Monday, March 16, 2015

WAZIRI MEMBE AKUTANA NA MTANZANIA ALIYESHINDA TUZO ZA COMMONWEALTH MJINI LONDON

Mhe. Bernard Membe (Mb.), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa akiwa na Julius James Shirima, mshindi wa Tuzo ya Vijana wa Nchi za Jumuiya ya Madola upande wa Afrika. Kwenye mazungumzo mafupi, Mhe. Membe alimpongeza Shirima kwa tuzo hizo na aliahidi kumpa ushirikiano kupitia Wizara anayoiongoza ili vijana wengi wa Kitanzania wanufaike na mchango wa Shirima na pia waige mfano wake na kuendelea kupeperusha vema bendera ya Tanzania.

Bw. Julius Shirima, mshindi wa Tuzo za Vijana wa nchi za Jumuiya ya Madola akiwa kwenye picha ya pamoja na Mhe. Bernard Membe, ambaye alifanya naye mazungumzo mara baada ya kumaliza kuendesha kikao cha Mawaziri wa Kikosi Kazi cha Jumuiya ya Madola mjini London hivi karibuni. Wengine kwenye picha ni Mhe. Peter Kallaghe, Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Mhe. Bernard Membe, Julius Shirima, Bi. Mindi Kasiga, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali na Balozi Celestine Mushy Mkuu wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa. 

Julius James Shirima akiwa amebeba Siwa ya Jumuiya ya Madola ambapo aliongoza maandamano ya Malkia Elizabeth kwenye sherehe hizo kama mshindi wa Tuzo za Vijana wa Nchi za Jumuiya ya Madola mwaka 2015. 

Malkia Elizabeth wa II, ambaye pia ni Mkuu wa Nchi 16 kati ya nchi 53 wanachama wa Jumuiya ya Madola akiwapongeza washindi Wanne wa Tuzo za Jumuiya ya Madola kutoka Afrika, Asia, Pacific na Karibian & Amerika, kabla ya kuzindua sherehe za Jumuiya hiyo mjini London, Uingereza. Pichani kulia ni Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo Mhe. Kamalesh Sharma ambaye ndiye aliyekabidhi tuzo hizo kwa niaba ya malkia.


Washindi wa Tuzo za Vijana wa Nchi za Jumuiya ya Madola kwenye picha ya pamoja. Kutoka kushoto, majina yao na eneo waliloshindia kwenye mabano ni Bi. Brianna Frueann 16 wa Samoa (Pacific), Bw. Julius Shirima 26 (Afrika), Bi. Gulalai Ismael wa Pakistan (Asia) na Bi. Nolana Lynch wa Trinidad na Tobago (Caribbean & Americas) 


Bw. Julius Shirima akiwa nje ya Jengo la Jumuiya ya Madola Jijini London Uingereza wakati wa sherehe za jumuiya hiyo.

Sunday, March 15, 2015

Ziara ya mafunzo kutoka U.S. Army War Collage ofisi za Uwakilishi wa Kudumu wa Tanzania umoja wa mataifa

Mhe. Balozi akielezea jambo mbele ya  kikundi  cha wanajeshi wanafunzi  ambao wapo katika  mafunzo  katika chuo cha U.S Army War Collage, wanafunzi hao walipata fursa ya kumuuliza Balozi maswali mbalimbali na ambayo yalijibiwa kwa ufasaha na  Mhe. Balozi.
Kiongozi wa Msafara akitoa zawadi yao kwa Mhe. Balozi kama kumbukumbu  na shukrani yao kwa kupokelewa na kwa Balozi kutenga muda wake kukutana nao.
Mhe. Balozi Tuvako  Manongi akiwa katika picha ya pamoja na Wanajeshi kutoka U.S Army War Collage,  miongoni mwa wanafunzi hao ni Mtanzania Luteni Kanali Juma Sipe kutoka JWTZ
Mhe. Balozi Manongi akiteta jambo na Luteni Kanali Juma Sipe  kutoka JWTZ ambayo  yuko mafunzoni U.S Army War Collage hapa Marekani

Mhe. Balozi Tuvako Manongi mwishoni mwa wiki alikutana na ujumbe wa wanawajeshi wanafunzi kutoka chuo cha Kijeshi (U.S. Army War Collage) ambao walikuwa katika ziara ya mafunzo. Miongoni mwa wanafunzi yupo Luteni Kanali Juma Sipe kutoka JWTZ. Ugeni huo ulitumia ziara hiyo kujifunza masuala mbalimbali yanayoihusu Tanzania kitaifa na kimataifa na uwepo wake kama nchi mwanachama wa Umoja wa Mataifa. 

TASWIRA KUTOKA UMOJA WA MATAIFA JIJINI NEW YORK

 Mhe. Waziri   Simba akisalimiana na  First Lady wa Kenya Mama Margaret Kenyatta, First Lady huyu   hukimbia mbio za marathon kama njia moja wapo ya kufatua  raslimali za kuwasaidi akina mama wenzie na watoto walio katika mazingira magumu.
Mkutano huu wa mbao ni wa waki mbili unafanyika sambamba na maadhimisho ya miaka 20 tangu kufanyika kwa mkutano wa kihistoria wa wanawake uliofanyika mwaka 1995 huko Beijing, China.
Pamoja na kuhudhuria mbalimbali inayohusianana Kimesheni   Kuhusu Hadhi ya Wanawake,   Mwakilishi wa Kudumu wa wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa,  alipata fursa ya kuwapokea na kuzungumza na wageni mbalimbali waliofika katika Uwakilishi wa Kudumu. Balozi Manongi akiwa na Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambao walikuwa  Jijini  New York  kwa shughuli za Kikazi.  
" Utanzania na uzalendo kwanza" ndivyo anavyoelekea kusema Mhe. Susan Lymo wakati yeye na wabunge wenzie   walipofika katika Uwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa.
Mhe. Waziri Sophia Simba  akiwa na  Mbunge wa Kawe Mhe. Halima Mdee,  Katibu Mkuu Anna Maembe, na Balozi  Tuvako Manongi katika moja wa  mikutano ya pembezoni iliyokuwa  inakwenda sambamba na  majadiliano  ya jumla ya Kamisheni ya 59. Mkutano huu  uliandaliwa na  Mke wa Rais wa  Kenya Mama, Margaret Kenyata,  ambapo alitumia fursa hiyo kuelezea shughuli anazozifanya  za kuwasaidia wanawake  na watoto wa nchi mwake hasa wale walio katika mazingira magumu. Kampeni yake inayoitwa Beyond Zero inalenga katika kufikisha huduma za afya


==============================================
Wajumbe wanaohudhuria Mkutano wa 59 wa Kamisheni kuhusu Hadhi ya Wanawake, kwa wiki kuanzia jumatano hadi Ijumaa wameendelea na jukumu kubwa la kujadiliana, kuhabaridha,a kubadilishana uzoefu, kuelimisha na hata kujifunza namna ya kuzikabilia changamato mbalimbali ambazo mwanamke na mtoto wea kike wanaendelea kukabiliana nazo. 

Mkutano huu wa mbao ni wa waki mbili unafanyika sambamba na maadhimisho ya miaka 20 tangu kufanyika kwa mkutano wa kihistoria wa wanawake uliofanyika mwaka 1995 huko Beijing, China. 

 Ujumbe wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wenye wajumbe kutoka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar unaongozwa na Mhe. Sophia Simba ( Mb) Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto na umekuwa ukishiriki majadiliano ya jumla na mikutano ya pembezo iliyobeba maudhui mbalimbali lakini yote yakilenga katika usawa wa jinsia na uwezeshwaji wa mwanamke.

TANZANIA HIGH COMMISSIONER’S SECRETARY IN LONDON WINS UK DIPLOMATIC AWARD

Present with Ms. Kiondo was H.E. Peter Kallaghe, Tanzania High commissioner to the UK (left). Mr. Blackson Bayewumi, President of the Commonwealth Youth Foundation.

==============================

Ms. Rose Kiondo, the Tanzania High Commissioner in UK’s Secretary has won a diplomatic award in London in the category of: Overall Best Customer Experience Award in the Professional & Government Services & Utilities Section.

Out of the 52 High Commissions in London and Embassies surveyed, her office was found leading at the forefront of delivering a leading customer experience. 

The two things that stood out during the deliberations in her case were: 

• Tanzanians/Customers at the Heart 

 • Listening & Responding 

And as a result there has been clear benefits in the Mission in terms of the growth of the relationship between the office of the High Commissioner and the outside world through customer engagement. 

Friday, March 13, 2015

Mkurugenzi wa Afrika kutoka China amaliza ziara nchini


Mkurugenzi wa Idara ya Afrika katika Wizara  ya Mambo ya Nje ya China, Balozi Liu Songtian akizungumza wakati wa mkutano wa pamoja na  Waandishi wa Habari (hawapo pichani) kuhusu ziara yake ya siku mbili aliyoifanya hapa nchini. Kushoto ni Balozi Abdulrahman Shimbo, Balozi wa Tanzania nchini China ambaye amefuatana na Mkurugenzi huyo. Kulia ni Balozi Lu Yoqing, Balozi wa China hapa nchini.
Sehemu ya Waandishi wa Habari wakati wa mkutano kati yao na ujumbe wa China na Tanzania  (hawapo pichani)
Sehemu ya wajumbe wakifuatilia mkutano kati ya ujumbe wa China, Tanzania  na Waandishi wa Habari ambao hawapo pichani.
Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Mbelwa Kairuki akijibu swali wakati wa mkutano na Waandishi wa Habari kuhusu ziara ya Balozi Liu nchini
Balozi Shimbo naye akizungumza wakati wa mkutano huo
Mkutano ukiendelea
 
Mkurugenzi wa Idara ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje ya China, Balozi Liu Songtian kwa pamoja na Balozi wa Tanzania nchini China Mhe. Shimbo wakijadili jambo wakati wakipitia Mchoro wa Ramani ya  Bandari ya Bagamoyo namna itakavyokuwa baada ya kumalizika ujenzi wake



Balozi Liu akipata maelezo alipotembelea Kijiji cha Makumbusho cha Kaole kilichopo Bagamoyo.

Picha na Reginald Philip





Tanzania na China kuendeleza ushirikiano kwenye Sekta ya Uwekezaji na Viwanda

Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Rajabu Gamaha akizungumza wakati wa mkutano kati yake na Mkurugenzi wa Idara ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje ya China, Balozi Liu Songtian  (hayupo pichani). Balozi Liu na ujumbe wake wapo nchini kwa ajili ya kufuatilia masuala ya uwekezaji na maendeleo ya viwanda Tanzania ikiwa ni miongoni mwa nchi tatu za Afrika zilizochaguliwa na China kwa ajili ya kuwa mfano katika uwekezaji na maendeleo ya viwanda. Nchi zingine ni Ethiopia na Kenya. Wengine katika picha ni Balozi Mbelwa Kairuki (kushoto kwa Bal. Gamaha), Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia, Mhe. Abdulrahman Shimbo (mwenye tai nyekundu), Balozi wa Tanzania nchini China na Kanali Mstaafu Joseph Simbakalia (kulia), Mkurugenzi Mkuu wa EPZA.
Mkurugenzi wa Idara ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje ya China, Balozi Liu Songtian akizungumza wakati wa mkutano kati yake na Balozi Gamaha na ujumbe wake. Kulia ni Balozi wa China hapa nchini, Mhe. Lu Yoqing
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka Maalum ya Uwekezaji (EPZA), Kanali Mstaafu Joseph Simbakalia akitoa mada kuhusu maeneo maalum ya uwekezaji yaliyopo nchini kwa ujumbe kutoka China unaoongozwa na Balozi Liu
Balozi Gamaha (katikati), akiwa pamoja na Balozi Shimbo (kushoto) na Balozi Kairuki (kulia) wakifuatilia mada iliyowasilishwa na Bw. Simbakalia (hayupo pichani)
Bw. Simbakalia akiendelea kutoa mada huku wajumbe kutoka China na Tanzania wakisikiliza
Balozi Liu akimkabidhi zawadi Balozi Gamaha
Balozi Mbelwa akimkabidhi Balozi Liu zawadi ya majani ya chai na kahawa ya Tanzania

Picha na Reginald Philip


=================================
Tanzania na China kuendeleza ushirikikiano katika Sekta ya Uwekezaji na Viwanda

Na Mwandishi Maalum

Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Rajabu Gamaha amaihakikishia Serikali ya China kuwa Tanzania itaendelea kuwa nchi ya amani na utulivu na kwamba inawaribisha wawekezaji kutoka nchi hiyo.

Balozi Gamaha aliyasema hayo Jijini Dar es Salaam alipokutana na ujumbe wa Maafisa kutoka China ukiongozwa na Mkurugenzi wa Idara ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje ya China, Balozi Liu Songtian. Ujumbe huo upo nchini kwa ziara ya kikazi ya kufuatilia hatua zilizofikiwa na Serikali ya Tanzania juu ya uamuzi wa China wa kuzifanya nchi tatu za Afrika ikiwemo Tanzania kuwa mfano katika masuala ya Uwekezaji na Maendeleo ya Viwanda.

Balozi Gamaha alisema kuwa moja ya vigezo muhimu katika kuvutia wawekezaji ni pamoja na nchi kuwa na amani na utulivu wa kisiasa, kigezo ambacho Tanzania inacho na itaendelea kukilinda.

“Pamoja na Tanzania kujiandaa na Uchaguzi Mkuu mwaka huu, bado naamini hakuna kitu kinaweza kuvuruga amani iliyopo. Hivyo kitu muhimu ni kuendeleza ushirikiano wetu uliopo ambao ni wa kuheshimiana na kufaidishana na si wa kinyonyaji”, alisema Balozi Gamaha.

Awali akizungumza wakati wa mkutano huo, Balozi Songtian alisema kwamba China ina nia ya dhati ya kushirikiana na Tanzania katika masuala ya uwekezaji na maendeleo ya viwanda kwa kuzingatia ushirikiano uliopo pia ni miongoni mwa nchi nzuri zaidi kwa uwekezaji hapa duniani.

Aidha, Balozi Songtian aliongeza kuwa China ipo tayari kushirikiana na Tanzania katika kuzifanyia kazi changamoto mbalimbali zinazojitokeza katika sekta ya uwekezaji ikiwemo miundombinu, teknolojia na elimu ya ufundi ili hatimaye iendelee kiviwanda.

“Lengo langu ni kufanya kazi pamoja ili kuhakikisha Tanzania na China zinafanikiwa katika Sekta ya Uwekezaji. Hivyo upo umuhimu mkubwa wa kusomesha watu wengi zaidi katika masuala ya Teknolojia na kuwa na Vyuo vingi zaidi vya Ufundi hapa Tanzania ili hatimaye tufanikiwe katika sekta ya Viwanda”, alisisitiza Balozi Songtian.

Aidha, Balozi Songtian alisema kuwa upo mpango wa Serikali ya China chini ya Mpango wa Ushirikiano wa China na Afrika (FOCAC) wa kuwaalika Wajasiriamali wachanga wapatao 500 kutoka Afrika kwenda nchini humo kwa ajili ya kujifunza masuala mbalimbali yatakayowasaidia kuendeleza shughuli zao.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Eneo Maalum la Uwekezaji (EPZA), Kanali Mstaafu Joseph Simbakalia ambaye aliwasilisha mada kuhusu Maeneo Maalum ya Uwekezaji hapa nchini, alisema kuwa Tanzania ni nchi ambayo ina fursa nyingi za uwekezaji na tayari kuna maeneo Maalum ya Uchumi yametengwa kwa kazi hiyo. Maeneo hayo ni pamoja na Bagamoyo, Dar es Salaam (Eneo la Benjamin William Mkapa) na Mtwara.

Pia, alieleza kuwa ili sekta ya uwekezaji nchini ikue na kufikia maendeleo ya viwanda ni muhimu kuimarisha rasimaliwatu, miundombinu ikiwemo barabara, reli, viwanja vya ndege, bandari, nishati ya umeme na sekta za kibenki.

Tanzania ni miongoni mwa nchi tatu za Afrika zilizochaguliwa na China kwa ajili ya kuwa mfano wa uwekezaji na maendeleo ya Viwanda. Nchi zingine ni Ethiopia na Kenya.


-Mwisho-


WAZIRI MEMBE AONGOZA MKUTANO WA MAWAZIRI WA JUMUIYA YA MADOLA


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Membe akiongoza Mkutano wa 45 wa Kikundi Kazi cha Mawaziri wa Jumuiya ya Madola, (Commonwealth Ministerial Action Group-CMAG) unaofanyika Mjini London, Uingereza tarehe 11 na 12 Machi, 2015. Waziri Membe ni Mwenyekiti wa Kikundi Kazi hicho ambaye aliteuliwa wakati wa Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Madola uliofanyika nchini Sri Lanka mwaka 2013. Kushoto kwa Waziri Membe ni Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo, Bw. Kamalesh Sharma.

 Mhe. Bernard Membe akijadiliana jambo na Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo, Bw. Sharma.
Mkutano ukiendelea




Thursday, March 12, 2015

Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Madola awasili London

Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Madola na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Tanzania Mhe. Bernard Membe akiwa na Waziri wa Masuala ya Afrika wa Uingereza Mhe. James Duddridge baada ya kuwasili Jijini London kwa ajili ya kikao cha kazi cha Jumuiya ya Madola tarehe 11-12 Machi 2015.

Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Madola na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Tanzania Mhe. Bernard Membe akiwa na Katibu Mkuu wa Sekretarieti ya Jumuiya ya Madola Mhe. Kamalesh Sharma kabla ya kuanza kikao cha faragha jijini London Uingereza leo.

Mhe. Bernard Membe, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Madola mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege Jijini London na kupokelewa na Balozi wa Tanzania nchini Uingereza Mhe. Peter Kallaghe na Naibu Mkuu Mkuu wa Ubalozi Msafiri Marwa (wa pili kushoto) na Mkuu wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa Balozi Celestine Mushy.  
(Picha ya Juu na Chini) Mhe. Bernard Membe, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na ujumbe wake kwenye mazungumzo ya kikazi na Mhe. James Duddridge, Waziri wa Masuala ya Afrika wa Uingereza mara baada ya kuwasili London Jumatano tarehe 11/03/2015.



(Picha ya Juu na Chini) Mhe. Bernard Membe, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Madola na ujumbe wake wakiwa kwenye kikao cha kazi na Katibu Mkuu wa Sekretarieti ya Jumuiya ya Madola Mhe. Kamalesh Sharma Jumatano tarehe 11/03/2015.


Monday, March 9, 2015

Wanawake Mambo ya Nje washiriki Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani


Wanawake wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wameungana na Wanawake wengine duniani kote katika kusherehekea Siku ya Wanawake Duniani, iliyofanyika katika Viwanja vya Mnazi mmoja, Jijini Dar es Salaam. Mgeni rasmi kwenye maadhimisho hayo alikuwa ni Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Salma Kikwete. Kauli mbiu ya maadhimisho ya mwaka huu ni "UWEZESHAJi WANAWAKE TEKELEZA WAKATI NI SASA"


Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu, Bibi Amisa Mwakawsago (aliyevaa miwani) akiwaongoza Wanawake wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kusherehekea siku ya wanawake duaniani katika Viwanja vya Mnazi Mmoja
Wanawake wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wakiwa katika maandamano.
Mama Salma Kikwete (Katikati) akiwapungia mkono wa kina Mama kutoka Wizara ya Mambo ya Nje waliokuwa wakipita mbele kwa furaha (Hawapo pichani), 
Wanawake wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wakipita mbele ya mgeni rasmi (hayupo pichani) wakiwa wamejawa na furaha na bashasha kuherehekea siku ya wanawake duniani.
Wanawake  kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wakiwa katika Picha ya Pamoja

Picha na Reginald Philip