Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya MrishoKikwete amesisitiza kuwa Serikali yake kamwe haijapata hata kufikiria kujenga barabara ya lami kukatisha Hifadhi ya Taifa ya Wanyapori ya Serengeti lakini bado Serikali itawapa wananchi wa Loliondo, mkoani Arusha, na Mugumu, mkoani Mara barabara nzuri ya lami.
Akizungumza na wananchi hao katika eneo la Wasso, Rais Kikwete amesemakuwa ujenzi wa kilomita 50 za kwanza za barabara hiyo inayopitia Loliondo utaanza msimu huu wa fedha kuanzia mjini Mugumu, Mkoani Mara.
“Tumesema na kusema mara nyingi tu kuwa hatukusudii kujenga barabara ya lami kukatisha Hifadhi ya Serengeti lakini tutawapa wananchi waLoliondo na Mugumu barabara za lami kwa maana ya barabara ya lami kutoka Mto wa Mbu kupitia Loliondo hadi kwenye mlango wa kuingiaHifadhi ya Serengeti upande wa Magharibi na kutoka Mugumu hadi langola kuingilia Hifadhi ya Serengeti upande wa Mashariki wa Hifadhi hiyo,” amesema Rais Kikwete huku akishangiliwa na wananchi.
Rais Kikwete amesema: “Watanzania wote wana haki sawa ya kupatiwamaendeleo kwa fedha zao wenyewe. Kuna haki gani wananchi wa sehemunyingine kupatiwa maendeleo kwa fedha za umma, lakini wale wa Loliondo na Mugumu kunyimwa haki hiyo? Waambie hao watu wanaolipwa kusema uongokuhusu ujenzi wa barabara hiyo waendelee. Wanapotosha ili waendelee
kulipwa. Lakini kwa hili la barabara hatutawasikiliza.”
Kuhusu umeme wa mjini Loliondo, Rais Kikwete amesema kuwa umeme wa Loliondo ni matokeo ya ahadi yake na wanaoukejeli umeme huo wakiuita wa jua (solar) wanakasirika kwa sababu Serikali imetimiza ahadi yake ya kuwapatia wananchi wa wilaya za Ngorongoro na Longido umeme. “Nasikia wanajekeli umeme, wanasema kuwa eti ni wa solar na kuwa hauwaki vizuri. Watu hawa ni wanafiki tu. Kwao yamekuwa maneno ya kawaida sasa. Yasiwawabaishe. Endeleeni na shughuli zenu,” amesema Rais Kikwete na kuahidi kuwa serikali itaongeza fedha ili kununua nguzo na nyaya zaidi ili kuwezesha majenereta yote manne yaliyofungwa Loliondo kufanya kazi. Kati ya majenereta hayo manne, ni moja tu linafanya kazi ingawa mahitaji ya umeme ni makubwa.Baada ya kumaliza hotuba yake, Rais Kikwete aliamua kwenda kutembelea kituo cha kuzalisha umeme cha Loliondo kujionea mwenyewe mitambo inavyofanya kazi na kupata maelezo.Wakati wa sherehe hiyo, ambako Rais Kikwete alikabidhi ng’ombe 64 za mwanzo kwa kaya 16, wananchi wa Wilaya Ngorongoro walimshukuru Rais Kikwete na Serikali yake kwa miradi ya umeme, maji, barabara ya lami, shule za kata na mradi wa kuwawezesha kwa ng’ombe.Kabla ya kuondoka Loliondo kwenda Dodoma, Rais Kikwete ametembeleaHospitali Teule ya Wilaya ya Ngorongoro ya Wasso ambako amewajuliahali wagonjwa kwenye hospitali hiyo.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
3 Agosti, 2012