
Wednesday, August 28, 2019
JAPAN YATOA DOLA BILIONI 20 KUSAIDIA MAENDELEO KWA NCHI ZA AFRIKA
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
JAPAN YATOA DOLA BILIONI 20 KUSAIDIA MAENDELEO KWA NCHI ZA AFRIKA
Japan imetangaza kutenga kiasi cha dola za kimarekani bilioni 20 kwa kipindi cha miaka mitatu kwa Nchi za Bara la Afrika ili kuziwezesha Nchi hizo kutekeleza miradi ya kimkakati ya maendeleo itakayoleta mageuzi ya kiuchumi katika Bara la Afrika huku Tanzania ikikazia mkakati wake wa uchumi wa viwanda.
Waziri Mkuu wa Japan, Mhe. Shinzo Abe ameyasema hayo wakati wa ufunguzi rasmi wa Mkutano wa Saba wa Kimataifa wa Tokyo kuhusu Maendeleo ya Afrika (Tokyo Internatinaol Conference on African Development TICAD7) uliofanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Pacifico jijini Yokohama na kuongeza kuwa Serikali ya Japan itaendelea kuchangia maendeleo ya Bara la Afrika kupitia program mbalimbali za ushirikiano kwa kuimarisha rasilimali watu, elimu ya awali kwa watoto na kuboresha huduma ya afya kwa wote.
Mhe. Abe amesema kuwa, kupitia Mpango wa TICAD, ushirikiano kati ya Japan na Afrika umeimarika na kwamba nchi hiyo itaendelea kuhakikisha inahamasisha Kampuni za Japan kuwekeza Afrika ambapo hadi sasa sekta binafsi ya Japan imewekeza dola za marekani bilioni 20 katika nchi mbalimbali za Afrika.
Akizungumzia program mbalimbali zinazotekelezwa na Japan katika kuchangia maendeleo ya Afrika ikiwemo ile ya ABE-African Businness Education Initiative, Waziri Mkuu huyo amesema kuwa tayari vijana zaidi ya 350 kutoka nchi mbalimbali za Afrika wanafanya mafunzo kwa vitendo kwenye Kampuni mbalimbali kupitia mpango huo na wengine 3000 ambao walishapitia mpango huo kama wawezeshaji.
Mhe. Abe amesema kuwa, Japan itaendelea kuchangia kwenye sekta ya afya hususan kwenye masuala ya dawa, lishe na kutoa mafunzo ya ujuzi kuhusu masuala hayo kwa nchi mbalimbali za Afrika. Pia Waziri Mkuu huyo amesisitiza kuwa nchi yake itaendelea kushirikiana na Afrika kwenye ujenzi wa miundombinu kama barabara na bandari pamoja kutoa wataalam kwani nchi yake haijawahi kupungukiwa wataalam.
Kwa upande wake Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa ambaye anahudhuria mkutano huo akimuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amesema Tanzania ni miongoni mwa Nchi za Afrika zinazozalisha malighafi zinazosafirishwa nje kwa ajili ya kuongezewa thamani jambo linalofanya Bara la Afrika Tanzania ikiwemo kujikuta ikisafirisha ajira na kutengeneza soko la bidhaa kutoka katika mataifa mengine na kwamba sasa Tanzania imedhamiria kupitia viwanda kutumia malighafi zake kuzalisha bidhaa mbalimbali na hivyo kutengeneza ajira kwa watu wake lakini pia kuuza nje ya nchi na kuzalisha fedha za kigeni.
Ameongeza kuwa kupitia mkakati wa Japan kwa nchi za Afrika Tanzania ni mojawapo ya nchi zitakazonufaika na mkakati huo na kuongeza kuwa mojawapo ya maeneo ya kuboresha ili kufikia azma ya Tanzania ya viwanda ni kujenga miundo mbinu imara itakayoweka msingi wa kufikia malengo hayo kwa kuwezesha usafirishaji wa bidhaa pamoja na malighafi zitakazotumika katika viwanda.
Kwa upande wake Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi amesema tofauti na mikutano iliyotangulia Mkutano huu wa TICAD saba kwa mara ya kwanza umeweka fursa ya kuwa na mpango kazi wa Yokohama ambapo badala ya kuwa na maazimio pekee sasa kutakuwa na fursa ya kuweka malengo vilevile kupima utekelezaji wake na upatikanaji wa fedha.
Rais wa Misri, Mhe. Abdel Fattah el-Sisi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika na Mwenyekiti mwenza wa Mkutano wa TICAD 7, Mhe. El-Sisi amesema kuwa Afrika kwa sasa inahitaji mapinduzi katika teknolojia na uvumbuzi ili kukabiliana na changamoto mbalimbali zinalolikabili Bara hilo ikiwemo ukosefu wa ajira kwa vijana na mabadiliko ya tabia. Aidha, ametoa rai kwa nchi zinalizoendelea kutekeleza ahadi zao pamoja na Mkataba wa Paris kuhusu kuzisaidia nchi za Afrika kukabiliana na changamoto ya mabadiliko ya tabianchi.
Aidha, Mhe. Rais El-Sisi alitumia fursa hiyo pia kuwakaribisha wawekezaji kutoka Japan kuwekeza Afrika pamoja na kuzitaka taasisi za kifedha za kimataifa kutoa masharti nafuu ya mikopo ili kukuza na kuimarisha uwekezaji na biashara barani Afrika.
Naye Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Mhe. Antonio Guteres ameipongeza Japan kwa ushirikiano wake na nchi za Afrika hususan katika kuunga mkono jitihada mbalimbali za kudumisha amani na usalama baranii humo. Pia amezipongeza nchi za Afrika kwa kuanzisha Mpango wa Eneo Huru la Biashara barani humo ambao kwa kiasi kikubwa utaimarisha sekta ya biashara na uwekezaji na kuchangia maendeleo ya nchi hizo. Mhe. Guteres amesisistiza kuwa nchi za Afrika kwa kushirikiana na Japan ziwekeze kwenye elimu bora kwa vijana hususan kwenye maeneo ya sayansi, hesabu na teknolojia kwani yana mchango mkubwa katika maendeleo.
Akizungumzia mabadiliko ya tabianchi, Mhe. Guteres amesema kuwa jitihada za pamoja zinahitajika ili kukabiliana na changamoto zitokanazo na mabadiliko hayo ambayo kwa kiasi kikubwa yanaziathiri nchi za Afrika. Katibu Mkuu huyo aliongeza kuwa ameitisha Mkutano kuhusu mabadiliko ya tabianchi utakaofanyika jijini New York, Marekani mwezi Septemba 2019 ili kwa pamoja nchi zijadili namna ya kuendelea kutatua changamoto hizo.
Kwa upande mwingine, Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika, Mhe. Moussa Faki Mahamat ambao hushirikiana na Japan kuandaa mikutano ya TICAD, amesema kuwa, Mkutano wa Saba umekuja na suluhisho kwa vijana kuhusu masuala ya teknolojia na uvumbuzi na kusisistiza kwamba suala hilo ni la kipaumbele kwa nchi za Afrika.
Mkutano wa Saba wa TICAD ambao umebeba kaulimbiu ya Kuiendeleza Afrika kupitia Watu, Teknolojia na Uvumbuzi, umehudhuriwa na zaidi ya washiriki 4,000 pamoja na Wakuu wa Nchi na Serikali kutoka nchi 44 za Afrika.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Yokohama, Japan.
28 Agosti 2019
WAZIRI MKUU ASHIRIKI TICAD7- YOKOHOMA,JAPAN
Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa (Mb) akisaliqmiana na Waziri Mkuu wa Mauritius Mhe Pravind Jugnauth walipokutana na kufanya mazungumzo katika Mji wa Yokohoma Japan. |
MHE. WAZIRI MKUU ATEMBELEA BANDA LA TANZANIA LA MAONESHO YA TICAD 7
Mhe. Waziri Mkuu akiangalia moja ya kipeperushi kuhusu maeneo ya vivutio vya utalii vilivyopo nchini alipotembelea banda la Tanzania kwenye Mkutano wa TICAD 7 unaofanyika jijini Yokohama, Japan |
Tuesday, August 27, 2019
WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA JAPAN AWAANDALIA HAFLA MAALUM MAWAZIRI WANAOSHIRIKI MKUTANO WA SABA WA TICAD
Mhe. Taro akizungumza wakati wa hafla hiyo ambapo ameendelea kuwahakikishia ushirikiano Mawaziri kutoka Afrika |
Mhe. Taro akizungumza huku Mawaziri wakimsikiliza |
Mhe. Prof. Kabudi akiwa katika meza moja na Mhe. Taro na Mawaziri wengine kutoka nchi za Afrika wanaoshiriki Mkutano wa Saba wa TICAD |
Subscribe to:
Posts (Atom)