|
Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba (Mb.) akizungumza katika kikao kati yake na Mabalozi na Wawakilishi
wa Mashirika wa Kimataifa Jijini
Dar es Salaam alipokutana nao
na kuwaelezea kilichotokea Hanang
mkoani Manyara na hatua zilizochukuliwa na Serikali katika kukabiliana na janga
hilo |
|
Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba (Mb.) akizungumza na Mabalozi na Wawakilishi
wa Mashirika wa Kimataifa (hawapo pichani) alipokutana nao
Jijini
Dar es Salaam na kuwaelezea kilichotokea Hanang
mkoani Manyara na hatua zilizochukuliwa na Serikali katika kukabiliana na janga
hilo |
|
Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba (Mb.) akiongoza Mabalozi na Wawakilishi
wa Mashirika wa Kimataifa kusimama kwa dakika moja kwa ajili ya kuwaombea wananchi waliopoteza maisha kutokana na maafa yaliyotokea Hanang mkoani Manyara alipokutana nao
Jijini
Dar es Salaam na kuwaelezea kilichotokea Hanang
mkoani Manyara na hatua zilizochukuliwa na Serikali katika kukabiliana na janga
hilo |
|
Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa
Mataifa nchini Bw. Zlatan Milišić akichangia jambo wakati wa kikao cha Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki
na Mabalozi na Wawakilishi wa Mashirika wa Kimataifa Jijini Dar es Salaam ambapo Waziri Makamba aliwaelezea
kilichotokea Hanang mkoani Manyara na hatua zilizochukuliwa na Serikali katika
kukabiliana na janga hilo
|
|
Baadhi ya Mabalozi na Wawakilishi wa Mashirika wa Kimataifa nchini wakimsikiliza Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Makamba alipokutana nao Jijini Dar es Salaam kuwaelezea
kilichotokea Hanang mkoani Manyara na hatua zilizochukuliwa na Serikali katika
kukabiliana na janga hilo
|
|
Balozi wa Somalia nchini, Mhe. Zahra Ali Hassan
akichangia jambo wakati wa kikao cha Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki
na Mabalozi na Wawakilishi wa Mashirika wa Kimataifa Jijini Dar es Salaam ambapo Waziri Makamba aliwaelezea
kilichotokea Hanang mkoani Manyara na hatua zilizochukuliwa na Serikali katika
kukabiliana na janga hilo |
|
Baadhi ya Mabalozi na Wawakilishi wa Mashirika wa Kimataifa nchini wakimsikiliza Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki alipokutana nao Jijini Dar es Salaam kuwaelezea
kilichotokea Hanang mkoani Manyara na hatua zilizochukuliwa na Serikali katika
kukabiliana na janga hilo
|
|
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Makamba akizungumza na Balozi wa Italia nnchini Mhe. Marco Lombardi alipokutana na Mabalozi na Wawakilishi wa Mashirika wa Kimataifa nchini Jijini Dar es Salaam kuwaelezea
kilichotokea Hanang mkoani Manyara na hatua zilizochukuliwa na Serikali katika
kukabiliana na janga hilo
|
|
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt. Samwel Shelukindo (kushoto) na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Stephen Mbundi (katikati) wakizungumza na mmoja wa washiriki wa kikao kati ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki alipokutana na Mabalozi na Wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa jijini Dar es Salam kuelezea yaliyotokea mkoani Manyara na jinsi Serikali ilivyokabiliana na janga hilo. |
|
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Makamba akizungumza na Balozi wa Marekani nchini Mhe. Michael Battle alipokutana na Mabalozi na Wawakilishi wa Mashirika wa Kimataifa nchini Jijini Dar es Salaam kuwaelezea
kilichotokea Hanang mkoani Manyara na hatua zilizochukuliwa na Serikali katika
kukabiliana na janga hilo
|
|
NaibuWaziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk akizungumza na Balozi wa Kenya nchini Mhe. Isack Njenga wakati wa Kikao kati ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Makamba na Mabalozi na Wawakilishi wa Mashirika wa Kimataifa nchini Jijini Dar es Salaam kuwaelezea
kilichotokea Hanang mkoani Manyara na hatua zilizochukuliwa na Serikali katika
kukabiliana na janga hilo
|
|
Mkurugenzi wa Mawasiliano Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Mindi Kasiga akizungumza kuwakaribisha Mabalozi na Wawakilishi wa Mashirika wa Kimataifa nchini Jijini Dar es Salaam kuzungumza na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Januari Makamba |
Mabalozi na Wawakilishi wa Mashirika
ya Kimataifa nchini wamepongeza jitihada zinazochukuliwa na Serikali katika
zoezi la uokoaji Hanang, kutokana na maporomoko ya tope kutoka katika mlima
Hanang kufuatia mvua kubwa iliyonyesha Mkoani Manyara tarehe 02 Disemba, 2023.
Mabalozi na Wawakilishi wa
Mashirika hayo wametoa pongezi hizo Jijini Dar es Salaam walipokutana na Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba (Mb.) aliyewaita
kuwaelezea kilichotokea Hanang mkoani Manyara na hatua zilizochukuliwa na Serikali
katika kukabiliana na janga hilo.
Akizungumza katika kikao hicho
Mhe. Waziri Makamba amesema maporomoko hayo ya tope yamesababisha vifo vya watu
72, kujeruhi watu 117, kuharibu mali za watu, makazi na miundombinu ya barabara,
maji na umeme.
“Serikali ya Tanzania inaishukuru
Jumuiya ya Kimataifa nchini kwa jinsi ilivyoikimbilia na kusaidia wahanga wa maporomoko
hayo hasa katika kusaidia urejeshaji wa huduma za muhimu za kibinadamu kwa
wananchi wa Katesh” alisema.
Amesema katika kukabiliana na
janga hilo, Serikali iliunda Kamati ya Kitaifa ya Maafa iliyo chini ya Ofisi ya
Waziri Mkuu inayoshirikiana na mamlaka ya Mkoa wa Manyara na kufungua akaunti
Maalum ya maafa kwa ajili ya kuratibu na upokeaji misaada mbalimbali ili kusaidia
wahanga wa maporomoko hayo na kuwezesha maisha ya watu kuendelea kama kawaida.
“Wahanga bado wanahitaji
misaada ya kibinadamu ya hali na mali, wengi wamepoteza makazi yao na kupoteza
wapendwa wao pamoja na kuharibika kwa miundombinu ya barabara, maji na umeme na
kusababisha maisha kusimama katika eneo hilo” alisema.
Amesema Serikali imeandaa
maeneo maalum kwa ajili ya kuwahifadhi na kuwahudumia wahanga kwa kuwapatia huduma
muhimu za kibinadamu, kuwatibu majeruhi, na kuwaokoa na kuwaondoa watu katika
maeneo yaliyoathiriwa.
Amesema Serikali inaendelea na
zoezi la kutafuta miili ya watu katika matope, kuhudumia shughuli za mazishi ya
watu waliofariki na kuwafariji watu waliopoteza wapendwa wao kutokana na
maporomoko hayo ili waweze kurejea katika hali zao za kawaida.
Naye Mwakilishi Mkazi wa Umoja
wa Mataifa nchini Mhe. Zlatan Milisick amepongeza hatua za haraka zilizochukuliwa
na Serikali katika zoezi la uokoaji wa wananchi na mali zao huko Hanang na kuongeza
kuwa Ofisi ya Umoja wa Mataifa Tanzania itaendelea kushirikiana na Serikali na kwamba
Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini yameungana na kuchanga misaada ya yao ya
kibinadamu kwa ajili ya kusaidia wahanga hao ambayo wataikabidhi kwa Serikali.
Balozi wa Kenya amesema Kenya kama
nchi jirani iko pamoja na Watanzania katika sala na maombi kuwaombea marehemu
na kutoa pole kwa familia za marehemu.
Akizungumza katika kikao hicho
Balozi wa Somalia nchini Mhe. Zahra Ali Hassan amesema Umoja wa Mabalozi wa
Afrika kwa umoja wao wameungana na kuwaingiza katika maombi wahanga wa
maporomoko hayo na kuchanga misaada ya kibinadamu ambayo wataikabidhi kwa
Serikali na kutoa pole kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na
Watanzania wote kwa maafa hayo makubwa yaliyotokea nchini.
Balozi wa Msumbiji Mhe. Ricardo Mtumbuida amesema Msumbiji inaungana
na Tanzania na kutoa pole kwa Mhe. Rais, Watanzania na wahanga wote na kuwaombea
marehemu wapumzike kwa amani.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.