Wednesday, December 20, 2023

BALOZI MBAROUK ASAINI KITABU CHA MAOMBOLEZO UBALOZI WA KUWAIT

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk (Mb.) amesaini kitabu cha maombolezo Ubalozi wa Kuwait Jijini Dar es Salaam kufuatia kifo cha Amir wa Kuwait, Sheikh Nawaf al-Ahmad Al-Sabah.

Kiongozi huyo alifariki tarehe 16 Disemba 2023 akiwa na umri wa miaka 86 ambapo aliongoza taifa hilo kwa miaka mitatu iliyopita. 

Balozi Mbarouk ametoa salamu za pole za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa Balozi wa Kuwait nchini, Mhe. Mubarak Mohammed Alsehaijan ambapo amemuelezea kiongozi huyo atakumbukwa daima kama mwanadiplomasia na kiongozi imara aliyejitolea maisha yake katika masuala ya amani.

“Kiongozi huyo atakumbukwa kama kiongozi mahiri wa Kuwait aliyeimarisha ushirikiano wa karibu kati ya Kuwait na Tanzania,” alisema Balozi Mbarouk. 

“Kwa niaba ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, tunapenda kutoa salamu zetu za pole kwa wananchi wa Kuwait kwa kuondokewa na kiongozi bora na mpenda amani. Roho yake Ipumzike mahali pema peponi,” aliongeza Mhe. Balozi Mbarouk

Balozi Mbarouk aliongeza kuwa Daima Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itamkumbuka Hayati Sheikh Nawaf al-Ahmad Al-Sabah kama kiongozi imara na aliyependa amani.


Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk akisalimiana na Balozi wa Kuwait nchini, Mhe. Mubarak Mohammed Alsehaijan baada ya kuwasili katika Ubalozi huo Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kusaini kitabu cha maombolezo kufuatia kifo cha Amir wa Kuwait, Sheikh Nawaf al-Ahmad Al-Sabah kilichotekea tarehe 16 Disemba 2023


Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk akisaini kitabu cha maombolezo katika Ubalozi wa Kuwait Jijini Dar es Salaam kufuatia kifo cha Amir wa Kuwait, Sheikh Nawaf al-Ahmad Al-Sabah kilichotekea tarehe 16 Disemba 2023

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk akisaini kitabu cha maombolezo katika Ubalozi wa Kuwait Jijini Dar es Salaam kufuatia kifo cha Amir wa Kuwait, Sheikh Nawaf al-Ahmad Al-Sabah kilichotekea tarehe 16 Disemba 2023

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk akimfariji Balozi wa Kuwait nchini Mhe. Mubarak Mohammed Alsehaijan katika Ubalozi wa Kuwait Jijini Dar es Salaam kufuatia kifo cha Amir wa Kuwait, Sheikh Nawaf al-Ahmad Al-Sabah kilichotekea tarehe 16 Disemba 2023



No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.