Tuesday, May 21, 2013

Deputy Permanent Secretary hold talks with UK' Royal College of Defence Studies



Ambassador Rajab Gamaha, Deputy Permanent Secretary of the Ministry Foreign Affairs and International Co-operation holding talks earlier today with Mr. Jeremy Jarvis, Senior Directing Staff of the Royal College of Defence Studies based in the UK together with the delegation of about twenty people in the Ministry in Dar es Salaam.   


Ambassador Rajabu Gamaha explains Tanzania's current state and its regional integration with neighboring countries during their meeting today in the Ministry, in Dar es Salaam.


Mr. Jeremy Jarvis, Senior Directing Staff of the Royal College of Defence Studies express his appreciation of the Tanzania Government's hospitality during their Study Tour Visit which encompasses Defence Studies students of post graduate programme in international strategic studies, which focuses on the themes of security, stability and prosperity.  Other in the photo are Ambassador Dora Msechu (2nd right), Director of the Department of Europe and Americas in the Ministry.  


Defence Studies students that included Mr. Stephen Shelley (left), Directing Staff of the Royal and Colonel Jonathan Calder-Smith (2nd left) of the British Army, Captain Masashi Kondo (3rd right), Japan Maritime Self-Defence Force and Mr. Teemu Pentilla (2nd right), from the Ministry of Defence, Finland. 

Ambassador Rajabu Gamaha expresses Tanzania's historical prosperity in security and stability in the region and within the country.  


Delegation from the UK' Royal College of Defence Studies during their meeting today with the Deputy Permanent Secretary in the Ministry of Foreign Affairs and International Co-operation in Dar es Salaam.  Also in the photo are British High Commissioner Dianna Melrose (2nd right) in the United Republic of Tanzania and Mr. Jeremy Jarvis (right), Senior Directing Staff of the UK' Royal College of Defence Studies.  


Members of the Tanzania Defence Force also were in attendance during the meeting.


All photos by Tagie Daisy Mwakawago 


Monday, May 20, 2013

Mhe. Membe azungumza na Mabalozi kuhusu Mkutano ujao wa Smart Partnership

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb) akizungumza na Mabalozi na Wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa yaliyopo hapa nchini (hawapo pichani) kuhusu Mkutano wa Kimataifa wa Majadiliano ya Ushirikiano kwa Manufaa ya Wote (Smart Partnership Global Dialogue 2013) utakaofanyika Jijini Dar es Salaam kuanzia tarehe 28 Juni hadi 01 Julai 2013. Mkutano huo ambao utahudhuriwa na Marais mbalimbali na Wajumbe zaidi ya 500 kutoka ndani na nje ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania unalenga  kuwanufaisha Watanzania kiuchumi, kiteknolojia na kijamii. Wengine katika picha ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. John Haule (kushoto) na Mkuu wa Mabalozi ambaye pia ni Balozi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo hapa nchini, Mhe. Juma  Khalfan Mpango.

Baadhi ya Mabalozi na Wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa nchini wakimsikiliza Mhe. Membe (hayupo pichani) alipozungumza nao kuhusu Mkutano wa Kimataifa wa Majadiliano ya Manufaa kwa Wote (Smart Partnership Global Dialogue 2013)

Mabalozi wengine wakimsikiliza Mhe. Membe (hayupo pichani)

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Rajabu Gamaha (kushoto, mstari wa kwanza) na Mkurugenzi na Mkuu wa Itifaki, Balozi Mohammed Maharage pamoja na baadhi ya Mabalozi wakimsiliza Mhe. Membe (hayupo pichani).

Meneja wa Maandalizi ya Mkutano wa Kimataifa wa Majadiliano ya Manufaa kwa Wote (Smart Partnership Global Dialogue 2013), Bibi Rosemary Jairo akiwaeleza Mabalozi na Wakuu wa Mashirika ya Kimataifa (hawapo pichani) hatua zilizofikiwa katika kuandaa mkutano huo.

Picha zaidi za baadhi ya Mabalozi waliohudhuria Mkutano huo.

Baadhi ya Mabalozi wakisikiliza kwa makini maelezo yaliyokuwa yakitolewa na Bibi Jairo (hayupo pichani) kuhusu maandalizi ya mkutano huo.

Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Mbelwa Kairuki akiwa na Bw. Japhet Mwaisupule, Afisa Mambo ya Nje Mkuu wakati wa mkutano kati ya Mhe. Membe na Mabalozi.

Mkuu wa Sekrtarieti ya Maandalizi ya Mkutano huo hapa nchini, Bibi Victoria Mwakasege (kushoto) akiwa  na Bibi Jairo wakati wa mkutano wa Mhe. Membe na Mabalozi.

Picha zaidi za mkutano kati ya Waziri Membe, Mabalozi na Wakuu wa Masharika ya Kimataita waliopo hapa nchini


Mhe. Membe akizungumza na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) kuhusu mazungumzo yake na Mabalozi. Wengine katika picha ni Mkuu wa Sekretarieti ya Maandalizi ya Mkutano wa Kimataifa wa Majadiliano kwa Manufaa ya Wote, Bibi Mwakasege (kulia) na Meneja wa Maandalizi ya Mkutano huo Bibi Jairo (kushoto).

Friday, May 17, 2013

Mhe. Membe amkaribisha nchini Naibu Katibu Mkuu wa Denmark anayeshughulikia masuala ya Maendeleo ya Kimataifa

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.), akizungumza na Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia masuala ya Maendeleo ya Kimataifa wa Denmark, Mhe. Charlotte Slente wakati wa hafla fupi ya Chakula cha Usiku kilichoandaliwa na Mhe. Membe kwa heshima ya Mhe. Slente katika Hoteli ya Hyatt Regency (Kilimanjaro) ya Jijini Dar es Salaam. Mhe. Slente alikuwa nchini kwa ziara ya kikazi.

Mhe. Membe akiendelea na mazungumzo na Mhe. Slente huku wajumbe waliofuatana nao kutoka Tanzania na Denmark wakisikiliza.



Ujumbe uliofuatana na Mhe. Slente akiwemo Balozi wa Denmark hapa nchini Mhe. Johnny Flento (kulia)

Mhe. Membe akimkabidhi Mhe. Slente zawadi ya picha ya kuchora inayoonesha vivutio vya utalii vya hapa nchini.



Mhe. Membe akiagana na mgeni wake Mhe. Slente mara baada ya mazungumzo yao

Mhe. Slente akielezwa jambo na Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Dora Msechu wakati akiagana nae.

Tanzania na Canada zasaini Mkataba wa Kulinda na Kukuza Uwekezaji


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K.Membe (Mb.), kwa pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje wa Canada, Mhe. John Baird wakisaini Mkataba wa Kulinda na Kukuza Uwekezaji (FIPA) kati ya Tanzania na Canada. Hafla hiyo fupi ilifanyika Wizarani tarehe 16 Mei, 2013.

Mhe. Membe na Mhe. Baird wakiendelea kusaini mkataba huo huku Maafisa wa Sheria kutoka Tanzania na Canada wakishuhudia. Kushoto kwa Mhe. Membe ni Bw. Abdallah Mtibora, Afisa Mambo ya Nje katika Kitengo cha Sheria, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.


Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Rajab Gamaha akiwa na Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika, Balozi Dora Msechu (katikati), na Mkurugenzi Msaidizi wa Idara hiyo Bibi Grace Shangali wakishuhudia uwekaji saini wa Mkataba wa FIPA.

Wajumbe wengine waliokuwepo kushuhudia tukio hilo la uwekaji saini wa Mkataba wa FIPA.

Mhe. Membe  na Mhe. Baird wakibadilishana Mkataba huo mara baada ya kusaini.
Mhe. Membe na Mhe. Baird wakionesha kwa Wajumbe Mkataba waliosaini.

Mhe. Membe akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu Mkataba wa FIPA.


Waandishi wa Habari pamoja na Wajumbe wengine wakimsiliza Mhe. Membe alipokuwa akitoa ufafanuzi kuhusu Mkataba wa Kukuza na Kulinda Uwekezaji kati ya Tanzania na Canada (FIPA).

Mhe. Baird nae akizungumza machache kuhusu mkataba huo.



Thursday, May 16, 2013

Mhe. Membe amkaribisha Waziri wa Mambo ya Nje wa Canada nchini

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akisalimiana na  Waziri wa Mambo ya Nje wa Canada,  Mhe. John Baird  alipowasili kwenye Hoteli ya Hyatty Regency Kilimanjaro kwa ajili ya kushiriki Chakula cha Mchana kilichoandaliwa kwa heshima yake na Mhe. Membe. Mhe. Baird yupo nchini kwa ziara ya kikazi ya siku mbili ambapo pamoja na mambo mengine pia watazungumza kuhusu kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Canada pamoja na kusaini Mkataba "Foreign Investment, Promotion and Protection Agreement" (FIPA).


Mhe. Membe akifurahia jambo wakati wa mazungumzo yake na Mhe. Baird.

Mhe. Membe akimweleza jambo Mhe. Baird wakati wa mazungumzo yao. Wengine katika picha ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Rajab Gamaha (wa tatu kushoto) na Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Dora Msechu.



Mhe. Membe akiendelea na mazungumzo huku Mhe. Baird akimsikiliza. Kushoto ni Balozi wa Canada hapa nchini Mhe. Alexandre Leveque.


Mhe. Membe akimkabidhi Mhe. Baird zawadi ya picha ya kuchora inayoonesha Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro  pamoja na wanyama aina ya Tembo.


Mhe. Baird akifurahia zawadi hiyo.

Mhe. Baird akimshukuru Mhe. Membe kwa kumpatia zawadi hiyo nzuri.

Wednesday, May 15, 2013

Mhe. Membe akutana kwa mazungumzo na Mwakilishi wa UNAMID

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) (kulia) akisalimiana na Mwakilishi Maalum na Msuluhishi  Mkuu wa  Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika katika Mgogoro wa Darfur (UNAMID), Mhe. Mohamed Ibn Chambas mara baada ya kuwasili Wizarani kwa mazungumzo. Katika mazungumzo yao walijadili masuala mbalimbali ya namna Vikosi vya UNAMID vinavyotekeleza majukumu yake huko Darfur  katika kulinda Amani. Tanzania pia imechangia katika Vikosi vya UNAMID Wanajeshi wapatao  1,129.
Mhe. Membe akiendelea na mazungumzo na Mhe. Chambas.

Ujumbe uliofuatana na Mhe. Chambas akiwemo Meja Jenerali Wyjones Kisamba (wa tatu kushoto), Kaimu Kamanda wa Vikosi vya kulinda amani vya UNAMID kutoka Tanzania. Kulia ni Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa hapa nchini, Dkt. Alberic Kacou.

Mhe. Chambas akimweleza Mhe. Membe jitihada mbalimbali zinazofanywa na UNAMID huko Darfur katika kuhakikisha amani katika Jimbo hilo lililopo Magharibi mwa Sudan inarejea.



Ujumbe kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa ukifuatilia kwa makini mazungumzo kati ya Mhe. Waziri Membe na Mhe. Chambas (hawapo pichani). Kushoto ni Bw. Nathaniel Kaaya, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Togolani Mavura (kulia), Msaidizi wa Waziri na Bi. Eva Ng'itu (katikati), Afisa Mambo ya Nje.

Picha zaidi za mazungumzo hayo.

Mhe. Membe akiagana na Mhe. Chambas baada ya kumaliza mazungumzo yao.

Tuesday, May 14, 2013

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI: UTEUZI WA MABALOZI WA TANZANIA NCHINI MAREKANI NA UMOJA WA FALME ZA KIARABU




220px-Coat of arms of Tanzania.svg f1f71


;

Mkurugenzi wa Ushirikiano wa Kimataifa akutana kwa mazungumzo na Mwakilishi wa UNIDO hapa nchini

Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy (kulia) akizungumza na Mwakilishi wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo ya Viwanda (UNIDO) hapa nchini, Bw. Emmanuel Kalenzi alipofika Wizarani leo. Katika mazungumzo yao walizungumzia kuhusu maendeleo ya viwanda hapa nchini ikiwa ni pamoja na juhudi zinazofanywa na UNIDO kwa kushirikiana na SIDO katika kuendeleza viwanda vidogo vidogo katika mikoa mbalimbali hapa nchini.

Bw. Kalenzi akifafanua jambo kwa Balozi Mushy wakati wa mazungumzo yao.

Balozi Mushy (katikati) akiendelea na mazungumzo na Bw. Kalenzi huku Bi. Jubilata Shao, Afisa Mambo ya Nje akinukuu mazungumzo hayo.

Balozi Mushy akiagana na Bw. Kalenzi mara baada ya mazungumzo yao.