Wednesday, March 9, 2016

Mke wa Rais wa Vietnam atembelea Ofisini kwa Mama Magufuli na Makumbusho ya Taifa

Mke wa Rais wa Vietnam, Mama Mai Thi Hahn akisaini Kitabu cha Wageni mara baada ya kuwasili kwenye Ofisi ya Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Janeth Magufuli zilizopo Ikulu, Dar es Salaam. Mama Mai Thi Hahn ameambata na Mhe. Rais wa Vietnam Toung Tang San ambaye yupo nchini kwa ziara ya siku 4 kuanzia tarehe 8 Machi 2016.
Mama Mai Thi Hahn akiwasalimia wanawake waliokuja kumlaki katika ofisi za Mhe. Mama Magufuli.
Mama Mai Thi Hahn akisalimiana na mmoja wa wasanii wa vikundi vya ngoma vilivyofika kumlaki katika eneo la Ofisi za Mama Magufuli
Mama Mai Thi Hahn akieleza umuhimu wa ziara yake na Mhe. Rais Toung Tang San ambapo alisema lengo la ziara hiyo ni kuimarisha ushirikiano  wa kihistoria uliopo kati ya nchi yake na Tanzania.
Mama Magufuli akimkabidhi Mama Mai Thi Hahn zawadi ya Kinyago mashuhuri cha "Umoja" kilichochongwa nchini Tanzania.
Pia Mama Mai Thi Hahn naye alikabidhi zawadi kwa Mama Magufuli.
Wake za Marais wakicheza ngoma na kikundi cha ngoma kilichokuwa kikitumbuiza ofisini hapo.
Mama Hahn na Mama Magufuli wakiagana na kina mama (hawapo pichani) mara baada ya kutembelea ofisini

 ..........Alipotembelea Makumbusho ya Taifa

Mama Hahn na Mama Magufuli wakisalimiana na baadhi ya wafanyakazi wa Makumbusho ya Taifa mara baada ya kuwasili.
Mama Mai Thi Hahn akisaini kitabu cha Wageni katika Ofisi za Makumbusho za Taifa
Mwenyeji wake Mama Janeth Magufuli naye akisaini kitabu cha wageni katika ofisi hizo.
Wakipokea maelezo ya Michoro kutoka kwa afisa wa makumbusha ya Taifa hayupo pichani inayoeleza historia ya nchi ya Tanzania na namna Wasanii walivyoweza kuwa wabunifu kwa kuchora picha nzuri zinazoeleza historia ya Taifa.
Afisa wa Makumbusho akiendelea kuelezea michoro mingine na maana zake ambapo makumbusho hiyo imekuwa ikihifadhi kumbukumbu hizo kwa ajili ya vizazi vya sasa na vijavyo katika kurithisha historia na wageni kuweza kuijua historia ya Tanzania
Wakiendelea kupokea maelezo.
Wakielezewa na Afisa wa Makumbusho ya Taifa  kuhusu picha zinazoonyesha historia ya utumwa ambapo wakati wa Ukoloni Tanzania ilikuwa miongoni mwa nchi ambazo watumwa walichukuliwa.
Maelezo juu ya  biashara ya pembe za ndovu enzi za ukoloni  yakiendelea kutolewa.
Mara baada ya kumaliza ziara hiyo Wake za Marais kwa pamoja walikabidhiwa zawadi ya vikapu vya asili na ofisi ya Makumbusho ya Taifa.

Rais wa Vietnam awasili nchini kuanza ziara ya kwanza ya kitaifa

Rais wa Jamhuri ya Kisoshalisti ya Vietnam, Mhe. Truong Tang San (kushoto) pamoja na mkewe Mama Mai Thi Hann wakipunga mkono mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Kambarage Nyerere kwa ajili ya kuanza ziara ya kwanza ya kitaifa nchini.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa akimpokea Rais wa Vietnam Mhe. Troung Tang San kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli mara baada ya kuwasili nchini
Waziri Mkuu Mhe. Majaliwa (kulia) akimtambulisha Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa Balozi Augustine Mahiga ( wa pili kushoto) kwa Rais wa Vietnam Mhe. Truong Tang San (mwenye tai ya Blue).
Rais Truong Tang San akisalimiana na Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Autralasia katika Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Mbelwa Kairuki
Rais Troung Tang San pamoja na Mkewe Bi. Mai Thi Hahn (mwenye nguo ya bluu) wakitizama kikundi cha ngoma kilichokuwapo Uwanja wa Ndege.
Waziri wa Mambo ya Nje akizungumza na waandishi wa habari waliojitokeza kumlaki Rais Truong Tang San
Waziri Mkuu Mhe. Majaliwa akiagana na Rais Truong Tang San mara baada ya kuwasili hotelini kwake.
 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Mhe. Paul Makonda akimweleza jambo Balozi Mbelwa wakati wa mapokezi ya Rais Truong wa Vietnam.

Tuesday, March 8, 2016

Waziri Mahiga akutana na Waziri wa Uingereza wa masuala ya Afrika


Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akimkaribisha Waziri wa Uingereza anayeshughulikia masuala ya Afrika, Mhe. James Duddridge, mara baada ya kuwasili katika ofisi za Wizara ambapo waliweza kufanya mazungumzo. 
Mhe. Waziri Mahiga akiendelea na Ukaribisho kwa Mhe. Balozi Diana Melrose ambaye aliambatana na Mhe. Waziri James Duddridge katika mazungumzo hayo.
Mhe. Waziri Mahiga akiwa katika mazungumzo na Mhe. Waziri wa Uingereza anayeshughulikia masuala ya Afrika ambapo katika mazungumzo yao waliweza kujadili masuala ya maendeleo hususan katika sekta ya uwekezaji na biashara pamoja na kuangalia namna Serikali ya Uingereza inavyoweza kushirikiana na Tanzania katika kukuza uchumi na kuimarisha viwanda.
Mhe. Balozi Diana Melrose pamoja na afisa aliyeambatana naye wakifuatilia mazungumzo kati ya Mhe. Waziri Mahiga na Mhe. Waziri James Duddridge.
Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika, Balozi Joseph Sokoine wa kwanza kushoto, akiwa pamoja na Afisa Mambo ya Nje, Bi. Mona Mahecha na Msaidizi wa Waziri Bw. Thobias Makoba kulia wakifuatilia mazungumzo pia.
Mhe. Waziri Mahiga akiagana na Waziri wa Uingereza anayeshughulikia masuala ya Afrika mara baada ya kumaliza mazungumzo.

Balozi Mahiga ala kiapo cha utii katika Bunge la Afrika Mashariki

Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Dkt. Augustine Mahiga (Mb.) akila kiapo mbele ya Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki, akiwa kama Waziri anayehusika na Shughuli za Ushirikiano wa Afrika Masahiriki kutoka Tanzania. Tukio hilo la kuapishwa kwa Waziri Mahiga limeshuhudiwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndungai (hawapo pichani), hafla hiyo imefanyika leo mchana jijini Dar es Salaam. 
Sehemu ya Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki wakishuhudia Balozi Mahiga akila kiapo (hayupo pichani).
Sehemu ya watumishi kutoka Serikalini wakifuatilia tukio hilo la uapisho. Mstari wa nbele katikati ni Mkuu wa Kitengo cha Habari na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Bi. Mindi Kasiga.
Sehemu nyingine ya viongozi kutoka Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa. Wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi wa Sera na Mipango, na kulia ni Katibu wa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Bw. Adam Issara.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa (Mb.) wa kwanza kushoto, Spika wa Bunge la Afrika Mashariki, Mhe. Daniel Kidega    na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Job Ndungai kwa pamoja wakiimba wimbo wa Afrika Mashariki kabla ya Kuapishwa kwa Waziri Mahiga (hayupo pichani). 
Wabungu wa Bunge la Afrika Mashariki nao wakiimba Wimbo wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Shughuli za Kibunge zikiendelea  mara baada ya kumalizika kwa tukio la Uapisho wa Balozi Mahiga
Picha na Reginald Philip


Waziri Mahiga afungua Mkutano wa Pili wa Vyama vya Kijamii vya ICGLR

Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Masahriki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Augustine Mahiga (Mb.) akizungumza katika ufunguzi wa Mkutano wa Pili wa Jukwaa la vyama visivyo vya Kiserikali (Vyama vya Kijamii), kutoka Nchi za Jumuiya ya Ukanda wa Maziwa Makuu (ICGLR) uliofanyika mapema leo katika Hoteli ya Ramada Jijini Dar es Salaam. Katika ufunguzi huo Waziri Mahiga aliwashukuru wajumbe kwa kuchagua kuufanyia mkutano wao hapa nchini vilevile kuwa na ushirikiano katika masuala ya kijamii ambayo yatapelekea kuondoa machafuko ya wenyewe kwa wenyewe katika nchi wanachama
Sehemu ya wajumbe wakimsikiliza kwa makini Balozi Mahiga (hayupo pichani) alipokuwa akifungua Mkutano huo.
Sehemu nyingine ya wajumbe kutoka Sudan Kusini nao wakifuatilia kwa makini ufunguzi huo.
Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa UN eneo la Maziwa Makuu Balozi Said Djinnit naye alipata fursa ya kuzungumza katika ufunguzi wa mkutano huo.
Sehemu ya Watumishi kutoka Wizara ya Mambo ya Nje Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa nao wakifuatilia kwa makini hotuba iliyokuwa ikitolewa na Mhe. Waziri Mahiga (hayupo pichani), wa kwanza kulia ni Katibu wa Waziri Mahiga, Bw. Adolf Mchemwa, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali, Bi. Mindi Kasiga (wa kwanza kushoto) na katikati ni Afisa Mambo ya Nje, Bw. Ally Ubwa
Mwenyekiti wa Kikanda wa Jukwaa la Vyama visivyo vya Kiserikalikutoka nchi za Maziwa Makuu, Bw. Joseph Butiku naye akizungumza katika ufunguzi wa Mkutano huo 
Mwakilishi wa Umoja wa Afrika eneo la Maziwa Makuu Bi. Altine Traore naye akizungumza
Meza kuu wakimsikilza Bi. Traore (hayupo pichani) alipo kuwa akitoa hotuba yake. 
Waziri Mahiga akizungumza na Waandishi wa Habari.
Picha ya Pamoja.

Picha na Reginald Philip

Waziri Mahiga ashiriki ibada ya kumuaga Marehemu Balozi Rwegasira

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Augustine Mahiga akitoa pole kwa niaba ya Wizara kwa familia ya aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Nje, Marehemu Balozi Joseph Rwegasira wakati wa ibada ya mazishi iliyofanyika katika Kanisa la Mtakatifu Petro Jijini Dar es Salaam.Balozi Mahiga alimwelezea Marehemu Balozi Rwegasira kuwa alikuwa kiongozi hodari wa kupigiwa mfano kutokana na moyo wake wa kufanya kazi kwa bidii na kujituma.
Ndugu na jamaa waliohudhuria ibada hiyo wakimsikiliza kwa makini Waziri Mahiga (hayupo pichani).
Sehemu nyingine ya watu waliohudhuria ibada hiyo
Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Jaji Joseph Sinde Warioba naye alipata fursa ya kutoa neno la pole kwa familia ya Marehemu Balozi Rwegasira.
Mmoja wa wanafamilia ya Balozi Rwegasira akisoma utaratibu wa kutoa heshima za mwisho za kuuaga mwili wa Balozi Rwegasira
Sehemu ya Viongozi wa Serikali na Vyama vya Kisiasa wakisikiliza utaratibu wa kutoa heshima za mwisho kwa  mwili wa Balozi Rwegasira.
Waziri Mahiga akimpa mkono wa pole Mama Rwegasira
Waziri Mahiga pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Aziz Mlima wakitoa heshima za mwisho kwa mwili wa Bolozi Rwegasira
Sehemu ya Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa wakitoa mkono wa pole kwa familia ya Balozi Rwegasira