Thursday, May 15, 2014

Waziri Membe afungua Mkutano wa Baraza la Wafanayakazi wa Mambo ya Nje


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.)-katikati) kwa pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. John Haule (wa tatu kutoka kushoto) na viongozi wengine wakiimba wimbo wa "Solidarity" wakati wa ufunguzi wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa uliofanyika kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam tarehe 15 Mei, 2014.
Mhe. Membe akitoa hotuba ya ufunguzi wa Baraza la Wafanayakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa ambapo alitoa rai kwa Wafanyakazi hao kujituma na kuongeza bidii katika utendaji kazi wao wa kila siku.
Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wakimsikiliza Waziri Membe alipofungua kikao cha Baraza hilo.
Katibu Mkuu, Bw. Haule nae akizungumza wakati wa ufunguzi wa Baraza hilo.

Baadhi ya Wajumbe wakimsikiliza Katibu Mkuu (hayupo pichani) wakati akizungumza. Kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Dushhood Mndeme.
Katibu wa Baraza la Wafanyakazi, Bibi Naomi Zegezege nae akizungumza wakati wa ufunguzi wa Baraza hilo huku Mhe. Membe na Viongozi wengine wakimsikiliza.
Kikao kikiendelea.
Mkurugenzi wa Idara ya Afrika na Mjumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Baloiz Vincent Kibwana akitoa neno la shukrani kwa niaba ya Wajumbe wa Baraza hilo.
Katibu Mkuu, Bw. Haule, Naibu Katibu Mkuu, Balozi Rajabu Gamaha na Viongozi wengine wakifurahia jambo wakati wa kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa Mambo ya Nje.
Waandishi wa Habari nao pia walikuwepo.
Waziri Membe akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa mara baada ya kulifungua.

Picha na Reginald Philip



Press Release



H.E. Jakaya Mrisho Kikwete, President of the United Republic of Tanzania addressed to H.E. Abdullah Gül, President of the Republic of Turkey following the tragic mining disaster, which occurred in Soma, Turkey on 14th May, 2014. The message reads as follows:

His Excellency,
Abdullah Gül,
President of the Republic of Turkey,
ANKARA.

Your Excellency and Dear Brother,

I have received with profound sorrow and shock the sad news about the tragic accident caused by terrible explosion at a coal mine in Soma, Turkey and claimed ……lives of more than 200 people.

On behalf of the Government and People of the United Republic of Tanzania, and indeed on my behalf, I wish at this difficult time, to express our deepest sympathies and condolences to you and through you express our deepest sympathies and condolences to you and through you to the bereaved families and relatives. We pray that the Almighty God give the families and relatives of the deceased strength and fortune to bear at this moment of agony distress.

May the Almighty God bring rapid and complete recovery to the injured and rest the souls of the deceased in eternal peace.

Please accept, Your Excellency and Dear Brother, the assurance of my highest consideration.





Jakaya Mrisho Kikwete
PRESIDENT OF THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA



Issued by the Ministry of Foreign Affairs and International Co-operation






Wednesday, May 14, 2014

Mhe. Membe amuaga Marehemu Balozi Flossie nyumbani kwake Malawi




Waziri wa Mambo ya Nje na Ushiriano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akisoma kwa majonzi Salamu za Pole za Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa Rais wa Malawi, Mhe. Joyce Banda kufuatia kifo cha ghafla cha aliyekuwa Balozi wa Malawi nchini Tanzania, Marehemu Flossie Gomile-Chidyaonga. Mhe. Waziri Membe alisoma salamu hizo wakati wa kumuaga Marehemu Balozi Flossie tukio hilo lilifanyika nyumbani kwa marehemu Kitongoji cha Limbe katika mji wa Blantyre nchini Malawi. Mhe. Membe alimwakilisha Rais Kikwete kwenye mazishi ya Balozi Flossie yaliyofanyika tarehe 14 Mei, 2014.
Mhe. Membe akiendelea kusoma salamu hizo huku Waziri wa Mambo ya Nje wa Malawi, Mhe. Ephraim Chiume (mwanye tai nyeusi) na Mume wa Rais wa Malawi, Jaji Mkuu Mstaafu, Banda (wa kwanza kulia mstari wa kwanza) wakimsikiliza.
Baadhi ya wananchi wakimsikiliza Mhe. Membe (hayupo pichani)
Mhe. Membe akimkabidhi Mhe. Chiume Salamu hizo mara baada ya kuzisoma.
Mhe. Chiume nae akisema machache wakati wa shughuli za kumuaga Balozi Flossie. Katika maelezo yake Mhe. Chiume kwa niaba ya Serikali ya Malawi alitoa shukrani za dhati kwa Serikali ya Tanzania kwa ushirikiano mkubwa wakati wote wa msiba wa Marehemu Balozi Flossie.
Mhe. Chiume akimtambulisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. John Haule ambaye alikuwa miongoni mwa wajumbe waliofuatana na Mhe. Membe nchini Malawi.
Baba Mdogo wa Marehemu Balozi Flossie, Dkt. Joseph Gomile nae akitoa neno wakati wa shughuli hizo za kumuaga Marehemu Balozi Flossie. Dkt. Gomile ambaye   anaishi nchini Tanzania kwa kipindi kirefu sasa nae aliishukuru Serikali ya Tanzania kwa mchango mkubwa katika msiba huo mzito wa mtoto wake.
Mhe. Membe. Mhe. Chiume na Mhe.  Jaji Mstaafu Banda wakimsikiliza Dkt. Gomile (hayupo pichani)
Baadhi ya Mabalozi na Wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa yaliyopo hapa nchini waliomsindikiza mwenzao Marehemu Balozi Flossie nao wakifuatilia matukio.
Jeneza lililobeba mwili wa Marehemu Baloz Flossie kama linavyoonekana katika eneo la nyumbani kwake likiwa limezungukwa na waombolezaji.
Balozi wa Tanzania nchini Malawi, Mhe. PatrickTsere  (kushoto)  akiwa na Balozi Vincent Kibwana, Mkurugenzi wa Idara ya Afrika na Mwakilishi kutoka Ubalozi wa Malawi hapa nchini mara baada ya shughuli za kuaga mwili wa Marehemu Balozi Flossie kumalizika.
Baadhi ya viongozi wa dini waliokuwepo.
Viongozi mbalimbali walioshiriki kumuaga Balozi Flossie katika eneo la nyumbani kwake kabla ya mazishi.
Marafiki wa Marehemu Balozi Flossie wakiwa katika simanzi kufuatia kifo cha mpendwa wao.
Mhe. Membe akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Mabalozi aliofuatana nao nchini Malawi mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere.

Tuesday, May 13, 2014

Waziri Membe awasili Malawi kumwakilisha Mhe. Rais Kikwete kwenye mazishi ya aliyekuwa Balozi wa Malawi nchini

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Blantyre nchini Malawi kwa ajili ya kushiriki mazishi ya aliyekuwa Balozi wa Malawi nchini Tanzania, Marehemu Flossie Gomile-Chidyaonga aliyefarikii dunia tarehe 09 mei, 2014 Jijini na Dar es Salaam na anatarajiwa kuzikwa tarehe 14 Mei, 2014. Mhe. Membe anamwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete kwenye mazishi hayo.
Balozi wa Tanzania nchini Malawi,  Mhe. Patrick Tsere akimweleza jambo Mhe. Membe wakati wa mapokezi.
Mhe. Membe akijaribu kumwelezea Rais wa Malawi, Mhe. Joyce Banda namna alivyozipokea taarifa za kifo cha Balozi Flossie. Kushoto kwa Mhe. Rais Banda ni mume wake Jaji Mkuu Mstaafu Banda na kulia kwa Mhe. Membe ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Malawi, Mhe. Ephraim Chiume.
Baadhi ya Wananchi wa Blantyre na sehemu nyingine za Malawi wakiwa uwanjani hapo wakati wa mapokezi ya Mwili wa aliyekuwa Balozi wa Malawi nchini Tanzania, Marehemu Flossie Gomile-Chidyaonga.
Mhe. rais Banda akisalimiana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. John Haule.
Mhe. Rais Banda akisalimiana na Balozi Vincent Kibwana, Mkurugenzi wa Idara ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
Mhe. Rais Banda akisalimiana na Mwakilishi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) nchini Tanzania pamoja na Mabalozi wengine waliofutana na Mhe. Membe nchi Malawi kwenye mazishi ya Marehemu Balozi Flossie.
Mhe. Rais Banda akimtambulisha kwa Mhe. Membe Mtoto pekee wa Marehemu Balozi Flossie-Gomile-Chidyaonga.

Mhe. Rais Banda, Mhe. Membe, Mhe. Chiume na Wajumbe wengine wakisubiri jeneza lililobeba mwili wa marehemu Balozi Flossie kuteremshwa kwenye ndege kwa ajili ya taratibu zingine.
Jeneza lililobeba mwili wa Marehemu Balozi Flossie likiwa limeteremshwa kwenye ndege.
Mhe. Rais Banda akihutubia mara baada ya mapokezi ambapo alitoa shukrani za dhati kwa Serikali ya Tanzania kwa ushirikiano.
Mhe. Membe nae akizungumza machache.
Wananchi wakifuatilia hotuba.
Mwakilishi wa Familia ya  Marehemu Balozi Flossie nae akizungumza kwa niaba ya familia hiyo.
Kwaya ikiimba wakati wa shughuli hizo.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) amemtaja aliyekuwa Balozi wa Malawi nchini Tanzania Marehemu Flossie-Gomile Chidyaonga kama Malkia wa Amani kwa vile alikuwa mstari wa mbele katika vikao vya usuluhishi na kutafuta amani kwenye Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) Malawi ikiwa ni Mwenyekiti wa jumuiya hiyo.
Mhe. Membe aliyasema hayo wakati wa mapokezi maalum ya Marehemu Balozi Chidyaonga yaliyofanyika katika Uwanja wa Ndege wa Blantayre nchini Malawi na kuhudhuriwa na Rais wa Malawi, Mhe. Joyce Banda, Viongozi wa Serikali ya Malawi, Familia ya Marehemu, Taasisi za Dini, Mabalozi na Wananchi kutoka sehemu mbalimbali za mji huo.

Mhe. Membe ambaye anamwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Kikwete kwenye mazishi ya Marehemu Balozi Flossie Gomile-Chidyaonga alisema kwamba Tanzania, Malawi, nchi za SADC na dunia kwa ujumla imempoteza mwanadiplomasia mahiri ambaye aliujua na kutekeleza wajibu wake ipasavyo.

“Kwa niaba ya Mhe. Rais Kikwete, Watanzania wote na mimi binafsi nakuomba Mhe. Rais Banda na Wananchi wa Malawi mpokee salamu zetu za pole kwa kumpoteza Balozi Flossie ambaye alikuwa mstari wa mbele katika masuala ya amani kwa Kanda ya SADC na ninamwita Malkia wa Amani kwa juhudi hizo alisema Mhe. Membe”.

Mhe. Membe aliongeza kusema kwamba kutokana na kufanya kazi kwa kujituma na kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Malawi, Marehemu  Balozi Flossie alikubalika Serikalini, kwa Mabalozi wenzake na hata katika Taasisi za Elimu ya Juu kama Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambako alishiriki katika kutoa mihadhara mara kwa mara.

Katika hotuba yake wakati wa mapokezi hayo, Rais wa Malawi Mhe. Joyce Banda alisema kuwa wameupokea msiba huo wa ghafla kwa majonzi makubwa ambapo kwa namna ya pekee aliishukuru Serikali ya Tanzania hususan Rais Kikwete kwa ushirikiano wa hali ya juu aliouonesha tangu msiba utokee na kutuma ujumbe mzito uliioongozwa na Waziri Membe kumsindikiza Marehemu Flossie nchini Malawi.

“Mimi binafsi na wananchi wa Malawi tunatoa shukrani za dhati kwa ndugu zetu Watanzania hususan  Mhe. Rais Kikwete kwa ushirikiano walioonesha katika kipindi hiki kigumu kwetu. Mhe. Rais Kikwete aliwasiliana na mimi akiwa safarini mara tu msiba ulipotokea. Alielezea kushtushwa na msiba huo wa ghafla kama mimi nilivyoshtushwa. Nilimweleza azma ya Serikali yangu kuhusu kutuma ndege kwa ajili ya kuufuata mwili wa ndugu yetu Flossie lakini alisema nimwachie  hilo ni jukumu lake na amelitekeleza kikamilifu kama tunavyoona” alisema kwa masikitiko Mhe. Banda.

Awali akizungumza kwa niaba ya Familia ya Marehemu Balozi Flossie, Msemaji wa Familia hiyo Bw. Andrew  naye aliishukuru Serikali ya Tanzania na kusema kuwa ushirikiano uliooneshwa katika kipindi hiki kigumu kwao unadhihirisha undugu mkubwa uliopo kati ya Tanzania na Malawi.

Baadhi ya Viongozi wa Serikali na Mabalozi waliofuatana na Mhe. Mhe. Membe kwenye msiba huu ni pamoja na Bw. John Haule, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikano wa Kimataifa, Balozi Vincent Kibwana, Mkurugenzi wa Idara ya Afrika, Kaimu Mkuu wa Mabalozi wanaowakilisha nchi zao Tanzania ambaye pia ni Balozi wa Zimbabwe, Balozi wa Zambia nchini, Mhe. Judith Kangoma, Balozi wa Norway nchini na Maafisa wa Ubalozi wa Malawi nchini.

Marehemu Balozi Flossie Gomile-Chidyaonga ambaye alifariki dunia katika Hospitali ya Aga Khan Jijini Dar es Salaam tarehe 09 Mei, 2014 anatarajiwa kuzikwa katika Mji wa Blantyre nchini Malawi tarehe 14 Mei, 2014.



Monday, May 12, 2014

Waziri Membe ashiriki kuuaga mwili wa aliyekuwa Balozi wa Malawi nchini

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akisaini kwa masikitiko makubwa Kitabu cha Maombolezo kufuatia kifo cha aliyekuwa Balozi wa Malawi hapa nchini, Hayati Flossie Gomile-Chidyaonga kilichotokea kwenye Hospitali ya Aga Khan Jijini Dar es Salaam tarehe 09 mei 2014.
Mhe. Membe akisalimiana na baadhi ya Mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa nchini kabla ya kuanza kwa shughuli za kuuaga mwili wa aliyekuwa Balozi wa Malawi hapa nchini Marehemu Flossie Gomile-Chidyaonga. Shughuli hiyo ilifanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam tarehe 12 Mei, 2014.
Mhe. Membe akizungumza wakati wa kuuaga mwili wa  aliyekuwa Balozi wa Malawi hapa nchini Marehemu Flossie Gomile-Chidyaonga. Mhe. Membe alimwelezea Hayati Balozi Flossie kama mtu aliyependa amani, mcheshi na msikivu. Alisema Hayati Balozi Flossie alikuwa mstari wa mbele katika suala la mgogoro kati ya Tanzania na Malawi kuhusu Mpaka katika Ziwa Nyasa.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. John Haule (wa pili kutoka kulia mstari wa kwanza) akiwa  na Balozi Vincent Kibwana  kulia), Mkurugenzi wa Idara ya Afrika  pamoja na Mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa nchini na  Wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa wakifuatilia hotuba ya Mhe. Membe (hayupo pichani) wakati akimwelezea Hayati Balozi Flossie.

Baadhi ya Wakuu wa Idara na Vitengo katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wakifuatilia hotuba ya Mhe. Membe (hayupo pichani) wakati wa kuuaga mwili wa aliyekuwa Balozi wa Malawi hapa nchini Hayati Flossie Gomile-Chidyaonga.
Mhe. Membe akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa aliyekuwa Balozi wa Malawi hapa nchini Hayati Flossie Gomile-Chidyaonga. 
Balozi wa Zambia hapa nchini, Mhe. Judith Kangoma Kapijimpanga akishindwa kujizuia wakati wa kuuaga mwili wa aliyekuwa Balozi wa Malawi hapa nchini Hayati Flossie Gomile-Chidyaonga.
Mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa nchini, Wakuu wa Mashirika ya Kimataifa, Viongozi kutoka Serikalini, Taasisi Binafsi na watu mbalimbali wakiuaga mwili wa aliyekuwa Balozi wa Malawi hapa nchini Hayati Flossie Gomile-Chidyaonga.
Picha na Reginald Philip

Mhe. Membe amwakilisha Mhe. Rais Kikwete kushuhudia uwekaji saini mkataba wa ujenzi wa Reli kati ya Kenya na China

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) wa tatu kutoka kushoto waliosimama) kwa pamoja na viongozi wengine   akiwemo Rais wa Rwanda, Mhe. Paul Kagame, Waziri Mkuu wa China, Mhe. Li Keqiang, Rais wa Kenya, Mhe. Uhuru Kenyatta, Rais wa Uganda, Mhe. Yoweri Museveni na Rais wa Sudan Kusini, Mhe. Salva Kiir wakishuhudia kusainiwa kwa Mkataba wa Ujenzi wa Reli ya kisasa  Afrika Mashariki kati ya Serikali ya Kenya na China. Mhe. Membe alimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete.

Mhe. Membe wakati wa mkutano kabla ya mkataba kusainiwa.

Waziri Membe akimsikiliza Waziri Mkuu wa China, Mhe. Li Keqiang wakati wa mazungumzo.

Mkutano wa viongozi ukiendelea.

Rais Museveni akiongea kwa niaba ya viongozi waalikwa waliohudhuria uwekaji saini wa Mkataba wa Ujenzi wa Reli kati ya Serikali ya China na Kenya.

Sunday, May 11, 2014

TANZIA

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa John M. Haule akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) Juu ya Kifo cha aliyekuwa Balozi wa Mwalawi nchini Tanzania Hayati Mhe. Flossie Chidyaonga kilichotokea kwenye Hospitali ya Aga Khan Jijini Dar es Salaam siku ya Ijumaa Tarehe 09 Mei 2014.

Bwa. John M. Haule akiendelea kuzungumza huku Mkurugenzi wa Idara ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Balozi Vicent Kibwana (kushoto) akiyafuatilia kwa makini mazungumzo hayo na waandishi wa Habari (hawapo pichani)

Mazungumzo yakiendelea kati ya waandishi wa habari na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa
Picha na Reginald Philip



TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Serikali  imepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha Balozi wa Malawi hapa nchini Hayati Mhe. Flossie Gomile Chidyaonga kilichotokea juzi Ijumaa tarehe 09 Mei, 2014. Balozi Chidyaonga alifariki akiwa njiani kupelekwa hospitali ya Aga Khan ya hapa Dar es Salaam.

 Balozi Flossie Chidyaonga alizaliwa tarehe 16 Juni, 1960 huko Blantyre nchini Malawi. Balozi Chidyaonga aliitumikia Serikali ya Malawi katika nyadhifa mbalimbali.  Kati ya mwaka 2006 hadi 2010 alikuwa Naibu Balozi wa Malawi nchini Uingereza na baadaye Kaimu Balozi hadi alipoteuliwa kuwa Balozi wa Malawi hapa Tanzanaia.

Siku ya Jumatatu, tarehe 05 Mei, 2014, Balozi Flossie Chidyaonga alishinda vizuri na kufanya shughuli zake kama kawaida. Hata hivyo, ilipofika usiku,  alijisikia vibaya na kupelekwa hospitali ya Aga Khan, Dar es Salaam ambapo alipatiwa Matibabu na kuwekwa mapunziko kuanzia saa 6 usiku hadi saa 12 asubuhi aliporuhusiwa na kupewa dawa za kutumia nyumbani. Balozi Chidyaonga aliendelea kutumia dawa hizo na hali kuonekana kuimarika hadi siku hiyo ya ijumaa, tarehe 09 Mei, 2014. Siku hiyo, aliamka vizuri hadi ilipofika majira ya saa 6 mchana, hali yake ilipobadilika na kukimbizwa tena hospitali ya Aga Khan ambapo alipokelewa Daktari alisema amekwishafariki. Sasa hivi, Mwili wa Marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Uchunguzi wa madaktari umeonesha kuwa marehemu amefariki kutokana na Mshipa Mkuu wa AORTA kuvimba na kupasuka kulikosababisha damu kukusanyika kwenye mfuko wa moyo na hivyo kufanya moyo ushindwe kufanya kazi yake.

Kesho tarehe 12 Mei, 2014 mwili wa Marehemu utachukuliwa kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na kupelekwa kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere ambapo kutafanyika misa ya kumuombea Marehemu na kutoa heshima za mwisho kuanzia saa 4 asubuhi. Mwili wa Marehemu unatarajiwa kusafirishwa kwenda Blantyre, Malawi siku ya Jumanne tarehe 13 Mei, 2014 na mazishi yanatarajiwa kufanyika siku ya Jumatano tarehe 14 Mei 2014 huko Blantyer, Malawi.

Katika kipindi chote alichokuwa mwakilishi wa Malawi hapa nchini, Balozi Chidyaonga alifanya kazi yake ya kukuza na kuendeleza ushirikiano kati ya nchi zetu mbili kwa umahiri wa hali ya juu. Siku zote alikuwa mstari wa mbele kutoa ushirikiano kwa Serikali na Mabalozi wenzake wanaowakilisha nchi zao hapa Tanzania.

Mungu aiweke roho ya marehemu Balozi Flossie Chidyaonga, mahali pema peponi.

AMEN

Imetolewa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa
 Dar Es Salaam, Tarehe 11 Mei, 2014