|
Balozi wa Tanzania nchini Ubelgiji, Luxembourg na Mwakilishi kwenye
Umoja wa Ulaya na Jumuiya ya Nchi za Afrika, Caribbean na Pacific (OACPS)
Mhe. Jestas Abuok
Nyamanga, akisaini kwa niaba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mkataba Mpya wa Ubia
baina ya Nchi za OACPS na Umoja wa Ulaya (Mkataba wa Samoa). Hafla ya kusaini
Mkataba huo ilfanyika tarehe 19 Desemba 2023 katika Makao Makuu ya OACPS Brussels Ubelgiji.
Wanaoshuhudia tukio hilo ni maafisa waandamizi kutoka Sekretarieti ya OACPS na
Umoja wa Ulaya. |
|
Balozi wa Tanzania nchini Ubelgiji, Luxembourg na Mwakilishi kwenye
Umoja wa Ulaya na Jumuiya ya Nchi za Afrika, Caribbean na Pacific (OACPS)
Mhe. Jestas Abuok
Nyamanga, akisaini kwa niaba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mkataba Mpya wa Ubia
baina ya Nchi za OACPS na Umoja wa Ulaya (Mkataba wa Samoa).
|
|
Mhe. Balozi Jestas Abuok Nyamanga (katikati) ameshika Mkataba Mpya
wa Ubia baina ya Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika, Caribbean na Pacific
(OACPS) na Umoja wa Ulaya baada ya kusainiwa katika hafla fupi
iliyofanyika Makao Makuu ya Jumuiya ya Afrika Caribbean na Pacific,
jijini Brussels Ubelgiji tarehe 19 Desemba 2023. Waliosimama pamoja naye ni
wawakilishi kutoka Umoja wa Ulaya na OACPS.
|
Kaimu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Nchi za
Afrika, Caribbean na Pacific (OACPS) Dkt. Ibrahim Richard akimpa mkono kumpongeza Mhe. Balozi Jestas Abuok Nyamanga baada ya kusaini
mkataba huo kwa niaba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
|
Mhe.Balozi Jestas
Abuok Nyamanga katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Ubalozi
wa Tanzania, Brussels baada ya kusaini Mkataba Mpya
wa Ubia baina ya Jumuiya ya Nchi za Afrika, Caribbean na Pacific (OACPS) na
Umoja wa Ulaya katika hafla iliyofanyika katika Makao Makuu ya OACPS Brussels tarehe
19 Desemba 2023. Aliyesimama kulia kwa Balozi Nyamanga ni Dkt. Ibrahim Richard Kaimu
Katibu Mkuu wa OACPS.
|
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.