Friday, May 17, 2013

Tanzania na Canada zasaini Mkataba wa Kulinda na Kukuza Uwekezaji


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K.Membe (Mb.), kwa pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje wa Canada, Mhe. John Baird wakisaini Mkataba wa Kulinda na Kukuza Uwekezaji (FIPA) kati ya Tanzania na Canada. Hafla hiyo fupi ilifanyika Wizarani tarehe 16 Mei, 2013.

Mhe. Membe na Mhe. Baird wakiendelea kusaini mkataba huo huku Maafisa wa Sheria kutoka Tanzania na Canada wakishuhudia. Kushoto kwa Mhe. Membe ni Bw. Abdallah Mtibora, Afisa Mambo ya Nje katika Kitengo cha Sheria, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.


Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Rajab Gamaha akiwa na Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika, Balozi Dora Msechu (katikati), na Mkurugenzi Msaidizi wa Idara hiyo Bibi Grace Shangali wakishuhudia uwekaji saini wa Mkataba wa FIPA.

Wajumbe wengine waliokuwepo kushuhudia tukio hilo la uwekaji saini wa Mkataba wa FIPA.

Mhe. Membe  na Mhe. Baird wakibadilishana Mkataba huo mara baada ya kusaini.
Mhe. Membe na Mhe. Baird wakionesha kwa Wajumbe Mkataba waliosaini.

Mhe. Membe akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu Mkataba wa FIPA.


Waandishi wa Habari pamoja na Wajumbe wengine wakimsiliza Mhe. Membe alipokuwa akitoa ufafanuzi kuhusu Mkataba wa Kukuza na Kulinda Uwekezaji kati ya Tanzania na Canada (FIPA).

Mhe. Baird nae akizungumza machache kuhusu mkataba huo.



Thursday, May 16, 2013

Mhe. Membe amkaribisha Waziri wa Mambo ya Nje wa Canada nchini

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akisalimiana na  Waziri wa Mambo ya Nje wa Canada,  Mhe. John Baird  alipowasili kwenye Hoteli ya Hyatty Regency Kilimanjaro kwa ajili ya kushiriki Chakula cha Mchana kilichoandaliwa kwa heshima yake na Mhe. Membe. Mhe. Baird yupo nchini kwa ziara ya kikazi ya siku mbili ambapo pamoja na mambo mengine pia watazungumza kuhusu kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Canada pamoja na kusaini Mkataba "Foreign Investment, Promotion and Protection Agreement" (FIPA).


Mhe. Membe akifurahia jambo wakati wa mazungumzo yake na Mhe. Baird.

Mhe. Membe akimweleza jambo Mhe. Baird wakati wa mazungumzo yao. Wengine katika picha ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Rajab Gamaha (wa tatu kushoto) na Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Dora Msechu.



Mhe. Membe akiendelea na mazungumzo huku Mhe. Baird akimsikiliza. Kushoto ni Balozi wa Canada hapa nchini Mhe. Alexandre Leveque.


Mhe. Membe akimkabidhi Mhe. Baird zawadi ya picha ya kuchora inayoonesha Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro  pamoja na wanyama aina ya Tembo.


Mhe. Baird akifurahia zawadi hiyo.

Mhe. Baird akimshukuru Mhe. Membe kwa kumpatia zawadi hiyo nzuri.

Wednesday, May 15, 2013

Mhe. Membe akutana kwa mazungumzo na Mwakilishi wa UNAMID

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) (kulia) akisalimiana na Mwakilishi Maalum na Msuluhishi  Mkuu wa  Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika katika Mgogoro wa Darfur (UNAMID), Mhe. Mohamed Ibn Chambas mara baada ya kuwasili Wizarani kwa mazungumzo. Katika mazungumzo yao walijadili masuala mbalimbali ya namna Vikosi vya UNAMID vinavyotekeleza majukumu yake huko Darfur  katika kulinda Amani. Tanzania pia imechangia katika Vikosi vya UNAMID Wanajeshi wapatao  1,129.
Mhe. Membe akiendelea na mazungumzo na Mhe. Chambas.

Ujumbe uliofuatana na Mhe. Chambas akiwemo Meja Jenerali Wyjones Kisamba (wa tatu kushoto), Kaimu Kamanda wa Vikosi vya kulinda amani vya UNAMID kutoka Tanzania. Kulia ni Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa hapa nchini, Dkt. Alberic Kacou.

Mhe. Chambas akimweleza Mhe. Membe jitihada mbalimbali zinazofanywa na UNAMID huko Darfur katika kuhakikisha amani katika Jimbo hilo lililopo Magharibi mwa Sudan inarejea.



Ujumbe kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa ukifuatilia kwa makini mazungumzo kati ya Mhe. Waziri Membe na Mhe. Chambas (hawapo pichani). Kushoto ni Bw. Nathaniel Kaaya, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Togolani Mavura (kulia), Msaidizi wa Waziri na Bi. Eva Ng'itu (katikati), Afisa Mambo ya Nje.

Picha zaidi za mazungumzo hayo.

Mhe. Membe akiagana na Mhe. Chambas baada ya kumaliza mazungumzo yao.

Tuesday, May 14, 2013

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI: UTEUZI WA MABALOZI WA TANZANIA NCHINI MAREKANI NA UMOJA WA FALME ZA KIARABU




220px-Coat of arms of Tanzania.svg f1f71


;

Mkurugenzi wa Ushirikiano wa Kimataifa akutana kwa mazungumzo na Mwakilishi wa UNIDO hapa nchini

Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy (kulia) akizungumza na Mwakilishi wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo ya Viwanda (UNIDO) hapa nchini, Bw. Emmanuel Kalenzi alipofika Wizarani leo. Katika mazungumzo yao walizungumzia kuhusu maendeleo ya viwanda hapa nchini ikiwa ni pamoja na juhudi zinazofanywa na UNIDO kwa kushirikiana na SIDO katika kuendeleza viwanda vidogo vidogo katika mikoa mbalimbali hapa nchini.

Bw. Kalenzi akifafanua jambo kwa Balozi Mushy wakati wa mazungumzo yao.

Balozi Mushy (katikati) akiendelea na mazungumzo na Bw. Kalenzi huku Bi. Jubilata Shao, Afisa Mambo ya Nje akinukuu mazungumzo hayo.

Balozi Mushy akiagana na Bw. Kalenzi mara baada ya mazungumzo yao.

Monday, May 13, 2013

Mhe. Membe akutana kwa mazungumzo na Mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa nchini

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) (katikati) akizungumza na Mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa nchini (hawapo pichani) kuhusu masuala mbalimbali ya kikanda na kitaifa. Katika Mkutano huo Mhe. Membe alifafanua juu ya hali ya kisiasa nchini Madagascar na Zimbabwe na kutoa taarifa za kuwasili kwa vikosi vya kulinda amani vya Tanzania huko Mashariki mwa DRC. Kuhusu masuala ya kitaifa Mhe. Membe alilitolea ufafanuzi suala la shambulio la bomu lilitokea hivi karibuni huko Arusha ambapo alisema kuwa Serikali inaendelea na uchunguzi  na kwa ujumla hali nchini ni tulivu. Wengine katika picha ni Bw. John Haule (kushoto), Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mhe.Khalfan  Juma Mpango (kulia), Mkuu wa Mabalozi na Balozi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo hapa nchini. Mkutano huo umefanyika katika Ukumbi wa Karimjee, Jijini Dar es Salaam tarehe 13 Mei, 2013.

Baadhi ya Mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini na Wakurugenzi wa Idara mbalimbali katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa  wakimsikiliza Mhe. Membe (hayupo pichani)

Mabalozi wengine wakimsikiliza Mhe. Membe (hayupo pichani)

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Rajab Gamaha (wa pili kushoto) kwa pamoja na baadhi ya Mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa nchini wakimsikiliza mhe. Waziri Membe (hayupo pichani) wakati alipozungumza na Mabalozi hao.


Mabalozi wengine na viongozi mbalimbali wa Wizara ya Mambo ya Nje wakimsikiliza Mhe. Membe (hayupo pichani)

Sehemu nyingine ya Mabalozi wakati Mhe. Membe alipozungumza nao.

Mkurugenzi na Mkuu wa Itifaki katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Mohammed Maharage (kushoto) akimsikiliza Mhe. Waziri (hayupo pichani) alipozungumza na Mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa nchini.


Balozi Mpango akitoa neno la shukrani kwa niaba ya Mabalozi wenzake mara baada ya Mhe. Membe kumaliza mazungumzo nao.



Picha zaidi za mkutano huo wa Mhe. Membe na Mabalozi.

Mhe. Membe akiagana na Balozi wa Umoja wa Ulaya hapa nchini, Mhe. Filiberto Sebregondi mara baada ya mazungumzo na Mabalozi hao.

Mhe. Waziri Membe akisalimiana na Balozi wa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), Mhe. Balozi Abdulla Ibrahim Al-Sowaidi hapa nchini baada ya kumaliza mazungumzo.

Mhe. Membe akiteta jambo na Balozi wa Vatican na Mwakilishi wa Papa hapa nchini, Mhe. Francisco Montecillo Padilla mara baada ya kuzungumza na Mabalozi hao.

Mhe. Membe akiasalimiana na Balozi wa Marekani hapa nchini Mhe. Alfonso Lenhardt aliyekuwepo wakati wa mkutano huo.

Balozi wa Rwanda hapa nchini akifuatana na Mhe. Membe alipomaliza mazungumzo na Mabalozi hao.

Mhe. Membe akizungumza na Waandishii wa Vyombo mbalimbali vya Habari juu ya mazungumzo yake  na Mabalozi wanaowakilisha nchi zao hao hapa nchini.

Mhe.Membe amtembelea Balozi wa Vatican nchini kumpa pole

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akisalimiana na Mhe. Francisco Montecillo Padilla, Balozi wa Vatican na Mwakilishi wa Papa hapa nchini mara baada ya kuwasili Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kumsalimia na kumpa pole kufuatia shambulio la bomu  lililotokea Jijini Arusha tarehe 5 Mei, 2013  na kupelekea watu watatu kufariki dunia na wengine zaidi ya 60 kujeruhiwa. Balozi Padilla alikuwa miongoni mwa wageni waalikwa  katika hafla ya ufunguzi rasmi wa Kanisa Katoliki la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi, Parokia ya Olasiti, Jimbo Kuu la Arusha wakati tukio hilo linatokea.

Mhe. Balozi Padilla akiwa katika  mazungumzo na Mhe. Membe kuhusu tukio hilo  ambapo pamoja na mambo mengine alisema kuwa anaamini suala hilo litapita na wahusika kupatikana na kuchukuliwa hatua za kisheria.
Mhe. Membe akiagana na Mhe. Balozi Padilla mara baada ya kuzungumza naye.

Hon. Membe hands out Credentials to new Honorary Consul of Botswana to Tanzania


Hon. Bernard K. Membe (MP), Minister for Foreign Affairs and International Co-operation hands out Credentials to new Honorary Consul Eng. Emmanuel D. Ole Naiko of Botswana to the United Republic of Tanzania at his office today in Dar es Salaam. 

Hon. Bernard K. Membe (MP), Minister for Foreign Affairs and International Co-operation in conversation with new Honorary Consul Eng. Emmanuel D. Ole Naiko representing Botswana to the United Republic of Tanzania.  Also in the meeting is his wife, Mrs. Hafsa Ole Naiko.

Permanent Secretary Mr. John M. Haule (left) was also present during the occasion. 

Deputy Permanent Secretary Ambassador Rajabu Gamaha (left) and Mr. Andrew Mwandembwa, Assistant Chief of Protocol were also present during the meeting.  

Hon. Bernard K. Membe (MP) (right), in a conversation with new Honorary Consul of Botswana to Tanzania and his family.

Hon. Bernard K. Membe (MP), Minister for Foreign Affairs and International Co-operation is in the group photo with new Honorary Consul Eng. Emmanuel D. Ole Naiko and his family during their meeting with the Minister today in Dar es Salaam.



All Photos by Tagie Daisy Mwakawago  



Sunday, May 12, 2013

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI: UTEUZI WA MABALOZI


220px-Coat of arms of Tanzania.svg f1f71


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, amefanya uteuzi wa Mabalozi Wapya kujaza nafasi zilizo wazi na kuanzisha Ofisi za Ubalozi nchini Uholanzi na Comoro.  Aidha Mheshimiwa Rais amefanya uhamisho wa Balozi kutoka kwenye kituo kimoja.

Mabalozi wateule na aliyehamishwa kituo ni kama ifuatavyo:-

Bw. Wilson M. K. Masilingi;
Ameteuliwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Uholanzi. Bw. Masilingi ni Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kituo cha Mikutano cha Kimataifa, Arusha, (AICC) na aliwahi kuwa Mbunge katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kati ya mwaka 1995 – 2010.  Aidha, katika kipindi cha mwaka 1998 – 2005 alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais mwenye dhamana ya masuala ya Utawala Bora.

Bw. Chabaka Faraji Ali Kilumanga, ameteuliwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Comoro. Hadi uteuzi huu unafanyika, Bw. Kilumanga alikuwa Balozi Mdogo katika ofisi ya Ubalozi nchini Uingereza.

Bw. Modest Jonathan Mero, ameteuliwa kuwa Balozi wa Tanzania kwenye Ofisi za Umoja wa Mataifa, Geneva.  Kabla ya uteuzi Bw. Mero alikuwa Afisa wa Mambo ya Nje Mwandamizi kwenye Ubalozi wa Tanzania katika Ofisi za Umoja wa Mataifa, New York.

Kadhalika, Mheshimiwa Rais amemhamisha Balozi Philip Sang’ka Marmo kutoka Ubalozi wa Jamhuri ya Watu wa China na kwenda Jamhuri ya Shirikisho la Ujerumani.
 


------MWISH0-----

(John M. Haule)
KATIBU MKUU,
WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA,
DAR ES SALAAM.

12 MEI, 2013