Wednesday, July 22, 2015

Wizara ya Mambo ya Nje yamuaga Balozi wa Sweden aliyemaliza muda wa kazi nchini

Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Irene Kasyanju akizungumza wakati wa hafla ya chakula cha mchana kilichoandaliwa na Wizara kwa ajili ya kumuaga Balozi wa Sweden hapa nchini ambaye amemaliza muda wake wa kazi, Mhe. Lennarth Hjelmaker. Hafla hiyo ilifanyika kwenye Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam hivi karibuni.
Balozi wa Sweden anayemaliza muda wake wa kazi hapa nchini, Mhe. Lennarth Hjelmaker akimsikiliza Balozi Kasyanju (hayupo pichani) wakati akitoa hotuba ya kumuaga Balozi huyo. Katikati ni Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Joseph Sokoine.
Balozi Sokoine akizungumza kuwakaribisha Wageni waalikwa kwenye hafla ya kumuaga Balozi wa Sweden aliyemaliza muda wake wa kazi hapa nchini.
Balozi Kasyanju (katikati) na Balozi Hjelmaker (kushoto) kwa pamoja na Mkuu wa Mabalozi ambaye pia ni Balozi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo hapa nchini, Mhe. Juma Halfan Mpango (kulia) wakimsikiliza Balozi Sokoine ambaye hayupo pichani.
Balozi Hjelmaker nae akitoa neno la shukrani kwa Serikali ya Tanzania kwa kumpatia ushirikiano mkubwa katika kipindi chote cha miaka mitano aliyokuwepo hapa nchini kama Balozi wa Sweden. 
Balozi Hjelmaker akizungumza huku wageni waalikwa wakimsikiliza
Balozi Kasyanju akimkabidhi Balozi Hjelmaker zawadi ya picha ya kuchora ya  Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro kama kumbukumbu yake ya vivutio vya utalii vilivyopo Tanzania
Balozi Kasyanju akiwa katika picha ya pamoja na Balozi Hjelmaker na Balozi Mpango
Maafisa Mambo ya Nje walioshiriki hafla hiyo
Picha ya pamoja
Balozi Kasyanju akiagana na Balozi Hjelmaker mara baada ya hafla ya kumuaga kukamilika.

Picha  na Reginald Philip

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.