Tuesday, September 8, 2015

Mfalme Letsie III wa Lesotho, atua nchini kwa ziara

 Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Kamilius Membe (Mb.), akisalimiana na Mfalme Letsie III wa Lesotho, muda mfupi baada ya kutua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, kabla ya kuelekea Jijini Arusha kuhudhuria Mkutano wa Kilele wa Dunia kuhusu Uimarishaji wa chakula (Global Summit on Food Fortification, na kuanza ziara ya siku tatu kuanzia leo 08 hadi 11 Septemba 2015.
Mfalme Letsie III wa Lesotho, akisalimiana na Balozi wa Tanzania Nchini Afrika Kusini, Balozi Radhia Msuya, muda mfupi baada ya Mfalme huyo kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere.
 Mfalme Letsie III wa Lesotho, akisalimiana na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bi. Zuhura Bundala, muda mfupi baada ya Mfalme huyo kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere.
 Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Kamilius Membe (Mb), akiwa ameongozana na mgeni wake, Mfalme Letsie III wa Lesotho, wakielekea chumba cha mapumziko, kabla ya kuelekea Jijini Arusha kuanza ziara ya siku mbili kuanzia leo 08 hadi 11 Septemba 2015.
Mhe. Bernard Membe (Mb), akifanya mazungumzo na Mfalme Letsie III wa Lesotho, kabla ya kuelekea Jijini Arusha kuhudhuria Mkutano wa Kilele wa Dunia kuhusu uimarishaji wa chakula (Global Summit on Food Fortification).
Mhe. Bernard Membe (Mb.), akiagana na mgeni wake, Mfalme Letsie III wa Lesotho.
===============================
PICHA NA REUBEN MCHOME.

Mabalozi Wateule Watatu Wawasilisha Nakala za Hati za Utambulisho.

Nakala za Hati za Utambulisho za Balozi Mteule wa Sweden.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Membe (Mb), akipokea Nakala za Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi Mteule wa Sweden hapa Nchini Mhe.Katarina Rangnitt, baada ya Balozi huyo kuwasilisha nakala hizo ofisini kwa Waziri Membe leo 08-09-2015.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Membe (Mb), akizungumza na Balozi Mteule wa Sweden hapa Nchini Mhe. Katarina Rangnitt, baada ya Balozi huyo kuwasilisha nakala za hati zake ofisini kwa Waziri leo.
Baadhi ya Maofisa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, na Msaidizi wa Balozi Mteule wa Sweden, wakifuatilia mazungumzo hayo.

 Mhe. Waziri Bernard Membe (Mb), akifurahia jambo na Balozi Mteule wa Sweden hapa Nchini Mhe.Katarina Rangnitt, baada ya Balozi huyo kuwasilisha nakala zake ofisini kwa Waziri leo.
==============================
Nakala za Hati za Utambulisho za Balozi Mteule wa Finland.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Membe (Mb), akipokea Nakala za Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi Mteule wa Finland hapa Nchini Mhe.Pekka Hukka, baada ya Balozi huyo kuwasilisha nakala hizo ofisini kwa Waziri leo 08-09-2015.
Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Membe (Mb), akizungumza na Balozi Mteule wa Finland hapa Nchini Mhe.Pekka Hukka, baada ya Balozi huyo kuwasilisha hati zake ofisini kwa Waziri leo.
Balozi Mteule wa Finland hapa Nchini Mhe.Pekka Hukka, akizungumza na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Membe (Mb), baada ya kuwasilisha Nakala za Hati zake za Utambulisho ofisini kwa Waziri leo 08-09-2015.

Baadhi ya Maofisa wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, na Msaidizi wa Balozi Mteule wa Finland wakifuatilia mazungumzo hayo.
====================
Nakala za Hati za Utambulisho za Balozi Mteule wa Uturuki.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Membe (Mb), akisalimiana na Balozi Mteule wa Uturuki hapa Nchini Mhe.Yasemin Eralp, baada ya Balozi huyo kuwasilisha Nakala za Hati zake za Utambulisho.
Mhe. Waziri Bernard Membe (Mb.), akizungumza na Balozi Mteule wa Uturuki hapa Nchini Mhe.Yasemin Eralp, ofisini kwake muda mfupi baada ya Balozi huyo kuwasilisha Nakala za Hati zake za Utambulisho.
Balozi Mteule wa Uturuki hapa Nchini Mhe.Yasemin Eralp, akisisitiza jambo kwa Mhe. Waziri Bernard Membe, baada ya Balozi huyo kuwasilisha Nakala za Hati zake za Utambulisho kwa Mheshimiwa Waziri.
Baadhi ya Maofisa wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, wakifuatilia mazungumzo hayo.
=======================
PICHA NA REUBEN MCHOME.

Monday, September 7, 2015

Ujumbe kutoka China wakutana na Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Hassan Simba Yahaya, akizungumza na Naibu Mkuu wa Jimbo la Guangdong Nchini China, Mhe. Luo Jun wakati ujumbe kutoka Idara ya Mambo ya Nje ya Jimbo hilo, ulipomtembelea ofisini kwake leo  Septemba 7, 2015.
Naibu Mkuu wa Jimbo la Guangdong Nchini China, Mhe. Luo Jun akisisitiza jambo kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Hassan Simba Yahaya katika mazungumzo hayo.
Ujumbe kutoka Idara ya Mambo ya Nje ya Jimbo la Guangdong Nchini China wakifuatilia kwa makini mazungumzo hayo. Jimbo la Guangdong ndilo lenye miji mikubwa nchini China ya Guangzhou na Shenzhen na pia Jimbo hilo ndilo linaloongoza kuwa na idadi kubwa ya watu yapata milioni 106.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Hassan Simba Yahaya,akizungumza jambo na Afisa Dawati - China, Medard Ngaiza wakati wa mazungumzo hayo.
 Mazungumzo yakiendelea
Naibu Katibu Mkuu akisisitiza jambo katika mazungumzo hayo.

Press Release

H.H Sheikh Khalifa bin Zayed Al Nahyan, President of UAE

PRESS RELEASE

H.E Dr. Jakaya Mrisho Kikwete, President of the United Republic of Tanzania has sent a condolence message to His Highness Sheikh Khalifa bin Zayed Al Nahyan, President of the United Arab Emirates following the killing of 45 Emirati solders while on duty in Yemen.

The message reads as follows;

“His Highness, Sheikh Khalifa bin Zayed Al Nahyan,
President of the United Arab Emirates,
ABU DHABI,

Your Highness,

I have received with great sorrow the sad news about the untimely killing of 45 Emirati soldiers in a missile attack in Yemen on Friday 04th September, 2015.

On behalf of the Government and People of the United Republic of Tanzania, and on my behalf, I wish to convey our most heartfelt condolences to you and through you to the Government and the People of the United Arab Emirates for the great loss of Emirati heroes.

The killing of 45 Emirati soldiers who were on duties in Yemen has touched many people around the World. They will be remembered for their tireless efforts and commitment in pursuit of international peace and security especially for their work in Yemen.

My Government condemns that killing as well as the ongoing political crisis in Yemen that was caused by Houthi rebels. Our Government calls upon to the international community in particular the United Nations to intervene the situation in Yemen. May the soul of the departed rest in eternal Peace”.

Issued By: The Ministry of Foreign Affairs and International Cooperation, Dar es Salaam

07th September, 2015

Sunday, September 6, 2015

Wajasiriamali wahimizwa kutumia internet kutangaza biashara zao

Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-Zanzibar, Bw. Salim Maulidi Salim akimkabidhi picha ya mlango wa asili ya Zanzibar, Mwenyekiti wa Watanzania wanaoishi jijini Birmingham, Bw. Prince Kateka II ikiwa ni ishara ya kukaribishwa Zanzibar.

Wafanyabiashara wamehimizwa kutumia mtandao wa internet kutangaza bidhaa na huduma wanazotoa kwa kuwa njia hiyo ni nafuu na inawafikiwa watu wengi kwa haraka. Hayo yalibainishwa na Bw. Dickson Inachee, Raia wa Uganda alipokuwa anatoa mada katika kongamano la siku mbili la Watanzania wanaoishi Uingereza lililomalizika jijini Birmingham siku ya Jumamosi tarehe 05 Septemba 2015. 

Bw. Inachee alieleza kuwa, kwa mujibu wa takwimu zilizopo zaidi ya watu milioni 9.3 wanatumia internet nchini Tanzania. Kati ya hao watu milioni 2.4 wanatumia mtandao wa face book, hivyo ukitangaza katika face book, tangazo lako litawafakia watu wengi kuliko kutumia vyombo vilivyozoeleka kama magazeti. 

Aliendelea kueleza kuwa tangazo katika face book linatozwa Dola moja ya Marekani na kwa Tanzania litawafikia watu milioni 2.4 lakini tangazo hilo hilo ukilitoa katika gazeti linalopendwa sana nchini Tanzania utatakiwa kulipa Dola 300 na litawafikia watu elfu 50 tu.  

Bw. Inachee alimalizia mada yake kwa kusisitiza kuwa, endapo wajasiliamali nchini Tanzania wanataka kufanya biashara kwa kutumia mbinu mpya za kibiashara, basi hawana budi kutumia internet kutangaza bidhaa zao kwa kuwa njia hiyo itawaondolea mzigo wa kulipa fedha nyingi katika vyombo vilivyozoeleka sanjari na kuwafikia watu wengi zaidi.


 Bw. Anthony Chaula akiwasilisha mada

Katika hatua nyingine, wanadiaspora walioshiriki kongamano hilo, wameridhishwa na hatua ya Serikali ya kuwapa hadhi maalum katika Katiba inayopendekezwa. Akiwasilisha mada katika kongamano hilo, Bw. Anthony, Chaula kutoka Idara ya Uhamiaji alisema kuwa Katiba inayopendekezwa itakapopitishwa, wanadiaspora watapewa hadhi maalum tofauti na ilivyo sasa ambapo wanaonekana kama wageni wengine.
s
Wakati wa kongamano hilo, baadhi ya Watanzania wanaoishi Uingereza walitumia fursa hiyo kutangaza shughuli zao za kibunifu wanazofanya katika nchi hiyo. Bw, Ayoub Mzee alizindua rasmi progaramu yake inayoitwa AITV APP. Programu hiyo inamwezesha mteja, kwa kutumia simu ya mkononi au kifaa kingine chenye internet kuangalia vituo takriban vyote vya televisheni vya Tanzania na Afrika kwa ujumla kwa gharama ya Dola za Marekani sita kwa mwezi.

 Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo yas Nje, Balozi Liberata Mulamula aksalimiana na Bw. Ayoub Mzee kabla ya kuzindua programu ya AITV APP.


Mtanzania mwingine Bw. Mediremtula ameanzisha kampuni inayojihusisha na utengenezaji wa tablet. Anasema aina ya tablet anayotengeneza inafanya vizuri kibiashara katika nchi za Uingereza na Urusi na hivi sasa yupo katika mchakato wa kutengeneza aina nyingine ya tablet kwa ajili ya Tanzania.

Katika masuala ya sanaa hasa ya uigizaji wa filamu, Watanzania wa Uingereza hawakuachwa nyuma. Kuna Watanzania wamecheza filamu ijulikanayo Goingbongo. Filamu hiyo imeigizwa katika viwango vya kimataifa na walioafanikiwa kuiangalia wamethibitisha kuwa ni ya kimataifa kweli.

Kongamano hilo lilifungwa rasmi na Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais- Zanzibar, Bw. Salim Maulidi Salim ambaye alisisitiza umuhimu wa wanadiaspora kuwekeza nyumbani kwa madhumuni ya kukuza uchumi na kuondoa tatizo la ukosefu wa ajira kwa jamaa zao.      
Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Mhe. Peter Kallaghe akitoa cheti cha kutambua mchasngo wa mmoja wa wadhamini wa kongamano. 
Na Ally Kondo, Birmingham