Friday, January 8, 2016

Tanzanian Mbwana Samatta wins African Player of the Year based in Africa



Mr. Mbwana Aly Samatta-2nd from left receiving an Award as the African Player of the Year based in Africa during an event that took place in Abuja, Nigeria on 7th January, 2016
=============================================




Press Release


The Tanzania Ministry of Foreign Affairs, East Africa, Regional and International Cooperation wishes to inform the world and all football fans that Mr. Mbwana Aly Samatta, the African Player of the Year based in Africa is a citizen of Tanzania and not of Botswana or Tunisia as was reported by NBC Sports.com and several other international media.  

Mr. Samatta is one of the star players of the Tanzania national team (Taifa Stars) currently playing for TP Mazembe Club in the Congo DRC.


The Tanzanian icon was announced by the Confederation of African Football (CAF) as the African Player of the Year based in Africa in an event that took place in Abuja, Nigeria on 07th January, 2016. Mr. Samatta becomes the first player from   East Africa to win the prestigious title.


The Ministry takes this opportunity to thank Mr. Samatta for placing Tanzania on the international football stage and congratulate him for the victory well deserved.


Issued by:

Government Communication Unit
Ministry of Foreign Affairs, East Africa, Regional and International Cooperation

8th January, 2016




Wednesday, January 6, 2016

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Mashauriano kuhusu mgogoro wa Burundi baina ya Tanzania, Angola, Uganda na Jumuiya ya Afrika Mashariki

Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa Mhe. Dkt. Augustine Mahiga ameihakikishia dunia leo kuwa mazungumzo ya kuleta amani nchini Burundi bado yanaendelea vizuri licha ya taarifa zilizosambaa kuwa mazungumzo hayo yamegonga mwamba.
Dkt. Mahiga ameyasema hayo kwenye mkutano na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa mashauriano baina yake na Mhe. George Pinto Chicoti, Waziri wa Mambo ya Nje wa Angola na Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa Nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu (ICGLR); Mhe. Dkt. Crispus Kiyonga, Waziri wa Ulinzi wa Uganda ambaye ni mwakilishi wa msuluhishi wa mgogoro wa Burundi Rais Yoweri Kaguta Museveni, pamoja na Dkt. Richard Sezibera, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki jijini Arusha tarehe 6 Januari 2016.
Akielezea madhumuni ya mashauriano hayo Dkt. Mahiga alisema kuwa wadau hawa wanaunga mkono na kusifu jitihada zinazofanyika ndani na nje ya Burundi zenye lengo la kutafuta suluhu ya kudumu ya mgogoro wa kisiasa na kiusalama nchini humo kwa njia ya majadiliano.
Aidha Waziri Mahiga alisema mazungumzo hayo pia yanalenga kubadilishana ushauri, mawazo na kuandaa taarifa ya pamoja kabla ya mikutano mikubwa ya kikanda; yaani ule wa Nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu (ICGLR Summit), Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC Summit) na Umoja wa Afrika (AU Summit) inayotarajiwa kufanyika mwezi Januari mwaka huu.
Dkt. Mahiga alisema mazungumzo yao yaliyojumuisha nchi za Tanzania, Angola na Uganda ambazo zimekasimiwa majukumu ya uenyekiti na usuluhishi na jumuiya zao, yatatoa uelewa wa pamoja wa jinsi ya kuendesha mashauriano ya kuleta amani ya kudumu kabla ya mikutano tarajiwa ambayo pamoja na mambo mengine, itajadili pia suala la amani na usalama nchini Burundi.
“Naomba nirudie tena mbele yenu waandishi wa habari kwa niaba ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, chini ya uongozi wa Rais Dkt. John Pombe Magufuli; kama wenyekiti wa jumuiya hii, bado tuna nia ya dhati kabisa ya kuhakikisha kuwa kwa pamoja tunapata suluhu ya mgogoro huu, ambayo ni muhimu sana kwa usalama na maendeleo ya eneo letu na bara la Afrika kwa ujumla” alisisitiza Dkt. Mahiga kabla ya kuanza mazungumzo ya faragha na viongozi wenzake.
Waziri Dkt. Mahiga alipongeza jitihada za wadau wengine na jumuiya ya kimataifa zinazoendelea ili kuhakikisha amani ya kudumu inapatikana nchini humo.
           
MWISHO.

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali kwa Umma,
Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Kikanda na Kimataifa.
06 Januari 2016


Naibu Waziri wa Mambo ya Nje akutana kwa mazungumzo na Balozi wa India nchini

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Dkt. Suzan Kolimba (Mb.) akizungumza na Balozi wa India nchini, Mhe. Sandeep Arya (kushoto), katika mazungumzo yao Mhe. Kolimba aliupongeza Ubalozi wa India kwa kuendelea kuboresha mahusiano kati ya Tanzania na India katika Sekta mbalimbali ikiwemo Sekta ya maji. Kwa upande, Balozi Arya alimpongeza Mhe. Naibu Waziri Kolimba kwa kuteuliwa katika wadhifa huo.
Balozi Arya naye akizungumza alipokutana na Naibu Waziri, Mhe. Dkt. Kolimba
Mkutano ukiendelea.


Picha na Reginald Philip.