Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo amewapisha Wakurugenzi wapya tisa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa ambao pia watakuwa na hadhi ya Kibalozi pamoja na Balozi mdogo wa Tanzania kwenye Umoja wa Mataifa.
Walioapishwa ni Ndugu Ramadhan Muombwa Mwinyi ambaye anakuwa Balozi Mdogo katika Ubalozi wa Tanzania kwneye Umoja wa Mataifa, Bw. Vincent Kibwana ambaye anakuwa Mkurugenzi, Idara ya Afrika; Ndugu Naimi Aziz ambaye anakuwa Mkurugenzi, Idara ya Ushirikiano wa Kikanda; Ndugu Celestine Mushy ambaye anakuwa Mkurugenzi, Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa; Ndugu Yahya Simba ambaye anakuwa Mkurugenzi, Idara ya Mashariki ya Kati, na Ndugu Bertha Somi ambaye ameteuliwa kuwa Mkurugenzi, Idara ya Diaspora.
Wengine ni Ndugu Irene Kasyanju aliyeteuliwa kuwa Mkurugenzi, Kitengo cha Sheria; Ndugu Dorah Msechu ambaye ameapishwa kuwa Mkurugenzi, Idara ya Ulaya na Amerika, Ndugu Mbelwa Kairuki ambaye anakuwa Mkurugenzi, Idara ya Asia na Australia, na Ndugu Silima Haji ambaye ameteuliwa kuwa Mkurugenzi, Idara ya Mambo ya Nje, Zanzibar.
Kabla ya uteuzi wake, Ndugu Muombwa alikuwa Katibu Mkuu Kiongozi Katika Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Ndugu Kibwana alikuwa Afisa Mambo ya Nje Mkuu, Ndugu Naimi Aziz alikuwa Mkurugenzi Msaidizi, Ndugu Mushy alikuwa Kaimu Katibu wa Waziri Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Ndugu Simba alikuwa Afisa Mambo ya Nje Mkuu, na Ndugu Somi alikuwa Afisa Mambo ya Nje Mkuu.
Naye Ndugu Kasyanju alikuwa Mkurugenzi Msaidizi, Ndugu Msechu alikuwa Mkurugenzi Msaidizi, Ndugu Kairuki alikuwa Msaidizi wa Rais (Hotuba), Ofisi ya Rais, Ikulu na Ndugu Haji alikuwa Afisa Mambo ya Nje Mkuu.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.