Monday, December 11, 2023

WAZIRI MAKAMBA AKAGUA MAENDELEO YA UJENZI WA JENGO LA OFISI YA WIZARA MTUMBA


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Makamba akifafanua jambo alipotembelea ujenzi wa ofisi za Wizara unaoendelea katika mjini wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Makamba (Mb) ametembelea mradi wa ujenzi wa jengo la ofisi za Wizara unaoendelea katika mjini wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma. 

Lengo la kutembelea mradi huo ni kujionea hatua iliyofikiwa katika ujenzi na kufanya mazungumzo na wasimamizi wa mradi ili kuwa baini uwepo wa changamoto zinazoweza kukwamisha ukamilishwaji wa mradi kwa wakati na viwango vinavyotarajiwa

Akizungumza na mkandarasi wakati wa ziara hiyo ya ukaguzi Mhe. Makamba amepongeza hatua iliyofikiwa na amemtaka mkandarasi wa ujenzi wa jengo hilo kuongeza kasi ili maradi huo ukamilike na kukabidhiwa kwa wakati.

“Pamoja na kazi nzuri iliyofanyika katika ujenzi wa jengo hili, bado kazi iliyobaki ni kubwa inabidi muongeze bidii zaidi ili mradi ukabidhiwe na jengo lianze kutumika na hatimaye kuleta haueni ya tatizo la uhaba wa ofisi kwa watumishi wa Wizara” amesema Mhe. Makamba

Katika ziara hiyo Mhe. Waziri Makamba aliambatana na Makatibu Wakuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt. Samuel Shelukindo, na Balozi Stephen Mbundi anayesimamia masuala ya Afrika Mashariki na watendaji wengine wa Wizara.

Jengo hilo litakalogharimu kiasi cha Shilingi bilioni 22.9 hadi kukamilika kwake lilianza kujengwa mwezi Januari 2022. Ujenzi huo unaogharamiwa na Serikali unalenga kuziwezesha Wizara na Taasisi za Serikali kuwa na majengo ya kudumu katika mji wa Serikali.

Mradi wa ujenzi wa jengo hilo unatekezwa na Umoja wa makampuni ya Sole works na mshauri elekezi ambaye ni Chuo Kikuu cha Ardhi. 

Mbali na kutembelea jengo Wizara Mhe. Waziri Makamba ametembelea ofisi za Wizara zilizopo katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) ambapo pia alipata fursa ya kuzungumza na watumishi mbalimbali waliokuwa wakiendelea na utekelezaji wa majukumu yao katika ofisi hizo
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Makamba akibadilishana mawazo na baadhi ya watumishi katika Idara ya Sera na Mipango katika ofisi za Wizara zilizopo katika Chuo Kikuu cha Dodoma
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Makamba (Mb) akiwasili katika eneo la ujenzi wa ofisi za Wizara unaoendelea katika mjini wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Makamba akiwa katika Ofisi za Wizara zilizopo katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) alipotembelea ofisi hizo tarihe 11 Disemba 2023 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Makamba akiwa katika viunga vya Ofisi ya Wizara Mtumba, jijini Dodoma
Twasira ya jengo la ofisi za Wizara linaloendelea kujengwa katika mjini wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Makamba akibadilishana mawazo na baadhi ya watumishi katika Idara ya Sera na Mipango katika ofisi za Wizara zilizopo katika Chuo Kikuu cha Dodoma
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Makamba akisikiliza maelezo kutoka kwa Mhandisi wa Wizara, Bw. John Kiswaga alipotembelea ujenzi wa ofisi za Wizara unaoendelea katika mjini wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Makamba akizungumza mmoja wa watumishi katika Idara Biashara, Uwekezaji na Sekta ya Uzalishaji alipotembelea ofisi za Wizara zilizopo katika Chuo Kikuu cha Dodoma

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.