Sunday, November 13, 2011

ZIARA YA DKT. SHEIN UARABUNI


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dkt. Ali Mohamed Shein,akizungumza na mwenyeji wake Sheikh Saud Bin Saqr Al Qasimi Kiongozi wa Ras Al Khaimah,wakati alipowasili katika kasri ya kiongozi huyo Mjini Ras Al Kahimah, jana akiwa katika ziara ya kukuza uhusiano wa mashirikiano na kukuza maendeleo ya sekta mbali mbali za maendeleleo kama Afya, Elimu, Biashara nyenginezo za maendeleo.
 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Ali Mohamed Shein akiagana na Daktari Bingwa wa upasuaji  Dr J.M.Gauer, kutoka nchini Switzerland, katika hospitali ya  Ras Al Khaimah, alipotembelea akiwa katika ziara ya kukuza uhusiano na ushirikiano wa  sekta mbali mbali za maendeleo, ikiwemo Afya, Elimu, Biashara na nyinginezo.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dkt. Ali Mohamed Shein akikaribishwa  na  Naibu Mtendaji Mkuu wa kampuni ya ujenzi ya Rak Ceramics, Abdalla Massaad,wakati alipotembelea  kuona vifaa mbali mbali  vya ujenzi huko Ras Al Khaimah,akiwa katika ziara ya kukuza uhusiano na mashirikiano katika sekta za maendeleo.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Ali Mohamed Shein akipata maelezo kutoka kwa Naibu Mtendaji Mkuu wa kampuni ya ujenzi ya Rak Ceramics, Abdalla Massaad,wakati alipotembelea  kuona vifaa mbali mbali  vya ujenzi huko Ras Al Khaimah,akiwa katikam ziara ya kukuza uhusiano na mashirikiano katika sekta za maendeleo.



Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Ali Mohamed Shein,pamoja na ujumbe wake wakiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa Hospitali ya Ras Al Khaimah,walipoitembelea hospitali hiyo wakiwa katika ziara ya kukuza uhusianao na ushirikiano katika sekta za maendeleo.
Picha na Ikulu, Zanzibar.


No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.