Friday, July 24, 2015

Kaimu Katibu Mkuu wa Mambo ya Nje afunga rasmi mafunzo ya SOFREMCO

Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Irene Kasyanju (kulia) akiwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Diplomasia, Balozi Mwanaidi Maajar wakati wa hafla fupi ya kufunga Mafunzo Maalum ya  Maafisa  Waandamizi wa Mambo ya Nje (SOFREMCO)  iliyofanyika Chuoni hapo Jijini Dar es Salaam hivi karibuni.
Kaimu Katibu Mkuu, Balozi Kasyanju na Balozi Maajar wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Viongozi wa Chuo na Wizara pamoja na Wahitimu wa Mafunzo ya Maafisa Waandamizi wa Mambo ya Nje.
Baadhi ya wahitimu wa kozi hiyo ya SOFREMCO wakifurahia
Wahitimu wengine wakiwa wenye nyuso za furaha
Kundi jingine la wahitimu hao

Wakufunzi wa Chuo cha Diplomasia wakibadilishana mawazo wakati wa hafla hiyo
Wahitimu nao wakipata wasaa wa kujadili namna kozi ilivyokuwa
Wahitimu wakipata picha za pamoja kwa kumbukumbu
Picha ya pamoja ya Maafisa waliohitimu Kozi ya Maafisa Waandamizi wa Mambo ya Nje
Wakifurahia
Picha zaidi

Kaimu Katibu Mkuu, Balozi Kasyanju akiongozana na Balozi Maajar na Viongozi wengine mara baada ya hafla  fupi ya kuwapongeza Wahitimu wa Mafunzo ya SOFREMCO kukamilika.


Thursday, July 23, 2015

Wizara ya Mambo ya Nje yamuaga Balozi wa Ubelgiji aliyemaliza muda wa kazi nchini



Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Irene Kasyanju akitoa hotuba wakati wa kumuaga Balozi wa Ubelgiji ambaye amemaliza muda wake wa kazi hapa nchini, Mhe. Adam Koeler huku Balozi huyo (wa kwanza kulia waliketi) na wageni waalikwa wakimsikiliza. Hafla hiyo ilifanyika katika Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam tarehe 22 Julai, 2015. Katika hotuba yake Balozi Kasyanju alimsifu Balozi Koeler kwa kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Ubelgiji.
Balozi Koeler pamoja na Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Joseph Sokoine wakimskiliza Balozi Kasyanju wakati wa hafla fupi ya kumuaga Balozi Koeler.
Balozi Koeler nae akizungumza wakati wa hafla ya kumuaga. Katika hotuba yake Balozi huyo aliishukuru Serikali ya Tanzania  kwa ushirikiano alioupata katika kipindi chote alichokuwepo hapa nchini  na kusifu ukarimu wa Watanzania.
Balozi Kasyanju kwa pamoja  na Mkuu wa Mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa nchini ambaye pia ni Balozi wa Congo (DRC), Mhe. Juma Halfan Mpango na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini, Bw. Alvaro Rodrigues wakimsikiliza Balozi Koeler (hayupo pichani) akihutubia.
Balozi Sokoine nae akizungumza machache wakati wa hafla ya kumuaga Balozi Koeler
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bi. Zuhura Bunndala (katikati) akiwa na wageni waalikwa wengine wakati wa hafla ya kumuaga Balozi wa Ubelgiji ambaye amemaliza muda wake wa kazi hapa nchini
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali, Bi. Mindi Kasiga (katikati) akiwa na Balozi wa Ujerumani hapa nchini, Mhe. Egon Kochanke (kushoto) pamoja na Afisa Mambo ya Nje, Bi. Felister Rugambwa wakati wa hafla ya kumuaga Balozi wa Ubelgiji.
Balozi wa Ireland hapa nchini, Mhe. Fionnuala Gilsenan (kulia) akiwa na Bw. Rodrigues (kushoto) na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa, Bi. Maulidah Hassan wakati wa hafla ya kumuaga Balozi wa Ubelgiji 
Wageni waalikwa wakati wa hafla hiyo
Bi. Kasiga ambaye alikuwa msheheshaji (MC) katika hafla hiyo akiwakaribisha  Mabalozi na wageni waalikwa kwenye hafla hiyo
Kaimu Katibu Mkuu, Balozi Kasyanju (kushoto) na Balozi Koeler (kulia) pamoja na wageni waalikwa wakimsikiliza Bi. Kasiga ambaye haonekani pichani
Juu na Chini ni Maafisa Mambo ya Nje wakifuatilia matukio kwenye hafla ya kumuaga Balozi wa Ubelgiji.
Balozi Koeler akiteta jambo na Balozi Sokoine
Balozi Kasyanju, Balozi Koeler na wageni waalikwa wakitakiana afya njema
Balozi Koeler akifurahia zawadi ya picha ya kuchora ya Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro aliyokabidhiwa na Kaimu Katibu Mkuu, Balozi Kasyanju huku akitamka kuwa "nitarudi Tanzania kuja kupanda Mlima Kilimanjaro".
Balozi Koeler akimshukuru Balozi Kasyanju kwa zawadi hiyo nzuri
Picha ya Pamoja.




Wednesday, July 22, 2015

Wizara ya Mambo ya Nje yamuaga Balozi wa Sweden aliyemaliza muda wa kazi nchini

Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Irene Kasyanju akizungumza wakati wa hafla ya chakula cha mchana kilichoandaliwa na Wizara kwa ajili ya kumuaga Balozi wa Sweden hapa nchini ambaye amemaliza muda wake wa kazi, Mhe. Lennarth Hjelmaker. Hafla hiyo ilifanyika kwenye Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam hivi karibuni.
Balozi wa Sweden anayemaliza muda wake wa kazi hapa nchini, Mhe. Lennarth Hjelmaker akimsikiliza Balozi Kasyanju (hayupo pichani) wakati akitoa hotuba ya kumuaga Balozi huyo. Katikati ni Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Joseph Sokoine.
Balozi Sokoine akizungumza kuwakaribisha Wageni waalikwa kwenye hafla ya kumuaga Balozi wa Sweden aliyemaliza muda wake wa kazi hapa nchini.
Balozi Kasyanju (katikati) na Balozi Hjelmaker (kushoto) kwa pamoja na Mkuu wa Mabalozi ambaye pia ni Balozi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo hapa nchini, Mhe. Juma Halfan Mpango (kulia) wakimsikiliza Balozi Sokoine ambaye hayupo pichani.
Balozi Hjelmaker nae akitoa neno la shukrani kwa Serikali ya Tanzania kwa kumpatia ushirikiano mkubwa katika kipindi chote cha miaka mitano aliyokuwepo hapa nchini kama Balozi wa Sweden. 
Balozi Hjelmaker akizungumza huku wageni waalikwa wakimsikiliza
Balozi Kasyanju akimkabidhi Balozi Hjelmaker zawadi ya picha ya kuchora ya  Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro kama kumbukumbu yake ya vivutio vya utalii vilivyopo Tanzania
Balozi Kasyanju akiwa katika picha ya pamoja na Balozi Hjelmaker na Balozi Mpango
Maafisa Mambo ya Nje walioshiriki hafla hiyo
Picha ya pamoja
Balozi Kasyanju akiagana na Balozi Hjelmaker mara baada ya hafla ya kumuaga kukamilika.

Picha  na Reginald Philip

Tuesday, July 21, 2015

Kongamano la Pili la Diaspora kufanyika hapa nchini mwezi Agosti


Kaimu Mkurugenzi Idara ya Diaspora Wizara ya Mambo ya Nje Bi. Rosemary Jairo akizungumza kwenye Mkutano na waandishi wa Habari juu ya Maandalizi ya Kongamano la Diaspora (Tanzania Diaspora and SMEs partnership 2015) litakalofanyika katika Hoteli ya Serena Jijini Dar Es Salaam kuanzia tarehe 13 hadi 15 Agosti 2015, likiwa na kaulimbiu isemayo 'Creating Linkages between Diaspora and local SMEs in Tanzania' 
Mkutano na waandishi wa habari ukiendelea
Picha na Reginald Philip

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA



Simu: 255-22-2114615, 211906-12
Barua pepe: nje@nje.go.tz
Barua pepe: gcu@nje.go.tz

Nukushi: 255-22-2116600

              


 



  
 


20 KIVUKONI FRONT P.O. BOX 9000,
11466 DAR    ES SALAAM,                             Tanzania.








TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kushirikiana na Kituo cha Uwekezaji cha Kimataifa (International Trade Centre UN-Agency) inafanya Maandalizi ya Kongamano la Diaspora (Tanzania Diaspora & SMEs Partnership Conference 2015). Kongamano husika litafanyika hapa Dar es Salaam, kuanzia tarehe 13 hadi 15 Agosti 2015 katika Hoteli ya Serena. Kongamano hilo litakuwa la pili kufanyika hapa nchini na litahusisha Diaspora na Wadau wa hapa Tanzania.

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Ofisi ya Rais na Utawala Bora – Zanzibar na Ofisi ya Waziri Mkuu ndio Wadau Wakuu katika Maandalizi ya Kongamano hili.
Kongamano la mwaka huu lina Kauli Mbiu, ‘Creating Linkages between Diaspora and Local SMEs in Tanzania’ na Dhumuni lake ni kuhamasisha Ushiriki wa Diaspora katika kukuza Biashara Ndogo na za Kati hapa nchini. Kongamano la mwaka huu pia litahusisha Mikoa ya Tanzania ambapo Mikoa itapata fursa ya kutangaza fursa za uwekezaji zilizopo Mikoani.
Kongamano hilo linatarajiwa kufunguliwa na Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kufungwa na Mhe. Dr. Ali Mohamed Shein, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.

Aidha, katika kuhitimisha kilele cha Kongamano hilo, Diaspora wanatarajiwa kufanya ziara Zanzibar tarehe 15 Agosti 2015, ikiwa ni sehemu ya mwaliko maalum kutoka Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Pamoja na Shughuli za Ufunguzi na Kilele, Matukio muhimu yatakuwa ni Maonesho ya Kibiashara, Majadiliano ya Mada kuhusu Ushirikishwaji wa Diaspora kwa Maendeleo ya Nchi hususan SMEs, uwekezaji Mikoani n.k.

Kongamano hilo litahudhuriwa na Watanzania Wanaoishi Ughaibuni (Diaspora) na wale waliorejea hapa nchini na Wadau wa Maendeleo kutoka hapa nchini.

Wizara ya Mambo ya Nje Usually integration involves one or more written agreements that describe the areas of cooperation in detail, as well as some coordinating bodies representing the countries involved.inawakaribisha kushiriki nasi katika Kongamano hilo. Tafadhali tembeleeni tovuti ya (www.tzdiaspora.com) kupata taarifa muhimu hususan kuhusu Ada za Ushiriki, fursa za Kufadhili na namna ya kujisajili.

Imetolewa na: Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Dar es Salaam
21 Julai, 2015