Sunday, October 11, 2015
Saturday, October 10, 2015
Rais Kikwete azindua Kiwanda cha Saruji kikubwa Afrika Mashariki na Kati.
Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Kiwanda cha Saruji kikubwa Afrika Mashariki na Kati cha Dangote Industries Limited kilichopo katika Kijiji cha Mgao Mkoani Mtwara, Tanzania. Kulia kwa Rais ni Mmiliki wa Kiwanda hicho, Alhaji Aliko Dangote na kushoto ni Mwakilishi wa Serikali ya Nigeria, Mallam Nasir Ahmad El-Rufai, Gavana wa Jimbo la Kaduna. Wengine ni Mke wa Rais Mama Salma Kikwete pamoja na wafanyibiashara kutoka nchini Nigeria nao wakishuhudia uzinduzi huo uliofanyika tarehe 10 Oktoba 2015.
Mheshimiwa Rais Dkt. Jakaya Kikwete akiweka saini kwenye kitabu cha wageni, muda mfupi baada ya kuzindua kiwanda hicho.
Mmiliki wa Kiwanda hicho, Alhaj Aliko Dangote, akifafanua jambo kwa Mheshimiwa Rais juu ya namna kiwanda hicho kinavyofanya kazi ya uzalishaji wa saruji
Mheshimiwa Rais akipewa maelezo na mmoja wa wataalamu ya namna kiwanda hicho kinavyofanya uzalishaji wa saruji.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete, akizungumza na Wafanyibiashara wa Tanzania na Nigeria pamoja na Wananchi waliojitokeza katika kushuhudia ufunguzi wa Kiwanda hicho cha pili kwa ukubwa Barani Afrika na cha kwanza kwa Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb) akizungumza na waandishi wa habari muda mfupi baada ya Mheshimiwa Rais Kikwete kuzindua kiwanda hicho.
Moja ya sehemu ya muonekano wa kiwanda hicho cha Dangote Industries Limited Tanzania.
Mheshimiwa Rais Jakaya Kikwete akizungumza jambo na mmiliki wa Kiwanda hicho, AlhajI Aliko Dangote.
Picha ya Pamoja.
=====================================
PICHA NA: Reuben Mchome.
Balozi Mulamula atembelea Ubalozi wa Tanzania, Washington DC
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula akisalimiana na watumishi wa Ubalozi wa Tanzania Washington DC mara baada ya kuwasili Ubalozini |
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula akisaini kitabu cha wageni Ubalozini Washington DC. |
Katibu Mkuu akiwa katika kikao na wafanyakazi wa Ubalozi wa Tanzania, Washington DC |
Katibu Mkuu akiwa katika picha ya pamoja na Maafisa wa Ubalozi wa Tanzania Washington |
Friday, October 9, 2015
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Taarifa
zaidi ya Mahujaji kutoka Tanzania huko Saudi Arabia
Idadi
ya mahujaji wa Tanzania waliopoteza maisha katika tukio la kukanyagana lililotokea
eneo la Mina, Makkah tarehe 24 Septemba, 2015 imeongezeka kutoka 11 na kufikia 12 hadi sasa.
Idadi hiyo imeongezeka kufuatia Bi. Aluiya Sharrif Saleh Abdallha kugundulika
kuwa ni miongoni mwa mahujaji waliofariki dunia katika tukio hilo. Bi. Abdallah
alienda Makkah kufanya ibada ya hijjah kupitia kikundi cha TCDO.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,
Dar es Salaam
09 Oktoba, 2015
Thursday, October 8, 2015
Kaimu Katibu Mkuu azungumza na waandishi wa Habari kuhusu Wiki ya Umoja wa Mataifa
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Bw. Alvaro Rodriguez, naye akizungumza na waandishi wa Habari (hawapo pichani). |
Maafisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Maafisa wa Umoja wa Mataifa nao wakifuatilia mkutano huo pamoja na waandishi wa Habari (hawapo pichani) |
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bi.Mindi Kasiga (kulia) akiwafafanulia jambo waandishi wa habari (hawapo pichani). |
Wednesday, October 7, 2015
Rais Kikwete apokea hati za utambulisho wa Mabalozi
Balozi mteule wa Hispania nchini Tanzania Mhe. Felix Costales akikabidhi hati ya utambulisho kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Jakaya Kikwete Ikulu jijini Dar es Salaam Oktoba 7, 2015. |
Balozi mteule wa Ubelgiji nchini Tanzania Mhe. Paul Cartier akikabidhi hati ya utambulisho kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Jakaya Kikwete Ikulu jijini Dar es Salaam Oktoba 7, 2015. |
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
JAMHURI
YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA
MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA
Simu: 255-22-2114615, 211906-12
Nukushi: 255-22-2116600 |
20 KIVUKONI FRONT,
P.O. BOX 9000,
11466 DAR ES SALAAM,
Tanzania.
|
Taarifa
zaidi ya Mahujaji kutoka Tanzania huko Saudi Arabia
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kwa masikitiko
makubwa imepokea majina mengine matatu ya Mahujaji kutoka Tanzania waliofariki
dunia kufuatia tukio la mkanyagano wa Mahujaji lililotokea eneo la Mina, Makkah
tarehe 24 Septemba, 2015. Vifo vya Mahujaji hao vinafanya idadi ya Watanzania
waliofariki kufuatia tukio hilo kufikia watu kumi na moja (11) hadi sasa.
Majina ya Mahujaji hao ambao wametambulika baada ya kupitia taarifa
zao za vidole zilizotolewa na Serikali ya Saudi Arabia ni Bw. Yusuf Ismail Yusuf kutoka kikundi cha Khidmat Islamiya, Bi. Rahma Salim Suweid kutoka kikundi
cha Ahlu Daawa na Bw. Issa Amir Faki.
Aidha, Ubalozi unaendelea kushughulikia taratibu za mazishi kwa
mahujaji ambao wamefariki dunia na miili yao kutambuliwa. Tunapenda kufafanua
kuwa mali za marehemu ikiwemo mizigo waliyokuwa nayo wakati wa Hijah
zitawasilishwa nyumbani Tanzania na vikundi walivyokuja navyo na kukabidhiwa
kwa jamaa wa marehemu.
Vile vile, Ubalozi unaendelea kufuatilia orodha mpya ya taarifa za
vidole iliyotolewa na Serikali ya Saudi Arabia kwa ajili ya kuwabaini Mahujai
wa Tanzania ambao bado hawajatambuliwa.
Wakati huo huo, Wizara ya Afya ya Saudi Arabia inaendelea
kukamilisha zoezi la kuchukua taarifa za vinasaba (DNA) vya Mahujaji wote
waliokufa na kujeruhiwa katika ajali hiyo na imeshauri wale wote waliopotelewa
na ndugu na jamaa zao kupima vinasaba (DNA) ili kuwabaini jamaa zao.
Pia, kwa vile mchakato wa kuwatambua wahanga wa ajali hiyo ni mgumu
na unachukua muda, Wizara inawaomba Watanzania kuwa na subira katika kipindi
hiki ambapo taarifa zaidi kuhusu wapendwa wetu zikiendelea kutolewa.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,
Dar es Salaam
07 Oktoba, 2015
Subscribe to:
Posts (Atom)