Friday, December 15, 2023

TANZANIA YAPONGEZWA KUWA MSTARI WA MBELE KUREJESHA AMANI DRC, ICGLR

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imepongezwa kwa kuendelea kuwa mstari wa mbele kurejesha amani katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Ukanda wa Maziwa Makuu.

Pongezi hizo zimetolewa Mjumbe Maalum wa Katibu Mkuu Umoja wa Mataifa katika Ukanda wa Maziwa Makuu, Mhe. Balozi Huang alipokutana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba (Mb.) Jijini Dar es Salaam

“Umoja wa Mataifa tunaipongeza Tanzania kwa kulinda misingi ya amani na kuwa mstari wa mbele katika kurejesha amani na usalama katika Ukanda wa Maziwa Makuu,” alisema Balozi Huang.

Mhe. Huang ameongeza kuwa ni wakati muafaka kwa viongozi wa Ukanda wa Maziwa Makuu kusaidia kuhakikisha kuwa amani inapatikana Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ili kuliwezesha taifa hilo kusonga mbele kiuchumi na kisiasa.

Kwa upande wake Waziri Makamba ameupongeza Umoja wa Mataifa kwa kuendelea kudumisha amani katika ukanda wa Maziwa Makuu kwani ndiyo njia itakayosaidia kuwalinda raia na kukuza uchumi katika ukanda huo.

“Tanzania chini ya uongozi imara wa Rais, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, inaamini amani ndio msingi pekee wa maendeleo kwa mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla,” alisema Waziri Makamba.

Pamoja na mambo mengine, Waziri Makamba amemhakikishia Balozi Huang kuwa Tanzania itaendelea kushirikiana na Umoja wa Mataifa na Jumuiya za Kimataifa na za Kikanda kurejesha amani na usalama katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Ukanda wa Maziwa Makuu.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba (Mb.) akimueleza jambo Mjumbe Maalum wa Katibu Mkuu Umoja wa Mataifa katika Ukanda wa Maziwa Makuu, Mhe. Balozi Huang walipokutana kwa mazungumzo Jijini Dar es Salaam

Mjumbe Maalum wa Katibu Mkuu Umoja wa Mataifa katika Ukanda wa Maziwa Makuu, Mhe. Balozi Huang akizungumza na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba walipokutana kwa mazungumzo Jijini Dar es Salaam

Mazungumzo baina ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba na Mjumbe Maalum wa Katibu Mkuu Umoja wa Mataifa katika Ukanda wa Maziwa Makuu, Mhe. Balozi Huang yakiendelea Jijini Dar es Salaam

Mazungumzo baina ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba na Mjumbe Maalum wa Katibu Mkuu Umoja wa Mataifa katika Ukanda wa Maziwa Makuu, Mhe. Balozi Huang yakiendelea Jijini Dar es Salaam

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba akimsikilza Mjumbe Maalum wa Katibu Mkuu Umoja wa Mataifa katika Ukanda wa Maziwa Makuu, Mhe. Balozi Huang walipokutana kwa mazungumzo Jijini Dar es Salaam



Thursday, December 14, 2023

FINLAND NCHI YA KWANZA YA NORDIC KUJADILIANA KIDIPOLOMASIA NA TANZANIA

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mara ya kwanza imefanya majadiliano ya kidiplomasia na Serikali ya Finland kwa lengo la kuimarisha, kukuza na kudumisha ushirikiano katika sekta mbalimbali za kipaumbele kwa maslahi ya pande zote mbili. 

Pamoja na Tanzania kuwa na uhusiano mzuri na nchi za Nordic, Finland ndiyo nchi ya kwanza kufanya majadiliano ya kidiplomasia na Tanzania. Chimbuko la majadaliano hayo ni kuendelea kuimarisha ushirikiano baina ya Tanzania na nchi za Umoja wa Ulaya. 

Mkutano huo kwa upande wa Tanzania umeongozwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba (Mb.) wakati upande wa Finland umeongozwa na Naibu Waziri katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Finland anayeshughulikia Ushirikiano wa Maendeleo ya Kimataifa, Mhe. Pasi Hellman. 

Akizungumza katika mkutano uliokutanisha pande hizo mbili leo tarehe 14 Disemba, 2023 Jijini Dar es Salaam, Waziri Makamba amesema kuwa kutetea na kulinda misingi ya demokrasia na utawala bora ni kipaumbele cha Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Waziri Makamba ameeleza kuwa maboresho yaliyofanyika katika sheria ya vyama vya siasa na sheria ya uchaguzi yameleta mageuzi katika kuendesha chaaguzi mbalimbali nchini na uhuru wa vyama vya siasa kuendesha shughuli zake nchini.

Aidha, Tanzania itaendelea kulinda na kukuza misingi ya haki za binadamu, demokrasia na utawala bora kama nguzo muhimu ya kuleta maendeleo endelevu nchini. 

Kwa upande wake, Naibu Waziri katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Finland anayeshughulikia Ushirikiaano wa Maendeleo ya Kimataifa, Mhe. Pasi Hellman amesema ushirikiano kati ya Finland na Tanzania umekuwa imara kwa zaidi ya miaka 50 na utaendelea kuimarika kutokana na misingi imara ya ushirikiano iliyopo baina ya mataifa hayo.

“Huu ni mkutano wetu wa kwanza wa majadiliano ya kidiplomasia kati ya Finland na Tanzania ambapo umelenga kuimarisha ushirikiano, kubadilishana ujuzi na uzoefu wa masuala mbalimbali yanayohusu diplomasia na maendeleo katika sekta mbalimbali baina ya nchi zetu”.

Kadhalika kupitia mkutano huo, viongozi hao pamoja na mambo mengine, wamejadili masuala ya biashara na uwekezaji, uwezeshaji kiuchumi, uwezeshaji wanawake, ushirikiano wa kikanda kati ya Ulaya na Afrika, kizazi cha usawa, hali ya hewa, mabadiliko ya tabianchi pamoja na masuala yanayohusu ulinzi na usalama.

Mkutano huo ulihudhuriwa na Makatibu Wakuu kutoka Wizara za Kisekta (Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Elimu, Uchukuzi, Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto, Ulinzi na Makamu wa Rais Mazingira).

Wengine ni Balozi wa Tanzania Nchini Finland, Balozi wa Finland nchini Tanzania pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC).


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba (Mb.) amekizungumza katika  mkutano baina ya Tanzania na Finland. Mkutano huo umelenga kuimarisha, kukuza na kudumisha ushirikiano katika sekta mbalimbali za kipaumbele kwa maslahi ya pande zote mbili.

Naibu Waziri katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Finland anayeshughulikia Ushirikiaano wa Maendeleo ya Kimataifa, Mhe. Pasi Hellman akichangia jambo wakati wa mkutano baina ya Tanzania na Finland, Jijini Dar es Salaam

Viongozi mbalimbali wakifuatilia Mkutano, Wa kwanza kushoto ni Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Samwel Shelukindo, Katibu Mkuu Wizara ya Uchukuzi, Prof. Godius Kahyarara (wa kwanza kushoto) na Balozi wa Tanzania nchini Finland, Mhe. Grace Olotu.

Balozi wa Finland nchini Tanzania Mhe. Theresa Zitting (wa kwanza kulia) pamoja na ujumbe ulioambatana na Mhe. Pasi wakifuatilia mkutano


Sehemu ya Ujumbe uliombatana na Naibu Waziri katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Finland anayeshughulikia Ushirikiaano wa Maendeleo ya Kimataifa, Mhe. Pasi Hellman  


Mkutano ukiendelea

Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini katika Wizara ya mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mindi Kasiga akielezea jambo katika Mkutano baina ya Tanzania na Finland
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba na Naibu Waziri katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Finland anayeshughulikia Ushirikiaano wa Maendeleo ya Kimataifa, Mhe. Pasi Hellman katika picha ya pamoja na wajumbe walioshiriki mkutano baina ya Tanzania na Finland 

 

Wednesday, December 13, 2023

WAZIRI MAKAMBA ATETA NA WATUMISHI WA WIZARA


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Makamba akizungumza na watumishi wa Wizara hiyo jijini Dodoma

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Makamba (Mb) amekutana na kuzungumza na watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki jijini Dodoma.

Akizingumza katika kikao na wafanyakazi hao, Waziri Makamba amewataka watumishi wa Wizara kuendelea kufanya kazi kwa bidii na kuzingatia weledi ili kuleta matokeo yanayotarajiwa na hivyo kuiletea nchi maendeleo 

Waziri Makamba pia amewataka watumishi wa Wizara kuhakikisha mienendo na matendo yao viakisi Wizara wanayoifanyia kazi.

Amesema Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki inaakisi muonekano wa nchi mbele ya mataifa mengine.

“Wizara inatazamwa kama taswira ya nchi, ni muhimu kuhakikisha mnazingatia namna mnavyoishi, mnavyovaa na mnavyoongea pia, kiujumla ni mwenendo na muonekano wenu ndivyo ambavyo nchi inavyoonekana au kuchukuliwa, nyinyi ni kioo cha nchi” alisisitiza Mhe. Waziri Makamba.

Amesema Wizara imepanga kuboresha mazingira ya kazi na kujenga udugu, urafiki ili kumfanya kila mtumishi kuipenda kazi yake.

Amesema uamuzi huo unatokana na ukweli kuwa mtumishi anatumia muda mwingi ofisini kuliko sehemu nyingine hivyo kuboresha mazingira husika ni jambo la msingi

Akiongelea changamoto mbalimbali zinazoikabili Wizara Waziri Makamba ameahidi kuzifanyia kazi ili kutimiza nia yake ya kuwa na mahala bora pa kufanyia kazi na hivyo kutoa matokeo yanayotarajiwa.

Kikao hicho kimehudhuriwa na Naibu Waziri Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk (Mb), Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt. Samwel Shelukindo, Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki anayeshughulikia Afrika Mashariki Balozi Stephen Mbundi, Wakurugenzi, watumishi wa Wizara na Wakuu wa Taasisi zilizo chini ya Wizara.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Makamba (Mb) akizungumza na Naibu Waziri Mhe. Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk (Mb) na Katibu Mkuu Balozi Dkt. Samwel Shelukindo (katikati) alipowasili katika Ukumbi wa Mikutano wa St. Gaspar Dodoma kuzungumza na watumishi wa Wizara
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Makamba akisalimiana na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki anayeshughulikia Afrika Mashariki Balozi Stephen Mbundi alipowasili katika Ukumbi wa Mikutano wa St. Gaspar Dodoma kuzungumza na watumishi wa Wizara
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Makamba akisisitiza jambo alipokuwa akizungumza na watumishi wa Wizara hiyo jijini Dodoma
Naibu Waziri Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk akizungumza na watumishi wa Wizara jijini Dodoma
Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakimsikiliza Waziri Mhe. January Makamba kwenye kwenye mkutano uliokuwa ukiendelea jijini Dodoma
Sehemu ya Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakimsikiliza Waziri Mhe. January Makamba kwenye kwenye mkutano uliokuwa ukiendelea jijini Dodoma
Sehemu ya Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakifurahia jambo wakati wa Mkutano Waziri Mhe. January Makamba uliokuwa ukiendelea jijini Dodoma
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt. Samwel Shelukindo akizungumza na watumishi wa Wizara jijini Dodoma
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki anayeshughulikia Afrika Mashariki Balozi Stephen Mbundi akizungumza na watumishi wa Wizara jijini Dodoma
Sehemu ya watumishi wakifuatilia mkutano

Mkutano ukiendelea
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Makamba na Naibu Waziri Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk wakiteta jambo

Monday, December 11, 2023

WAZIRI MAKAMBA AKAGUA MAENDELEO YA UJENZI WA JENGO LA OFISI YA WIZARA MTUMBA


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Makamba akifafanua jambo alipotembelea ujenzi wa ofisi za Wizara unaoendelea katika mjini wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Makamba (Mb) ametembelea mradi wa ujenzi wa jengo la ofisi za Wizara unaoendelea katika mjini wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma. 

Lengo la kutembelea mradi huo ni kujionea hatua iliyofikiwa katika ujenzi na kufanya mazungumzo na wasimamizi wa mradi ili kuwa baini uwepo wa changamoto zinazoweza kukwamisha ukamilishwaji wa mradi kwa wakati na viwango vinavyotarajiwa

Akizungumza na mkandarasi wakati wa ziara hiyo ya ukaguzi Mhe. Makamba amepongeza hatua iliyofikiwa na amemtaka mkandarasi wa ujenzi wa jengo hilo kuongeza kasi ili maradi huo ukamilike na kukabidhiwa kwa wakati.

“Pamoja na kazi nzuri iliyofanyika katika ujenzi wa jengo hili, bado kazi iliyobaki ni kubwa inabidi muongeze bidii zaidi ili mradi ukabidhiwe na jengo lianze kutumika na hatimaye kuleta haueni ya tatizo la uhaba wa ofisi kwa watumishi wa Wizara” amesema Mhe. Makamba

Katika ziara hiyo Mhe. Waziri Makamba aliambatana na Makatibu Wakuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt. Samuel Shelukindo, na Balozi Stephen Mbundi anayesimamia masuala ya Afrika Mashariki na watendaji wengine wa Wizara.

Jengo hilo litakalogharimu kiasi cha Shilingi bilioni 22.9 hadi kukamilika kwake lilianza kujengwa mwezi Januari 2022. Ujenzi huo unaogharamiwa na Serikali unalenga kuziwezesha Wizara na Taasisi za Serikali kuwa na majengo ya kudumu katika mji wa Serikali.

Mradi wa ujenzi wa jengo hilo unatekezwa na Umoja wa makampuni ya Sole works na mshauri elekezi ambaye ni Chuo Kikuu cha Ardhi. 

Mbali na kutembelea jengo Wizara Mhe. Waziri Makamba ametembelea ofisi za Wizara zilizopo katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) ambapo pia alipata fursa ya kuzungumza na watumishi mbalimbali waliokuwa wakiendelea na utekelezaji wa majukumu yao katika ofisi hizo
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Makamba akibadilishana mawazo na baadhi ya watumishi katika Idara ya Sera na Mipango katika ofisi za Wizara zilizopo katika Chuo Kikuu cha Dodoma
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Makamba (Mb) akiwasili katika eneo la ujenzi wa ofisi za Wizara unaoendelea katika mjini wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Makamba akiwa katika Ofisi za Wizara zilizopo katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) alipotembelea ofisi hizo tarihe 11 Disemba 2023 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Makamba akiwa katika viunga vya Ofisi ya Wizara Mtumba, jijini Dodoma
Twasira ya jengo la ofisi za Wizara linaloendelea kujengwa katika mjini wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Makamba akibadilishana mawazo na baadhi ya watumishi katika Idara ya Sera na Mipango katika ofisi za Wizara zilizopo katika Chuo Kikuu cha Dodoma
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Makamba akisikiliza maelezo kutoka kwa Mhandisi wa Wizara, Bw. John Kiswaga alipotembelea ujenzi wa ofisi za Wizara unaoendelea katika mjini wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Makamba akizungumza mmoja wa watumishi katika Idara Biashara, Uwekezaji na Sekta ya Uzalishaji alipotembelea ofisi za Wizara zilizopo katika Chuo Kikuu cha Dodoma

Sunday, December 10, 2023

WAJASIRIAMALI KUTOKA NCHI WANACHAMA WA EAC WAPONGEZWA KWA KUCHANGIA MAENDELEO

Serikali za Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) zitaendelea kuthamini mchango unaotolewa na sekta isiyo rasmi katika  kukuza maendeleo ya nchi hizo ikiwemo ajira.

 

Kauli hiyo imetolewa na Mwakilishi wa Balozi wa Tanzania nchini Burundi, Brigedia Jenerali Salum Mnumbe wakati akizungumza kwenye Maadhimisho ya Siku ya Tanzania maarufu kama Tanzania Day yaliyofanyika jijini Bujumbura, Burundi ikiwa ni sehemu ya shughuli za Maonesho ya 23 ya Wajasiriamali Wadogo na wa Kati wa Jumuiya ya Afrika Mashariki yanayoendelea jijini hapa.

 

Amesema kuwa Nchi Wanachama wa Afrika Mashariki zilianzisha Maonesho hayo kwa kutambua na kuthamini mchango unaotolewa na sekta isiyo rasmi katika maendeleo ya nchi hizo ikiwemo kuzalisha fursa za ajira kwa wingi na kuzalisha bidhaa zinazotumiwa zaidi na wananchi.

 

“Lengo la kuanzisha maonesho hayo lilikuwa ni kuwapatia fursa wajasiriamali wa sekta hii ili waweze kushiriki katika uzalishaji na kuwawezesha kukua na kuingia kwenye sekta rasmi” amesema Brig. Jen. Mnumbe.

 

Pia amewahamasisha Wajasiriamali hao kushirikiana na Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kuongeza bidii katika kuzalisha bidhaa bora kwa viwango vya kimataifa na kuzitangaza bidhaa hizo ndani na nje ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ili kuongeza wigo wa soko.

 

Pia amewataka kuendelea kushirikiana, kubadilishana mawazo na ujuzi katika uzalishaji wa bidhaa na utengenezaji wa vifungashio na kuthaminisha.

 

Kadhalika ametumia fursa hiyo kuwapongeza na kuwashukuru wajasiriamali kutoka Tanzania wanaoshiriki maonesho hayo kwa kuandaa bidhaa zenye ubunifu, ubora wa hali ya juu na zenye asili ya kitanzania.

 

Maadhimisho ya Tanzania Day yaliambatana na shughuli mbalimbali zilizofanywa na wajasiriamali wa Tanzania kwa kuonesha utamaduni wa Tanzania pamoja na bidhaa mbalimbali zinazozalishwa nchini. Miongoni mwa shuguli zilizofanywa ni pamoja na maonesho ya mavazi ya asili, ngoma za asili na muziki. 

 

Maonesho ya 23 ambayo yamewashirikisha wajasiriamali 1,500 kutoka nchi zote wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, wakiwemo 259 kutoka Tanzania yanafanyika kwa mara ya tatu nchini Burundi tangu kuanzishwa kwake mwaka 1999.

Mgeni Rasmi na  Mwakilishi wa Balozi wa Tanzania nchini Burundi, Brigedia Jenerali Salum Mnumbe akizungumza kwenye maadhimisho ya Siku ya Tanzania iliyofanyika jijini Bujumbura, Burundi ikiwa ni sehemu ya Maonesho ya 23 ya Wajasiriamali Wadogo na wa Kati kutoka Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki yanayoendelea jijini hapa kuanzia tarehe 05 hadi 15 Desemba 2023
Mgeni Rasmi na  Mwakilishi wa Balozi wa Tanzania nchini Burundi, Brigedia Jenerali Salum Mnumbe (kushoto) akiwa jukwaa kuu na wageni wengine waalikwa walioshiriki maadhimisho ya Siku ya Tanzania iliyofanyika jijini Bujumbura, Burundi ikiwa ni sehemu ya Maonesho ya 23 ya Wajasiriamali Wadogo na wa Kati kutoka Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki yanayoendelea jijini hapa kuanzia tarehe 05 hadi 15 Desemba 2023. Kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Biashara, Uwekezaji na Sekta za Uzalishaji katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Bernard Haule na katikati ni Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki anayeshughulikia masuala ya Fedha na Biashara, Bi. Annette Mutaawe.
Mgeni Rasmi, Brigedia Jenerali Mnumbe akiwa jukwaa kuu na wageni waalikwa
Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki anayeshughulikia masuala ya Fedha na Biashara, Bi. Annette Mutaawe akitoa salamu za Sekretarieti ya Jumuiya hiyo wakati wa maadhimisho ya Siku ya Tanzania iliyofanyika jijini Bujumbura, Burundi


Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya Wajasiriamali Wadogo na wa Kati Afrika Mashariki, Bw. Josephat Rweyemamu naye akizungumza
Brigedia Jenerali Mnumbe akipokea zawadi ya kitabu kutoka kwa Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki anayeshughulikia masuala ya Fedha na Biashara, Bi. Annette Mutaawe alipotembelea banda la Sekretariei ya Jumuiya hiyo

Mgeni Rasmi na  Mwakilishi wa Balozi wa Tanzania nchini Burundi, Brigedia Jenerali Salum Mnumbe akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika banda la Tanzania kabla ya kuanza kwa sherehe za maadhimisho ya Siku ya Tanzania iliyofanyika jijini Bujumbura, Burundi ikiwa ni sehemu ya Maonesho ya 23 ya Wajasiriamali Wadogo na wa Kati kutoka Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki yanayoendelea jijini hapa kuanzia tarehe 05 hadi 15 Desemba 2023

Mgeni Rasmi na  Mwakilishi wa Balozi wa Tanzania nchini Burundi, Brigedia Jenerali Salum Mnumbe akipata maelezo kutoka kwa Mjasiriamali wa Tanzania alipotembelea mabanda ya wajasiriamali hao wakati wa maadhimisho ya Siku ya Tanzania iliyofanyika jijini Bujumbura, Burundi ikiwa ni sehemu ya Maonesho ya 23 ya Wajasiriamali Wadogo na wa Kati kutoka Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki yanayoendelea jijini hapa kuanzia tarehe 05 hadi 15 Desemba 2023

Mgeni Rasmi na  Mwakilishi wa Balozi wa Tanzania nchini Burundi, Brigedia Jenerali Salum Mnumbe akipata maelezo kutoka kwa Mjasiriamali wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo alipotembelea mabanda ya wajasiriamali  kutoka nchi za EAC wakati wa maadhimisho ya Siku ya Tanzania iliyofanyika jijini Bujumbura, Burundi ikiwa ni sehemu ya Maonesho ya 23 ya Wajasiriamali Wadogo na wa Kati kutoka Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki yanayoendelea jijini hapa kuanzia tarehe 05 hadi 15 Desemba 2023
Watanzania wakiwa na furaha wakati wa  wa maadhimisho ya Siku ya Tanzania iliyofanyika jijini Bujumbura, Burundi ikiwa ni sehemu ya Maonesho ya 23 ya Wajasiriamali Wadogo na wa Kati kutoka Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki yanayoendelea jijini hapa kuanzia tarehe 05 hadi 15 Desemba 2023
Sehemu nyingine ya Watanzania


Wajasiriamali kutoka Tanzania wanaoshiriki Maonesho ya 23 ya Wajasiriamali Wadogo na wa Kati kutoka Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki yanayoendelea jijini Bujumbura wakionesha ubunifu wa mavazi mbalimbali wanayotengeza ikiwa ni shamrashara za kuadhimisha siku ya Tanzania 
Mkurugenzi wa  Ajira na Ukuzaji Ujuzi katika Ofisi ya Waziri Mkuu, Bw. Ally Msaki (wa nne kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Watanzania walioshiriki maadhimisho ya Siku ya Tanzania iliyofanyika jijini Bujumbura, Burundi ikiwa ni sehemu ya Maonesho ya 23 ya Wajasiriamali Wadogo na wa Kati kutoka Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki yanayoendelea jijini hapa kuanzia tarehe 05 hadi 15 Desemba 2023


Picha ya pamoja