Saturday, May 21, 2022

WAZIRI MULAMULA AFANYA ZIARA KATIKA MAHAKAMA YA KIMATAIFA YA KESI MASALIA ZA MAUAJI YA KIMBARI (IRMCT)

 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula amefanya ziara ya kikazi katika Mahakama ya Kimataifa ya Kesi Masalia za Mauaji ya Kimbari (IRMCT) tarehe 21 Mei 2022 katika eneo la Lakilaki, jijini Arusha.

Pamoja na mambo mengine dhumuni la ziara hiyo lilikuwa kukutana na Uongozi wa IRMCT na kujadili utekelezaji wa majukumu mbalimbali ya kimsingi unaofanywa na taasisi hiyo sambamba na yale ya kimahakama.

Waziri Mulamula alitumia nafasi hiyo kueleza kuwa Tanzania inathamini imani inayotolewa na mashirika ya kimataifa pamoja na kikanda ya kuifanya kuwa mwenyeji wa mashirika hayo na kutoa nafasi za ajira kwa Watanzania.

‘’ Serikali inafuatilia kwa karibu utendaji kazi wa Mahakama hii, hivyo ni vema mkatekeleza kwa tija malengo mahsusi ya kuanzishwa kwake,” alisema Balozi Mulamula.

Pia akasisitiza kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ipo tayari kutoa ushirikiano wa kiutendaji wakati wowote itakapohitajika ili kuiwezesha Mahakama kutekeleza majukumu yake ya msingi ikiwemo kukamilisha taratibu za kesi zilizosalia na lile la kuwa kituo cha kumbukumbu kwa kesi hizo linatekelezwa kwa ufanisi.

Naye Msajili wa Mahakama hiyo Bw. Abubaccar Tambadou amemshukuru Mheshimiwa Waziri Mulamula kwa kuthamini Mahakama hiyo na kutenga muda wake kujadili masuala mbalimbali ya kiutendaji.

Pia akaeleza kuwa kikao hicho kimewezesha kupatikana kwa ufumbuzi wa papo kwa papo katika baadhi ya mambo na kuleta uelewa wa pamoja kati ya uongozi wa Mahakama na Serikali mwenyeji juu ya masuala ya kiutendaji wa taasisi hiyo.

Naye Jaji wa Mahakama hiyo Mheshimiwa William Sekule alifafanua kwa kina juu ya utekelezaji wa majukumu mbalimbali ya kimahakama na pia akaeleza kuwa kufanikiwa kwa Mahakama hiyo kunahitaji msaada kutoka kwa nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa na nchi mwenyeji katika kutetea maslahi mbalimbali kwa ajili ya kuwezesha uendeshaji wa shughuli za taasisi.

‘’Naipongeza Tanzania kwa kuendelea kuwa mstari wa mbele katika kupigania upatikanaji wa bajeti ya uendeshaji wa Mahakama, hivyo ni vema tukatambua thamani ya mahakama hii kuendelea kuwepo nchini na kukamilisha majukumu yake,” alisema Jaji Sekule.

Tangu Baraza Kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa lipitishe Azimio Nambari 1966 mwaka 2010 la kuanzisha Mahakama hiyo nchini, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilisimamia hatua mbalimbali za awali ili kuhakikisha ujenzi wa Mahakama hii unakamilika hususan upatikanaji wa eneo la ujenzi, uwepo wa huduma ya umeme, barabara na maji katika eneo la Lakilaki Jijini Arusha.

 ================================================


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula (kulia) akifafanua jambo wakati wa kikao na Uongozi wa Mahakama ya Kimataifa ya  Kesi Masalia za Mauaji ya Kimbari  kilichofanyika tarehe 21 Mei 2022 katika eneo la Lakilaki, jijini Arusha. Pembeni ya Mhe. Waziri ni Mkurugenzi wa Kitengo cha Sheria katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Caroline Chipeta.

Kutoka kushoto ni Msajili wa Mahakama ya Kimataifa ya Kesi Masalia za Mauaji ya Kimbari (IRMCT) Bw. Abubaccar Tambadou na Jaji wa Mahakama hiyo Mheshimiwa William Sekule akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Mahakama kwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula.

Ujumbe kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ulioambatana na Mhe. Waziri katika ziara hiyo ukifatilia majadiliano katika kikao hicho. Kushoto ni Msaidizi wa Mhe. Waziri, Bw. Seif Kamtunda na Kulia ni Afisa Mambo ya Nje, Bi. Laila Kagombora.

Uongozi wa Mahakama ya Kimataifa ya Kesi Masalia za Mauaji ya Kimbari (IRMCT) ukifatilia majadiliano ya kikao.

Kikao kikiendelea

Picha ya Pamoja Waziri Mulamula na Msajili wa Mahakama Bw. Tambadou na Mhe. Jaji Sekule.

Picha ya pamoja ujumbe wa Wizara ya Mambo ya Nje  na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ukiongozwa na Mhe. Waziri Mulamula na Uongozi wa IRMCT.

Waziri Mulamula akipata maelezo katika chumba cha Mahakama na taratibu nyingine za uendeshaji wa kesi katika mahakama hiyo.

Muonekano wa chumba cha Mahakama.

Waziri Mulamula akipata maelezo kutoka kwa afisa anayesimamia Makavazi (Archieve) ya mahakama hiyo.

Waziri Mulamula akipata ufafanuzi juu ya uendeshaji na usimamizi wa Makataba inayosimamiwa IRMCT ambapo alielezwa kuwa hadi sasa Makataba hiyo inashirikiana na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Chuo Kikuu cha Makumila kutoka Tanzania na Chuo  Kikuu cha Makelele kutoka Uganda.

Picha ya pamoja Mheshimiwa Waziri na Watanzania wanaofanya kazi IRMCT


TANZANIA YAFUNGUA KONSELI KUU GUANGZHOU, CHINA


Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tarehe 20 Mei 2022 imefungua Konseli Kuu mjini Guangzhou China. Uwepo wa Konseli Kuu katika mji huo kuta iwezesha Tanzania kutumia vyema fursa za biashara na uchumi na kurahisisha upatikanaji wa huduma kwa Watanzania wanaoishi na kufanya shughuli mbalimbali katika mji huo. 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula akihutubia kwenye hafla ya ufunguzi wa Konseli Kuu hiyo kwa njia ya mtandao alisema kufungua ubalozi huo sambamba na kuendeleza uhusiano mzuri wa kidiplomasia na biashara katika ya Tanzania na China , Konseli Kuu hiyo ni muhimu katika kuhudumia Jumuiya ya Watanzania ambapo ndio idadi kubwa zaidi kuliko miji yote ya China.

"Guangzhou imekuwa mshirika mkubwa wa kibiashara kati ya China na Tanzania ambapo kwa mwaka 2020/2021 kupitia mji huu biashara kati ya Tanzania na China ilifukia shilingi dola za Marekani 6.74. Hivyo ni matumaini yetu kwa kuwa na Konseli Kuu hapa biashara kati ya Tanzania na China itakuwa maradufu” alisema Mhe. Balozi Liberata Mulamula

Konseli Mkuu wa Konseli Kuu ya Tanzania mjini Guangzhou Bw. Khatibu Makenga, akizungumza kwenye hafla ya ufunguzi alisema Konseli hiyo italeta msukumo mpya wa biashara, uwekezaji na mahusiano ya kiutamaduni baina ya Tanzania na China.

Kwa upande wake Bw. Luo Jun, Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Mambo ya Nje ya jimbo la Guangdong, akizungumza katika halfa ya ufunguzi alisema mji wa Guanzhou licha ya kuwa ni lango kubwa la biashara kati ya China na Mataifa mengine duniani una historia ya kipekee kwenye historia ya ushirikiano baina ya Tanzania na China. Aliongeza kusema Guangzhou ni kielelezo cha ushirikiano na urafiki baina ya Tanzania na China. 
Konseli Mkuu wa Konseli Kuu ya Tanzania mjini Guangzhou Bw. Khatibu Makenga na Viongozi wa Mamlaka mbalimbali kutoka mji wa Guangzhou na Guangdong wakikata utepe kuashiria ufunguzi wa Konseli Kuu ya Guangzhou, China.
Hafla ufunguzi ikiendelea


Konseli Mkuu wa Konseli Kuu ya Tanzania mjini Guangzhou Bw. Khatibu Makenga akihutubia wakati wa hafla ya ufunguzi wa Konseli Kukuu hiyo

Friday, May 20, 2022

DKT MPANGO: SERIKALI ITAENDELEA KUSHIRIKIANA NA UN

Na Mwandishi wetu, Dar

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Mpango ameuhakikishia Umoja wa Mataifa (UN) kuwa Serikali itaendelea kushirikiana na Umoja huo katika miradi mbalimbali ya maendeleo.

Dkt. Mpango aliyasema hayo leo Jijini Dar es Salaam katika uzinduzi wa Mpango wa Tatu wa Maendeleo (UNSDCF) wa Miaka Mitano (2022-2027) wa ushirikiano baina ya Tanzania na Umoja wa Mataifa nchini Jijini Dar es Salaam.

Dkt. Mpango ameongeza kuwa Serikali itaendelea kufanya kazi kwa pamoja Mashirika ya Kimataifa ili kuleta mafanikio ya nchi ya Tanzania.

Kwa upande wake Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula (Mb) aliishukuru UN kwa kazi nzuri ambayo wameifanya ya kusuma maendeleo ya nchi ya Tanzania.

Balozi Mulamula aliongeza kuwa Serikali itaendelea kushirikiana kufanya kazi pamoja na UN kwa lengo la kuhakikisha inajenga mazingira mazuri ili kuweza kufanikiwa kimaendeleo.

Naye Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi, Mhandisi Zena Said alisema mpango huo umejumuisha maendeleo ya watu wa Zanzibar ili kuleta maendeleo. 

Awali Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Tanzania, Zlatan Milisic alisema mfumo wa Umoja wa Mataifa nchini Tanzania umebaini maeneo manne ya kimkakati kwa maendeleo endelevu 2030.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Mpango akihutubia katika uzinduzi wa Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Miaka Mitano (2022-2027) wa ushirikiano baina ya Tanzania na Umoja wa Mataifa nchini Jijini Dar es Salaam

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Mpango akizindua Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Miaka Mitano (2022-2027) Jijini Dar es Salaam

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula (Mb) akiwasilisha hotuba yake wakati wa uzinduzi wa Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Miaka Mitano (2022-2027) Jijini Dar es Salaam

Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi, Mhandisi Zena Said akiwasilisha hotuba yake wakati wa uzinduzi wa Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Miaka Mitano (2022-2027) Jijini Dar es Salaam

Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Tanzania, Zlatan Milisic akizungumza na washiriki wakati wa uzinduzi wa Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Miaka Mitano (2022-2027) Jijini Dar es Salaam

Balozi wa Canada nchini Tanzania, Mhe. Pamela O'Donnell  akizungumza na washiriki wakati wa uzinduzi wa Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Miaka Mitano (2022-2027) Jijini Dar es Salaam


BALOZI MBAROUK ASAINI KITABU CHA MAOMBOLEZO UAE

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk amesaini Kitabu cha Maombolezo kufuatia kifo cha Rais wa UAE, Sheikh Khalifa bin Zayed bin Sultan Al Nahyan katika Ubalozi wa nchi hiyo leo Jijini Dar es Salaam.

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk akisaini Kitabu cha Maombolezo kufuatia kifo cha Rais wa UAE, Sheikh Khalifa bin Zayed bin Sultan Al Nahyan katika Ubalozi wa nchi hiyo leo Jijini Dar es Salaam

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk akisaini Kitabu cha Maombolezo kufuatia kifo cha Rais wa UAE, Sheikh Khalifa bin Zayed bin Sultan Al Nahyan katika Ubalozi wa nchi hiyo leo Jijini Dar es Salaam

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk akiteta jambo na Balozi wa Umoja wa Falme za Kiarabu nchini Mhe. Khalifa Abdulrahman Mohamed Al-Marzooqi baada ya kusaini kitabu cha maombolezo katika Ubalozi wa nchi hiyo leo Jijini Dar es Salaam


Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk akiagana na Balozi wa Umoja wa Falme za Kiarabu nchini Mhe. Khalifa Abdulrahman Mohamed Al-Marzooqi baada ya kusaini kitabu cha maombolezo katika Ubalozi wa nchi hiyo leo Jijini Dar es Salaam


Thursday, May 19, 2022

Balozi wa Tanzania, Kuwait Awasilisha Hati za Utambulisho

Balozi wa Tanzania nchini Kuwait, Mhe. Said Mussa akiwasilisha Hati za Utambulisho kwa Naibu Amiri na Mwanamfalme wa Kuwait, Sheikh Mishal Al-Ahmad Al-Jaber Al-Sabah jijini Kuwait. 
Balozi wa Tanzania nchini Kuwait, Mhe. Said Mussa akiwa katika mazungumzo na Naibu Amiri na Mwanamfalme wa Kuwait, Sheikh Mishal Al-Ahmad Al-Jaber Al-Sabah jijini Kuwait baada ya kuwasilisha Hati za Utambulisho. 

Tuesday, May 17, 2022

BALOZI MULAMULA ATETA NA UJUMBE WA WAFANYABIASHARA SWITZERLAND

Na Mwandishi Wetu, Dar

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb) amekutana kwa mazungumzo na Ujumbe wa wafanyabiashara kutoka Nchini Switzerland katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.

Balozi Mulamula ameuhakikisha ujumbe wa wafayabiashara hao kuwa mazingira ya biashara na uwekezaji nchini ni salama na hivyo wasisite kuwekeza.

“Serikali imejitahidi sana kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji hivyo nawasihi kutumia fursa hiyo kuwekeza hapa nchini katika sekta mbalimbali ikiwemo, kilimo, nishati, madini na nyinginezo," alisema Balozi Mulamula

Nae Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya 'Global Network', Bw. Stefan Barny emeipongeza Serikali ya Awamu ya Sita kwa maboresho makubwa katika sekta ya biashara na uwekezaji.

“Mazingira ya biashara hapa Tanzania nilikuwa nayasikia tu, ila baada ya kuja na kuonana pamoja na kujadiliana na wadau wa sekta za biashara na uwekezaji tumeridhishwa na mazingira ya biashara hapa Tanzania,” alisema Bw. Barny.

Bw. Barny ameongeza kuwa atawashawishi wafanyabiashara wenzake kutoka Uswisi kuja kuwekeza Tanzania kwan fursa za biashara na uwekezaji zinazopatikana Tanzania ni nyingi.

“Tumepanga kuwekeza katika sekta ya kilimo hasa katika sekta za kilimo hasa katika usindikaji wa mazao ya chakula, biashara na uwekezaji, madini na nishati....tumepanga kufungua kiwanda rasmi hapa Tanzania mwakani,” aliongeza Bw. Barny

Kikao hicho pia kilihudhuriwa na Balozi wa Switzerland hapa Nchini, Mhe. Didier Chassot, Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mindi Kasiga

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula akizungumza na Ujumbe wa Wafanyabiashara kutoka nchini Switzerland katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam. Ujumbe huo uliongozwa na Balozi wa Switzerland hapa Nchini, Mhe. Didier Chassot

Balozi wa Switzerland hapa Nchini, Mhe. Didier Chassot akimueleza jambo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula wakati alipokuwa akizungumza na Ujumbe wa Wafanyabiashara kutoka nchini Switzerland katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula akimueleza jambo Balozi wa Switzerland hapa Nchini, Mhe. Didier Chassot. Kulia ni Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mindi Kasiga



Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula katika picha ya pamoja na Ujumbe wa Wafanyabiashara kutoka nchini Switzerland, Balozi wa Switzerland hapa Nchini, Mhe. Didier Chassot, Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mindi Kasiga na Afisa Mambo ya Nje, Bibi. Kisa Mwaseba



Monday, May 16, 2022

WAZIRI MULAMULA ASAINI KITABU CHA MAOMBOLEZO U.A.E

Na Mwandishi wetu, Dar

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula (Mb) amesaini kitabu cha maombolezo katika Ubalozi wa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), nchini kufuatia kifo cha Rais wa Umoja wa Falme za Kiarabu, Sheikh Khalifa bin Zayed Al-Nahyan kilichotokea tarehe 13 Mei 2022.

Baada ya kusaini kitabu cha maombolezo katika Ubalozi wa UAE nchini, Jijini Dar es Salaam Balozi Mulamula ametoa salamu za pole kwa Serikali ya UAE na kuwasihi wananchi wake kuendelea kuwa watulivu wakati huu wa msiba wa kuondokewa na kiongozi wao.

“Kusaini kitabu cha maombolezo ni ishara ya ushirikiano, umoja na undugu wetu na ndugu zetu wa UAE. Kifo cha Rais wa UAE, Sheikh Khalifa bin Zayed Al-Nahyan kimewagusa pia Watanzania kwa kuwa Tanzania na UAE zina uhusiano mzuri,” alisema Balozi Mulamula.

Aliyekuwa Rais wa UAE, Sheikh Khalifa bin Zayed Al-Nahyan alifariki dunia tarehe 13 Mei, 2022 akiwa na umri wa miaka 73 baada ya kuugua kwa muda.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula (Mb) akisaini kitabu cha maombolezo katika Ubalozi wa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), nchini kufuatia kifo cha Rais wa Umoja wa Falme za Kiarabu, Sheikh Khalifa bin Zayed Al-Nahyan kilichotokea tarehe 13 Mei 2022

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula (Mb) akisaini kitabu cha maombolezo katika Ubalozi wa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), nchini kufuatia kifo cha Rais wa Umoja wa Falme za Kiarabu, Sheikh Khalifa bin Zayed Al-Nahyan kilichotokea tarehe 13 Mei 2022

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akizungumza na Balozi wa Umoja wa Falme za Kiarabu nchini Mhe. Khalifa Abdulrahman Mohamed Al-Marzooqi baada ya kusaini kitabu cha maombolezo katika Ubalozi huo kufuatia kifo cha Rais wa Umoja wa Falme za Kiarabu, Sheikh Khalifa bin Zayed Al-Nahyan kilichotokea tarehe 13 Mei 2022

Balozi wa Umoja wa Falme za Kiarabu nchini Mhe. Khalifa Abdulrahman Mohamed Al-Marzooqi akimueleza jambo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula baada ya kusaini kitabu cha maombolezo 



Friday, May 13, 2022

UNAIDS YAPONGEZA JITIHADA ZA SERIKALI KUKABILIANA NA UKIMWI

Na Mwandishi wetu, Dar

Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Ukimwi (UNAIDS) limepongeza jitihada zinazochukuliwa na Serikali ya Tanzania katika kupambana na maambukizi ya Virusi vya UKIMWI nchini.

Pongezi hizo zimetolewa na Mkurugenzi Mkazi wa UNAIDS nchini, Dkt. Leo Zekeng  alipoagana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula katika Ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam baada ya kumaliza muda wake wa uwakilishi nchini.

Dkt. Zekeng amepongeza jitihada zinazoendelea kuchukuliwa na Serikali katika kukabiliana na maambukizi ya Ukimwi hasa katika eneo la utoaji wa elimu kwa jamiii, kuanzishwa kwa Sera ya kudhibiti Maambukizi ya Virusi vya UKIMWI pamoja na mikakati mbalimbali ya kupambana na Maambukizi ya Virusi vya UKIMWI.

“Nilipowasili Tanzania miaka mitano iliyopita takriban asilimia 62 ya Watanzania walikuwa wanafahamu hali ya afya zao hasa kwa ugonjwa wa UKIMWI, ila sasa nafurahi kuwa takribani asilimia 90 ya Watanzania wanafahamu hali ya afya zao, hili ni jambo kubwa sana katika jamii,” alisema Dkt. Zekeng.

Dkt. Zekeng amesema malengo ya UNAIDS ni kuhakikisha kuwa kufikia mwaka 2025 hakutakuwa na mtoto atakayezaliwa na Maambukizi ya Virusi vya UKIMWI. 

Akizungumza katika tukio hilo, Balozi Mulamula amempongeza Dkt. Zekeng kwa kazi nzuri ya kutoa elimu na kampeni dhidi ya Maambukizi ya Virusi vya UKIMWI ambapo kupitia kampeni hizo maambukizi ya ugonjwa huo nchini yamepungua kwa kiasi kikubwa.

“Elimu kuhusu maambukizi ya Virusi vya UKIMWI imekuwa msaada mkubwa katika jamii yetu, tunawashukuru UNAIDS kwa misaada ya dawa hasa ARVs pamoja na kampeni mbalimbali za kuelimisha jamiii juu ya maambukizi ya virusi vya UKIMWI ambapo hadi sasa jamii imepata uelewa wa kujikinga na ugonjwa huo na maambukizi yamepungua kwa kiasi kikubwa,” alisema Balozi Mulamula.

Balozi Mulamula ameongeza kuwa miaka ya nyuma kulikuwa na unyanyapaa mkubwa katika jamii zetu lakini kutokana na elimu kuhusu maambukizi ya virusi vya UKIMWI pamoja na kampeni mbalimbali ambazo zimekuwa zikitolewa na UNAIDS kwa umma zimesaidia kupunguza unyanyapaa na maambukizi ya virusi vya Ukimwi nchini.

Aidha, Waziri Mulamula amemsihi Dkt. Zekeng kuwa balozi mzuri wa Tanzania kokote aendako Duniani ambapo Dkt. Zekeng ameahidi kuwa balozi mzuri wa Tanzania na kusisitiza kuwa Tanzania ni nyumbani kwake hivyo wakati wote atakuwa balozi mzuri.

Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Ukimwi (UNAIDS) nchini, Dkt. Leo Zekeng  akizungumza na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula katika Ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam. Wa kwanza kulia ni Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirkiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mindi Kasiga akifuatiwa na Afisa kutoka Wizarani.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akimueleza jambo Mkurugenzi Mkazi wa UNAIDS nchini, Dkt. Leo Zekeng katika Ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akimueleza jambo Mkurugenzi Mkazi wa UNAIDS nchini, Dkt. Leo Zekeng katika Ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam. Mwingine pichani ni Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirkiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mindi Kasiga. 


Maongezi ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula na Mkurugenzi Mkazi wa UNAIDS nchini, Dkt. Leo Zekeng yakiendelea katika Ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akimkabidhi zawadi ya picha ya mlima Kilimanjaro Mkurugenzi Mkazi wa UNAIDS nchini, Dkt. Leo Zekeng katika Ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mkazi wa UNAIDS nchini, Dkt. Leo Zekeng katika Ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mkazi wa UNAIDS nchini, Dkt. Leo Zekeng katika Ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam. Wengine pichani ni Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirkiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mindi Kasiga akifuatiwa na Afisa kutoka Wizarani.



Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akiagana na Mkurugenzi Mkazi wa UNAIDS nchini, Dkt. Leo Zekeng katika Ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam




Thursday, May 12, 2022

SERIKALI YAELEZEA MAFANIKIO ZIARA ZA RAIS MAREKANI, UGANDA NA ROYAL TOUR

Na Mwandishi Wetu, Dar

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Zuhura Yunus, amefafanua mafanikio ya ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, nchini Marekani iliyojumuisha uzinduzi wa Filamu ya “Tanzania; The Royal Tour." Pamoja na ziara ya Rais nchini Uganda. 

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika Ikulu jijini Dar es salaam, Bi. Yunus amesema ziara ya Rais nchini Marekani imekuwa na faida ya kusainiwa kwa mikataba saba kati ya kampuni za Marekani na Tanzania zenye lengo la kufanya biashara na uwekezaji nchini yenye gharama za zaidi ya shilingi Trilioni 11. 

Naye Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula (Mb) ameelezea ziara ya Rais nchini Uganda ambayo iliwezesha  kufanyika kwa mkutano maalum na wadau wa sekta za mafuta na gesi kuhusiana na ujenzi wa bomba la mafuta.

"Tulikuwa na mkutano maalum juu ya ujenzi wa bomba la mafuta kutoka Uganda hadi Tanzania, tayari hatua ya ulipaji fidia kwa wananchi imekamilika na  ujenzi wa bomba hilo utaanza hivi karibuni", alisema Balozi Mulamula.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Rais ya kuitangaza Tanzania, Dkt. Hassan Abbasi, amesema Filamu ya Royal Tour imeonesha mafanikio makubwa sana na kwa sasa filamu hiyo imeendelea kusambazwa katika vituo vya televisheni karibu 300 kati ya 350 nchini Marekani na kwa hapa nchini tayari filamu hiyo imesambazwa katika vituo vyote vya televisheni.

Naye Katibu Mkuu  Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara Prof. Godius Kahyarara amesema filamu ya Royal Tour ina manufaa ya moja kwa moja kwa Taifana  inatarajiwa kuleta wawekezaji, watalii na wafanyabiashara na kuongeza kuwa wao kama Wizara wameandaa mkutano na wadau ili kupanga mikakati ya kuwekeza katika sekta ya utalii.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Utalii (TTB), Bw. Amos Nko amesema TTB inatangaza kwa kasi vivutio vya utalii ili kuvutia watalii wengi kuja nchini. 

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu Bibi Zuhura Yunus akizungumza na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) kuhusu ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan nchini Marekani na Uganda katika Mkutano uliofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akiwaelezea Waandishi wa Habari (hawapo pichani) mafanikio ya ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan nchini Marekani na Uganda katika Mkutano uliofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam 

Katibu Mkuu Wizara ya Sanaa, Utamaduni, na Michezo, Dkt. Hassan Abbas akiwaelezea Waandishi wa Habari (hawapo pichani) mafanikio ya ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan nchini Marekani na Uganda katika Mkutano uliofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam

Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika, Balozi Swahiba Mndeme (wa kwanza kushoto) na Mkurugenzi wa Kitengo cha mawasiliano Serikalini Balozi Mindi Kasiga (wa nne kulia) Maafisa waandamizi wa Serikali pamoja na Waandishi wa Habari  wakifuatilia mafanikio ya ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan nchini Marekani na Uganda katika Mkutano uliofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam







MWAKILISHI MKAZI WA AfDB AWASILISHA BARUA ZA UTAMBULISHO

Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB) nchini Tanzania, Bibi. Patricia Laverley amewasilisha Barua za Utambulisho kwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Libarata Mulamula katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.

Baada ya kupokea barua za utambulisho, viongozi hao pamoja na mambo mengine, walijadiliana masuala ya miundombinu endelevu pamoja na uboreshaji wa mazingira katika sekta binafsi.

Bibi. Laverley amemhakikishia Balozi Mulamula ushirikiano wa kutosha kutoka AfDB katika kuchochea utekelezaji wa miradi mbalimbali inayofadhiliwa na bank hiyo hapa nchini.

Nae Balozi Mulamula amemhakikishia ushirikiano wa kutosha kutoka Serikalini wakati wote wa utekelezaji wa majukumu yake hapa nchini na kuonmgeza kuwa AfDB imekuwa mdau mkubwa wa maendeleo ya Tanzania jambo ambalo ni ishara ya uhusiano mzuri uliopo baina ya Tanzania na bank hiyo. 


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Libarata Mulamula akipokea barua za utambulisho kutoka kwa Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB) nchini Tanzania, Bibi. Patricia Laverley katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Libarata Mulamula akizungumza na Mwakilishi Mkazi wa AfDB nchini Tanzania, Bibi. Patricia Laverley katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

Mazungumzo ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Libarata Mulamula na Mwakilishi Mkazi wa AfDB nchini Tanzania, Bibi. Patricia Laverley yakiendelea katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Libarata Mulamula akiagana na Mwakilishi Mkazi wa AfDB nchini Tanzania, Bibi. Patricia Laverley yakiendelea katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam



TANZANIA, JAMAICA KUONGEZA MAENEO MAPYA YA USHIRIKIANO

Na Mwandishi Wetu, Dar 

Serikali ya Tanzania na Jamaica zimeahidi kuongeza maeneo mapya ya ushirikiano katika sekta za utalii, biashara na uwekezaji pamoja na elimu kwa maslahi mapana ya pande zote mbili.

Ahadi hiyo imetolewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula (Mb) wakati alipokutana kwa mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje na Biashara wa Jamaica Mhe. Kamina Smith katika Ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.

“Leo nimekutana na Mhe. Smith na tumejadili na kudhamiria kuongeza maeneo mapya ya ushirikiano katika sekta za utalii, biashara na uwekezaji, elimu, uwezeshaji wa wanawake kiuchumi pamoja na vijana 

Tanzania na Jamaica tumedhamiria kufanya kazi kwa karibu katika kutafuta njia bora ya kufungua fursa mpya kwa maslahi ya mataifa yote mawili,” alisema Balozi Mulamula 

Nae Waziri wa Mambo ya Nje na Biashara wa Jamaica Mhe. Kamina Smith amesema kuwa Tanzania imekuwa na uhusiano mzuri na Jamaica ambapo uhusiano huo umekuwa ni chachu ya maendeleo inayopelekea kuongeza maeneo mapya ya ushirikiano katika sekta za utalii, biashara na uwekezaji na elimu.

“Ushirikiano uliopo baina ya mataifa yetu mawili umekuwa chachu ya maendeleo na lengo la ushirikiano huu ni kukuza, kuendeleza na kuimarisha uchumi wetu,” alisema Mhe. Smith

Katika tukio jingine, Waziri Mulamula amekutana na Kufanya Mazungumzo na Balozi wa Misri nchini, Mhe. Mohamed Gaber Abouelwafa.  

Pamoja na mambo mengine, viongozi hao wamejadili masuala ya kuendeleza na kuimarisha uhusiano katika sekta mbalimbali ikiwemo biashara na uwekezaji, elimu, pamoja na afya. 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akizungumza na Waziri wa Mambo ya Nje na Biashara wa Jamaica, Mhe. Kamina Smith katika Ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

Waziri wa Mambo ya Nje na Biashara wa Jamaica, Mhe. Kamina Smith akimueleza jambo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula katika Ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

Mazungumzo ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula na Waziri wa Mambo ya Nje na Biashara wa Jamaica, Mhe. Kamina Smith yakiendelea katika Ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam



Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akimsikiliza Balozi wa Misri nchini, Mhe. Mohamed Gaber Abouelwafa walipokutana kwa mazungumzo katika Ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akizungumza Balozi wa Misri nchini, Mhe. Mohamed Gaber Abouelwafa walipokutana kwa mazungumzo katika Ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

Mazungumzo ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula na Balozi wa Misri nchini, Mhe. Mohamed Gaber Abouelwafa yakiendelea katika Ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam