Sunday, December 10, 2023

WAJASIRIAMALI KUTOKA NCHI WANACHAMA WA EAC WAPONGEZWA KWA KUCHANGIA MAENDELEO

Serikali za Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) zitaendelea kuthamini mchango unaotolewa na sekta isiyo rasmi katika  kukuza maendeleo ya nchi hizo ikiwemo ajira.

 

Kauli hiyo imetolewa na Mwakilishi wa Balozi wa Tanzania nchini Burundi, Brigedia Jenerali Salum Mnumbe wakati akizungumza kwenye Maadhimisho ya Siku ya Tanzania maarufu kama Tanzania Day yaliyofanyika jijini Bujumbura, Burundi ikiwa ni sehemu ya shughuli za Maonesho ya 23 ya Wajasiriamali Wadogo na wa Kati wa Jumuiya ya Afrika Mashariki yanayoendelea jijini hapa.

 

Amesema kuwa Nchi Wanachama wa Afrika Mashariki zilianzisha Maonesho hayo kwa kutambua na kuthamini mchango unaotolewa na sekta isiyo rasmi katika maendeleo ya nchi hizo ikiwemo kuzalisha fursa za ajira kwa wingi na kuzalisha bidhaa zinazotumiwa zaidi na wananchi.

 

“Lengo la kuanzisha maonesho hayo lilikuwa ni kuwapatia fursa wajasiriamali wa sekta hii ili waweze kushiriki katika uzalishaji na kuwawezesha kukua na kuingia kwenye sekta rasmi” amesema Brig. Jen. Mnumbe.

 

Pia amewahamasisha Wajasiriamali hao kushirikiana na Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kuongeza bidii katika kuzalisha bidhaa bora kwa viwango vya kimataifa na kuzitangaza bidhaa hizo ndani na nje ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ili kuongeza wigo wa soko.

 

Pia amewataka kuendelea kushirikiana, kubadilishana mawazo na ujuzi katika uzalishaji wa bidhaa na utengenezaji wa vifungashio na kuthaminisha.

 

Kadhalika ametumia fursa hiyo kuwapongeza na kuwashukuru wajasiriamali kutoka Tanzania wanaoshiriki maonesho hayo kwa kuandaa bidhaa zenye ubunifu, ubora wa hali ya juu na zenye asili ya kitanzania.

 

Maadhimisho ya Tanzania Day yaliambatana na shughuli mbalimbali zilizofanywa na wajasiriamali wa Tanzania kwa kuonesha utamaduni wa Tanzania pamoja na bidhaa mbalimbali zinazozalishwa nchini. Miongoni mwa shuguli zilizofanywa ni pamoja na maonesho ya mavazi ya asili, ngoma za asili na muziki. 

 

Maonesho ya 23 ambayo yamewashirikisha wajasiriamali 1,500 kutoka nchi zote wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, wakiwemo 259 kutoka Tanzania yanafanyika kwa mara ya tatu nchini Burundi tangu kuanzishwa kwake mwaka 1999.

Mgeni Rasmi na  Mwakilishi wa Balozi wa Tanzania nchini Burundi, Brigedia Jenerali Salum Mnumbe akizungumza kwenye maadhimisho ya Siku ya Tanzania iliyofanyika jijini Bujumbura, Burundi ikiwa ni sehemu ya Maonesho ya 23 ya Wajasiriamali Wadogo na wa Kati kutoka Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki yanayoendelea jijini hapa kuanzia tarehe 05 hadi 15 Desemba 2023
Mgeni Rasmi na  Mwakilishi wa Balozi wa Tanzania nchini Burundi, Brigedia Jenerali Salum Mnumbe (kushoto) akiwa jukwaa kuu na wageni wengine waalikwa walioshiriki maadhimisho ya Siku ya Tanzania iliyofanyika jijini Bujumbura, Burundi ikiwa ni sehemu ya Maonesho ya 23 ya Wajasiriamali Wadogo na wa Kati kutoka Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki yanayoendelea jijini hapa kuanzia tarehe 05 hadi 15 Desemba 2023. Kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Biashara, Uwekezaji na Sekta za Uzalishaji katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Bernard Haule na katikati ni Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki anayeshughulikia masuala ya Fedha na Biashara, Bi. Annette Mutaawe.
Mgeni Rasmi, Brigedia Jenerali Mnumbe akiwa jukwaa kuu na wageni waalikwa
Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki anayeshughulikia masuala ya Fedha na Biashara, Bi. Annette Mutaawe akitoa salamu za Sekretarieti ya Jumuiya hiyo wakati wa maadhimisho ya Siku ya Tanzania iliyofanyika jijini Bujumbura, Burundi


Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya Wajasiriamali Wadogo na wa Kati Afrika Mashariki, Bw. Josephat Rweyemamu naye akizungumza
Brigedia Jenerali Mnumbe akipokea zawadi ya kitabu kutoka kwa Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki anayeshughulikia masuala ya Fedha na Biashara, Bi. Annette Mutaawe alipotembelea banda la Sekretariei ya Jumuiya hiyo

Mgeni Rasmi na  Mwakilishi wa Balozi wa Tanzania nchini Burundi, Brigedia Jenerali Salum Mnumbe akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika banda la Tanzania kabla ya kuanza kwa sherehe za maadhimisho ya Siku ya Tanzania iliyofanyika jijini Bujumbura, Burundi ikiwa ni sehemu ya Maonesho ya 23 ya Wajasiriamali Wadogo na wa Kati kutoka Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki yanayoendelea jijini hapa kuanzia tarehe 05 hadi 15 Desemba 2023

Mgeni Rasmi na  Mwakilishi wa Balozi wa Tanzania nchini Burundi, Brigedia Jenerali Salum Mnumbe akipata maelezo kutoka kwa Mjasiriamali wa Tanzania alipotembelea mabanda ya wajasiriamali hao wakati wa maadhimisho ya Siku ya Tanzania iliyofanyika jijini Bujumbura, Burundi ikiwa ni sehemu ya Maonesho ya 23 ya Wajasiriamali Wadogo na wa Kati kutoka Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki yanayoendelea jijini hapa kuanzia tarehe 05 hadi 15 Desemba 2023

Mgeni Rasmi na  Mwakilishi wa Balozi wa Tanzania nchini Burundi, Brigedia Jenerali Salum Mnumbe akipata maelezo kutoka kwa Mjasiriamali wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo alipotembelea mabanda ya wajasiriamali  kutoka nchi za EAC wakati wa maadhimisho ya Siku ya Tanzania iliyofanyika jijini Bujumbura, Burundi ikiwa ni sehemu ya Maonesho ya 23 ya Wajasiriamali Wadogo na wa Kati kutoka Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki yanayoendelea jijini hapa kuanzia tarehe 05 hadi 15 Desemba 2023
Watanzania wakiwa na furaha wakati wa  wa maadhimisho ya Siku ya Tanzania iliyofanyika jijini Bujumbura, Burundi ikiwa ni sehemu ya Maonesho ya 23 ya Wajasiriamali Wadogo na wa Kati kutoka Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki yanayoendelea jijini hapa kuanzia tarehe 05 hadi 15 Desemba 2023
Sehemu nyingine ya Watanzania


Wajasiriamali kutoka Tanzania wanaoshiriki Maonesho ya 23 ya Wajasiriamali Wadogo na wa Kati kutoka Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki yanayoendelea jijini Bujumbura wakionesha ubunifu wa mavazi mbalimbali wanayotengeza ikiwa ni shamrashara za kuadhimisha siku ya Tanzania 
Mkurugenzi wa  Ajira na Ukuzaji Ujuzi katika Ofisi ya Waziri Mkuu, Bw. Ally Msaki (wa nne kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Watanzania walioshiriki maadhimisho ya Siku ya Tanzania iliyofanyika jijini Bujumbura, Burundi ikiwa ni sehemu ya Maonesho ya 23 ya Wajasiriamali Wadogo na wa Kati kutoka Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki yanayoendelea jijini hapa kuanzia tarehe 05 hadi 15 Desemba 2023


Picha ya pamoja


No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.