Thursday, October 22, 2015

Taarifa kwa Vyonbo vya Habari


Taarifa zaidi kuhusu Mahujaji kutoka Tanzania waliofariki au kujeruhiwa huko Saudi Arabia

Mahujaji wengine wawili kutoka Tanzania ambao walikuwa hawaonekani tokea ajali ya kukanyagana kwa mahujaji ilipotokea Makkah nchini Saudi Arabia tarehe 24 Septemba 2015 wametambuliwa kuwa, ni miongoni mwa mahujaji waliofariki  dunia. Kutambuliwa kwa mahujaji hao kunafanya idadi ya mahujaji wa Tanzania waliopoteza maisha katika ajali hiyo kufikia ishirini na saba (27). Majina kamili ya mahujaji hao ni Bw. Juma Yussuf Bakula na Bw. Ahmad Awadh Namongo kutoka Kikundi cha Ahlu Dawaa.
Hadi sasa mahujaji kumi na tatu (13) kutoka Tanzania bado hawajulikani walipo na jitihada za kuwatafuta bado zinaendelea.

Kwa upande wa mahujaji wanne ambao walikuwa wanapatiwa matibabu kutokana na kuugua au kujeruhiwa, mmoja wao ni Bw. Mustafa Ali Mchina ambaye alikuwa amelezwa katika chumba cha wagonjwa mahututi katika mji wa Maddinah alifariki dunia tarehe 17 Oktoba 2015 na kuzikwa Maddinah siku hiyo hiyo. Bi. Mahjabin Taslim Khan ambaye alijeruhiwa katika ajali hiyo na kusababisha kukatwa mguu wake amepata nafuu na alirejea nchini tarehe 20 Oktoba 2015. Mwingine ni Bi. Hidaya Mchomvu ambaye alijeruhiwa pia bado yupo hospitali akiendelea kupatiwa matibabu. Hujaji wanne ni Bw. Ahmed Abdallah Jusab ambaye anasumbuliwa na ugonjwa wa moyo alifanyiwa upasuaji wa kumuwekea kifaa cha kuongeza mapigo ya moyo tarehe 19 Oktoba 2015 na alitarajiwa kurejea nchini tarehe 21 Oktoba 2015.
 
Serikali ya Saudi Arabia inaendelea kutoa taarifa zaidi za kuwatambua mahujaji waliofariki dunia au kujeruhiwa katika ajali hiyo na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa itaendelea kutoa taarifa kwa umma kuhusu wahanga wa ajali hiyo kadri itakapokuwa inazipokea.

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,
Dar es Salaam
22 Oktoba, 2015

Waziri Membe aagana na watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula akifungua hafla ya kumuaga Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe iliyoandaliwa na watumishi wa Wizara hiyo na kufanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere
Baadhi ya watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa waliohudhuria hafla hiyo
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Hassan Simba Yahya akitoa muhtsari wa shughuli chache ambazo Waziri Membe alizisimamia kwa umahiri mkubwa katika kipindi chake cha miaka 9 ya Uwazi wa Mambo ya Nje. Waliokaa ni Mhe. Membe na Balozi Mulamula ambao wanasikiliza kwa maikini shughuli zilizotekelezwa na Mhe. Waziri Membe.

Waheshimiwa Mabalozi wanaowakilisha Tanzania katika nchi mbalimbali, Wakuu wa Idara/Vitengo na watumishi wakisikiliza kwa makini shughuli ambazo Mhe. Waziri Membe amezisimamia ipasavyo ikiwemo suala la maslahi ya watumishi.

Sehemu nyingine ya Waheshimiwa Mabalozi wanaowakilisha Tanzania katika nchi mbalimbali, Wakuu wa Idara/Vitengo na watumishi wakisikiliza kwa makini shughuli ambazo Mhe. Waziri Membe amezisimamia ipasavyo ikiwemo suala la maslahi ya watumishi

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bi. Mindi Kasiga akitangaza Tuzo na Zawadi mbalimbali ambazo zitatolewa kwa ajili ya Mhe. Waziri na Naibu Waziri na Wenza wao.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (kushoto) akisoma maneno yaliyoandikwa katika Tuzo ya Uongozi iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje na kukabidhiwa na Katibu Mkuu, Balozi Liberata Mulamula 

Waziri Membe akifurahia zawadi iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje.

Waziri Membe akipokea zawadi kwa niaba ya Mama Membe ambaye hakuweza kufika katika hafla hiyo. Bi. Amisa Mwakawago, Mkurugenzi Msaidizi katika Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu alikabidhi zawadi hiyo kwa niaba ya Wizara.

Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa, Mhe. Begum Karim Taj naye akikabidhi zawadi kwa Mhe. Waziri kwa niaba ya Waheshimiwa Mabalozi wa Tanzania

Naibu Katibu Mkuu, Balozi Hassan Simba Yahya akipokea zawadi kwa niaba ya Naibu Waziri, Mhe. Dkt. Mahadhi Juma Maalim ambaye hakuweza kuhudhuria hafla hiyo kutokana na majukumu ya kitaifa.

Balozi Mulamula na Mama Mwakawago wakionesha zawadi ya Mama Mahadhi Juma Maalim.
Waheshimiwa Mabalozi wanaowakilisha Tanzania katika nchi mbalimbali, Wakuu wa Idara/Vitengo na watumishi wakishuhudia zoezi la utoaji wa zawadi.

Waziri Membe akiongea na watumishi wa Wizara wakati wa hafla hiyo.
Mkuu wa Itifaki, Balozi Juma Maharage akitoa neno la shukrani katika hafla hiyo

Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy naye akiongea machache katika hafla hiyo

Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati, Bw. Elibariki Maleko akionekana mtu mwenye furaha katika hafla hiyo, baada ya kutangazwa kuwa ameteuliwa kuwa Naibu Balozi wa Tanzania nchini Uganda. Wengine waliotangazwa kuwa Naibu Mabalozi ni Bi. Rosemary Jairo, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Diaspora ambaye anakuwa Naibu Balozi nchini Afrika Kusini na Bw. Andy Mwandembwa, Mkurugenzi Msaidizi katika Idara ya Itifaki ambaye anakuwa Naibu Balozi nchini Sweden.

Wakati wa maakuli. Mhe. Waziri akiwa ameshikilia sahani ya chakula na anyemfuatia ni Katibu Mkuu anayeonekana akichota chakula

Naibu Katibu Mkuu naye anajichotea chakula

Waheshimiwa Mabalozi nao wanajichotea chakula

Mhe. Waziri, Katibu Mkuu na Naibu Katibu Mkuu wakiwa katika picha ya pamoja na Waheshimiwa Mabalozi na Wakuu wa Idara/Vitengo

Mhe. Waziri, Katibu Mkuu na Naibu Katibu Mkuu wakiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa Idara/Vitengo.

Mhe. Waziri, Katibu Mkuu na Naibu Katibu Mkuu wakiwa katika picha ya pamoja na Wasaidizi wa Waziri na Naibu Waziri.
Mhe. Waziri, Katibu Mkuu na Naibu Katibu Mkuu wakiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu.
Mhe. Waziri, Katibu Mkuu na Naibu Katibu Mkuu wakiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali.
Mhe. Waziri, Katibu Mkuu na Naibu Katibu Mkuu wakiwa katika picha ya pamoja na Waheshimiwa Mabalozi Wanawake.


Balozi Mpya wa Misri awasilisha Nakala za Hati za Utambulisho

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (kulia) akimkaribisha Balozi mpya wa Misri, Mhe. Yasser Ahmed Al Eldin Elshawaf   katika ofisi yake. Balozi Mpya wa Misri alikuja ofisini kwa Mhe. Waziri kwa ajili ya kuwasilisha Nakala za Hati za Utambulisho                     

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe akipokea Nakala za Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi Mpya wa Misri, Mhe. Yasser Ahmed Al Eldin Elshawaf

Waziri Membe akishikana mkono na Balozi mpya wa Misri mara baada ya kupokea Nakala za Hati za Utambulisho.

Waziri Membe akiangalia na kufurahia zawadi aliyokabidhiwa na Balozi mpya wa Misri

Waziri Membe akiagana na Balozi mpya wa Misri nara baada ya zoezi la kuwasilisha Nakala za Hati za Utambulisho kukamilika                              

Wednesday, October 21, 2015

Waziri Membe akutana na Kiongozi wa Timu ya Waangalizi wa Uchaguzi Mkuu kutoka Umoja wa Afrika.

Kiongozi wa timu ya waangalizi wa Uchaguzi Mkuu kutoka Umoja wa Afrika (AU), ambaye pia ni Rais Mstaafu wa Msumbiji Mhe. Armando Emilio Guebuza akizungumza na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Membe ambapo Waziri Membe alimueleza kiongozi huyo hali ya utulivu na amani inavyoendelea katika kipindi chote tangu kuanza kwa kampeni kuelekea siku ya uchaguzi mkuu hapo tarehe 25-10-2015.
Mkurugenzi wa Idara ya Afrika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Samwel William Shelukindo(kushoto) pamoja na baadhi ya wajumbe wa timu hiyo ya waangalizi wa Umoja wa Afrika wakifuatilia mazungumzo hayo.
Kiongozi wa timu ya waangalizi wa Uchaguzi Mkuu kutoka Umoja wa Afrika ambaye pia ni Rais Mstaafu wa Msumbiji Mhe. Armando Emilio Guebuza akisisitiza jambo katika mazungumzo hayo.
Msaidizi wa Waziri Bw. Thobias Makoba (katikati) pamoja na Ofisa wa Wizara ya Nje anayeshughulikia masuala ya Afrika Bi. Zuleha Tambwe wakifuatilia mazungumzo hayo.
Mhe. Membe akifurahia jambo na Mhe. Guebuza mara baada ya kumaliza Mazungumzo yao.

          Rais Mstaafu wa Msumbiji na Kiongozi wa timu ya waangalizi wa Uchaguzi Mkuu kutoka Umoja wa Afrika Mhe.    Armando Emilio Guebuza, akiagana na Mheshimiwa                         Membe mara baada ya Mazungumzo hayo.
                               =================
                         PICHA NA: REUBEN MCHOME.

Monday, October 19, 2015

Waziri Membe awausia Mabalozi wa Tanzania

Katika picha ya kwanza, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe akiongea na Waheshimiwa Mabalozi wanaowakilisha Tanzania katika nchi mbalimbali na Wakuu wa Idara/Vitengo wa Wizara ya Mambo ya Nje. Wengine katika picha hiyo ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Dkt. Mahadhi Juma Maalim na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Balozi Liberata Mulamula. Waziri Membe aliwataka Mabalozi hao kuhakikisha kuwa mafanikio ya kidiplomasia ambayo Serikali ya awamu ya nne imeyapata yanadumishwa na kuendelezwa katika kiwango cha juu zaidi. picha nyingine ni Waheshimiwa Mabalozi waliohudhuria kikao hicho.

Mhe. Membe anaonekana akifurahia zawadi ya ramani inayoonesha mandhari mbalimbali za nchi ya Japan. Zawadi hiyo alikabidhiwa na Balozi wa Tanzania nchini Japan, Mhe. Batilda S. Burian

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI





Taarifa zaidi kuhusu Mahujaji kutoka Tanzania waliofariki na kujeruhiwa huko Saudi Arabia

Mahujaji wengine watatu kutoka Tanzania ambao walikuwa hawaonekani tokea ajali ya kukanyagana kwa mahujaji ilipotokea Makkah nchini Saudi Arabia tarehe 24 Septemba 2015 wametambuliwa kuwa, ni miongoni mwa mahujaji waliofariki  dunia. Kutambuliwa kwa mahujaji hao kunafanya idadi ya mahujaji wa Tanzania waliopoteza maisha katika ajali hiyo kufikia ishirini na tano (25). Majina kamili ya mahujaji hao ni Bi. Faiza Ahmed Omar na Bi. Rehema Ausi Rubaga kutoka kikundi cha Khidmati Islamiya pamoja na Bw. Masoud Juma Khamis kutoka Kikundi cha Ahlu Dawaa.

Hadi sasa mahujaji kumi na tano (15) kutoka Tanzania bado hawajulikani walipo na jitihada za kuwatafuta bado zinaendelea. Aidha, miili ya mahujaji kumi na tisa (19) kutoka Tanzania tayari imeshazikwa nchini Saudi Arabia.
 
Serikali ya Saudi Arabia inaendelea kutoa taarifa zaidi za kuwatambua mahujaji waliofariki dunia au kujeruhiwa katika ajali hiyo na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa itaendelea kutoa taarifa kwa umma kuhusu wahanga wa ajali hiyo kadri itakapokuwa inazipokea.

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,
Dar es Salaam
19 Oktoba, 2015

Sunday, October 18, 2015

Balozi Kasyanju awasilisha Hati za Utambulisho kwa Mtukufu Alexandre

Mheshimiwa Balozi Irene F. M. Kasyanju akiwasilisha Hati za Utambulisho kwa Mtukufu Willem-Alexander Claus George Ferdinand, Mfalme wa Uholanzi.
Mheshimimwa Balozi Irene F. M. Mkwawa Kasyanju akiwasili kwenye Kasri la Mfalme wa Uholanzi
Balozi Irene F.M. Kasyanju akiwa katika picha ya pamoja na Mtukufu Willem-Alexander Claus George Ferdinand, Mfalme wa Uholanzi.