Sunday, December 10, 2023

WAJASIRIAMALI WAHAMASISHWA KUCHANGAMKIA SOKO HURU LA BIASHARA LA AFRIKA

 

Wajasiriamali Wadogo na wa Kati kutoka Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wametakiwa kuchangamkia fursa za Soko Huru la Biashara Barani Afrika (AfCFTA) kwa kujua matakwa ya kisheria ya soko hilo, kuongeza thamani ya bidhaa zao na kutumia teknolojia.

 

Rai hiyo imetolewa na Afisa Forodha Mkuu wa Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, Bw. Donald Tindamanyire wakati akiwasilisha mada kuhusu “Umuhimu wa Kuwandaa Wajasiriamali Wadogo na wa Kati Kuchangamkia Fusa za Soko Huru la Biashara kwa Wajasiriama” kwenye maadhimisho ya “SIKU YA TANZANIA” yaliyofanyika jijini Bujumbura tarehe 10 Desemba 2023.

 

Bw.  Tindamanyire amesema  kuwa wajasiriamali wana nafasi kubwa katika kutumia soko hilo la Afrika na kueleza kuwa kinachohitajika sasa ni wajasiriamali hao kujifunza taratibu mbalimbali zinazohitajika kwenye kulifikia soko hilo zikiwemo sheria, taratibu na kanuni za ufanyaji biashara za kuvuka mipaka ili kuepuka vikwazo vinavyoweza kujitokeza pindi wanapohitaji kulitumia soko hilo.

 

Ameongeza kusema kuwa, wajasiriamali pia wanatakiwa kuboresha na kuongeza thamani ya bidhaa zao pamoja na kutumia teknolojia ili kuzalisha kwa wingi na kuweza kuingia kwenye ushindani na nchi zingine za Afrika.

 

Kadhalika Bw. Tindamanyire ametoa wito kwa Serikali za Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kuwashirikisha wajasiriamali wadogo kutoa maoni kwenye uandaaji wa Itifaki  mbalimbali zinazohusu biashara za kuvuka mipaka kabla ya kuanza utekelezaji wake pamoja na kuboresha miundombinu kama barabara na reli ili kurahisisha usafirishaji wa bidhaa mbalimbali.

 

Pia Bw.  Tindamanyire alitumia fursa hiyo kuwahimiza wanawake na vijana kutumia fursa ya soko hilo ambalo limeandaa Itifaki Mahsusi kuhusu kundi hilo la watu engo la kuanzishwa kwa soko huru la bishara barani Afrika ni kukuza na kuimarisha biashara miongoni mwa nchi za Afrika ambayo kimsingi bado ni ndogo ukilinganisha na biashara kati ya Afrika na nchi za Asia na Ulaya.

 

Wajasiriamali 259 kutoka Tanzania wanashiriki Maonesho ya 23 ya Wajasiriamali Wadogo na wa Kati ya Jumuiya ya Afrika Mashariki yanayofanyika nchini humo kuanzia tarehe 05 hadi 15 Desemba 2023. Pamoja na mambo mengine maonesho hayo hutenga siku kwa kila nchi mwanachama kujitangaza kupitia shughuli mbalimbali ikiwemo utamaduni kama muziki, mavazi na vyakula.

 

Itifaki ya Soko Huru la Biashara Barani Afrika hadi sasa imeridhiwa na nchi 47 kati ya 54 za Afrika ikiwemo Tanzania na imeanza kutumika tangu mwezi Januari 2021.

Afisa Forodha Mkuu wa Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, Bw. Donald Tindamanyire  akiwasilisha mada kuhusu “Umuhimu wa Kuwandaa Wajasiriamali Wadogo na wa Kati Kuchangamkia Fusa za Soko Huru la Biashara kwa Wajasiriama” ikiwa ni sehemu maadhimisho ya “SIKU YA TANZANIA” yaliyofanyika jijini Bujumbura tarehe 10 Desemba 2023.

Afisa Forodha Mkuu wa Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, Bw. Donald Tindamanyireakiendelea kuwasilisha mada kuhusu “Umuhimu wa Kuwandaa Wajasiriamali Wadogo na wa Kati Kuchangamkia Fusa za Soko Huru la Biashara kwa Wajasiriama” kwenye maadhimisho ya “SIKU YA TANZANIA” yaliyofanyika jijini Bujumbura tarehe 10 Desemba 2023.

Wadau mbalimbali wakiwemo wajasiriamali kutoka Tanzania wakifuatilia mada kuhusu “Umuhimu wa Kuwandaa Wajasiriamali Wadogo na wa Kati Kuchangamkia Fusa za Soko Huru la Biashara kwa Wajasiriama” ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya “SIKU YA TANZANIA” yaliyofanyika jijini Bujumbura tarehe 10 Desemba 2023.

Sehemu nyingine ya washiriki

Wadau wakifuatilia mada

Sehemu nyingine ya wadau wakati wa uwasilishwaji mada

Mwonekano wa mabanda ya wajasiriamali wanaoshiriki maonesho ya 23 ya Jumuiya ya Afrika Mashariki
























 

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.